Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب التسمية في أوله والحمد في آخره
01-Mlango Wa Kutaja Jina La Allaah Mwanzoni na Kumaliza Kwa Kumshukuru
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن عُمَرَ بنِ أبي سَلمة رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( سَمِّ اللهَ ، وَكُلْ بِيَمِينكَ ، وكُلْ مِمَّا يَليكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Abu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ambaye amesema: Aliniambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Mtaje Allaah, na kula kwa mkono wa kuume (kulia) na kula kilicho mbele yako." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أكَلَ أحَدُكُمْ فَلْيَذْكُرِ اسْمَ اللهِ تَعَالَى، فإنْ نَسِيَ أنْ يَذْكُرَ اسْمَ اللهِ تَعَالَى في أوَّلِهِ، فَلْيَقُلْ: بسم اللهِ أوَّلَهُ وَآخِرَهُ )) رواه أَبُو داود والترمذي، وقال: (( حديث حسن صحيح )).
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokula mmoja wenu na alitaje jina la Allaah Ta'aalaa, lakini anaposahau kulitaja jina la Allaah Ta'aalaa mwanzoni, aseme: 'Bismi Llaahi Awwalahu wa Aakhirahu - Kwa jina la Allaah mwanzoni na mwishoni." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 3
وعن جابرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( إِذَا دَخَلَ الرَّجُلُ بَيْتَهُ ، فَذَكَرَ اللهَ تَعَالَى عِنْدَ دُخُولِهِ ، وَعِنْدَ طَعَامِهِ ، قَالَ الشَّيْطَانُ لأَصْحَابِهِ : لاَ مَبِيتَ لَكُمْ وَلاَ عَشَاءَ ، وَإِذَا دَخَلَ فَلَمْ يَذْكُرِ اللهَ تَعَالَى عِنْدَ دُخُولِهِ ، قَالَ الشَّيْطَانُ : أدْرَكْتُمُ المَبِيتَ ؛ وَإِذَا لَمْ يَذْكُرِ اللهَ تَعَالَى عِنْدَ طَعَامِهِ ، قَالَ : أدْرَكْتُم المَبيتَ وَالعَشَاءَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Anapoingia mtu nyumbani kwake, na akamtaja Allaah Ta'aalaa pale anapoingia na anapokula, shetani anamwambia sahibu yake: 'Hakuna malazi (sehemu ya kulala) wala chakula kwako leo.' Na anapoingia, na asimtaje Allaah Ta'aalaa wakati anapoingia (nyumbani kwake), shetani anasema: 'Kwa uchache tumepata malazi.' Na asipomtaja Allaah Ta'aalaa wakati anapokula, shetani anasema: 'Umepata malazi na chakula cha usiku'." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : كُنَّا إِذَا حَضَرْنَا مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم طَعَاماً ، لَمْ نَضَعْ أيدِينَا حَتَّى يَبْدَأَ رَسُولُ الله صلى الله عليه وسلم فَيَضَعَ يَدَهُ ، وَإنَّا حَضَرْنَا مَعَهُ مَرَّةً طَعَاماً ، فَجَاءتْ جَارِيَةٌ كَأنَّهَا تُدْفَعُ ، فَذَهَبَتْ لِتَضَعَ يَدَهَا في الطَّعَامِ ، فَأَخَذَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بِيَدِهَا ، ثُمَّ جَاءَ أَعْرَابِيّ كأنَّمَا يُدْفَعُ ، فَأخَذَ بِيَدهِ ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ الشَّيْطَانَ يَسْتَحِلُّ الطَّعَامَ أنْ لا يُذْكَرَ اسمُ اللهِ تَعَالَى عَلَيْهِ ، وَإنَّهُ جَاءَ بهذِهِ الجارية لِيَسْتَحِلَّ بِهَا ، فأَخَذْتُ بِيَدِهَا ، فَجَاءَ بهذا الأعرَابيّ لِيَسْتَحِلَّ بِهِ ، فَأخذْتُ بِيَدِهِ ، والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ ، إنَّ يَدَهُ في يَدِي مَعَ يَدَيْهِمَا )) ثُمَّ ذَكَرَ اسْمَ اللهِ تَعَالَى وَأكَلَ. رواه مسلم .
Na amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Tulikuwa tunapohudhuria chakula pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hatuanzi kula (kwa kutia mikono yetu) mpaka aanze kutia mkono wake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na kwa hakika tulihudhuria chakula siku moja pamoja naye, akaja haraka haraka kijakazi kama kwamba ana njaa sana na akataka kuingiza mkono wake (ili apate kula) lakini Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaushika mkono wake. Kisha akaja bedui haraka kama kwamba ana njaa mno na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaushika mkono wake. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika shetani anakihalalisha kwake chakula ambacho jina la Allaah halikutajwa juu yake. Na hakika amekuja na huyu kijakazi ili akihalalishe chakula, hivyo nikaushika mkono wake. Akaja na huyu bedui ili akihalalishe kwayo, nami nikamshika mkono wake. Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake! Hakika mkono wake (shetani) upo katika mkono wangu pamoja na mikono yao." Kisha akataja jina la Allaah Ta'aalaa na akala chakula hicho." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أُمَيَّةَ بن مَخْشِيٍّ الصحابيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم جَالِسَاً، وَرَجُلٌ يَأكُلُ، فَلَمْ يُسَمِّ اللهَ حَتَّى لَمْ يَبْقَ مِنْ طَعَامِهِ إِلاَّ لُقْمَةٌ ، فَلَمَّا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ ، قَالَ : بِسْمِ اللهِ أوَّلَهُ وَآخِرَهُ ، فَضَحِكَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم ، ثُمَّ قَالَ : (( مَا زَالَ الشَّيْطَانُ يَأكُلُ مَعَهُ ، فَلَمَّا ذَكَرَ اسمَ اللهِ اسْتَقَاءَ مَا فِي بَطْنِهِ )) رواه أَبُو داود والنسائي .
Imepokewa kutoka kwa Umayyah bin Makhshiyy, ambaye ni Swahaaba (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameketi chini na yupo mtu aliyekuwa akila chakula bila ya kutaja jina la Allaah na akaendelea mpaka likabaki tonge moja tu. Alipolinyanyua tonge hilo mdomoni mwake alisema: "Bismi Llaahi Awwalahu wa Aakhirahu (Kwa jina la Allaah mwanzoni na mwishoni)." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitabasamu, kisha akasema: "Shetani aliendelea kula naye lakini aliporaja jina la Allaah, shetani alitapika chakula chote kilichokuwa tumboni mwake." [Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 6
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَأكُلُ طَعَاماً في سِتَّةٍ مِنْ أصْحَابِهِ ، فَجَاءَ أعْرَابِيٌّ ، فَأكَلَهُ بلُقْمَتَيْنِ . فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أما إنَّهُ لَوْ سَمَّى لَكَفَاكُمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akila chakula pamoja na Swahaaba zake sita, alikuja bedui akawa ni mwenye kula kwa matonge mawili. Hapo akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ama kwa hakika lau angetaja jina la Allaah basi chakula hicho kingewatosha." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن أَبي أُمَامَة رضي الله عنه: أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا رَفَعَ مَائِدَتَهُ، قَالَ: (( الْحَمْدُ للهِ حَمداً كَثِيراً طَيِّباً مُبَاركَاً فِيهِ، غَيْرَ مَكْفِيٍّ ، وَلاَ مُوَدَّعٍ ، وَلاَ مُسْتَغْنَىً عَنْهُ رَبَّنَا )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimaliza kula na kitambara cha chakula kunyanyuliwa, akisema: "Alhamdullillaah Kathiyran Twayyban Mubaarakan Fihi Ghayra Makfiyyi walaa muwadda'in walaa Mustaghnan 'anhu Rabbana "Sifa zote njema, nyingi zilizo nzuri anastahiki Allaah na iliyojaa baraka ndani yake isiyoepikika (kwa kuwa Ndiye Mwenye kulisha na wala Yeye halishwi na yeyote) na wala hamuachi mwenye kumuomba wala hatuwezi kuwa na ukwasi nayo, ee Rabb." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 8
وعن معاذِ بن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أكَلَ طَعَامَاً، فَقال : الحَمْدُ للهِ الَّذِي أطْعَمَنِي هَذَا، وَرَزَقنِيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلاَ قُوَّةٍ ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Mu'aadh bin Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: Yeyote anayekula chakula kisha akasema: "Alhamdullillaahil Ladhiy Atw'amaniy hadhaa wa Razaqaniyhi min ghayri Hawli minniy walaa Quwwah - Sifa zote njema Anastahiki Allaah ambaye kwamba Amenilisha mimi hichi (chakula) na Akaniruzuku mimi bila ya hila au juhudi na nguvu kutoka kwangu. Huyo atakuwa ni mwenye kusamehewa madhambi yake yaliyotangulia." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب لا يَعيبُ الطّعام واستحباب مَدحه
02-Mlango Wa Kutokitia Kasoro Chakula na Kupendeza Kukisifu
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هُريرة رضي الله عنه ، قَالَ : مَا عَابَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم طَعَامَاً قَطُّ ، إن اشْتَهَاهُ أكَلَهُ ، وَإنْ كَرِهَهُ تَرَكَهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakukitia kasoro chakula kabisa, akikipenda atakila, na kama hakipendi atakiacha." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah].
Hadiyth – 2
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم سَأَلَ أهْلَهُ الأُدْمَ ، فقالوا : مَا عِنْدَنَا إِلاَّ خَلٌّ ، فَدَعَا بِهِ ، فَجَعَلَ يَأكُلُ ، ويقول : (( نِعْمَ الأُدْمُ الخَلُّ ، نِعْمَ الأُدْمُ الخَلُّ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwauliza watu wa nyumbani kwake wampe mchuzi. Wakasema: "Sisi hatuna chochote isipokuwa siki. Aliwaambia wamletee (hiyo siki). Akawa anaila na kusema: "Mchuzi ulio bora ni siki; Mchuzi ulio bora ni siki." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله من حضر الطعام وهو صائم إِذَا لَمْ يفطر
03-Mlango Wa Anachosema Anayeletewa Chakula Naye Amefunga
Alhidaaya.com [4]
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا دُعِيَ أحَدُكُمْ فَلْيُجِبْ، فَإنْ كَانَ صَائِماً فَلْيُصَلِّ، وَإنْ كَانَ مُفْطِراً فَلْيَطْعَمْ )) رواه مسلم.
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoalikwa mmoja wenu chakula basi anatakiwa aitikie kwa kukubali mwaliko. Ikiwa amefunga basi aache na ikiwa hakufunga basi ale chakula hicho (kilichoandaliwa)." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله من دُعي إِلَى طعام فتبعه غيره
04-Mlango Wa Anachosema Aliyealikwa Chakula Akafuatwa na Mtu Mwengine
Alhidaaya.com [4]
عن أَبي مسعود البَدْريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : دعا رَجُلٌ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم لِطَعَامٍ صَنعَهُ لَهُ خَامِسَ خَمْسَةٍ ، فَتَبِعَهُمْ رَجُلٌ ، فَلَمَّا بَلَغَ البَابَ ، قَالَ النَّبيّ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ هَذَا تَبِعَنَا ، فَإنْ شِئْتَ أنْ تَأْذَنَ لَهُ ، وَإنْ شِئْتَ رَجَعَ )) قَالَ : بل آذَنُ لَهُ يَا رَسُولَ الله . متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Ibn Mas'uwd Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alialikwa na mtu kwa chakula alichowatayarishia watu watano (pamoja na Nabiy). Akaja pamoja na hao watu watano mtu mwingine. Walipofika mlangoni, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Hakika huyu mtu ametufuata, ukitaka kumruhusu, mruhusu, na ukitaka arudi atarudi." Akasema: "Bali mruhusu, Ee Rasuli wa Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الأكل مِمَّا يليه ووعظه وتأديبه من يسيء أكله
05-Mlango Wa Kula Kilicho Mbele Yake na Kumpa Waadhi na Kumfundisha Adabu Mwenye Kukosea Katika Kula
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن عمر بن أَبي سَلمَة رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنْتُ غُلاماً في حِجْرِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم، وَكَانَتْ يَدِي تَطِيشُ في الصَّحْفَةِ ، فَقَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا غُلامُ ، سَمِّ اللهَ تَعَالَى ، وَكُلْ بِيَمينِكَ ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Abu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Nilikuwa kijana mdogo katika malezi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), mkono wangu ukawa unatembea katika sahani ya chakula. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniambia: "Ee kijana! Mtaje Allaah, na kula kwa mkono wa kuume (kulia) na kula kilicho mbele yako." [Al-Bukhaariy, Musli, Maalik, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن سلمةَ بن الأَكْوَع رضي الله عنه : أنَّ رَجُلاً أَكَلَ عِنْدَ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم بِشِمَالِهِ ، فَقَالَ : (( كُلْ بِيَمِينِكَ )) قَالَ : لا أسْتَطِيعُ . قَالَ : (( لاَ اسْتَطَعْتَ )) ! مَا مَنَعَهُ إِلاَّ الكِبْرُ ! فَمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Salamah bin 'Amru bin Al-Akwa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: "Kuna mtu ambaye alikula mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mkono wa kushoto. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 'Kula kwa mkono wa kulia.' Akasema: 'Siwezi.' Akasema: 'Hutaweza.' Haikumfanya yeye asifuate agizo la Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa ni kibri, hivyo hakuweza tena kuunyanyua mkono mdomoni mwake." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب النّهي عن القِرَانِ بين تمرتين ونحوهما إِذَا أكل جماعة إِلاَّ بإذن رفقته
06-Mlango Wa Unaokataza Kubana Tende Mbili na Mfano Wake Katika Tonge Moja Kama Anakula na Wenzake Isipokuwa Kwa Ruhusa Yao
Alhidaaya.com [4]
عن جَبَلَة بن سُحَيْم ، قَالَ : أصَابَنَا عَامُ سَنَةٍ مَعَ ابن الزُّبَيْرِ ؛ فَرُزِقْنَا تَمْراً، وَكَانَ عبدُ الله بن عمر رضي الله عنهما يَمُرُّ بنا ونحن نَأكُلُ، فَيقُولُ : لاَ تُقَارِنُوا ، فإنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى عنِ القِرَانِ ، ثُمَّ يَقُولُ : إِلاَّ أنْ يَسْتَأذِنَ الرَّجُلُ أخَاهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Jabalah bin Suhaym kwamba: Tulipatikana na ukame mwaka mmoja tukiwa pamoja na Ibn Zubayr, naye akawa anatupa tende na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) alikuwa anatupitia tukiwa tunakula na kusema: "Musibane tende, hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kubana, kula tende mbili kwa mlo mmoja." Kisha akasema: "Isipokuwa mtu miongoni mwenu atakapomuomba ruhusa ndugu yake." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقوله ويفعله من يأكل وَلاَ يشبع
07-Mlango Wa Anachosema na Anachofanya Mwenye Kula Lakini Asishibe
Alhidaaya.com [4]
عن وَحْشِيِّ بن حرب رضي الله عنه : أنَّ أصحابَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، قالوا : يَا رسولَ اللهِ ، إنَّا نَأكُلُ وَلاَ نَشْبَعُ ؟ قَالَ : (( فَلَعَلَّكُمْ تَفْتَرِقُونَ )) قالوا : نَعَمْ . قَالَ: (( فَاجْتَمِعُوا عَلَى طَعَامِكُمْ، وَاذْكُرُوا اسْمَ اللهِ ، يُبَارَكْ لَكُمْ فِيهِ )) رواه أَبُو داود.
Imepokewa kutoka kwa Wahshiy bin Harb (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimuuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Sisi tunakula lakini hatushibi." Akasema: "Huenda nyinyi mnakula mbali mbali (kila mtu kivyake)." Wakasema: "Ndio." Akasema: "Kusanyikeni pamoja kwenye chakula chenu (kuleni pamoja) na mtaje jina la Allaah, nanyimtabarikiwa kwayo." [Abu Daawuwd]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الأمر بالأكل من جانب القصعة والنهي عن الأكل من وسطها
08-Mlango Wa Amri ya Kula Pambizoni Mwa Sahani na Kukatazwa Kula Katikati Yake
Alhidaaya.com [4]
فِيهِ : قَوْله صلى الله عليه وسلم : (( وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ )) متفق عَلَيْهِ كما سبق .
Ndani yake ni kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na kula kilicho mbele yako." [Al-Bukhaariy na Muslim], kama ilivyotanguliwa kutajwa.
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( البَرَكَةُ تَنْزِلُ وَسَطَ الطعَامِ ؛ فَكُلُوا مِنْ حَافَتَيْهِ ، وَلاَ تَأكُلُوا مِنْ وَسَطِهِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Baraka inashuka katikati ya chakula, kwa hivyo kuleni kwa pambizoni mwake na wala msile kutokea katikati yake." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na amesema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن بُسْرٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ للنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَصْعَةٌ يُقَالُ لَهَا : الغَرَّاءُ يَحْمِلُهَا أرْبَعَةُ رجالٍ ؛ فَلَمَّا أضْحَوْا وَسَجَدُوا الضُّحَى أُتِيَ بِتِلْكَ الْقَصْعَةِ ؛ يعني وَقَدْ ثُردَ فِيهَا ، فَالتَفُّوا عَلَيْهَا ، فَلَمَّا كَثُرُوا جَثَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم . فَقَالَ أعرابيٌّ : مَا هذِهِ الجِلْسَةُ ؟ فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ جَعَلَنِي عَبْداً كَريماً ، وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّاراً عَنِيداً )) ، ثُمَّ قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( كُلُوا مِنْ حَوَالَيْهَا ، وَدَعُوا ذِرْوَتَها يُبَارَكْ فِيهَا )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيد .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Busr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na gudulia kubwa liliokuwa likiitwa Al-Gharraa'u na lilikuwa likibebwa na watu wanne. Baada ya Swahaaba kuswali Swalaah ya Dhuhaa, gudulia hili lilikuwa likiletwa likiwa limejaa Thariid (aina fulani ya mchuzi) na watakaa pambazoni mwake. Pindi wanapokuwa watu ni wengi, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikaa chini kwa magoti, mapaja yake na vidole vyake vya miguu vikigusa chini katika ardhi. Bedui akauliza: "Ni mkao gani huu mliokaa?" Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah amenijaalia mimi kuwa mja mtukufu (mwenye tabia nzuri) wala hakunijaalia kuwa mwenye kibri na kuchukua haki za watu pasi na haki yoyote." Kisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Kuleni pambazoni mwa gudulia na acheni sehemu iliyonyanyuka ya katikati na mtabarikiwa kwayo." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Jayd (nzuri)].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهية الأكل متكئاً
09-Mlango Wa Kuchukiza Kula Kwa Kutegemea
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي جُحَيْفَةَ وَهْبِ بن عبد الله رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ آكُلُ مُتَّكِئاً )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Juhayfah Wahb bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mimi sili (chakula) nikiwa nimeegemea." [Al-Bukhaariy]
قَالَ الخَطَّابِيُّ : المُتَّكئُ هاهُنَا : هُوَ الجالِسُ مُعْتَمِداً عَلَى وِطَاءٍ تحته ، قَالَ : وأرادَ أنَّهُ لا يَقْعُدُ عَلَى الوِطَاءِ وَالوَسَائِدِ كَفِعْل مَنْ يُريدُ الإكْثَارَ مِنَ الطَّعَام ، بل يَقْعُدُ مُسْتَوفِزاً لاَ مُسْتَوطِئاً ، وَيَأكُلُ بُلْغَةً . هَذَا كلامُ الخَطَّابيِّ ، وأشارَ غَيْرُهُ إِلَى أنَّ الْمُتَّكِئَ هُوَ المائِلُ عَلَى جَنْبِه ، والله أعلم .
Amesema Al-Khatwaabiy: "Mwenye kutegemea hapa ni yule anayekaa kwa kuegemea mto ulio chini yake. Amesema: "Na kusudio ni kuwa yeye (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa ni mwenye kukaa juu ya mto kama kitendo cha mwenye kutaka kula zaidi (chakula kingi). Bali alikuwa akikaa wima sio mwenye kuegemea." Na ameashiria mwengine asiyekuwa yeye ya kwamba mwenye kuegemea ni yule anayejilaza kwa ubavu wake.
Hadiyth – 2
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : رَأَيْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم جَالِساً مُقْعِياً يَأكُلُ تَمْراً . رواه مسلم .
Na amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameketi chini amenyanyua magoti yake akila tenda." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب الأكل بثلاث أصابع واستحباب لعق الأصابع ، وكراهة مسحها قبل لعقهاواستحباب لعق القصعة وأخذ اللقمة الَّتي تسقط منه وأكلها ومسحها بعد اللعق بالساعد والقدم وغيرها
10-Mlango Wa Kupendeza Kula Kwa Vidole Vitatu na Sunnah ya Kuramba Vidole na Karaha ya Kuvifuta Kabla ya Kuviramba na Kupendeza Kuramba Sahani na Kuchukua Tonge Lililo Anguka na Kulila
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أكَلَ أَحَدُكُمْ طَعَاماً ، فَلاَ يَمْسَحْ أَصَابِعَهُ حَتَّى يَلْعَقَهَا أَوْ يُلْعِقَها )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokula mmoja wenu asiufute mkono wake mpaka aurambe au aurambishe." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abuu Daawuwd]
Hadiyth – 2
وعن كعب بن مالك رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يَأكُلُ بثَلاَثِ أصابعَ ، فإذا فَرَغَ لَعِقَهَا . رواه مسلم .
Amesema Ka'b bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akila chakula kutumia vidole vitatu na anapomaliza alikuwa akiviramba. [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أمر بلعق الأصابع والصحفة ، وقال : (( إنَّكُمْ لاَ تَدْرُونَ في أيِّ طَعَامِكُمُ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha kurambwa vidole na sahani na akasema: "Hakika nyinyi hamjui ni katika sehemu gani ya chakula chenu imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أحَدِكُمْ ، فَلْيأخُذْهَا فَلْيُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً ، وَلْيَأْكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْهَا لِلشَّيْطَان ، وَلاَ يَمْسَحْ يَدَهُ بالمِنْدِيل حَتَّى يَلْعَقَ أصَابِعَهُ ، فَإنَّهُ لاَ يَدْري في أيِّ طَعَامِهِ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ikianguka tonge la mmoja wenu na aliokote na aondoshe uchafu na alile wala asimwachie shetani. Pia asifute mkono wake kwa kitambara mpaka avirambe vidole vyake, kwani yeye hajui ni sehemu gani ya chakula chake imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ الشَّيْطَانَ يَحْضُرُ أحَدَكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيْءٍ مِنْ شَأنِهِ ، حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ ، فإذَا سَقَطَتْ لُقْمَةُ أحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً ، ثُمَّ لِيَأْكُلْهَا وَلاَ يَدَعْهَا للشَّيْطَانِ ، فإذا فَرَغَ فَلْيَلْعَقْ أصابِعَهُ ، فإنَّهُ لا يَدْري في أيِّ طعامِهِ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Imepokes kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika shetani anahudhuria pamoja na mmoja wenu katika mambo yake yote mpaka anakuwa pamoja naye anapokula. Hivyo, linapoanguka tonge la mmoja wenu na aliokote na aliondoshe uchafu, kisha alile wala asimuachie shetani. Anapomaliza kula na avirambe vidole vyake, kwani hakika yake hajui ni sehemu gani chakula imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 6
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم إِذَا أكَلَ طَعَاماً ، لَعِقَ أصَابِعَهُ الثَّلاَثَ ، وقال : (( إِذَا سقَطَتْ لُقْمَةُ أحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا ، ولْيُمِطْ عنها الأذى ، وَليَأكُلْهَا ، وَلاَ يَدَعْها لِلْشَّيْطَان )) وأمَرَنا أن نَسْلُتَ القَصْعَةَ ، وقال : (( إنَّكُمْ لا تَدْرُونَ في أيِّ طَعَامِكُمُ البَرَكَةُ )) رواه مسلم .
Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alipokuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akila chakula, akiviramba vidolevyake vitatu, na akasema: "Ikianguka tonge ya mmoja wenu na aliokote na aondoshe uchafu na aile wala asimuachie shetani kabisa, na akasema: "Hakika nyinyi hamjui ni katika sehemu gani ya chakula chenu imo baraka." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن سعيد بنِ الحارث : أنّه سأل جابراً رضي الله عنه عنِ الوُضُوءِ مِمَّا مَسَّتِ النَّارُ ، فَقَالَ : لا ، قَدْ كُنَّا زَمَنَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم لا نَجِدُ مِثْلَ ذَلِكَ الطَّعامِ إِلاَّ قليلاً ، فإذا نَحْنُ وجَدْنَاهُ ، لَمْ يَكُنْ لنا مَنَادِيلُ إِلاَّ أكُفَّنا ، وسَواعِدَنَا ، وأقْدامَنَا ، ثُمَّ نُصَلِّي وَلاَ نَتَوَضَّأُ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Haarith kwamba alimuuliza Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) : "Je, ni wajibu wa kuchukua wudhu baada ya kula chakula kilichopikwa kwa moto?" Alisema: "Hapana! Hakika sisi tulikuwa katika zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nadhra kupata mfano wa chakula hicho; na tulipokuwa tukipata chakula aina hiyo basi hatukuwa na kitambara cha kufuta vitanga vyetu, mkono yetu na miguu yetu, kisha tulikuwa tunaswali bila ya kutawadha." [Al-Bukhaariy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تكثير الأيدي عَلَى الطعام
11-Mlango Wa Kuongezeka Mikono Katika Chakula
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( طَعَامُ الاثنينِ كافِي الثلاثةِ ، وطَعَامُ الثَّلاَثَةِ كافي الأربعة )) متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Chakula cha wawili kinawatosha watatu, na cha watatu kinawatosha wanne." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( طَعَامُ الوَاحِدِ يَكْفِي الاثْنَيْنِ ، وَطَعَامُ الاثْنَيْنِ يَكْفِي الأَرْبَعَةَ ، وَطَعَامُ الأرْبَعَةِ يَكْفِي الثَّمَانِيَةَ )) رواه مسلم .
Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Chakula cha mmoja kinawatosha wawili, na cha wa wawili kinawatosha wanne, na cha wanne kinawatosha wanane." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب أدب الشرب واستحباب التنفس ثلاثاً خارج الإناء وكراهة التَّنَفُّس في الإناء واستحباب إدارة الإناء عَلَى الأيمن فالأيمن بعد المبتدئ
12-Mlango Wa Adabu za Kunywa na Kupendeza Kupumua Mara Tatu Nje ya Chombo na Karaha Kupumua Ndani ya Chombo
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم كَانَ يَتَنَفَّسُ في الشَّرابِ ثَلاثاً . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipumua mara tatu nje ya chombo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَشْرَبُوا وَاحِداً كَشُرْبِ البَعِيرِ ، وَلَكِنِ اشْرَبُوا مَثْنَى وَثُلاَثَ ، وَسَمُّوا إِذَا أنْتُمْ شَرِبْتُمْ ، وَاحْمَدُوا إِذَا أنْتُمْ رَفَعْتُمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Msinywe kwa mara moja (mkupuo mmoja) kama anavyokunywa ngamia lakini kunyweni mara mbili na tatu. Na litajeni jina la Allaah mnapokunywa na mshukuruni kwa kumsifu pindi mnapomaliza." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 3
وعن أَبي قَتَادَة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى أنْ يُتَنَفَّسَ في الإناءِ . متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupumua ndani ya chombo (hicho anachokunywia maji)." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]
Hadiyth – 4
وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِيَ بِلَبَنٍ قَدْ شِيبَ بماءٍ ، وَعَنْ يَمِينهِ أعْرَابيٌّ ، وَعَنْ يَسَارِهِ أَبُو بَكْر رضي الله عنه ، فَشَرِبَ ، ثُمَّ أعْطَى الأعْرابيَّ ، وقال : (( الأيْمَنَ فالأيْمَنَ )) متفق عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa maziwa yaliyochanganywa na maji, na kulikuwa na badui kuliani mwake na Abu Bakr (Radhwiya Allahu 'anhu) alikuwa kushotoni mwake. Alikunywa kisha akampa yule Mbedui, na akasema: "Kuliani, kuliani." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 5
وعن سهلِ بن سعدٍ رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم أُتِيَ بِشرابٍ ، فَشَرِبَ مِنْهُ وَعَنْ يَمِينِهِ غُلامٌ ، وَعَنْ يَسَارِهِ أشْيَاخٌ ، فَقَالَ للغُلامِ : (( أتَأْذَنُ لِي أنْ أُعْطِيَ هؤُلاَءِ ؟ )) فَقَالَ الغُلامُ : لا واللهِ ، لا أُوثِرُ بنَصيبـي مِنْكَ أَحَداً . فَتَلَّهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم في يَدِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa kinywaji, akanywa kutoka kwayo, na kuliani kwake alikuwepo kijana na kushotoni kwake kulikuwa na mzee. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akamuuliza yule kijana: "Utaniruhusu niwape hawaa (yaani wazee)?" Yule kijana akajibu: "Naapa kwa Allaah! simpendelei yeyote achukuwe hisa yangu kutoka kwako." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akampa huyo kijana kile kinywaji kwenye mkono wake. [Al-Bukhaariy na Muslim] . Na huyu kijana alikuwa ni 'Abdallaah bin 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu)
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة الشرب من فم القربة ونحوها وبيان أنه كراهة تنـزيه لا تحريم
13-Mlango Wa Karaha ya Kunywa Kutoka Kwa Mdomo wa Kiriba na Mfano Wake na Kubainisha Kuwa Hii ni Karaha Si Ile Ambayo ni Haramu
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي سعيدٍ الْخُدْريِّ رضي الله عنه ، قَالَ : نَهَى رسول الله صلى الله عليه وسلم عن اخْتِنَاثِ الأَسْقِيَةِ . يعني : أن تُكْسَرَ أفْواهُها ، وَيُشْرَبَ مِنْهَا . متفق عَلَيْهِ .
Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'anhu) amekataza kuvikunja viriba vya maji, anakusudia kuikunja midomo hiyo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : نَهَى رسول الله صلى الله عليه وسلم أن يُشْرَبَ مِنْ فِيِّ السِّقَاءِ أَوْ القِرْبَةِ . متفق عَلَيْهِ .
Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kunywa kutoka kwa mdomo wa kiriba." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أم ثابتٍ كَبْشَةَ بنتِ ثابتٍ أُختِ حَسَّانَ بن ثابتٍ رضي الله عنهما ، قالت : دخل عَلَيَّ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم فَشَرِبَ مِنْ فيِّ قِرْبَةٍ مُعَلَّقَةٍ قَائِماً ، فَقُمْتُ إِلَى فِيهَا فَقَطَعْتُهُ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Ummu Thaabit Kabshah bint Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) dadake Hassaan bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliingia kwangu Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akanywa kutoka kwa mdomo wa kiriba kilichotundikwa akiwa amesimama. Nilisimama na kuukata mdomo wa kiriba hicho na kuuhifadhi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كراهة النفخ في الشراب
14-Mlango Wa Karaha ya Kupulizia Ndani ya Kinywaji
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَى عَن النَّفْخ في الشَّرَاب ، فَقَالَ رَجُلٌ : القَذَاةُ أراها في الإناءِ ؟ فَقَالَ : (( أهرقها )) . قَالَ : إنِّي لا أرْوَى مِنْ نَفَسٍ وَاحدٍ ؟ قَالَ : (( فَأَبِنِ القَدَحَ إِذَاً عَنْ فِيكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupulizia ndani ya kinywaji. Akasema mtu mmoja: "Je, nitafanyaje kuhusu vitu vinavyoelea katika kinywaji?" Akasema: "Vitoe." Akasema: "Kiu yangu haimaliziki kwa mkupuo mmoja." Akasema: "Unaweza kupumua, lakini kiweke chombo nje ya mdomo wako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نهى أن يُتَنَفَّسَ في الإناءِ أَوْ يُنْفَخَ فِيهِ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kupumulia ndani ya chombo na kupulizia ndani yake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب بيان جواز الشرب قائماً وبيان أنَّ الأكمل والأفضل الشرب قاعداً
15-Mlango Wa Kubainisha Kujuzu Kunywa Kwa Kusimama na Kubainisha Kuwa ni Bora Zaidi Kunywa Kwa Kukaa
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : سَقَيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم مِنْ زَمْزَمَ ، فَشَربَ وَهُوَ قَائِمٌ . متفق عَلَيْهِ .
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimpa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) maji ya Zamzam akanywa huku amesimama." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]
Hadiyth – 2
وعن النَّزَّالِ بن سَبْرَةَ رضي الله عنه ، قَالَ : أَتَى عَلِيٌّ رضي الله عنه بَابَ الرَّحْبَةِ ، فَشَربَ قائِماً ، وقال : إنِّي رَأَيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم فَعَلَ كما رَأَيْتُمُوني فَعَلْتُ . رواه البخاري .
An-Nazzaal bin Sabrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alikuja 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwenye mlango wa Rahbah (sehemu pana iliyopo kufah) na akanywa akiwa amesimama, na akasema: "Hakika mimi nimemuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya kama mnavyoniona nikifanya." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كُنَّا عَلَى عهدِ رسول الله صلى الله عليه وسلم نَأكُلُ وَنَحْنُ نمشِي ، وَنَشْرَبُ ونَحْنُ قِيامٌ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Tulikuwa tukila katika zama za Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nasi tunatembea na tukinywa nasi tumesimama." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 4
وعن عمرو بن شعيب ، عن أبيه ، عن جَدِّهِ رضي الله عنه ، قَالَ : رأيتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَشْرَبُ قَائِماً وقَاعِداً . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Shu'ayb kutoka kwa babake kutoka kwa babu yake (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: "Nilimuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akinywa kwa kusimama na kwa kukaa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 5
وعن أنس رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم : أنه نَهى أن يَشْرَبَ الرَّجُلُ قَائِماً . قَالَ قتادة : فَقُلْنَا لأَنَسٍ : فالأَكْلُ ؟ قَالَ : ذَلِكَ أَشَرُّ – أَوْ أخْبَثُ – رواه مسلم . وفي رواية لَهُ : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم زَجَرَ عَن الشُّرْب قائِماً .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikataza kunywa kwa kusimama. Amesema Qataadah: Tukamuuliza Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Je, kula?" Akasema: "Hiyo ni baya zaidi au ni chafu zaidi." [Muslim]
Na katika riwaayah yake nyengine: "Hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekemea kunywa kwa kusimama."
Hadiyth – 6
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ يَشْرَبَنَّ أحَدٌ مِنْكُمْ قَائِماً ، فَمَنْ نَسِيَ فَلْيَسْتَقِيء )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asinywe mmoja wenu kwa kusimama, na anayesahau basi ajitapishe." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب كون ساقي القوم آخرهم شرباً
16-Mlango Wa Kupendeza Kuwa Mwandazi Awe wa Mwisho Kunywa
Alhidaaya.com [4]
عن أَبي قتادة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( ساقي القوم آخِرُهُمْ شُرْباً )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Qataadah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mnyweshaji wa watu ndiye wa mwisho wao kunywa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب جواز الشرب من جميع الأواني الطاهرة غير الذهب والفضة
وجواز الكرع – وَهُوَ الشرب بالفم من النهر وغيره بغير إناء ولا يد –وتحريم استعمال إناء الذهب والفضة في الشرب والأكل والطهارة وسائر وجوه الاستعمال
17-Mlango Wa Kujuzu Kunywa Kutoka Katika Vyombo Vyote Vilivyo Tohara Isipokuwa Vya Dhahabu na Fedha, Kujuzu Al-Kar'i (Nayo ni kunywa Kwa Kutumia Mdomo Moja Kwa Moja Mtoni Bila ya Chombo Chochote au Mkono
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : حَضَرَتِ الصَّلاَةُ فقامَ مَن كَانَ قَريبَ الدَّارِ إِلَى أهْلِهِ ، وبَقِيَ قَوْمٌ ، فأُتِيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِمَخْضَبٍ مِنْ حِجَارَةٍ ، فَصَغُرَ المخْضَبُ أنْ يَبْسُطَ فِيهِ كَفَّهُ ، فَتَوَضَّأَ القَوْمُ كُلُّهُمْ . قالوا : كَمْ كُنْتُمْ ؟ قَالَ : ثَمَانِينَ وزيادة . متفق عَلَيْهِ ، هذه رواية البخاري .
وفي رواية لَهُ ولمسلم : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم دَعَا بإناءٍ مِنْ ماءٍ ، فَأُتِيَ بقَدَحٍ رَحْرَاحٍ فِيهِ شَيْءٌ مِنْ ماءٍ ، فَوَضَعَ أصابعَهُ فِيهِ . قَالَ أنسٌ : فَجَعلْتُ أنْظُرُ إِلَى الماءِ يَنْبُعُ مِنْ بَيْن أصَابِعِهِ ، فَحَزَرْتُ مَنْ تَوضَّأ مَا بَيْنَ السَّبْعِينَ إِلَى الثَّمَانينَ .
Amesema Anas (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba wakati wa Swalaah ulifika, hivyo wale ambao nyumba zao zilikuwa karibu walikwenda kushika wudhu na wengine wakabakia na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Aliletewa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) chombo kilichotengenezwa kwa mawe kilichokuwa na maji ndani yake. Kilikuwa ni chombo kidogo sana kinachoweza kufunikwa na kitanga cha mkono. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alishika wudhu na watu wote waliokuwa pamoja nae pia walishika wudhu. Tukasema: "Mlikuwa wangapi?" Akasema: "Themanini au na ziada kidogo." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni riwaayah ya Al-Bukhaariy]
Na katika riwaayah ya Muslim: Hakika Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliitisha chombo cha maji. Akaletewa chombo kikubwa lakini chembamba kilichokuwa na maji kidogo. Alitia vidole vyake ndani yake. Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Niliona maji yakitoka baina ya vidole vyake. Makisio ya idadi ya watu walioshika wudhu kwa kutumia maji hayo ni baina ya sabini na themanini."
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن زيد رضي الله عنه ، قَالَ : أتَانَا النبيُّ صلى الله عليه وسلم فَأَخْرَجْنَا لَهُ مَاءً في تَوْرٍ مِنْ صُفْر فَتَوَضَّأَ . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Zayd (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Alikuja kwetu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nasi tukamletea maji katika chombo cha shaba, naye akashika wudhu (kutumia maji hayo). [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن جابر رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم دَخَلَ عَلَى رَجُلٍ مِن الأَنْصَارِ ، وَمَعَهُ صَاحِبٌ لَهُ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنْ كَانَ عِنْدَكَ مَاءٌ باتَ هذِهِ اللَّيْلَةَ في شَنَّةٍ وَإلاَّ كَرَعْنَا )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia kwa Answaar akiwa pamoja na sahibu yake. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Ikiwa una maji kidogo yaliyobakia kutoka jana usiku katika kigudulia chako (cha ngozi) tupatie tunywe na ikiwa huna basi tutakunywa moja kwa moja kwa midomo yetu kutoka kwa kijito." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن حذيفة رضي الله عنه ، قَالَ : إنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم نَهَانَا عَن الحَرِير ، وَالدِّيباجِ ، والشُّربِ في آنِيَة الذَّهَب والفِضَّةِ ، وقال : (( هي لَهُمْ في الدُّنْيَا ، وهِيَ لَكُمْ في الآخِرَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kuvaa hariri na dibaji na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha na akasema: "Vitu hivyo ni vyao hapa duniani na ni vyenu Aakhirah." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أُمِّ سلمة رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( الَّذِي يَشْرَبُ في آنِيَةِ الفِضَّةِ ، إنَّمَا يُجَرْجِرُ في بَطْنِهِ نَارَ جَهَنَّمَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية لمسلم : (( إنَّ الَّذِي يَأكُلُ أَوْ يَشْرَبُ في آنِيَةِ الفِضَّةِ وَالذَّهَبِ )) .
وفي رواية لَهُ : (( مَنْ شَرِبَ في إناءٍ مِنْ ذَهَبٍ أَوْ فِضَّةٍ ، فَإنَّمَا يُجَرْجِرُ في بَطْنِهِ نَارَاً مِنْ جَهَنَّم )) .
Imepokewa kutoka kwa Ummu Salamah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anayekunywa katika chombo cha fedha anaangushia moto tumboni mwake." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad].
Na katika riwaayah ya Muslim: "Hakika anayekula au kunywa katika chombo cha fedha na dhahabu."
Na katika riwaayah yake: "Mwenye kunywa katika chombo cha dhahabu au fedha, hakika anaangushia tumboni mwake moto kutoka Jahanam."
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/280
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10316&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Kitabu%20Cha%20Nidhamu%20Ya%20Chakula%20-%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A3%D9%8E%D8%AF%D9%8E%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%B7%D9%91%D9%8E%D8%B9%D8%A7%D9%85
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10956&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutaja%20Jina%20La%20Allaah%20Mwanzoni%20na%20Kumaliza%20Kwa%20Kumshukuru
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10961&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutokitia%20Kasoro%20Chakula%20na%20Kupendeza%20Kukisifu
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10962&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Anachosema%20Anayeletewa%20Chakula%20Naye%20Amefunga
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10963&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Anachosema%20Aliyealikwa%20Chakula%20Akafuatwa%20na%20Mtu%20Mwengine
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10964&title=05-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kula%20Kilicho%20Mbele%20Yake%20na%20Kumpa%20Waadhi%20na%20Kumfundisha%20Adabu%20Mwenye%20Kukosea%20Katika%20Kula
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10965&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Unaokataza%20Kubana%20Tende%20Mbili%20na%20Mfano%20Wake%20Katika%20Tonge%20Moja%20Kama%20Anakula%20na%20Wenzake%20Isipokuwa%20Kwa%20Ruhusa%20Yao
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10966&title=07-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Anachosema%20na%20Anachofanya%20Mwenye%20Kula%20Lakini%20Asishibe
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10967&title=08-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Amri%20ya%20Kula%20Pambizoni%20Mwa%20Sahani%20na%20Kukatazwa%20Kula%20Katikati%20Yake
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10968&title=09-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuchukiza%20Kula%20Kwa%20Kutegemea
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10973&title=10-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kula%20Kwa%20Vidole%20Vitatu%20na%20Sunnah%20ya%20Kuramba%20Vidole%20na%20Karaha%20ya%20Kuvifuta%20Kabla%20ya%20Kuviramba%20na%20Kupendeza%20Kuramba%20Sahani%20na%20Kuchukua%20Tonge%20Lililo%20Anguka%20na%20Kulila
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10974&title=11-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuongezeka%20Mikono%20Katika%20Chakula
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10975&title=12-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Adabu%20za%20Kunywa%20na%20Kupendeza%20Kupumua%20Mara%20Tatu%20Nje%20ya%20Chombo%20na%20Karaha%20Kupumua%20Ndani%20ya%20Chombo
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10988&title=13-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Karaha%20ya%20Kunywa%20Kutoka%20Kwa%20Mdomo%20wa%20Kiriba%20na%20Mfano%20Wake%20na%20Kubainisha%20Kuwa%20Hii%20ni%20Karaha%20Si%20Ile%20Ambayo%20ni%20Haramu
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10989&title=14-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Karaha%20ya%20Kupulizia%20Ndani%20ya%20Kinywaji
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10990&title=15-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kubainisha%20Kujuzu%20Kunywa%20Kwa%20Kusimama%20na%20Kubainisha%20Kuwa%20ni%20Bora%20Zaidi%20Kunywa%20Kwa%20Kukaa
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10991&title=16-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kuwa%20Mwandazi%20Awe%20wa%20Mwisho%20Kunywa
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10992&title=17-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kujuzu%20Kunywa%20Kutoka%20Katika%20Vyombo%20Vyote%20Vilivyo%20Tohara%20Isipokuwa%20Vya%20Dhahabu%20na%20Fedha%2C%20Kujuzu%20Al-Kar%27i%20%28Nayo%20ni%20kunywa%20Kwa%20Kutumia%20Mdomo%20Moja%20Kwa%20Moja%20Mtoni%20Bila%20ya%20Chombo%20Chochote%20au%20Mkono