Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل السلام والأمر بإفشائه
01-Mlango Wa Kutoleana Salamu na Maamrisho ya Kutoa Salamu
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿٢٧﴾
Enyi walioamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salamu wenyewe. Hivyo ni bora kwenu ili mpate kukumbuka. [An-Nuwr: 27]
فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً ۚ ﴿٦١﴾
Mtakapoingia majumbani toleaneni salaam; maamkizi kutoka kwa Allaah, yenye Baraka, mazuri. [An-Nuwr: 61]
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا ۗ ﴿٨٦﴾
Na mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo. [An-Nisaa: 86]
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ﴿٢٤﴾ إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ﴿٢٥﴾
Je, imekufikia hadithi ya wageni wahishimiwao wa Ibraahiym? Walipoingia kwake wakasema: Salaam! Akasema: Salaam watu wasiotambulikana. [Adh-Dhaariyaat: 24-25]
Hadiyth – 1
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ رجلاً سأل رسول الله صلى الله عليه وسلم : أيُّ الإسْلاَمِ خَيْرٌ ؟ قَالَ : (( تُطْعِمُ الطَّعَامَ ، وَتَقْرَأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba kuna mtu mmoja aliyemuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ni Uislamu gani ulio bora?" Akasema: "Kulisha watu chakula na kuwatolea salamu unaowajua na usiowajua." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَمَّا خَلَقَ اللهُ آدَمَ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : اذْهَبْ فَسَلِّمْ عَلَى أُولئِكَ – نَفَرٍ مِنَ المَلاَئِكَةِ جُلُوس – فَاسْتَمِعْ مَا يُحَيُّونَكَ ؛ فَإنَّهَا تَحِيَّتُكَ وَتَحِيَّةُ ذُرِّيتِكَ . فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، فقالوا : السَّلاَمُ عَلَيْكَ وَرَحْمَةُ اللهِ ، فَزَادُوهُ : وَرَحْمَةُ اللهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Allaah Ta'aalaa alipomuumba Aadam alimwambia: 'Nenda ukawatolee salamu wale Malaaikah waliokaa na kisha usikilize majibu yao, kwani jibu watakalo toa ndio litakalokuwa jibu lako na la wazawa wako (kizazi chako).' Adam akasema: 'Assalaamu 'Alaykum - Amani iwe juu yenu.' Wakasema: 'Assalaamu 'Alayka Wa Rahmatullaah -Amani iwe juu yako na rehma ya Allaah.' Wakaongeza: 'Wa Rahmatullaah.' [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أَبي عُمَارة البراءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : أمرنا رسول الله صلى الله عليه وسلم بِسَبْعٍ : بِعِيَادَةِ المَرِيضِ ، وَاتِّبَاعِ الجَنَائِزِ ، وَتَشْمِيتِ العَاطِسِ ، وَنَصْرِ الضَّعيفِ ، وَعَوْنِ المَظْلُومِ ، وَإفْشَاءِ السَّلاَمِ ، وَإبْرَارِ المُقسِمِ . متفقٌ عَلَيْهِ ، هَذَا لفظ إحدى روايات البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu 'Ummarah Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamuru kufanya mambo saba: "kumtembelea mgonjwa, kulisindikiza jeneza, kumuombea dua anapopiga chafya, kumnusuru dhaifu, kumsaidia aliyedhulumiwa, kueneza salamu na kutekeleza kiapo." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya riwaayah moja ya Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لاَ تَدْخُلُوا الجَنَّةَ حَتَّى تُؤمِنُوا ، وَلاَ تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا ، أوَلاَ أدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ ؟ أفْشُوا السَّلاَمَ بَيْنَكُمْ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hamutaingia Peponi mpaka Muamini, na wala hamtaamini mpaka mpendane. Je, niwaonyesheni kitu ambacho lau mutakifanya mutapendana? Enezeni salamu baina yenu." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي يوسف عبد الله بن سلام رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم، يقول : (( يَا أيُّهَا النَّاسُ ، أفْشُوا السَّلاَمَ ، وَأطْعِمُوا الطَّعَامَ ، وَصِلُوا الأرْحَامَ ، وَصَلُّوا والنَّاسُ نِيَامٌ ، تَدْخُلُوا الجَنَّةَ بِسَلاَم )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Yusuf 'Abdillaah bin Salaam (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Enyi watu! Toleaneni salamu na mulishe watu chakula na unganisheni kizazi na swalini wakati watu wamelala, mutaingia Peponi kwa salama na amani." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن الطُّفَيْل بن أُبَيِّ بن كعبٍ : أنَّه كَانَ يأتي عبد الله بن عمر ، فيغدو مَعَهُ إِلَى السُّوقِ ، قَالَ : فإذَا غَدَوْنَا إِلَى السُّوقِ ، لَمْ يَمُرَّ عَبدُ الله عَلَى سَقَّاطٍ وَلاَ صَاحِبِ بَيْعَةٍ ، وَلاَ مِسْكِينٍ ، وَلاَ أحَدٍ إِلاَّ سَلَّمَ عَلَيْهِ ، قَالَ الطُّفَيْلُ : فَجِئْتُ عبد الله بنَ عُمَرَ يَوْماً، فَاسْتَتْبَعَنِي إِلَى السُّوقِ ، فَقُلْتُ لَهُ : مَا تَصْنَعُ بالسُّوقِ ، وَأنْتَ لا تَقِفُ عَلَى البَيْعِ ، وَلاَ تَسْأَلُ عَنِ السِّلَعِ ، وَلاَ تَسُومُ بِهَا ، وَلاَ تَجْلِسُ في مَجَالِسِ السُّوقِ ؟ وَأقُولُ : اجْلِسْ بِنَا هاهُنَا نَتَحَدَّث ، فَقَالَ : يَا أَبَا بَطْنٍ – وَكَانَ الطفَيْلُ ذَا بَطْنٍ – إنَّمَا نَغْدُو مِنْ أجْلِ السَّلاَمِ ، فنُسَلِّمُ عَلَى مَنْ لَقيْنَاهُ . رواه مالك في المُوطَّأ بإسنادٍ صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Twufayl bin Ubayy bin Ka'b anaeleza kwamba alikuwa akimzuru 'Abdillaah bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) asubuhi, ambaye alikuwa akimchukua sokoni. Twufayl anasema: :Tulipokuwa tukielekea sokoni, 'Abdillaah alikuwa hapiti kwa wachuuzi wadogo (wenye kuuza vitu duni), wala wafanya biashara wala masikini wala mtu mwingine yeyote isipokuwa alikuwa akiwasalimia." Akasema Twufayl: "Nilikuwa kwake siku moja kama kawaida yangu na akanitaka nimfuate sokoni. Nikamwambia: 'Utafanaya nini sokoni, kwani wewe huulizi bei ya vitu wala huuzi wala hukai katika vikazi vya sokoni? Tukae hapa ili tuzungumze'." Akasema: "Ee Abu Batwn (na alikuwa Twufayl mwenye tumbo kubwa)! Hakika sisi tunakwenda sokoni asubuhi kwa ajili ya kuwasalimia (tunaokutana nao)." [Maalik katika Al-Muwatwaa' yake kwa Isnaad Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب كيفية السلام
02-Mlango Wa Jinsi ya Kutoa Salamu
Alhidaaya.com [4]
يُسْتَحَبُّ أنْ يَقُولَ المُبْتَدِئُ بالسَّلاَمِ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ . فَيَأتِ بِضَميرِ الجَمْعِ ، وَإنْ كَانَ المُسَلَّمُ عَلَيْهِ وَاحِداً ، وَيقُولُ المُجيبُ : وَعَلَيْكُمْ السَّلاَمُ وَرَحْمَةُ الله وَبَرَكَاتُهُ ، فَيَأتِي بِوَاوِ العَطْفِ في قَوْله : وَعَلَيْكُمْ .
Inapendeza aseme mwenye kuanza na salamu: "Assalaamu 'Alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh." kwa dhamiri ya wingi japokuwa mwenye kusalimiwa ni mmoja: Na mwenye kujibu atasema: "Wa 'Alaykumus Salaam wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh."
Hadiyth – 1
عن عِمْرَان بن الحصين رضي الله عنهما ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ ثُمَّ جَلَسَ ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( عَشْرٌ )) ثُمَّ جَاءَ آخَرُ ، فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ ، فَقَالَ : (( عِشْرُونَ )) ثُمَّ جَاءَ آخَرُ ، فَقَالَ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ الله وَبَركَاتُهُ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ ، فَقَالَ : (( ثَلاثُونَ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Amesema 'Imraan bin Al-Huswayn (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na akasalimia kwa kusema: "Assalaamu 'Alaykum." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na yule mtu akakaa chini. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Kumi." Kisha alikuja mtu mwingine akasema: "Assalaamu 'Alaykum wa Rahmatullaah." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na yule mtu akakaa, naye akasema: Ishirini." Kisha akaja mwingine, akasema: "Assalaamu 'Alaykum wa Rahmatullaah wa Barakaatuh." Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na yule mtu akakaa, naye akasema: Thelathini." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 2
وعن عائشةَ رضي الله عنها ، قالت : قَالَ لي رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( هَذَا جِبريلُ يَقْرَأُ عَلَيْكِ السَّلاَمَ )) قالت : قُلْتُ : وَعَلَيْهِ السَّلاَمُ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Huyu Jibriyl anakusalimia." Akasema ('Aaishah): Nikasema: "Na juu yake Amani na Rehma za Allaah na Baraka Zake." [Al-Bukhaari na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أنسٍ رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا تكلم بِكَلِمَةٍ أعَادَهَا ثَلاثَاً حَتَّى تُفهَمَ عَنْهُ ، وَإِذَا أتَى عَلَى قَوْمٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ سلم عَلَيْهِمْ ثَلاَثاً . رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) alisema kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akizungumza alikuwa akirudia maneno mara tatu mpaka afahamike. Na alipokuwa akija kwa watu na kuwasalimia alikuwa akirudia mara tatu (Alikuwa akifanya hivi ikiwa watu ni wengi). [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن المِقْدَادِ رضي الله عنه في حدِيثهِ الطويل ، قَالَ : كُنَّا نَرْفَعُ للنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم نَصِيبَهُ مِنَ اللَّبَنِ ، فَيَجِيءُ مِنَ اللَّيْلِ ، فَيُسَلِّمُ تَسْلِيماً لاَ يُوقِظُ نَائِماً ، وَيُسْمِعُ اليَقْظَانَ ، فَجَاءَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَسَلَّمَ كَمَا كَانَ يُسَلِّمُ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Al-Miqdaad (Radhwiya Allaahu 'anhu) katika hadiyth yake ndefu amesema: Tulikuwa tukimpelekea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) fungu lake la maziwa, kwa hiyo anakuja usiku anasalimia kusalimia kusikoamsha mwenye kulala, Anamsikizisha aliye macho, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaja akasalimia kama alivyokuwa akisalimia." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أسماء بنتِ يزيد رضي الله عنها : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ في المَسْجدِ يَوْماً ، وَعُصْبَةٌ مِنَ النِّسَاءِ قُعُودٌ ، فَألْوَى بِيَدِهِ بالتسْلِيمِ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Asmaa' bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita Msikitini siku moja na kipote cha wanawake kilikuwa kimekaa, alitoa ishara ya kuwasalimia kwa kuinua mkono wake." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 6
وعن أَبي جُرَيٍّ الهُجَيْمِيِّ رضي الله عنه ، قَالَ : أتيت رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فقلتُ : عَلَيْكَ السَّلامُ يَا رسول الله . قَالَ : (( لاَ تَقُلْ عَلَيْكَ السَّلامُ ؛ فإنَّ عَلَيْكَ السَّلاَمُ تَحِيَّةُ المَوتَى )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) ، وَقَدْ سبق بِطُولِهِ .
Amesema Abu Jurayyi Al-Juhaymiyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), nikamwambia: "Alaykas Salaamu Yaa Rasuulallaah" "Amani iwe juu yako ee Rasuli wa Allaah." (Nabiy) Akasema: "Usiseme 'Alayka Salaam, kwani "Alaykas Salaam ni salamu kwa wafu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب آداب السلام
03-Mlango Wa Adabu za Salam
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يُسَلِّمُ الرَّاكِبُ عَلَى المَاشِي ، وَالمَاشِي عَلَى القَاعِدِ ، وَالقَليلُ عَلَى الكَثِيرِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
وفي رواية للبخاري : (( والصغيرُ عَلَى الكَبيرِ )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Aliyepanda atamsalimia anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa miguu atamsalimia aliyekaa na wachache watawasalimia walio wengi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Na katika riwaayah ya Al-Bukhaariy: "Na mtoto atamsalimia mkubwa."
Hadiyth – 2
وعن أَبي أُمَامَة صُدَيِّ بن عجلان الباهِلي رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ أَوْلى النَّاسِ بِاللهِ مَنْ بَدَأهُمْ بِالسَّلامِ )) رواه أَبُو داود بإسنادٍ جيدٍ .
ورواه الترمذي عن أَبي أُمَامَةَ رضي الله عنه ، قِيلَ : يَا رسول الله ، الرَّجُلانِ يَلْتَقِيَانِ أَيُّهُمَا يَبْدَأُ بِالسَّلاَمِ ؟ ، قَالَ : (( أَوْلاَهُمَا بِاللهِ تَعَالَى )) قَالَ الترمذي : (( هَذَا حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Swudayy bin 'Ajlaan Al-Baahiliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika aliye karibu zaidi na Allaah ni yule anayeanza kutoka salamu." [Abu Daawuwd kwa Isnaad nzuri].
Na ameipokea At-Tirmidhiy kutoka kwa Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Aliulizwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Watu wawili wanaokutana, ni yupi anayefaa kutoa salamu?" Akasema: "Yule aliye karibu na Allaah Ta'aalaa." [At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب إعادة السلام عَلَى من تكرر لقاؤه عَلَى قرب بأن دخل ثم خرج
ثُمَّ دخل في الحال ، أَو حال بينهما شجرة ونحوهما
04-Mlango Wa Kupendeza Kurudia Salamu kwa Yule Mnayekutana Naye Mara Nyingi kwa Ukaribu wa Kuingia Kisha Kutoka au Ukawatenganisha Wao Mti na Mfano wake
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه في حديثِ المسِيءِ صلاته : أنّه جَاءَ فَصَلَّى ، ثُمَّ جَاءَ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِ ، فَرَدَّ عَلَيْهِ السَّلاَمَ ، فَقَالَ : (( ارْجِعْ فَصَلِّ فَإنَّكَ لَمْ تُصَلِّ )) فَرَجَعَ فَصَلَّى ، ثُمَّ جَاءَ فَسَلَّمَ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ ثَلاثَ مَرَّاتٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuhusu yule mtu aliyekosea katika Swalaah yake: ya kwamba alikuja akaswali, kisha akaja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumsalimia. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimjibu na kumwambia: "Rudi ukaswali, kwani wewe hujaswali." Yule mtu alirudi kuswali, kisha akaja na kumtolea salamu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka akafanya hilo mara tatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ ، فَإنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ ، أَوْ جِدَارٌ ، أَوْ حَجَرٌ ، ثُمَّ لَقِيَهُ ، فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ )) رواه أَبُو داود .
Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokutana mmoja wenu na nduguye amsalimie. Baada ya hapo ikiwa watatenganishwa na mti au ukuta au jabali (jiwe), kisha wakakutana tena basi amsalimie tena." [Abu Daawuwd]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب السلام إِذَا دخل بيته
05-Mlango Wa Kupendeza Kutoa Salamu Unapoingia Nyumbani
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتًا فَسَلِّمُوا عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللَّـهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً ۚ ﴿٦١﴾
Mtakapoingia majumbani toleaneni salaam; maamkizi kutoka kwa Allaah, yenye Baraka, mazuri. [An-Nuwr: 61]
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( يَا بُنَيَّ ، إِذَا دَخَلْتَ عَلَى أهْلِكَ ، فَسَلِّمْ ، يَكُنْ بَرَكَةً عَلَيْكَ ، وعلى أهْلِ بَيْتِكَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ee mtoto wangu! Unapoingia kwa familia yako basi watolee salamu na hiyo itakuwa ni baraka kwako na kwa watu wa nyumbani kwako." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب السلام عَلَى الصبيان
06-Mlango Wa Kuwatolea Salamu Watoto
Alhidaaya.com [4]
عن أنس رضي الله عنه : أنَّهُ مَرَّ عَلَى صِبْيَانٍ ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ ، وقال : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَفْعَلُهُ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa yeye alipita kwa watoto, akawatolea salamu na akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب سلام الرجل على زوجته والمرأة من محارمه
وعلى أجنبية وأجنبيات لا يخاف الفتنة بهن وسلامهن بهذا الشرط
07-Mlango Wa Mume Kumtolea Salamu Mkewe na Mwanamke Kuwasalimia Maharimu Zake na kwa Kuwatolea Salamu Wageni Wanaume au Wanawake Ikiwa Hapana Hofu ya Fitna na Kuwasalimia kwa Sharti Hili
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن سهل بن سعدٍ رضي الله عنه ، قال : كَانَتْ فِينَا امْرَأةٌ – وفي رواية : كَانَتْ لَنَا عَجُوزٌ – تَأخُذُ مِنْ أصُولِ السِّلْقِ فَتَطْرَحُهُ فِي القِدْرِ ، وَتُكَرْكِرُ حَبَّاتٍ مِنْ شَعِيرٍ ، فَإذَا صَلَّيْنَا الْجُمُعَةَ ، وَانْصَرَفْنَا ، نُسَلِّمُ عَلَيْهَا ، فَتُقَدِّمُهُ إلَيْنَا . رواه البخاري .
Amesema Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Kulikuwa na mwanamke kwetu, na katika riwaayah nyenginemwanamke mzee, ambaye alikuwa akitia katika chungu mizizi ya viazi vitamu na akiongeza shayiri kidogo na kuzipika pamoja. Tulipomaliza Swalaah ya Ijumaa na kutoka, tulikuwa tunamtolea salamu, naye alikuwa akitupatia chakula hicho." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن أُم هَانِىءٍ فاخِتَةَ بنتِ أَبي طالب رضي الله عنها ، قالت : أتيت النبيَّ صلى الله عليه وسلم يَوْمَ الفَتْحِ وَهُوَ يَغْتَسِلُ ، وَفَاطِمَةُ تَسْتُرُهُ بِثَوْبٍ ، فَسَلَّمْتُ ... وَذَكَرَتِ الحديث . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwaUmmu Haani' Faakhitah bint Abu Twaalib (Radhwiya Allaahu 'anhaa) ambaye amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya ufunguzi (Kutekwa kwa Makkah) akiwa anaoga na Faatwimah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amemsitiri kwa nguo (aliyoishika kumziba asionekane). Nilimtolea salamu na nikaitaja Hadiyth. [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أسماءَ بنتِ يزيدَ رضي الله عنها ، قالت : مَرّ عَلَيْنَا النّبيُّ صلى الله عليه وسلم فِي نِسوَةٍ فَسَلَّمَ عَلَيْنَا . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) ، وهذا لفظ أَبي داود .
ولفظ الترمذي : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم مَرَّ في المَسْجِدِ يَوْماً ، وَعُصْبَةٌ مِنَ النِّسَاءِ قُعُودٌ ، فَأَلْوَى بِيَدِهِ بالتَّسْلِيمِ .
Amesema Asmaa' bint Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita kwenye kikundi cha wanawake na akatutolea salamu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم ابتدائنا الكافر بالسلام وكيفية الرد عليهم
واستحباب السلام عَلَى أهل مجلسٍ فيهم مسلمون وكفار
08-Mlango Wa Uharamu wa Kuanza Kuwatolea Salamu Makafiri na Namna ya Kuwajibu na Kupendeza Kutoa Salamu kwa Watu wa Kikazi Czhenye Mchanganyiko wa Waislamu na Makafiri
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ تَبْدَأُوا اليَهُودَ وَلاَ النَّصَارَى بالسَّلامِ ، فَإِذَا لَقِيتُمْ أَحَدَهُمْ في طَرِيق فَاضطَرُّوهُ إِلَى أَضْيَقِهِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musianze kuwatolea salamu Mayahudi na Manasara. Munapokutana na mmoja wao walazimisheni kuitia pambizoni mwa njia (wadhikini katika kupita kwao barabarani)." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا سَلَّمَ عَلَيْكُمْ أهْلُ الكِتَابِ فَقُولُوا : وَعَلَيْكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Wanapo wasalimia Ahlul Kitaab, wajibuni: 'Wa 'alaykum (Nanyi iwe juu yenu)' " [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 3
وعن أُسَامَة رضي الله عنه : أنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم مَرَّ عَلَى مَجْلِسٍ فِيهِ أخْلاَطٌ مِنَ المُسْلِمِينَ وَالمُشْرِكينَ – عَبَدَة الأَوْثَانِ - واليَهُودِ فَسَلَّمَ عَلَيْهِم النبيُّصلى الله عليه وسلم . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Usamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipita katika baraza iliyokuwa na mchanganyiko wa Waislamu na Mushirikina - wanao abudu masanamu na Mayahudi, naye akawatolea salamu." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب السلام إِذَا قام من المجلس
وفارق جلساءه أَوْ جليسه
09-Mlango Wa Kupendeza Kutoa Salamu Unapofika na Kuondoka Katika Kikazi au Kuwaacha Wakazi Wake
Alhidaaya.com [4]
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا انْتَهى أَحَدُكُمْ إِلَى المَجْلِسِ فَلْيُسَلِّمْ ، فَإذَا أرَادَ أنْ يَقُومَ فَلْيُسَلِّمْ ، فَلَيْسَتِ الأُولَى بِأحَقّ مِنَ الآخِرَةِ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofika mmoja wenu katika kikazi atoe salamu na akitaka kuondoka pia atoe salamu. Hiyo ni kwa sababu salamu ya kwanza si bora kuliko ya mwisho." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الاستئذان وآدابه
10-Mlango Wa Kuomba Ruhusa na Adabu Zake
Alhidaaya.com [4]
قَالَ الله تَعَالَى:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتًا غَيْرَ بُيُوتِكُمْ حَتَّىٰ تَسْتَأْنِسُوا وَتُسَلِّمُوا عَلَىٰ أَهْلِهَا ۚ ﴿٢٧﴾
Enyi walioamini! Msiingie nyumba zisizokuwa nyumba zenu mpaka muombe ruhusa na muwatolee salamu wenyewe. [An-Nuwr: 27]
وَإِذَا بَلَغَ الْأَطْفَالُ مِنكُمُ الْحُلُمَ فَلْيَسْتَأْذِنُوا كَمَا اسْتَأْذَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ ﴿٥٩﴾
Na watoto miongoni mwenu watakapofikia baleghe, basi waombe idhini (wakati wote) kama walivyoomba idhini wale wa kabla yao. [An-Nuwr: 59]
Hadiyth – 1
عن أَبي موسى الأشعري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( الاسْتِئْذَانُ ثَلاثٌ ، فَإنْ أُذِنَ لَكَ وَإِلاَّ فَارْجِعْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kubisha hodi ni mara tatu, ukiruhusiwa ingia na ikiwa vinginevyo basi urudi." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن سهلِ بنِ سعدٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّمَا جُعِلَ الاسْتِئذَانُ مِنْ أجْلِ البَصَرِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kuomba ruhusa kumefanywa ili mtu asichungulie." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]
Hadiyth – 3
وعن رِبْعِيِّ بن حِرَاشٍ ، قَالَ : حَدَّثَنَا رَجُلٌ مِنْ بَنِي عَامِرٍ أنَّهُ اسْتَأذَنَ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ في بيتٍ ، فَقَالَ : أألِج ؟ فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم لِخَادِمِهِ : (( أُخْرُجْ إِلَى هَذَا فَعَلِّمهُ الاسْتِئذَانَ ، فَقُلْ لَهُ : قُلِ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، أأدْخُل ؟ )) فَسَمِعَهُ الرَّجُلُ ، فَقَالَ : السَّلامُ عَلَيْكُمْ ، أَأَدْخُل ؟ فَأذِنَ لَهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم فدخلَ . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .
Imepokewa kutoka kwa Rib'iyy bin Hiraash (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alituhadithia mtu kutoka katika ukoo wa 'Aamir (Bani 'Aamir) kwamba alitaka ruhusa kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa nyumbani kwake, akasema: "Je, niingie (A-alij)?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia mtumishi wake: "Nenda kwa huyu mtu umuelimishe namna ya kutaka ruhusa, umwambie: "Sema: Assalaamu 'Alaykum, je niingie (A-adkhul)?" Akasikia yule mtu, naye akasema: "Assalaamu 'Alaykum, (A-adkhul) je, niingie?" Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu, naye akaingia." [Abu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 4
عن كِلْدَةَ بن الحَنْبل رضي الله عنه ، قَالَ : أتَيْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَدَخَلْتُ عَلَيْهِ وَلَمْ أُسَلِّمْ ، فَقَالَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( ارْجِعْ فَقُلْ : السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ ، أَأَدْخُل ؟ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwake Kildah bin Al-Hanbal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na nikaingia bila kutoa salamu. Akasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Rudi na useme: Assalaamu 'Alaykum, (Aadkhul) je, niingie?" [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy na akasema ni Hadiyth Hasan]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب بيان أنَّ السنة إِذَا قيل للمستأذن : من أنت ؟
أن يقول : فلان ، فيسمي نفسه بما يعرف به من اسم أَوْ كنية
وكراهة قوله : (( أنا )) ونحوها
11-Mlango Wa Kubainisha Kuwa Sunnah kwa Mwenye Kubisha Anapoulizwa: "Nani?" Asema: "Fulani", Alitaje Jina Lake Linalijulikana au Kun-yah (Jina la Utani) na Karaha ya Kusema: "Mimi" na Mfano Wake
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
وعن أنس رضي الله عنه في حديثه المشهور في الإسراءِ ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( ثُمَّ صَعَدَ بي جِبْريلُ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا فَاسْتَفْتَحَ ، فقِيلَ : مَنْ هذَا ؟ قَالَ : جِبْريلُ، قِيلَ : وَمَنْ مَعَكَ ؟ قَالَ : مُحَمَّدٌ ، ثُمَّ صَعَدَ إِلَى السَّمَاءِ الثَّانِيَةِ فاسْتَفْتَحَ ، قِيلَ : مَنْ هَذَا ؟ قَالَ : جِبْريل ، قِيلَ : وَمَنْ مَعَكَ ؟ قَالَ : مُحَمَّدٌ وَالثَّالِثَةِ وَالرَّابِعَةِ وَسَائِرِهنَّ وَيُقَالُ فِي بَابِ كُلِّ سَمَاءٍ : مَنْ هَذَا ؟ فَيَقُولُ : جِبْريلُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas katika Hadiyth mashuhuri ya Israa' amesema: kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kisha akapanda nami Jibriyl mpaka wingu wa dunia (wingu wa kwanza), akataka mlango ufunguliwa." Akaulizwa: "Nani huyo?" Akasema: "Jibriyl". Pakasemwa: "Na uko pamoja na nani?" Akasema: "Muhammad". Kisha akapanda nami Jibriyl wingu wa pili, na wa tatu, na wa nne na nyingine zote. Na alikuwa akiulizwa katika kila mlango wa wingu: "Ni nani huyu?" Naye akijibu: "Jibriyl". [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 2
وعن أَبي ذرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : خَرَجْتُ لَيْلَةً مِنَ اللَّيَالِي ، فَإذَا رسول الله صلى الله عليه وسلم يَمْشِي وَحْدَهُ، فَجَعَلْتُ أمْشِي فِي ظلِّ القمَرِ، فَالْتَفَتَ فَرَآنِي ، فَقَالَ: (( مَنْ هَذَا ؟ )) فقلتُ : أَبُو ذَرٍّ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nilitoka usiku mmoja na kumuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitembea peke yake. Nikawa mimi natembea katika kivuli cha mwezi. Alizunguka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuniona, akasema: "Ni nani huyu?" Nikasema: "Abu Dharr." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 3
وعن أُمِّ هانىءٍ رضي الله عنها ، قالت : أتيتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَغْتَسِلُ وَفَاطِمَةُ تَسْتُرُهُ ، فَقَالَ : (( مَنْ هذِهِ ؟ )) فقلتُ : أنا أُمُّ هَانِىءٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ummu Haani' (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba amesema: Nilikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa naoga na Faatwimah anamsitiri (kwa pazia). Akasema: "Nani huyu?" Nikasema: "Ni mimi Ummu Haani'." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن جابر رضي الله عنه ، قَالَ : أتَيْتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم فَدَقَقْتُ البَابَ ، فَقَالَ : (( مَنْ هَذَا ؟ )) فَقُلتُ : أَنَا ، فَقَالَ : (( أنَا ، أنَا ! )) كَأنَّهُ كَرِهَهَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwake Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nilimwendea Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nikagonga mlango akauliza: "Nani huyo?" Nikamjibu: "Mimi". Akasema: "Mimi, mimi!" kama vile amelichukia jibu hilo. [Al-Bukhaariy na Muslim].
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب تشميت العاطس إِذَا حمد الله تَعَالَى وكراهة تشميته إذا لَمْ يحمد الله تَعَالَى
وبيان آداب التشميت والعطاس والتثاؤب
12-Mlango Wa Kupendeza Kumuombea Dua Aliyekwenda Chafya Anapomuhimidi Allaah Ta'aalaa na Karaha ya Kumuombea Ikiwa Hakumuhimidi Allaah Ta'aalaa na Kubainisha Adabu Unapopiga Chafya na Kupiga Miayo
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ الله يُحِبُّ العُطَاسَ ، وَيَكْرَهُ التَّثَاؤُبَ ، فَإذَا عَطَسَ أَحَدُكُمْ وَحَمِدَ الله تَعَالَى كَانَ حَقّاً عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ سَمِعَهُ أنْ يَقُولَ لَهُ : يَرْحَمُكَ اللهُ ، وَأَمَّا التَّثَاؤُبُ فَإنَّمَا هُوَ مِنَ الشَّيْطَانِ ، فَإذَا تَثَاءبَ أحَدُكُمْ فَلْيَرُدَّهُ مَا اسْتَطَاعَ ، فَإنَّ أحَدَكُمْ إِذَا تَثَاءبَ ضَحِكَ مِنْهُ الشَّيْطَانُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah anapenda chafya na anachukia miayo. Hivyo, anapochemua mmoja wenu na akamshukuru Allaah Ta'aalaa inakuwa ni haki kwa Muislamu mwenye kusikia kumwambia: "Yarhamuka Allaah (Allaah Akurehemu)." Ama kuhusu kwenda miayo, hakika inatokana na shetani. Hivyo, anapokwenda miayo mmoja wenu ajaribu kujizui, kwani anayekwenda miyao huchekwa na shetani." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا عَطَسَ أحَدُكُمْ فَلْيَقُلْ : الحَمْدُ للهِ ، وَلْيَقُلْ لَهُ أخُوهُ أَوْ صَاحِبُهُ : يَرْحَمُكَ الله . فإذَا قَالَ لَهُ : يَرْحَمُكَ اللهُ ، فَليَقُلْ : يَهْدِيكُمُ اللهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ )) رواه البخاري .
Na Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapopiga chafya mmoja wenu aseme: "Alhamdulillaah (Kuhimidiwa ni kwa ni kwa Allaah)." Na aseme nduguye au sahibu yake: 'Yarhamka Allaah', naye aseme: 'Yahdikumu Allaahu wa Yuslih Baalakum (Allaah akuongozeni na akutengezeeni hali yenu)'." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( إِذَا عَطَسَ أحَدُكُمْ فَحَمِدَ اللهَ فَشَمِّتُوهُ، فَإنْ لَمْ يَحْمَدِ الله فَلاَ تُشَمِّتُوهُ )) رواه مسلم.
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Anapokwenda chafya mmoja wenu na akamshukuru Allaah (kwa kusema Alhamdulillaah) asi muombeeni dua na ikiwa hakumshukuru Allaah basi hamuna haja ya kumuombea." [Muslim]
Hadiyth – 4
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : عَطَسَ رَجُلانِ عِنْدَ النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَشَمَّتَ أَحَدَهُمَا وَلَمْ يُشَمِّتِ الآخَرَ ، فَقَالَ الَّذِي لَمْ يُشَمِّتْهُ : عَطَسَ فُلانٌ فَشَمَّتَّهُ ، وَعَطَسْتُ فَلَمْ تُشَمِّتْنِي ؟ فَقَالَ : (( هَذَا حَمِدَ الله ، وَإنَّكَ لَمْ تَحْمَدِ الله )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Walikwenda chafya watu wawili mbele ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), akamuombea dua mmoja wao na hakumuombea yule mwengine. Akasema yule ambaye hakuombewa dua: "Amekwenda chafya fulani nawe ukamuombea dua na mimi nimepiga chafya na hukuniombea." Akasema: "Huyu amemshukuru Allaah amesema: (Alhamdulillaah) na wewe hukumshukuru Allaah." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 5
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا عَطَسَ وَضَعَ يَدَهُ أَوْ ثَوْبَهُ عَلَى فِيهِ ، وَخَفَضَ - أَوْ غَضَّ - بِهَا صَوْتَهُ . شك الراوي . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alikuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapokwenda chafya akiweka mkono wake ili kuhafifisha sauti yake (au kuuma). Ametia shaka mpokezi. [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
Hadiyth – 6
وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ اليَهُودُ يَتَعَاطَسُونَ عِنْدَ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يَرْجُونَ أنْ يَقُولَ لَهُمْ : يَرْحَمُكُم الله ، فَيَقُولُ : (( يَهْدِيكُم اللهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Walikuwa Mayahudi wakienda chafya mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakitarajia ya kwamba atawaambia: "Yarhamuka Allaah." Lakini alikuwa akisema: "Yahdiikumu Allaahu wa Yuslih Baalakum." [Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 7
وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا تَثَاءبَ أحَدُكُمْ فَلْيُمْسِكْ بِيَدِهِ عَلَى فِيهِ ؛ فَإنَّ الشَّيْطَانَ يَدْخُلُ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokwenda miayo mmoja wenu aufinike mdomo wake kwa mkono wake, kwani usipofanya hivyo shetani ataingia." [Muslim]
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب المصافحة عِنْدَ اللقاء وبشاشة الوجه وتقبيل يد الرجل الصالح وتقبيل ولده شفقة ومعانقة القادم من سفر وكراهية الانحناء
13-Mlango Wa Kupendeza Kupeana Mikono Mnapokutana na Kufurahi na Kuubusu Mkono wa Mcha Mungu (na Mwema) na Kubusu Mtoto Kudhihirisha Mapenzi na Kumkumbatia Anayetoka Safari na Karaha ya Kuinamisha Kichwa Mbele Yake
Alhidaaya.com [4]
Hadiyth – 1
عن أَبي الخطاب قتادة ، قَالَ : قُلْتُ لأَنَسٍ : أكَانَتِ المُصَافَحَةُ في أصْحَابِ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : نَعَمْ . رواه البخاري .
Amesema Abil Khatwaab Qataadah (Radhwiya Allahu 'anhu): Nilimuuliza Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Je, Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakisalimiana kwa kupeana mikono?" Akasema: "Ndio." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 2
وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ: لَمَّا جَاءَ أهْلُ اليَمَنِ، قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( قَدْ جَاءكُمْ أهْلُ اليَمَنِ )) وَهُمْ أوَّلُ مَنْ جَاءَ بِالمُصَافَحَةِ. رواه أَبُو داود بإسناد صحيح.
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Walipokuja watu kutoka Yemen, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Wamekujieni watu wa Yemen, na wao ndio wa kwanza kuanzisha (kusalimiana kwa) kupeana mikono." [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Hadiyth – 3
وعن البراءِ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ مُسْلِمَينِ يَلْتَقِيَانِ فَيَتَصَافَحَانِ إِلاَّ غُفِرَ لَهُمَا قَبْلَ أنْ يَفْتَرِقَا )) رواه أَبُو داود .
Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aesema: "Hakuna Waislaamu wawili wanaokutana na kupeana mikono isipokuwa wanasamehewa kabla ya kuachana." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 4
وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رَجُلٌ : يَا رسولَ اللهِ ، الرَّجُلُ مِنَّا يَلْقَى أخَاهُ، أَوْ صَدِيقَهُ، أينحَنِي لَهُ ؟ قَالَ : (( لاَ )) . قَالَ : أفَيَلْتَزِمُهُ وَيُقَبِّلُهُ ؟ قَالَ : (( لاَ )) قَالَ : فَيَأخُذُ بِيَدِهِ وَيُصَافِحُهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Mtu mmoja aliuliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Mtu anakutana na nduguye au rafiki yake, je, amuinamie (kama ishara)?" Akasema: "Laa." Akauliza tena: "Je, amsalimie kwa kumpa mkono?" Akasema: "Ndio." [At-Tirmdhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 5
وعن صَفْوَانَ بن عَسَّالٍ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ يَهُودِيٌّ لِصَاحِبِهِ : اذْهَبْ بِنَا إِلَى هَذَا النَّبيِّ ، فَأتَيَا رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، فَسَألاهُ عَنْ تِسْعِ آياتٍ بَيِّنَاتٍ ... فَذَكَرَ الْحَدِيث إِلَى قَوْلهِ : فقَبَّلا يَدَهُ وَرِجْلَهُ ، وقالا : نَشْهَدُ أنَّكَ نَبِيٌّ . رواه الترمذي وغيره بأسانيد صحيحةٍ .
Imepokewa kwa Swafwaan bin 'Assaal (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba amesema: Alisema Myahudi kwa sahibu yake: "Tupeleke kwa Nabiy huyu." Wakamjia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakamuuliza ishara tisa za wazi (Hizi ni zile alizopatiwa Nabiy Muwsaa 'Alayhis Salaam); Akataja Hadiyth hadi kauli yake: Basi wakaubusu mkono wake na mguu wake, wakasema: "Tunashuhudia kwamba wewe ni Nabiy." [At-Tirmidhiy na wengineo kwa Isnaad zilizo Swahiyh]
Hadiyth – 6
وعن ابن عمر رضي الله عنهما قِصَّة ، قَالَ فِيهَا : فَدَنَوْنَا مِنَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَقَبَّلْنَا يَدَه . رواه أَبُو داود .
Na kutoka Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amehadithia ndani yake: Mwisho wa kisomo tulifika karibu na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuubusu mkono wake." [Abuu Daawuwd]
Hadiyth – 7
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَدِمَ زَيْدُ بْنُ حَارِثَةَ المَدِينَةَ وَرسولُ الله صلى الله عليه وسلم في بَيتِي ، فَأتَاهُ فَقَرَعَ البَابَ ، فَقَامَ إِلَيْهِ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يَجُرُّ ثَوْبَهُ ، فَاعْتَنَقَهُ وَقَبَّلَهُ . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Na amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba alifika Zayd bin Al-Haarithah Madiynah na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yupo nyumbani kwangu. Alikuja na kugonga mlango, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), naye aliinuka kwenda kumpokea kwa haraka huku anaburuza nguo yake, akamkumbatia na kumbusu." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 8
وعن أَبي ذَرٍّ رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ لي رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا تَحقِرَنَّ منَ الْمَعرُوف شَيْئاً ، وَلَوْ أنْ تَلْقَى أخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْقٍ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Musichukie jema lolote hata ikiwa ni kukutana na ndugu yako kwa uso wa tabasamu na bashasha." [Muslim]
Hadiyth – 9
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَبَّلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الحَسَنَ بنَ عَلِيٍّ رضي الله عنهما ، فَقَالَ الأقْرَعُ بن حَابِسٍ : إنَّ لِي عَشْرَةً مِنَ الْوَلَدِ مَا قَبَّلْتُ مِنْهُمْ أحَدَاً . فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ لاَ يَرْحَمْ لاَ يُرْحَمْ ! )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimbusu Al-Hasan bin 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) na Aqra' bin Haabis akiwa pamoja naye. Aqra' akasema: "Hakika mimi nina watoto kumi lakini sijambusu hata mmoja kati yao." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwangalia, na kisha kusema: "Yeyote asiyewarehemu (wenzake) basi harehemewi (na Allaah)." [Al-Bukhaary na Muslim]
Links
[1] http://alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/280
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10319&title=05-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Kitabu%20Cha%20Maamkizi%20Ya%20Salaam%20-%20%D9%83%D9%90%D8%AA%D8%A7%D8%A8%D9%8F%20%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%91%D9%8E%D9%84%D8%A7%D9%85
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11022&title=01-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kutoleana%20Salamu%20na%20Maamrisho%20ya%20Kutoa%20Salamu
[6] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11023&title=02-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Jinsi%20ya%20Kutoa%20Salamu
[7] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11024&title=03-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Adabu%20za%20Salam
[8] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11025&title=04-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kurudia%20Salamu%20kwa%20Yule%20Mnayekutana%20Naye%20Mara%20Nyingi%20kwa%20Ukaribu%20wa%20Kuingia%20Kisha%20Kutoka%20au%20Ukawatenganisha%20Wao%20Mti%20na%20Mfano%20wake
[9] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11026&title=05-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kutoa%20Salamu%20Unapoingia%20Nyumbani
[10] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11028&title=06-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuwatolea%20Salamu%20Watoto
[11] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11027&title=07-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Mume%20Kumtolea%20Salamu%20Mkewe%20na%20Mwanamke%20Kuwasalimia%20Maharimu%20Zake%20na%20kwa%20Kuwatolea%20Salamu%20Wageni%20Wanaume%20au%20Wanawake%20Ikiwa%20Hapana%20Hofu%20ya%20Fitna%20na%20Kuwasalimia%20kwa%20Sharti%20Hili
[12] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11029&title=08-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Uharamu%20wa%20Kuanza%20Kuwatolea%20Salamu%20Makafiri%20na%20Namna%20ya%20Kuwajibu%20na%20Kupendeza%20Kutoa%20Salamu%20kwa%20Watu%20wa%20Kikazi%20Czhenye%20Mchanganyiko%20wa%20Waislamu%20na%20Makafiri
[13] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11030&title=09-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kutoa%20Salamu%20Unapofika%20na%20Kuondoka%20Katika%20Kikazi%20au%20Kuwaacha%20Wakazi%20Wake
[14] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11031&title=10-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuomba%20Ruhusa%20na%20Adabu%20Zake
[15] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11032&title=11-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kubainisha%20Kuwa%20Sunnah%20kwa%20Mwenye%20Kubisha%20Anapoulizwa%3A%20%22Nani%3F%22%20Asema%3A%20%22Fulani%22%2C%20Alitaje%20Jina%20Lake%20Linalijulikana%20au%20Kun-yah%20%28Jina%20la%20Utani%29%20na%20Karaha%20ya%20Kusema%3A%20%22Mimi%22%20na%20Mfano%20Wake
[16] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11042&title=12-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kumuombea%20Dua%20Aliyekwenda%20Chafya%20Anapomuhimidi%20Allaah%20Ta%27aalaa%20na%20Karaha%20ya%20Kumuombea%20Ikiwa%20Hakumuhimidi%20Allaah%20Ta%27aalaa%20na%20Kubainisha%20Adabu%20Unapopiga%20Chafya%20na%20Kupiga%20Miayo
[17] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Falhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11043&title=13-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kupendeza%20Kupeana%20Mikono%20Mnapokutana%20na%20Kufurahi%20na%20Kuubusu%20Mkono%20wa%20Mcha%20Mungu%20%28na%20Mwema%29%20na%20Kubusu%20Mtoto%20Kudhihirisha%20Mapenzi%20na%20Kumkumbatia%20Anayetoka%20Safari%20na%20Karaha%20ya%20Kuinamisha%20Kichwa%20Mbele%20Yake