Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (http://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Hadiyth: Fadhila Za لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ

Hadiyth: Fadhila Za لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ

Hadiyth Mbalimbali [1]

                           

 

 

Bonyeza Viungo Vifuatavyo Upate Masharti Yake:

 

 

Sharh (Maelezo) Ya Masharti Ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّه [2]

 

Masharti Ya لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ مُحَمدا رَسُول الله [3]

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share [4]

01-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Dhikri Bora Kabisa

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

01-Dhikri Bora Kabisa Ni Laa Ilaaha Illa Allaah

 

 

 

عَنْ جَابِرٍ  رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: ((أَفْضَلُ الذِّكْرِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الحَمْدُ لِلَّهِ))  رواه الترمذي وقال: حديث حسن   

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) amesema: Nimemsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema:  ((Dhikri bora kabisa ni Laa ilaaha illa Allaah  na du'aa bora kabisa ni Alhamdulillah)) [At-Tirmidhiy amesema: Hadiyth Hasan, Ibn Maajah na  ameisahihisha Al-Albaaniy: Swahiyh Al-Jaami’ (1104), Swahiyh Ibn Maajah (3080)  Swahiyh At-Tirmidhiy (3383)]

 

 

 

 

 

 

Share [5]

02-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Iko Daraja Ya Juu Kabisa

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

02-Laa Ilaaha Illa Allaah: Iko Daraja Ya Juu Kabisa

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صلى الله عليه و آله وسلم):  ((الإيمَانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ)) أَوْ ((بِضْعٌ وَسِتُّونَ شُعْبَةً، فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ،  وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنْ الطَّرِيقِ، وَالْحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنْ الإِيمَانِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Iymaan ni sabiini na kitu)) au alisema ((Tanzu sitiini na kitu. Ilio bora kabisa ni kauli ya ‘Laa ilaaha illa-Allaah’, na ya chini kabisa ni kuondosha taka njiani. Na kuona hayaa ni utanzu katika tanzu za Iymaan)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Faida: Bidhw’ ni idadi baina ya tatu na tisa.

 

 

 

Share [6]

03-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayefariki Akiwa Anajua Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

 

03-Atakayefariki Akiwa Anajua Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah

 

 

 عَنْ عُثْمَانَ بِنْ عَفَّان رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ  أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Uthmaan bin ‘Afaan (رضي الله عنه) amesema:  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayefariki akiwa anajua kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah ataingia Jannah)). [Muslim]

 

 

Share [7]

04-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayeshuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah… Allaah Atamuingiza Jannah Kwa ‘Amali Alizonazo

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

04-Atakayeshuhudia Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah … Allaah Atamuingiza Jannah Kwa ‘Amali Zozote Alizonazo:

 

 

عن عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رضي الله عنه  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللّهِ صلى الله عليه وسلم: ((مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَالْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنْ الْعَمَلِ))

Imepokelewa kutoka kwa ‘Ubaadah Bin Swaamit (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayeshuhudia kwa kuamini na kukiri moyoni kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na neno Lake Alilompelekea Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo)) [Al-Bukhaariy (3/1267) (3252), Muslim (1/57) (28) Ahmad (5/313) (22727), Ibn Hibbaan (1/431) (202), An-Nasaaiy (6/331) (11132)].

Share [8]

05-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayesema Na Akakanusha Wanaoabudiwa Asiyekuwa Allaah Italindwa Mali Na Uhai Wake Na Hesabu Yake Itakuwa Kwa Allaah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

05-Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akakanusha Wanaoabudiwa Asiyekuwa Allaah Italindwa Mali Yake Na Uhai Wake Na Hesabu Yake Itakuwa Kwa Allaah

 

 

 

عَنْ أَبِي مَالِكٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: ((مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَكَفَرَ بِمَا يُعْبَدُ مِنْ دُونِ اللَّهِ حَرُمَ مَالُهُ وَدَمُهُ وَحِسَابُهُ عَلَى اللَّهِ)) مسلم‏

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Maalik kutoka kwa baba yake amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akisema: ((Atakayesema “Laa ilaaha illa Allaah” na akakanusha wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai wake) na hesabu yake iko kwa Allaah)) [Muslim]

 

 

Share [9]

06-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Abashiriwe Jannah Mwenye Kushuhudia Akiwa Na Yakini Moyoni Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah.

 Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Ila Allaah

 

06-Abashiriwe Jannah Mwenye Kushuhudia Akiwa Na Yakini Moyoni

Kwamba Laa Ilaaha Illa Allaah.

 

 

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwita:

 

((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))

((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki ila Allaah akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)) [Muslim]

 

 

 

 

 

 

 

 

Share [10]

07-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atatoka Motoni Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akiiwa Moyoni Mwake Kuna Kheri (Iymaan) Kiasi Cha Uzani Wa Shairi Au Mbegu Au Punje

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah [11]

07-Atatoka Motoni Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akiwa Moyoni Mwake Kuna Khayr (Iymaan) Kiasi Cha Uzani Wa Shairi Au Mbegu Au Punje

 

 

عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((يَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ شَعِيرَةٍ مِنْ خَيْرٍ، وَيَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ بُرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ، وَيَخْرُجُ مِنَ النَّارِ مَنْ قَالَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَفِي قَلْبِهِ وَزْنُ ذَرَّةٍ مِنْ خَيْرٍ))  الْبخاري ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atatoka motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah (hakuna muabudiwa wa haki ila Allaah)) akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha uzani wa shairi. Na Atatoka motoni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha mbegu moja. Na atatoka motoni anayesema: laa ilaaha illa Allaah akiwa moyoni mwake kuna khayr (iymaan) kiasi cha uzani wa punje)). [Al-Bukhaariy (44) Muslim (193)]

 

Share [12]

08-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Kauli Thabiti Ya Uhai Wa Dunia Na Aakhirah

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah [11]

 

08-Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Kauli Thabiti Ya Uhai Wa Dunia Na Aakhirah

 

 

 عَنْ الْبَرَاء بْن عَازِب رَضِيَ اللَّه عَنْهُ أَنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((الْمُسْلِم إِذَا سُئِلَ فِي الْقَبْر شَهِدَ أَنْ لاَ إِلَه إِلاَّ اللَّه وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُول اللَّه فَذَلِكَ قَوْله (يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ))) البخاري  وَرَوَاهُ مُسْلِم أَيْضًا وَبَقِيَّة الْجَمَاعَة

Imepokelewa kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Muislamu akiulizwa katika kaburi, atashuhudia kwamba: "Laa ilaaha illa-Allaah wa anna Muhammadar-Rasuwlu-Allaah" [Hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli wa Allaah] hiyo ndiyo maana ya kauli ya Allaah: “Allaah Huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika uhai wa dunia na Aakhirah”)). [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

 

 

Share [13]

09-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayefurahika Zaidi Kwa Shafaa Ya Nabiy Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Kwa Niyyah Safi Moyoni Au Nafsini Mwake

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

09-Atakayefurahika Zaidi Kwa Shafaa Ya Nabiy Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Kwa Niyyah Safi Moyoni Au Nafsini Mwake

 

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ  قُلْتُ يَا رَسُولَ اللهِ مَنْ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ؟ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلى اللهُ عليهِ وَسَلَّمَ: ((لَقَدْ ظَنَنْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ أَنْ لا يَسْأَلَني عَنْ هذَا الْحَدِيِثِ أَحَدٌ أَوَّلَ مِنْكَ لِما رَأَيْتُ مِنْ حِرْصِكَ عَلَى الْحَدِيثِ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَنْ قَالَ: لا إِلهَ إِلاَّ اللهُ خَالِصَاً مِنْ قَلْبِهِ أَوْ نَفْسِهِ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Nani atakayefurahika kabisa kwa Shafaa’ah (uombezi) wako Siku ya Qiyaamah: Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Nlidhani ee Abaa Hurayrayh kwamba hakuna yeyote asiyekuwa wewe atakayeniuliza maelezo haya kwa vile jinsi nilivyoona himma yako juu ya jambo hili. Atakayefurahika zaidi kati ya watu kwa Shafaa’ah yangu Siku ya Qiyaamah ni atakayesema: laa ilaaha illa Allaah – hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, kwa niyyah safi moyoni mwake au nafsi yake)). [Al-Bukhaariy]

 

Share [14]

10-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Allaah Ameharamisha Moto Anayesema Laa Ilaaha Illa Akitafuta Kwayo Wajihi Wa Allaah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

10-Allaah Ameharamisha Moto Anayesema Laa Ilaaha Illa Allaah Akitafuta Kwayo Wajihi Wa Allaah

 

 

عن عِتْبَانَ بْن مَالِكٍ الْأَنْصارِيَّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ عَلَى النَّارِ مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ يَبْتَغِي بِذَلِكَ وَجْهَ اللَّهِ ))

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Itbaan bin Maalik Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika Allaah Ameharamisha An-Naar kwa anayesema: laa ilaaha illa Allaah akitafuta Wajihi wa Allaah)). [Al-Bukhaariy (425), Muslim (33)] 

 

 

Share [16]

11-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayekiri Na Kushuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah Akiyasadikisha Moyoni Ataharamishwa Na Moto.

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

11-Atakayekiri Na Kushuhudia Laa Ilaaha Illa Allaah Akiyasadikisha Moyoni Ataharamishwa Na Moto.

 

 

عَنْ أنَس بِن مالِك رضي الله عنه عن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال: (( مَا مِنْ أَحَدٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ صِدْقًا مِنْ قَلْبِهِ إِلَّا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَى النَّارِ))

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna mtu atakayekiri na kushuhudia kwa kusadikisha moyoni mwake kwamba: laa ilaaha illa Allaah – hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa Allaah Atamharamisha na Moto)). [Al-Bukhaariy (128) Muslim (32)]

 

 

Share [17]

12-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Miongoni Mwa Mambo Matano Yatakayokuwa Mazito Katika Mizani Siku Ya Qiyaamah

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

12-Miongoni Mwa Mambo Matano Yatakayokuwa Mazito Katika Mizani Siku Ya Qiyaamah

 

 

عن ثوبان رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((بَخٍ بَخٍ لِخمسٍ ما أثقلَهُنَّ في الميزانِ : لا إلهَ إلَّا اللهُ، وسبحانَ اللهِ، والحمدُ للهِ ، واللهُ أكبرُ، والولَدُ الصالِحُ يُتوَفَّى للمرْءِ المسلِمِ فيَحتَسِبُهُ)) النسائي وابن حبان والحاكم ، وأحمد ، وصححه الألباني في صحيح  الترغيب والجامع    

 

Imetoka kwa Thuwbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu)  ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Heko heko kwa vitu vitano, uzito gani vitakavyokuwa  katika Mizani; Laa Ilaah Illa  Allaah, Wa-Allaahu Akbar, Wa Subhaanah-Allaah, Wa-AlhamduliLLah, na mtoto mwema atakayekufa na wazazi wake wanatarajia thawabu kutoka kwa Allaah)) [An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Al-Haakim, Ahmad, na kaisahihisha Al-Albaaniy katika:  Swahiyh At-Targhiyb (1557), Swahiyh Al-Jaami'(2817)]

 

 

Share [18]

13-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah:Moto Hautamgusa Atakayeruzukiwa Kauli Hiyo Katika Mauti Yake

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

13- Moto Hautamgusa Atakayeruzukiwa Kauli Hiyo Katika Mauti Yake

 

 

عن أَبِي هُرَيْرَةَ، وَأَبِي سَعِيدٍ، أَنَّهُمَا شَهِدَا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:  ((إِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ. يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَأَنَا أَكْبَرُ. وَإِذَا قَالَ الْعَبْدُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا وَحْدِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَا شَرِيكَ لَهُ. قَالَ : صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا شَرِيكَ لِي .وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ  قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، لِي الْمُلْكُ، وَلِيَ الْحَمْدُ . وَإِذَا قَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ . قَالَ: صَدَقَ عَبْدِي، لَا إِلَهَ إِلَّا أَنَا، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِي. ثم قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:  مَنْ رُزِقَهُنَّ عِنْدَ مَوْتِهِ لَمْ تَمَسَّهُ النَّارُ))

 

Kutoka kwa Abuu Hurayrah na Abuu Sa’iyd (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) wameshuhudia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

((Mja akisema: “laa ilaaha illa Allaah wa Allaahu Akbar – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na Allaah ni Mkubwa.”  Allaah ‘Azza wa Jalla Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Nami ni Mkubwa.” Akisema mja: “Laa ilaaha illa Allaah Wahdahu – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah Pekee.” Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi Pekee.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu laa shariyka Lahu - hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hana mshirika.” Husema: “Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi sina Mshirika.”.Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, ufalme na Himdi ni Zake.” Husema: Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, Ufalme na Himdi ni Zangu.” Na atakaposema: “Laa ilaaha illa Allaahu, walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah – hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah.” Husema: Amesadikisha mja Wangu, hakuna mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi na hakuna uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka Kwangu.” Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: Atakayeruzukiwa [kauli] hiyo wakati wa mauti yake, An-Naar [Moto] hautomgusa)). [Ibn Maajah (3794) na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (713)]

 

 

 

Share [19]

14-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Kusema Subhaana Allaah... Laa Ilaaha Allaah Naipenda Zaidi Kuliko Kilichoangaziwa Na Jua

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

 

14- Kusema Subhaana Allaah WalhamduliLLaah Wa Laa Ilaaha Illa Allaah Wa Allaahu Akbar Naipenda Zaidi Kuliko Kila Kilichoangaziwa Na Jua

 

 

عَنْ أبي هريرة رضي الله عنه: قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((لأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إَلَهَ إلاَّ اللهُ، واللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إَلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ)) مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kusema kwangu: Subhaana-Allaah, WalhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar (Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki  ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa) naipenda zaidi kuliko kila kilichoangaziwa na jua))  [Muslim]

 

 

Share [20]

15-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Kutamka Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Miongoni Mwa Swadaqah

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

15-Kutamka Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Miongoni Mwa Swadaqah

 

 

عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه:  أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ  بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ: ((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ 

  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Watu katika Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ee Rasuli wa Allaah! Watu wenye mali wameondoka na thawabu nyingi; wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga na wanatoa swadaqah kwa fadhila za mali zao. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, kwani Allaah Hakukujaalieni njia ya kutolea swadaqah? Hakika kila (kutamka) Tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah. Na kila Takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah. Na kila Tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah, na kila Tahliyl (Laa ilaaha illa Allaah) ni swadaqah. Na kuamarisha mema ni swadaqah. Na kukataza munkari ni swadaqah. Na mmoja wenu kujimai (na mkewe) ni swadaqah.”  Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah. Hivi mmoja wetu kujitoshelezea kwa shahawa yake atakuwa anapata thawabu? Akasema: “Mnaonaje kama atajitosheleza kwa njia ya haraam angelipata dhambi? Hivyo basi ikiwa atafanya kwa njia ya halaal, atapata thawabu.”  [Muslim]

 

 

Share [21]

16-Fadhila Za Laa Iaaha Illa Allaah: Atakayekuwa Maneno Yake Ya Mwisho Ni Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah

 Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

 www.alhidaaya.com [15]

 

16-Atakayekuwa Maneno Yake Ya Mwisho Ni Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah

 

 

 عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((مَنْ كَانَ آخِرُ كَلامِهِ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ)) رواه أبو داود ( 3116 ) وحسَّنه الألباني في "إرواء الغليل" ( 3 / 149 ).

 

Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayekuwa maneno yake ya mwisho ni Laa ilaaha illa Allaah ataingia Jannah)). [Abuu Daawuwd, Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Irwaa Al-Ghaliyl (3/149), Swahiyh Al-Jaami’ (6479), Swahiyh Abiy Daawuwd (3116)].

 

 

Share [22]

17-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Kughufuriwa Makosa Japokuwa Ni Mfano Wa Povu La Bahari

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

17-Kughufuriwa Makosa Japokuwa Ni Mfano Wa Povu La Bahari

 

 

Akitamka mtu: “Laa ilaaha illa Allaah …” kila baada ya Swalaah baada ya Adkhaar za Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr mara thelathini na tatu kila moja na akamalizia kwa: “Laa ilaaha illa Allaah…” mara moja:

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه  عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((مَنْ سَبَّحَ اللَّهَ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَحَمِدَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَكَبَّرَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ فَتْلِكَ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ وَقَالَ تَمَامَ الْمِائَةِ لا إِلَهَ إِلاّ اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ)) رواه مسلم  

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakaye Sabbih (Subhaana Allaah) kila baada ya Swalaah mara thelathini na tatu, akaleta tahmiyd (AlhamduliLLaah) mara thelathini na tatu akaleta takbiyra (Allaahu Akbar) mara thelathini na tatu, akamalizia kwa: “Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr [Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu]  ataghufuriwa makosa yake japokuwa ni mfano wa povu la bahari)). [Muslim (1/418) [597]]

 

 

Share [23]

18-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Atakayetamka Baada Ya Wudhu ... Atafunguliwa Milango Minane Ya Jannah Aingie Autakao

 Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

 www.alhidaaya.com [15]

 

18-Atakayetamka Baada Ya Wudhu “Ash-hadu An Laa Ilaaha Illa Allaah...

Atafunguliwa Milango Minane Ya Jannah Aingie Autakao

 

عَنْ عُمَرَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم : ((مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ، فَيُسْبِغُ اَلْوُضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ)) أَخْرَجَهُ مُسْلِم

 

Kutoka kwa ‘Umar (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu anayetawadha vizuri, kisha akasema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, wa ash-hadu anna Muhammad ‘Abduhuu wa Rasuwluhu” (Nashuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake, hana mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake) ila atafunguliwa milango minane ya Jannah aingie wowote aupendao kati ya hiyo.” [Imetolewa na Muslim na At-Tirmidhiy]

 

 

Share [24]

19-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Maneno Bora Kabisa Waliyotamka Manabii Wote

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com  [25] 

 

19-Maneno Bora Kabisa Waliyotamka Manabii Wote

 

 

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال:  ((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni: “Laa Ilaaha illa Allaah Wah-dahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr” [Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu])) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184), Silsilatu Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/6), Swahiyh At-Targhiyb (1536)]

 

 

Share [26]

20-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayeamka Usingizi Akasema: “laa ilaaha illa Allaah…” Atataqabaliwa Du’aa Na Swalaah Yake.

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com  [25]

 

20-Atakayeamka Usingizi Akasema: ““Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu…” Atataqabaliwa

Du’aa Na Swalaah Yake.

 

 

 عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ  وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ. ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي  أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ, فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))

 

Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: “Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah” (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah), kisha akasema: “Rabbigh-fir-liy” [ee Allaah, nighufurie] au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake)). [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

 

Share [27]

21-Fadhila Za Laa ilaaha Illa-Allaah: Du’aa Anapopatwa Mtu Na Janga, Dhiki, Balaa: Laa ilaaha illa-Allaahul-‘Aliymul-Haliym...

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

21-Du’aa Anapopatwa Mtu Na Janga, Dhiki, Balaa

 

www.alhidaaya.com [15]

 

 

  عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما  قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ عِنْدَ الْكَرْبِ ‏: ((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ الْعَلِيمُ الْحَلِيمُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَوَاتِ وَرَبُّ الأَرْضِ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ))

Imepokelewa kutoka kwa ibn ‘Abbaas  (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema katika hali ya janga (balaa):

 

Laa ilaaha illa-Allaahul-‘Aliymul-Haliym. Laa ilaaha illa-Allaahu Rabbul-‘Arshil-‘Adhwiym. Laa ilaaha illa-Allaahu Rabbus-samawaati wa Rabbul-ardhwi wa Rabbul-‘Arshil-Kariym.

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Aliye Mjuzi, Mvumilivu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Rabb wa ‘Arsh Adhimu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Rabb wa mbingu na Rabb wa ardhi na Rabb wa ‘Arsh tukufu. [Al-Bukhaariy (7/154) [6346], Muslim (4/2092) [2730]]

 

 

Share [28]

22-Fadhila Za Laa ilaaha Illa-Allaah: Thawabu Za Kuacha Huru Watumwa Kumi Kuandikiwa Mema Mia Kufutiwa Maovu Mia Ni Kinga Ya Shaytwaan Na Atakuwa Mtu Bora Kabisa

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

22-Thawabu Za Kuacha Huru Watumwa Kumi,

Kuandikiwa Mema Mia, Kufutiwa Maovu Mia,

Ni Kinga Ya Shaytwaan Kwa Siku Hiyo,

Na Hatakuwa Mtu Yeyote Mbora Kumshinda Ila Yule Aliyefanya Zaidi Yake

www.alhidaaya.com [15]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ : ((مَنْ قَالَ : لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ ، كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ ، وَكُتِبَتْ لَهُ مِائَةُ حَسَنَةٍ ، وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِائَةُ سَيِّئَةٍ، وَكَانَتْ لَهُ حِرْزًا مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِيَ ، وَلَمْ يَأْتِ أَحَدٌ بِأَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ ، إِلَّا أَحَدٌ عَمِلَ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ)) البخاري  ومسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema kwa siku mara mia,

 

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr.  

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah  Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa maovu mia moja, na atakuwa na kinga ya shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

Share [29]

23-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Unapohangaika Kupata Usingizi Sema: Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar...

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

23-Unapohangaika Kupata Usingizi Sema Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar..

 

 

عن عائشة أم المؤمنين رضي الله عنها ان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم إذا تضوَّر مِن اللَّيلِ قال: ((لا إلهَ إلَّا اللهُ الواحدُ القهَّارُ ربُّ السَّمواتِ والأرضِ وما بينَهما العزيزُ الغفَّارُ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akihangaika kupata usingizi usiku akisema:

 

لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ الـواحِدُ القَهّـار، رَبُّ السَّـمواتِ وَالأرْضِ وَما بَيْـنَهـما، العَزيـزُ الغَـفّار

Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar. Rabbus-samawaati wal ardhwi wamaa baynahumaal-’Aziyzul-Ghaffaar.

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah  Al-Waahid (Mmoja Pekee) Al-Qahhaar (Mshindi Mwenye kudhibiti na kudhalilisha). Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, Al-’Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima) Al-Ghaffaar (Mwingi wa kughufuria)) [An-Nasaaiy katika As-Sunan Al-Kubraa (10700), Swahiyh Ibn Maajah (5530), Swahiyh Al-Jaami’ (4693), Al-Haakim na ameisahihisha Adh-Dhahabiy (1/540), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah (864) na Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah (757)]

 

 

Share [30]

24-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah… Allaah Humsadiki Na Akiwa Katika Ugonjwa Akafa Ameahidi Kuwa Moto Hautamla.

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

24-Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah, Wa-Allaahu Akbar....

Allaah Humsadiki Na Akiwa Katika Ugonjwa Akafa Ameahidi Kuwa Moto Hautamla.

 

 

عن أَبي سعيد الخُدْرِيِّ وأَبي هريرة رضيَ اللَّه عنهما ، أَنهُما شَهِدَا على رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنه قال: ((مَنْ قَالَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ ، صَدَّقَهُ رَبُّهُ فَقَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَأَنَا أَكْبَرُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي لا شَرِيكَ لِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا لِيَ الْمُلْكُ وَلِيَ الْحَمْدُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ ، قَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِي)) وَكَانَ يَقُولُ: ((مَنْ قَالَهَا فِي مَرَضِهِ ثُمَّ مَاتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ))

Abu Sa’iyd Al-Khudriyy na Abu Hurayrah (رضي الله عنهما), wameshuhudia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa”, Rabb wake Amemsadiki, Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Nami ni Mkubwa”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Peke Yangu”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Mpweke Hana mshirika”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi Peke Yangu Sina mshirika”. Na akisema; “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, ni Wake Ufalme na Himdi ni Zake”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Ufalme ni Wangu na Himdi ni Zangu”. Na Akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa Zangu.”)) Na Alikuwa (Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Atakayesema hayo akiwa mgonjwa akafariki, moto hautamla)) [At-Tirmidhiy [3430], Ibn Maajah [3794], na ameisahihisha Al-Albaaniy. Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/152), Swahiyh Ibn Maajah (2/317), Swahiyh At-Targhiyb (3481)]

 

 

Share [31]

25-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Nguzo Ya Kwanza Ya Kiislamu: Laa Ilaaha Illa Allaah ...

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

25-Laa  Ilaaha Illa Allaah Ni Nguzo Ya Kwanza Ya Kiislamu

 

 عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: ((بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ: شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan Abdillaah bin 'Umar bin Al-Khattwaab  (رضي الله عنه)  amesema:  Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba: Laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) na Muhammad ni Rasuli Wake,  kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Share [32]

26-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah:Hakuna Anayeweza Kukizuia Alichokitoa Allaah Wala Alichokizuia Wala Utajiri Wa Mtu Hautamsaidia Aliyetajiri Mbele Ya Allaah

 

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

 

26- Hakuna Anayeweza Kukizuia Alichokitoa Allaah Wala Alichokizuia Wala Utajiri Wa Mtu Hautamsaidia Aliye Tajiri Mbele Ya Allaah

 

 

 عَنْ وَرَّادٍ، كَاتِبِ الْمُغِيرَةِ قَالَ: كَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى الْمُغِيرَةِ: اكْتُبْ إِلَىَّ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ فَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ نَبِيَّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ: (( لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهْوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ ‏))

Warraad (Mwandishi wa Al-Mughiyrah bin Shu'bah) amesema: Mu’aawiyah alimwandikia Al-Mughiyrah: Niandikie ambayo uliyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):  Basi akamwandikia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  alikuwa akisema kila baada ya kumaliza Swalaah:  

 

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Allaahumma laa maani’a limaa A’-twayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye ni Muweza wa kila kitu.  Ee Allaah hapana anayeweza kukizuia Ulichokitoa, na wala kutoa Ulichokizuia, na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

 

Tanbihi: Hii ni mojawapo wa Adhkaar za kila baada ya Swalaah.

 

 

Share [33]

27-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Alllaah: Laa Ilaaha Illa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu … Du’aa Inayotakabaliwa Ambayo Mna Jina Adhimu Kabisa

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com [15]

 

27- Laa Ilaaha Illa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu … Du’aa Inayotakabaliwa Ambayo Mna Jina Adhimu Kabisa

 

 

  عن ‏عَبْدِ اللَّهِ بن بُرَيْدَةَ الأسْلَمِيِّ ‏عن‏ ‏أبِيهِ (رضي الله عنهما) ‏قال: ‏سَمِعَ النَّبِيُّ (‏صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ‏رَجُلاً يَدْعُو وَهُوَ يَقُولُ: "اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ‏ ‏كُفُوًا ‏‏أحَدٌ" فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))   

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah Al-Aslamiyy, kutoka kwa baba yake  (رضي الله عنهما)   kwamba  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   alimsikia mtu akiomba:

 

اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ‏ ‏كُفُوًا ‏‏أحَدٌ

(Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja, Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakuzaa na wala Hakuzaliwa, Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye) Akasema: ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa Ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy  (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb  (1640)]