Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Atakayetaja Mazuri Ya Watu Wa Bid’ah Atakuwa Naye Anaeneza Bid’ah

 

Mtu Ambaye Atataja Mazuri Ya Watu Wa Bid’ah Atakuwa Naye Anaeneza Bid’ah

 

Shaykh  Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan

 

Kutoka: Sharh Lum’at-il-I’tiqaad, Uk. 269

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Manhaj ya Ahlus Sunnah ni mtu kuwasusia Ahlul Bid'ah ili waache Bid’ah zao. Ikiwa mtu hatowagomea, basi itakuwa unawasaidia na kukubaliana na wanayoyafanya na kuwadanganya wengine.

 

Ikiwa Wanachuoni na wale viigizo bora (Mashaykh na Madaa’iyyah) watawagomea, watu pia watakuja kuwatenga. Itakuja pia kusababisha wahisi aibu kwa watu. Ndio maana watu wa Bid’ah walikuwa wanajificha wakati wa Maswahaba na zile karne bora. Watu wa Bid’ah walianza kujitokeza katika karne ya nne baada ya zile karne bora kutoweka.

Haifai kusema kama jinsi wajinga wa leo wanavyosema, haki ni kuwa ni lazima mtu ataje kwanza mazuri ya watu wa bid’ah kisha bid’ah zao. Wao huita Muwaazanaat, usawa.

 

Kwa njia hii huenea Bid’ah. Sisi hatujaamrishwa kutaja yale mema mazuri. Hilo tumuachie nalo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Isitoshe, vipi tutakuwa tunajua mazuri yao na kwamba kweli yanachukuliwa vizuri na Allaah? Sisi hatujaamrishwa hilo.

 

Sisi tulichoamrishwa tu ni kuonyesha makosa ili watu waepukane nayo na ili mtu huyo aje kutubia kwa Allaah ('Azza Wa Jalla) ikiwa Allaah Anamtakia mazuri. Kutaja sifa zake nzuri kunawafanya watu kuchukulia Bid’ah ni kitu chepesi.

 

 

 

Share