Achari Ya Ndimu Na Karoti

Achari Ya Ndimu Na Karoti

Vipimo

Ndimu – 20

Karoti - 3

Pilipili nyekundu - Kiasi mteko wa mkono

Ndimu ziada za kukamulia - Nyingi kiasi 

Chumvi - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Kata ndimu katikati bila ya kuachana vipande (slit)
  2. Kwangua karoti ukate vipande virefurefu
  3. Kata pilipili katikati bila ya kuchana
  4. Changanya vizuri vyote katika bakuli kubwa kisha tia katika chupa ya achari.
  5. Kamua ndimu juisi yake ifunike ndimu na karoti katika chupa.
  6. Weka juani muda wa siku chache mpaka zilainike na kuwa tayari

Kidokezo:

Hakikisha huingizi maji katika achari ili isiharibike.

                                 

 

  Bis-swihhah wal-hanaa (kunywa kwa siha na kufurahika)

 

 

Share