Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 17-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Mambo Yaliyokatazwa - كِتابُ الأمور الْمُنهى عَنْها > 004-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Umbeya, Nako ni Kueneza Maneno Baina ya Watu kwa Njia ya Kuleta Ufisadi

004-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Umbeya, Nako ni Kueneza Maneno Baina ya Watu kwa Njia ya Kuleta Ufisadi

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تحريم النميمة

وهي نقل الكلام بَيْنَ الناس عَلَى جهة الإفساد

004-Mlango Wa Kuharamishwa Umbeya, Nako ni Kueneza Maneno Baina ya Watu kwa Njia ya Kuleta Ufisadi

 

Alhidaaya.com [1]

 

قال الله تَعَالَى :

هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ﴿١١﴾

Mwingi wa kukashifu, mpitaji huku na kule kwa kufitinisha. [Al-Qalam: 11]

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ﴿١٨﴾

Hatamki kauli yeyote isipokuwa anaye mchungaji aliyejitayarisha (kurekodi). [Qaaf: 18]

 

Hadiyth – 1

وعن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لا يَدْخُلُ الجَنَّةَ نَمَّامٌ )).متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Peponi mmbeya (mwenezaji uvumi / msingiziaji) [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 2

وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم مرَّ بِقَبْرَيْنِ فَقَالَ : (( إنَّهُمَا يُعَذَّبَانِ ، وَمَا يُعَذَّبَانِ في كَبيرٍ ! بَلَى إنَّهُ كَبِيرٌ : أمَّا أَحَدُهُمَا ، فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ ، وأمَّا الآخَرُ فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنْ بَوْلِهِ )) . متفق عَلَيْهِ . وهذا لفظ إحدى روايات البخاري .

Amesimulia Ibn 'Abbaas  (رضي الله عنهما): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)    aliyapitia makaburi mawili na akasema: “Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na wala hawaadhibiwi kwa sababu ya jambo kubwa (la kuwashinda kulitekeleza au kujiepusha nalo).” Kisha hapo hapo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ”Hapana! Bali ni kubwa (dhambi kubwa na adhabu zake)!  Ama mmoja wao, huyu alikuwa akipita kufitinisha watu, na ama mwingine, huyu alikuwa hajikingi na mkojo wake [anapokojoa].” [Al-Bukhaariy na Muslim]" [Al-Bukhaariy na Muslim, na hili tamshi ni moja ya riwaayah za Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن مسعود رضي الله عنه : أن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( أَلاَ أُنَبِّئُكُمْ مَا العَضْهُ ؟ هي النَّمَيمَةُ ؛ القَالَةُ بَيْنَ النَّاسِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Je, niwajulishe nyinyi 'Adhhu ni nini? Huo ni uongo na kuzungusha maneno baina ya watu." [Muslim]

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11295

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11295&title=004-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kuharamishwa%20Umbeya%2C%20Nako%20ni%20Kueneza%20Maneno%20Baina%20ya%20Watu%20kwa%20Njia%20ya%20Kuleta%20Ufisadi