TAAHIYYAATU (TASHAHHUD) YA
Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa kwa tashahhud baada ya kumaliza rakaa ya pili. Swalah ikiwa ya rakaa mbili kama Alfajiri, hukaa "muftarishan"([1])
Alimuamrisha hivyo aliyeswali vibaya kwa kumuambia: ((Utakapokaa katikati ya Swalah, jitulize, na utandaze paja lako la kushoto na lete tashahhud)).([3])
Abu Huraryah (رضي الله عنه) amesema: "Rafiki yangu (صلى الله عليه وآله وسلم) amenikataza kuchutama (iq'aa) mchutamo wa mbwa."([4]) [katika riwaaya nyingine] Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akikataza kuchutama
Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)anapokaa katika tashahhud huweka kiganja chake cha mkono wa kulia juu ya paja [katika usimulizi mwingine: goti] la kulia, na huweka kiganja chake cha kushoto katika paja [katika usimulizi mwengine: goti] la kushoto([6]). Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiweka kisugudi cha mkono wake wa kulia katika paja lake la kulia.([7])
Pia (صلى الله عليه وآله وسلم)alimkataza mtu aliyekaa katika Swalah hali ya kuwa anautegemea mkono wake wa kushoto akamwambia: ((Hakika hiyo ni Swalah ya Mayahudi))([8]). Na katika kauli nyingine: ((Usikae hivi, kwani hakika hiki ni kikao cha wale wanaoadhibiwa))([9]). Katika Hadiyth nyingine: ((Ni kitako cha wale walioghadhibikiwa [Na Allaah]))([10]).
[1] An-Nasaaiy(1/173) ikiwa na isnaad Swahiyh. "Muftarishan" ni kukalia tumbo la mguu wa kushoto na kuusimamisha unyayo wa mguu wa kulia
[2] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.
[3] Abu Daawuud na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad nzuri.
[4] Atw-Twayaalisiy, Ahmad na Ibn Abi Shaybah. Kuhusu "iq'aa", Abu 'Ubaydah na wengineo wamesema: "Ni mtu anapogandamiza kikalio chake ardhini, akiweka muundi wake wima, na kuegemeza mikono yake ardhini
[5] Muslim, Abu 'Awaanah na wengineo. Imetolewa katika Al-Irwaa (316).
[6] Muslim na Abu 'Awaanah.
[7]Abu Daawuud na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Inayokusudiwa ni kwamba hakutenganisha viwiko vyake na ubavu wake
[8]Al-Bayhaqiy na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Imetolewa pamoja inayofuatia katika Al-Irwaa (380).
[9] Ahmad na Abu Daawuud ikiwa na isnaad nzuri.
[10] 'Abdur-Razaaq; 'Abdul-Haqq amekiri ni Swahiyh katika Ahkaam yake (Namba 1284 katika utafiti wangu).
Links
[1] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F4159&title=043-Sifa%20Ya%20Swalah%20Ya%20Mtume%20%28Swalla%20Allaahu%20%27Alayhi%20Wa%20Aalihi%20Wa%20Sallam%29%3A%20Tahiyyaatu%20%28Tashahhud%29%20Ya%20Kwanza