Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > 17-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Kitabu Cha Mambo Yaliyokatazwa - كِتابُ الأمور الْمُنهى عَنْها > 104-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kumuashiria muislamu kwa Silaha na Mfano wake Sawa ni kwa Kweli au Mzaha na Katazo la Kuwa na Upanga Nje ya Ala yake

104-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kukatazwa Kumuashiria muislamu kwa Silaha na Mfano wake Sawa ni kwa Kweli au Mzaha na Katazo la Kuwa na Upanga Nje ya Ala yake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب النهي عن الإشارة إلى مسلم بسلاح ونحوه

سواء كان جاداً أو مازحاً ، والنهي عن تعاطي السيف مسلولاً

104-Mlango Wa Kukatazwa Kumuashiria muislamu kwa Silaha na Mfano wake Sawa ni kwa Kweli au Mzaha na Katazo la Kuwa na Upanga Nje ya Ala yake

 

Alhidaaya.com [1]

 

Hadiyth – 1

عن أبي هريرة رضي الله عنه ، عن رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال : (( لاَ يُشِرْ أحَدُكُمْ إلَى أخِيهِ بِالسِّلاحِ ، فَإنَّهُ لاَ يَدْرِي لَعَلَّ الشَّيْطَانَ يَنْزعُ فِي يَدِهِ ، فَيَقَع فِي حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ )) . متفق عليه .

وفي رواية لمسلم قال : قال أبو القاسم صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ أشَارَ إلَى أخِيهِ بِحَدِيدَةٍ ، فَإنَّ المَلاَئِكَةَ تَلْعَنُهُ حَتَّى يَنْزعَ ، وَإنْ كَانَ أخَاهُ لأَبِيهِ وَأُمِّهِ ))

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Asimuashirie mmoja wenu nduguye kwa silaha, kwani yeye hajui huenda shetani akaitowa mkononi mwake (akaleta maafa, kujeruhi, au kifo), hivyo kumfanya aingie katika shimo la moto." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na Musli katika riwaayah yake amesema: Amesema Abul Qaasim: "Mwenye kumuashiria chuma nduguye, hakika Malaaikah anamlaani mpaka akiondoshe, japokuwa atakuwa ni ndugu yake halisa (kwa baba na mama)."  

 

Hadiyth – 2

وعن جابر رضي الله عنه قال : نهى رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنْ يُتَعَاطَى السَّيْفُ مَسْلُولاً . رواه أبو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Amesema Jaabir (Radhwiya Allaahu 'anhu): Amekataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mtu kumpatia upanga usiokuwa katika ala yake mwenziwe. [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Share [2]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/11425

Links
[1] http://www.alhidaaya.com/
[2] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F11425&title=104-Riyaadhw%20Asw-Swaalihiyn%3A%20Mlango%20Wa%20Kukatazwa%20Kumuashiria%20muislamu%20kwa%20Silaha%20na%20Mfano%20wake%20Sawa%20ni%20kwa%20Kweli%20au%20Mzaha%20na%20Katazo%20la%20Kuwa%20na%20Upanga%20Nje%20ya%20Ala%20yake