Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Fataawaa: 'Itikaaf (Kubakia Msikitini Kufanya 'Ibaadah)

Fataawaa: 'Itikaaf (Kubakia Msikitini Kufanya 'Ibaadah)

Fataawa Za Ramadhwaan-'Iyd [1]

 

 

 

www.alhidaaya.com [2]

 

 

 

 

Share [3]

01- Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Nini Maana Ya ‘Itikaaf?

Nini Maana Ya ‘Itikaaf?

 

 Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

 

Maana ya Mu’takif:  Mwenye kuingia katika niyyah ya I’tikaaf.

 

1. Nini Maana Ya ‘Itikaaf?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ni kujiweka faragha kwa ajili ya ‘ibaadah na kujipwekesha kwa Allaah kwayo. Na hii ndio kujipwekesha ki-shariy’ah. Na wengineo wakasema kuhusu maana ya I’tikaaf ni kukata mahusiano na kila kiumbe kwa yale yanayohusiana na kuwahudumia viumbe.

 

 

[Majmu’w Al-Fataawaa (15/438)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

I’tikaaf ni mtu kujilazimisha kubakia Msikitini kwa ajili ya utiifu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), ili ajitenge na watu na ashughulike katika utiifu kwa Allaah na ajiweke faragha nayo. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/155)] 

 

 

Share [5]

02- Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Nini Hukmu Ya I’tikaaf?

Nini Hukmu Ya I’tikaaf?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

 

 

2. Nini Hukmu Ya I’tikaaf?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

I’tikaaf ni Sunnah kwa wanaume na wanawake.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/442)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ni Sunnah ya kutafuta Laylatul-Qadr.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/156)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

I’tikaaf katika Ramadhwaan ni Sunnah aliyoifanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika uhai wake, kisha wake zake wakafanya I’tikaaf baada yake. Na Ahlul-‘Ilm (Wanachuoni) kwa ijmaa’ wakasema kuwa ni Sunnah. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawa (20/158)]

 

 

Share [6]

03- Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Je, I’tikaaf Inafaa Ki-Shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan

Je, I’tikaaf Inafaa Ki-Shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

3. Je, I’tikaaf Inafaa Ki-shariy’ah Miezi Mingineyo Isiyokuwa Ramadhwaan?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Inafaa ki-shariy’ah Ramadhwaan na miezi mingineyo na ikiwa pamoja na Swiyaam ni bora zaidi.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/438)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Inapasa ki-shariy’ah iwe katika Ramadhwaan pekee, lakini ikiwa mtu atafanya I’tikaaf ghairi ya Ramadhwaan itakuwa inafaa.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/159-160)]

 

 

Share [8]

05-Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad: Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi Kuwa Na Swawm

Kufanya I´itikaaf Haishurutishwi  Kuwa Na Swawm

 

Shaykh ´Abdul-Muhsin Al-‘Abbaad (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

SWALI:

 

Je, ni sharti mtu ili afanye I´tikaaf awe ana Swawm? 

 

 

JIBU:

Hapakudhihiri kitu kwangu kuwa ni sharti hilo (la mtu awe katika Swawm) kutokana na kufanya kwake (Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) I´tikaaf siku kumi za Shawwaal, haikuthibiti kuwa alifunga. Hakuna kinachoonesha kuwa alifunga. 

 

 

[Bawaabah Al-Haramayn Ash-Shariyfayn] [9]

 

 

Share [10]

06-Imaam Ibn Baaz: Je, Ili I’tikaaf Iwe Sahihi Inalazimika Mtu Awe Katika Swawm?

Je, Ili I’tikaaf Iwe Sahihi Inalazimika Mtu Awe Katika Swawm?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

06. Je, Ili I’tikaaf Iwe Sahihi Inalazimika Mtu Awe Katika Swawm?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Sahihi ni kwamba haina ulazima mtu awe katika Swawm. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/441)]

 

 

Share [11]

07-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Je, I’tikaaf Inajuzu Wakati Wowote Ule Nje Ya Masiku Kumi Ya Mwisho Ya Ramadhwaan?

Je, I’tikaaf Inajuzu Wakati Wowote Ule Nje Ya Masiku Kumi Ya Mwisho Ya Ramadhwaan?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

07-Je, I’tikaaf Inajuzu Wakati Wowote Ule Nje Ya Masiku Kumi Ya Mwisho Ya Ramadhwaan?

 

Jibu:  Naam, I’tikaaf inajuzu wakati wowote ule lakini iliyo bora kabisa ni ya katika masiku kumi ya Ramadhwaan. 

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah (10/410)]

 

 

Share [12]

08-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Je, I’tikaaf Ya Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?

Je, I’tikaaf Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

08-Je, I’tikaaf Ya Mwanamke Ni Sawa Na Ya Mwanaume?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

I’tikaaf ya mwanamke ki-shariy’ah ni sawasawa na ya mwanaume lakini tu iambatane na sharti kwamba haitomsababisha ufisadi au fitnah. Pindi itakaposababisha kuwa ni ufisadi au fitnah basi hapo hapaswi kufanya I’tikaaf. Au kama I’tikaaf itamsababisha asiwe na (majukumu na) watoto wake nyumbani mwake au asitimize haki za mumewe basi hapaswi kufanya I’tikaaf.

 

 

[Nuwr ‘Alaa Ad-Darb]

 

 

Share [13]

09-Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Sehemu Gani Inapaswa Kutekelezwa I’itikaaf?

Sehemu Gani Inapaswa Kutekelezwa I’itikaaf?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

09-. Sehemu Gani Inapaswa Kutekelezwa I’itikaaf?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Sehemu inayopaswa kutekelezwa I’tikaaf ni Misikitini ambayo inasimamishwa Swalaah za Jamaa’ah.

 

 

[Majmu’w Al-Fataawaa (15/42)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Katika kila Msikiti, ikiwa ni Misikiti inayoswaliwa Ijumaa au katika Misikiti isiyoswaliwa humo. Lakini iliyo bora ni iwe katika Misikiti inayoswalishwa humo (Jamaa’ah). 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/155)]

 

 

Share [14]

10-Imaam Ibn Baaz: Je, I’tikaaf Inajuzu Katika Masjid Al-Haraam Kwa Ajili Ya Wanawake Na Wanaume?

Je, I’tikaaf Inajuzu Katika Masjid Al-Haraam (Makkah) Kwa Ajili Ya Wanawake Na Wanaume?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

10-Je, I’tikaaf Inajuzu Katika Masjid Al-Haraam (Makkah) Kwa Ajili Ya Wanawake Na Wanaume?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Hakuna makatazo kutekelezwa I’tikaaf katika Masjid Al-Haraam na Masjid An-Nabawiy Ash-Shariyf, ikiwa ni wanaume au wanawake na ikiwa haiwaletei madhara wanaoswali wala haimuudhi yeyote basi hakuna ubaya hivyo.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/440)]

 

 

Share [15]

11-Imaam Ibn Baaz na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu?

Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) na Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

11-Je, I’tikaaf Inasihi Katika Misikiti Mingineyo Isiyokuwa Ile Mitatu? (Masjid Al-Haraam (Makkah), Masjid An-Nabawiy (Madiynah), Masjid Al-Aqswaa (Palestina).

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. I’tikaaf inasihi katika Misikiti mingineyo isiyokuwa katika mitatu isipokuwa ikiwa mtu ametoa nadhiri kutekeleza I’tikaaf katika Misikiti mitatu basi hapo inamlazimu atekeleze I’tikaaf humo ili atimize nadhiri yake. 

 

b. Isipokuwa ikiwa haiswaliwi Swalaah ya jamaa’ah humo basi I’tikaaf haisihi kutekelezwa humo. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/444)]

 

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Inajuzu I’tikaaf katika Misikiti mingineyo isiyokuwa ile mitatu na ikiwa Hadiyth hii ni swahiyh “Isifanywe I’tikaaf isipokuwa Misikiti mitatu”, basi iliyokusudiwa ni kwamba I’tikaaf humo ni yenye ukamilifu na bora zaidi. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawa 20/160)]

 

 

Share [16]

12-Imaam Ibn Baaz : Mwanamke Atekeleze Wapi I’tikaaf Akipenda Kufanya Hivyo?

Mwanamke Atekeleze Wapi I’tikaaf Akipenda Kufanya Hivyo?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

12-Mwanamke Atekeleze Wapi I’tikaaf Akipenda Kufanya Hivyo?

 

Mwanamke akitaka kutekeleza I’tikaaf, basi iwe katika Msikiti ambao hauna tahadharisho la ki-shariy’ah lakini ikiwa kuna tahadharisho la ki-shariy’ah basi asifanye I’tikaaf humo. 

 

 

[Majmuw’ Al-Faataawaa (20/163)]

Share [17]

13-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Vyumba Vya Matumizi Vya Masjid Vinafaa Kutumika Kwa I'tikaaf?

Vyumba Vya Matumizi Vya Masjid Vinafaa Kutumika Kwa I'tikaaf?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

13-Chumba Cha Mlinzi Na Chumba Cha Wasimamizi Wa Zakaah Katika Masjid; Je, Vinafaa Kutumika Kwa Ajili Ya I’tikaaf?

 

a. Vyumba vilivyomo ndani ya Msikiti pamoja na milango yake yote hukmu zake ni za Msikiti.

 

b. Lakini ikiwa ni nje ya Msikiti, basi si katika Msikiti ijapokuwa ikiwa milango yake imo ndani ya Msikiti.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah (10/412)]

 

 

Share [18]

14-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?

Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

14-Zipi Nguzo Za I’tikaaf Na Sharti Zake? Na Je, Inasihi Bila Ya Swawm?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. Nguzo ya I’tikaaf ni kulazimika (kufanyika I’tikaaf) katika Msikiti kwa ajili ya utiifu kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kumwabudu Yeye, na kujikurubisha Kwake na kujipwekesha katika kumwabudu.

 

b. Ama sharti zake, basi ni kama zilivyo sharti za ‘ibaadah zote miongoni mwazo ni: Uislamu, akili, na inasihi kwa asiyebaleghe, na inasihi kwa mwanaume na mwanamke.

 

c. Na inasihi bila ya Swawm, na inasihi katika Misikiti yote.

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/162)]

 

 

 

Share [19]

15-Imaam Ibn Baaz: I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?

Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

15. Je, I’tikaaf Ina Wakati Maalumu Katika Kuingia Na Kutoka Kwake Na Je, Inajzu Kuikata?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. Kauli ya sahihi kabisa ya Ahlul-‘Ilm ni kwamba haina wakati maalumu.

 

b. Na Sunnah ni mtu aingie akiwa Mu’takif  pindi anapotia niyyah kwa ajili ya I’tikaaf na atoke baada ya kumaliza muda wake alionuiya.

 

c. Na anaweza kuikata ikiwa atahitaji kufanya hivyo kwa sababu I’tikaaf ni Sunnah haipasi kujiwajibisha nayo ikiwa ni mwenye udhuru.

 

d. Na I’tikaaf inapendekezeka katika makumi ya mwisho ya Ramadhwaan na ni mustahabu kwa mwenye kuingia I’tikaaf aingie akiwe Mu’takif baada ya Swalaah  ya Alfajiri kuanzia siku ya ishirini na moja, kama alivyofanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na atoke inapomalizika masiku kumi (ya mwisho). 

 

 

[Majmu’w Al-Fataawaa (15/442)]

 

Share [20]

16-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: I’tikaaf Inaanza Lini?

I’tikaaf Inaanza Lini?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

 

16. I’tikaaf Inaanza Lini?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

‘Ulamaa wote wamekubaliana kwamba I’tikaaf inaanza usiku wa (kuamkia tarehe) ishirini na moja, na si Alfajiri ya ishirini na moja.  

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/160)]

 

Share [21]

17-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Lini Anapaswa Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf Yake?

Lini Anapaswa Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf Yake?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

 

17. Lini Anapaswa Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Anatoka Mu’takif kutoka katika I’tikaaf yake inapomalizika Ramadhwaan, na Ramadhwaan humalizika kwa kuzama jua usiku wa ‘Iyd. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/170)]

Share [22]

18-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kutiya Niyyah I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Ramadhwaan Kisha Kutoka Usiku Wa Mwisho

 

 

Kutiya Niyyah I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Ramadhwaan Kisha Kutoka Usiku Wa Mwisho

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

 

18. Aliyetia Niyyah Kuingia I’tikaaf Makumi Ya Mwisho Katika Ramadhwaan Kisha Akataka Kutoka Usiku Wa Mwisho; Je, Kuna Makosa Juu Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ikiwa hakuwekea nadhiri na kukata kwake ni katika siku ya mwisho au kabla yake, basi hakuna dhambi juu yake. Lakini linalopendekezeka zaidi ni akamilishe ili apate kutekeleza Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani yeye hakuwa akitoka kwenye I’tikaaf yake mpaka iingie mwezi wa Shawwaal.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/184)]

 

Share [23]

19-Imaam Ibn Baaz: Nini Kimpasacho Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake?

 

 

Nini Kimpasacho Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) 

 

www.alhidaaya.com [7]

 

19. Nini Kimpasacho Mu’takif Katika Kutekeleza I’tikaaf Yake?

 

 Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ni juu ya Mu’takif atimize I’tikaaf yake na ajishughulishe na dhikru-Allaah na ‘ibaadah wala asitoke isipokuwa kwa haja anayohitaji mwana Aadam kama kwenda msalani kukojoa na kadhaalika, au akihitaji chakula ikiwa hakupata uwezekano wa mwenye kumtayarishia chakula basi atoke kwa ajili ya haja yake hiyo wala haijuzu kwa mwanamke amwendee mumewe hali ya kuwa yeye mke yuko kwenye I’tikaaf. 

Na kadhaalika Mu’takif haimpasi kumwendea mkewe, na lilo bora kwake ni kwamba asizungumze na watu lakini akiwa ametembelewa na baadhi ya ndugu zake au mwanamke ametembelewa na baadhi ya mahaarim wake akazungumza nao (wanaume) au akazungumza na wanawake wenzake, basi hakuna neno.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/440)]

 

 

Share [24]

20-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?

 

 

Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

20. Yepi Yanayopendekezeka Kwa I’tikaaf?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Yanayopendekeza kwake ni mtu kujishughulisha na utiifu kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) katika kusoma Qur-aan, na dhikru-Allaah, na Swalaah na kadhaalika, na wala asipoteze muda wake katika yasiyokuwa na faida humo.’

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/175)]

 

 

 

Share [25]

21-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?

 

 

Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

21. Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ama kutoka kwake kutoka Masjid, ‘Ulamaa wameigawa katika sehemu tatu:

 

  1. Inafaa: nayo ni kutoka kwa jambo lisokuwa na budi kutendwa linalokubalika ki-shariy’ah mfano kutoka kuswali jamaa’ah au jambo la kimaumbile kama kukidhi haja kama vile kwenda msalani kukojoa na chooni.

 

  1. Kutoka kwa ajili ya utiifu isiyomwajibika kama kumtembelea mgonjwa, au kuhudhuria janaazah basi hiyo ikiwa alijiwekea sharti mwanzo wa I’tikaaf yake, basi haina ubaya. Lakini ikiwa hakujiwekea sharti  basi haipasi.

 

  1. Kutoka katika jambo linalopinga hukmu ya I’tikaaf kama vile kufanya biashara, na kujamiiana na ahli yake na kadhaalika. Haya hayajuzu ikiwa kwa kuweka sharti au kutokuwekea sharti (I’tikaaf yake).

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/157)]

 

Share [26]

22-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?

 

 

 Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

22. Je Inajuzu Kwa Mu’takif Aende Nyumbani Kwake Kwa Ajili Ya Kula Chakula Na Kuoga?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymin (Rahimahu Allaah) amesema:

 

  1. Inajuzu kwa Mu’takif aende nyumbani kwake kwa ajili ya kula chakula ikiwa hakupata mwenye kumtayarishia chakula (au kumletea hapo Msikitini). Lakini ikiwa amepata wa kumtayarishia chakula Msikitini, basi asitoke kwa sababu Mu’takif hatoki isipokuwa kwa jambo ambalo hana budi nalo.

 

  1. Ama kuoga, ikiwa ni kutokana na janaba, basi inamuwajibika atoke, kwa sababu hakuna budi kuwa afanye ghuslu (ajitwaharishe). Lakini ikiwa si kutokana na janaba bali ni kwa ajili ya kujimwagia kujiburudisha kwa kuoga maji baridi, basi asitoke kwa sababu hili ni jambo amejiwajibisha mwenyewe. Lakini ikiwa kwa ajili ya kuondosha harufu inayomtia shaka kubakia kwake basi anaweza kutoka. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]

 

 

Share [27]

23-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?

 

 

Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?

 

 Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

23. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Apige Simu Kukidhi Haja Za Baadhi Ya Waislamu?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

a. Inajuzu kwa Mu’takif kutumia simu kwa ajili ya kuwakidhia haja za Waislamu ikiwa simu iko katika Msikiti ambao anatekeleza I’tikaaf, kwa sababu hatoki nje ya Msikiti.

 

b. Ama ikiwa nje ya Msikiti basi asitoke kwa ajili ya jambo hilo. Na kuwakidhia haja Waislamu ikiwa mtu huyo ndiye mwenye jukumu nao basi asikae I’tikaaf kwa sababu kuwakidhia haja Waislamu kuna umuhimu zaidi kuliko kutekeleza I’tikaaf. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/180)]

 

Share [28]

24-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Inajuzu Kwa Mu’takif Amtembelee Mgonjwa? Au Inamuajibikia Kufanya Da’wah?

 

 

 Inajuzu Kwa Mu’takif Amtembelee Mgonjwa? Au Inamuajibikia Kufanya Da’wah?

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

 

24. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Amtembelee Mgonjwa? Au Inamuajibikia Kufanya Da’wah?

 

Sunnah ni kwamba asitembelee mgonjwa wakati akiwa katika I’tikaaf, wala haiwajibiki da’wah wala kuwakidhia haja ahli zake wala kuhudhuruia janaazah, wala asitoke nje ya Msikiti kwa ajili ya kwenda kazini kwake.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah (10/410)]

 

Share [29]

25-Imaam Ibn Baaz: Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah

Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

25. Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Kwa Ajili Ya Kwenda Kutekeleza ‘Umrah?

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

 

  1. Ikiwa I’tikaaf yake ameiwekea nadhiri kwa wakati maalumu basi inamlazimika kuikamilisha, kwa sababu kutimiza nadhiri ni katika utiifu na jambo la kulazimika.

 

  1. Na ikiwa ni ya kujitolea tu basi akitaka ataikamilisha na akitaka ataikata aende ‘Umrah. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (15/446)]

 

 

Share [30]

26-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Mu’takif Katika Al-Haram Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?

 

Mu’takif Anayekuwa Katika Al-Haram Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

 

26. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Anayekuwa Katika Al-Haram (Makkah) Apande Sakafu Za Juu Kwa Ajili Ya Kusikiliza Duruws?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Kupanda sakafu za juu ya Msikiti hiyo haidhuru kwani kutoka katika mlango wa Msikiti wa chini  kupanda juu kwenye sakafu si chochote bali ni hatua chache, na pia anakusudia kurudi (chini) Msikitini pia. Basi hakuna ubaya katika hili. 

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/181)]

 

Share [31]

27-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?

 

Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

27. Lipi Bora Kwa Mwenye Majukumu; Atekeleze I’tikaaf Au Atimize Majukumu Yake?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

  1. Ikiwa mtu ana majukmu ya ahli zake na ikiwa amewajibika nayo, basi ni waajib kwake kuyatimiza na hivyo basi, kutekeleza I’tikaaf huwa ni dhambi kwake.

 

  1. Na ikiwa si yenye kuwajibika kwake, basi hata hivyo kuyatimiza huwa ni bora kwake kuliko I’tikaaf.

 

  1. Ama mtu aliyekuwa huru, basi I’tikaaf inakuwa ni haki kwake ki-shariy’ah. Lakini ikiwa ana majukumu katika makumi ya mwanzo, lakini kisha akawa huru kisha akataka kutekeleza I’tikaaf masiku yaliyobakia basi hakuna neno.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/178)]

 

 

 

Share [32]

28-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Inajuzu Kwa Mu’takif Abadilishe Sehemu Kuhamahama Ndani Ya Msikiti?

 

Inajuzu Kwa Mu’takif Abadilishe Sehemu Kuhamahama Ndani Ya Msikiti?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

 

28. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Abadilishe Sehemu Kuhamahama Ndani Ya Msikiti?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Inajuzu kwa Mu’takif kbadilisha sehemu katika Msikiti katika pande zozote zile.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/177)]

 

Share [33]

29-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn : Mu’takif Katika Masjid Al-Haraam Afanye Twawaaf Kuzunguka Al-Ka’bah?

 

Mu’takif Katika Masjid Al-Haraam Afanye Twawaaf Kuzunguka Al-Ka’bah?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com [7]

 

29. Je, Inajuzu Kwa Mu’takif Katika Masjid Al-Haraam (Makkah) Afanye Twawaaf Kuzunguka Al-Ka’bah?

 

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:

 

Ikiwa yuko Masjid Al-Haraam afanye Twawaaf, kwa sababu I’tikaaf haimaanishi kwamba mtu agande sehemu moja asibadilishe sehemu, bali maana ya I’tikaaf ni kujiambatanisha na Masjid.

 

 

[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/180)]

 

 

 

Share [34]

31-Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aali Ash-Shaykh: Wanawake Kwenda Masjid Kuswali Taraawiyh Na I´tikaaf

Wanawake Kwenda Msikitini Kuswali Taraawiyh Na I´tikaaf

 

Shaykh ´Abdul-´Aziyz Aali Ash-Shaykh (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com [4]

 

 

SWALI:

 
Je, inajuzu kwa mwanamke ambaye hajaolewa kwenda Msikitini wakati wa futari, kisha abakie Msikitini mpaka ifike wakati wa Taraawiyh? Na je inajuzu kwake kufanya I’tikaaf siku 10 za mwisho Msikitini? 

 

 

JIBU:

 

Lililo asili na bora zaidi ni kuwa Swalaah ya mwanamke aswali nyumbani. Lakini kwenda (mwanamke) Msikitini, kama haitosababisha fitnah inajuzu.

 

Anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):  

"Ikiwa mmoja wenu mke wake atamuomba ruhusa ya kwenda, asimkatalie".

Na anasema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa):

"Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali Swalaatul-Fajr, wakihudhuria naye Swalaah waumini wanawake, wakirudi (majumbani kwao) hakuna aliyekuwa akiwajua kutokana na giza".

 

Kwa hiyo wanaweza kwenda kuswali Msikitini ikiwa kama haitosababisha fitnah, na wajisitiri vizuri, na wasichanganyike na wanaume.

 

Hali kadhalika wanaweza kwenda kufanya I’tikaaf Msikitini kama hakutokuwa fitnah. 

  

 

Share [35]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8390

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8390&title=Fataawaa%3A%20%27Itikaaf%20%28Kubakia%20Msikitini%20Kufanya%20%27Ibaadah%29
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8575&title=01-%20Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Nini%20Maana%20Ya%20%E2%80%98Itikaaf%3F
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8576&title=02-%20Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Nini%20Hukmu%20Ya%20I%E2%80%99tikaaf%3F
[7] http://www.alhidaaya.com/
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8577&title=03-%20Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inafaa%20Ki-Shariy%E2%80%99ah%20Miezi%20Mingineyo%20Isiyokuwa%20Ramadhwaan
[9] http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8393&title=05-Shaykh%20%C2%B4Abdul-Muhsin%20Al-%E2%80%98Abbaad%3A%20Kufanya%20I%C2%B4itikaaf%20Haishurutishwi%20Kuwa%20Na%20Swawm
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8578&title=06-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Je%2C%20Ili%20I%E2%80%99tikaaf%20Iwe%20Sahihi%20Inalazimika%20Mtu%20Awe%20Katika%20Swawm%3F
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8579&title=07-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inajuzu%20Wakati%20Wowote%20Ule%20Nje%20Ya%20Masiku%20Kumi%20Ya%20Mwisho%20Ya%20Ramadhwaan%3F
[13] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8580&title=08-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Ya%20Mwanamke%20Ni%20Sawa%20Na%20Ya%20Mwanaume%3F%20
[14] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8581&title=09-Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Sehemu%20Gani%20Inapaswa%20Kutekelezwa%20I%E2%80%99itikaaf%3F
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8582&title=10-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inajuzu%20Katika%20Masjid%20Al-Haraam%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Wanawake%20Na%20Wanaume%3F
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8583&title=11-Imaam%20Ibn%20Baaz%20na%20Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Je%2C%20I%E2%80%99tikaaf%20Inasihi%20Katika%20Misikiti%20Mingineyo%20Isiyokuwa%20Ile%20Mitatu%3F%20%20
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8584&title=12-Imaam%20Ibn%20Baaz%20%3A%20Mwanamke%20Atekeleze%20Wapi%20I%E2%80%99tikaaf%20Akipenda%20Kufanya%20Hivyo%3F
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8585&title=13-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Vyumba%20Vya%20Matumizi%20Vya%20Masjid%20Vinafaa%20Kutumika%20Kwa%20I%27tikaaf%3F
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8586&title=14-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Zipi%20Nguzo%20Za%20I%E2%80%99tikaaf%20Na%20Sharti%20Zake%3F%20Na%20Je%2C%20Inasihi%20Bila%20Ya%20Swawm%3F
[20] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8587&title=15-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20I%E2%80%99tikaaf%20Ina%20Wakati%20Maalumu%20Katika%20Kuingia%20Na%20Kutoka%20Kwake%20Na%20Je%2C%20Inajzu%20Kuikata%3F
[21] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8588&title=16-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20I%E2%80%99tikaaf%20Inaanza%20Lini%3F
[22] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8589&title=17-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Lini%20Anapaswa%20Mu%E2%80%99takif%20Kutoka%20Katika%20I%E2%80%99tikaaf%20Yake%3F
[23] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8590&title=18-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kutiya%20Niyyah%20I%E2%80%99tikaaf%20Makumi%20Ya%20Mwisho%20Ramadhwaan%20Kisha%20Kutoka%20Usiku%20Wa%20Mwisho
[24] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8591&title=19-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Nini%20Kimpasacho%20Mu%E2%80%99takif%20Katika%20Kutekeleza%20I%E2%80%99tikaaf%20Yake%3F
[25] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8592&title=20-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Yepi%20Yanayopendekezeka%20Kwa%20I%E2%80%99tikaaf%3F
[26] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8593&title=21-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Nini%20Hukmu%20Ya%20Mu%E2%80%99takif%20Kutoka%20Katika%20I%E2%80%99tikaaf%3F%20
[27] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8594&title=22-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Aende%20Nyumbani%20Kwake%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kula%20Chakula%20Na%20Kuoga%3F
[28] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8595&title=23-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Apige%20Simu%20Kukidhi%20Haja%20Za%20Baadhi%20Ya%20Waislamu%3F
[29] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8596&title=24-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Amtembelee%20Mgonjwa%3F%20Au%20Inamuajibikia%20Kufanya%20Da%E2%80%99wah%3F
[30] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8597&title=25-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Hukmu%20Ya%20Mu%E2%80%99takif%20Kutoka%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kwenda%20Kutekeleza%20%E2%80%98Umrah
[31] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8598&title=26-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Mu%E2%80%99takif%20Katika%20Al-Haram%20Apande%20Sakafu%20Za%20Juu%20Kwa%20Ajili%20Ya%20Kusikiliza%20Duruws%3F
[32] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8599&title=27-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Lipi%20Bora%20Kwa%20Mwenye%20Majukumu%3B%20Atekeleze%20I%E2%80%99tikaaf%20Au%20Atimize%20Majukumu%20Yake%3F%20
[33] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8600&title=28-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Inajuzu%20Kwa%20Mu%E2%80%99takif%20Abadilishe%20Sehemu%20Kuhamahama%20Ndani%20Ya%20Msikiti%3F%20
[34] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8601&title=29-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%20%3A%20Mu%E2%80%99takif%20Katika%20Masjid%20Al-Haraam%20Afanye%20Twawaaf%20Kuzunguka%20Al-Ka%E2%80%99bah%3F
[35] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8394&title=31-Shaykh%20%C2%B4Abdul-%C2%B4Aziyz%20Aali%20Ash-Shaykh%3A%20Wanawake%20Kwenda%20Masjid%20Kuswali%20Taraawiyh%20Na%20I%C2%B4tikaaf