Kuongeza Rakaah Moja Baada Ya Imaam Kumaliza Witr
Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Kuna watu wengine wanaposwali Witr na Imaam na anapotoa salaam wanainuka na kuswali Raka'ah moja nyingine, kwa sababu wanataka kuswali zaidi kabla ya kuswali Witr baadaye usiku. Nini hukumu ya kufanya hivi? Je, Inahesabika kuwa amekwenda kinyume na Swalah pamoja na Imaam?
JIBU:
Hatuoni ubaya wowote kufanya hivyo, na ‘Ulamaa wamesema pia hakuna ubaya kufanya hivyo ili Swalaah yake ya Witr iwe ndiyo Swalaah ya mwisho usiku. Atahesabika kuwa ameswali na Imaam mpaka kamaliza kwa sababu amekaa naye hadi kamaliza kisha ndio kaongeza Raka'ah moja kwa sababu inayokubalika katika Shariy’ah ili apate kuswali tena baadaye usiku. Wala haimaanishi kwamba hakubakia na Imaam mpaka mwisho lakini hakumaliza tu naye na kaichelewesha kidogo.
[Imaam ‘Abdul-‘Aziyz bin Baaz -Al-Jawaab As-Swahiyh min Ahkaam Swalaat Al-Layl Wat-Taraawiyh - Uk. 41]
Kushika Mswahafu Katika Swalaah Ya Taraawiyh Kumfuatilizia Imaam
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukumu ya kukamata Msahafu ili kumfuatiliza Imaam anayewalisha Swalah ya Taraawiyh katika Ramadhaan?
JIBU:
1. Kushika Msahafu ni kinyume na Sunnah kwa sababu nyingi:
2. Inamzuia mtu kuweza kuweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto
3. Inasababisha harakati nyingi kama kufungua Msahafu, kufunga na kuuweka chini ya kwapa.
4. Harakati hizo zinawashawishi wanaoswali naye.
5. Inamzuia mwenye kuswali kutazama sehemu ya kusujudu. 'Ulamaa wengi wameona na kusema kuwa kutazama sehemu ya kusujudu ni Sunnah na bora.
6. Anayefanya hivyo (kushika Msahafu) huenda akasahau kama yuko katika Swalah isipokuwa ikiwa moyo wake umenyenyekea katika Swalah, kwani bila ya kushika Msahafu, kusimama kwake kunakuwa kwa unyenyekevu kutokana na kuweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto, akiinamisha kichwa chake kutazama sehemu ya kusujudu. Hivi humsababisha kumkumbusha kuwa yuko katika Swalah na yuko na Imaam.
[Gazeti la Da'awah Nambari 1771 – Ukurasa 45]
Imaam Kutoa Mawaidha Baina Ya Swalaah Za Taraawiyh
Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, inajuzu kwa Imaam wa Masjid ambaye anaswalisha watu katika Tarawiyh kuwakumbusha watu wakati wa mapumziko na kuzungumzia juu ya Swalaah na juu ya kumfuata Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwaonya baadhi ya watu wa bid’ah na washirkina?
JIBU:
Yote ni sawa.
Ikiwa kama ni tukio limetokea, ni waajib kufanya hivyo.
Ikiwa ni ada (Imaam) kuonya watu kila baada Raka’ah na mfano wake, hii ni kinyume na Manhaj ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
[Silsilatul-Hudaa Wan-Nuwr (656)]
Mwanamke Kwenda Kuswali Tarawiyh Kwa Kuvunja Amri Ya Mumewe
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke akitoka kwenda kuswali Taraawiyh msikitini na mumewe hayuko radhi naye, kwani alimwambia aswali nyumbani atapata thawabu; je, Swalaah yake imesihi?
JIBU:
Tunamuambia mume usimzuie mkewe kwenda kuswali msikitini kwani Nabiy amekataza hivyo. Amesema: ((Msiwakataze wanawake kwenda katika nyumba za Allaah)) [Muslim]
Na tunamwambia mke: “Mtii mume wako maana bila shaka amekukataza kwa maslaha au khofu ya fitnah kama alivyosema kuwa Swalaah yako nyumbani ni bora kuliko msikitini kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Na nyumba zao ni bora kwao))”
[Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)]
Kuswali Taraawiyh Ramadhwaan Ni Lazima Aswali Mwezi Mzima?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Anayeanza kuswali Taraawiyh inampasa aendelee nayo Ramadhwaan nzima? (Au anaweza kuswali na kuacha?)
JIBU:
La! Si lazima aendelee nayo mwezi mzima kwa sababu ni Sunnah iliyosisitizwa ambayo akiswali atapata thawabu na akiacha hatokuwa na dhambi. Lakini kwa kuacha kuswali atakosa thawabu nyingi kama tulivyobainisha kabla.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fataawaa Ramadhwaan Mjalada 2, Uk 837 Fataawaa 831, Fiqh Al-'Ibadaat libni 'Uthaymiyn Uk. 205-206]
Tofauti Ya Taraawiyh, Qiyaamul-Layl Na Tahajjud
Imaam Bin Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Ipi tofauti kati ya Taaraawiyh, Qiyamul-Layl naTahajjud?
JIBU:
Swalah ya usiku huitwa Tahajjud na huitwa Qiyamul-Layl kama Anavyosema. Allaah (Ta'aalaa):
وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾
Na katika usiku, amka uswali nayo (tahajjud) ni ziada ya Sunnah kwako. Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa 17: 79]
Na Anasema (Subhaanahu):
يَا أَيُّهَا الْمُزَّمِّلُ﴿١﴾
Ee uliyejifunika. [Al-Muzzammil 73: 1-2]
Na Anasema (Subhaanahu) katika Suwrah Adh-Dhaariyaat kuhusu waja wenye taqwa:
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ﴿١٦﴾
Wakichukua yale Atakayowapa Rabb wao. Hakika wao walikuwa kabla ya hapo ni wahisani.
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ﴿١٧﴾
Walikuwa kidogo tu katika usiku wakilala kwa raha. [Adh-Dhaariyaat 51: 16-17]
Ama kuhusiana na Taraawiyh, ‘Ulamaa wanaiita Qiyamul-Layl katika ile sehemu ya kwanza ya usiku katika Ramadhwaan kwa ajili yake, kwa kuwa Swalaah hii haiswaliwi kwa muda mrefu tena. Na inajuzu kuiita Tahajjud au Qiyamul-Layl wala hakuna shaka katika hilo.
[Al-Mawqi' Ar-Rasmiy - Imaam ‘Abdul-‘Aziyz Bin Baaz] [11]
Tofauti Ya Taraawiyh Na Qiyaam Na Kurefusha Katika Siku Kumi Za Mwisho
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)
www.alhidaaya.com [13]
SWALI:
Je, kuna tofauti baina ya Taraawiyh na Qiyaam? Na je kuna dalili za kufanya makhsusi (Swalaah) katika kumi la mwisho kwa kurefusha Qiyaam, na rukuu na sujuwd?
JIBU:
Swalaah zote hizo katika Ramadhwaan zinaitwa “Qiyaam” kama alivyosema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ
“Atakayesimama Ramadhwaan kwa iymaan na kutaraji malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia.”
[Ahmad katika Musnad ndani ya ‘Baaqiy Musnad Al-Mukthiriyn’ (7729) na Al-Bukhaariy katika ‘Baab Al-Iymaan’ (37)]
Basi atakaposimama pamoja na Iymaan kiasi atakachowepesishiwa, inaitwa: “Qiyaam”.
Lakini katika (masiku) kumi ya mwisho, inapendekezwa kurefusha kwa sababu imewekwa katika shariy’ah kuhuisha usiku kwa Swalaah na Qiraa (cha Qur-aan) na du’aa kwa vile Rasuli (‘Alayhis-Swalaatu was-Salaam) alikuwa akihuisha usiku wote katika (masiku) kumi ya mwisho, na kwa hivyo ikawa ni shariy’ah kurefusha ndani yake (ndani ya masiku hayo) kama alivyorefusha Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Hakika yey alikuwa akisoma katika baadhi ya usiku Al-Baqarah, na An-Nisaa na Aal-‘Imraan katika rakaa moja.
Kwa hiyo kusudio ni kwamba (‘Alayhis-Swalaatu was-Salaam) alikuwa akirefusha (Swalaah) katika kumi la mwisho na akikesha ndipo ikawekwa shariy’ah kwa watu kukesha na kurefusha humo ili kumuiga (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kinyume na (masiku) ishirini ya mwanzo, ambapo Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa akikesha, bali alikuwa akisimama Qiyaam na akilala (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyokuja katika Hadiyth.
Ama katika kumi za mwisho, alikuwa (‘Alayhis-Swalaatu was-Salaam) akikesha usiku wote na akiamsha ahli zake na akikaza izaar kikoi chake (akizidisha mkazo mkubwa) (‘Alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa sababu humo (katika masiku kumi hayo ya mwisho) kuna usiku uliobarikiwa, Laylatul-Qadr.
[Fataawa Ibn Baaz] [14]
Kuswali Taraawiyh Nyumbani Ni Bora Au Kuiswali Msikitini?
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaahu)
www.alhidaaya.com [13]
SWALI:
Kuna miongoni mwa Twulaabul-'Ilm anasema kuwa kuiswali Swalaah ya Taraawiyh nyumbani ni bora zaidi kuliko kuiswali Msikitini. Akitolea ushahidi Hadiyth isemayo, "Swalaah ya Naafilah nyumbani ni bora kuliko Msikitini kwa daraja ishirini na tano. Anasema kuwa Swalaah ya Taraawiyh ni Naafilah na ndio kauli ya Imaam Maalik. Hili ndilo analolieleza wanafunzi. Je, yepi maoni yako?
JIBU:
Hili ni kosa.
Hili ni kosa kubwa, linakwenda kinyume na uongofu wa Salafus-Swaalih.
(Salafus-Swaalih) Walikuwa wakikusanyika Misikitini wakiswali Taraawiyh. Taraawiyh ni nembo iliyo dhahiri katika Shariy´ah za Dini. Iswaliwe Msikitini.
Kuiswali Msikitini ni bora kuliko kuiswali nyumbani. Hata kama kuiswali nyumbani inajuzu, lakini kuiswali Misikitini na kudhihirisha nembo hii na kuwa pamoja na Waislamu ni bora.
Tofauti Baina Ya Swalaah Ya Taraawiyh Na Swalaah Ya Qiyaam
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
www.alhidaaya.com [13]
SWALI:
Nini Tofauti Ya Swalaah Ya Taraawiyh Ambayo ni baada ya Swalaah ya ‘Ishaa na Swalaah Ya Qiyaam Ambayo ni mwisho wa Usiku katika Ramadhwaan
JIBU:
Hakuna tofauti baina ya hizo mbili.
Swalaah ya Taraawiyh ima ni mwanzo wa usiku au mwisho wa usiku.
Lakini katika masiku ya mwisho ya Ramadhwaan, watu wanapenda kukesha usiku kufuata mwendo wa Rasuli (‘Alayhis-Swalaatu was-Salaam) kwa sababu alikuwa akiuhuisha usiku mzima katika masiku kumi ya mwisho.
Na kwa ajili hiyo, ndio (watu) wakakifanya Qiyaamu (kisimamo cha usiku) kuwa ni mwisho wa usiku.
Na Swalaah khafifu ambayo inaitwa Taraawiyh (huwa wanaiswali) mwanzo wa usiku. Na wala hakuna ubaya (kufanya) hivyo (kuswali mara mbili usiku kwa kuiswali moja mapema baada ya ‘Ishaa, na nyingine mwisho wa usiku).
[Silsilat Liqaat Al-Baab Al-Maftuwh, 107]
Bid’ah Za Ramadhwaan: Kumdhukuru Allaah Kila Baada Ya Rakaa Za Taraawiyh
Al-Lajnah Ad-Daaimah
Adkhaar au kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa pamoja baada ya kila Swalaah ya fardhi au Naafilah (Sunnah ya ziada) au baina ya Rakaa za Taraawiyh ni bid’ah ya kuzushwa na imethibiti kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema:
((Atakayezusha katika jambo letu hili (Dini yetu) ambalo halimo basi litarudishwa))
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (2529)]
Taraawiyh Au Qiyaam Kuswali Baada Ya 'Ishaa Na Usiku
Katika Makumi Ya Mwisho
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
www.alhidaaya.com [13]
Katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan, Waislamu huongeza juhudi katika ‘ibaadah wakifuata muongozo wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuitafuta Laylatul-Qadr ambayo ni bora kuliko miezi elfu.
Wanaoswali rakaa ishirini na tatu mwanzo wa mwezi, huzigawa Swalaah katika masiku kumi ya mwisho ili waswali rakaa kumi mwanzo wa usiku (baada ya ‘Ishaa) ambayo inaitwa Taraawiyh. Kisha huswali kumi zingine usiku wa manane, huku wakizirefusha na kufuatilia rakaa tatu za Witr ambazo wanaziita (hiyo Swalaah ya usiku wa manane) ni Qiyaam.
Hayo majina ya Swalaah hizo ni kuzitofautisha tu. Lakini ukweli ni kwamba zote zinaweza kuitwa Taraawiyh au kuitwa Qiyaam.
Ama wale wanaoswali rakaa kumi na moja au kumi na tatu mwanzo wa usiku, huzidisha rakaa kumi katika masiku kumi ya mwisho ambayo huswali usiku wa manane, huku wakizirefusha na kutafuta fadhila za masiku kumi ya mwisho kwa kuongeza juhudi kufanya mema, kwa kufuata waliotangulia katika Maswahaba na wengineo walioswali rakaa ishirini na tatu kama ilivyotajwa juu. Hivyo basi wanajumuisha rai mbili; Rai yenye kupendekeza kuswali rakaa kumi na tatu katika masiku ishirini ya mwanzo. Na Rai yenye kupendekeza kuswali rakaa ishirini na tatu katika masiku kumi ya mwisho.
[It-haaf Ahlil-Iymaan bi Majaalisi Shahri Ramadhwaan]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8416&title=Fataawaa%3A%20Qiyaam%20Al-Layl%3A%20Tarawiyh%20Tahajjud%20Witr
[4] http://www.alhidaaya.com
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8423&title=01-Imaam%20Bin%20Baaz%3A%20Kuongeza%20Rakaah%20Moja%20Baada%20Ya%20Imaam%20Kumaliza%20Witr
[6] http://www.alhidaaya.com
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8425&title=02-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kushika%20Msahafu%20Katika%20Swalaah%20Ya%20Taraawiyh%20Kumfuatilizia%20Imaam
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8426&title=03-Imaam%20Al-Albaaniy%3A%20Imaam%20Kutoa%20Mawaidha%20Baina%20Ya%20Swalaah%20Za%20Taraawiyh
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8427&title=04-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Mwanamke%20Kwenda%20Kuswali%20Taraawiyh%20Kwa%20Kuvunja%20Amri%20Ya%20Mumewe
[10] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8430&title=07-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kuswali%20Taraawiyh%20Ramadhwaan%20Ni%20Lazima%20Aswali%20Mwezi%20Mzima%3F
[11] http://www.binbaz.org.sa/fatawa/1019
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8431&title=08-Imaam%20Bin%20Baaz%3A%20Tofauti%20Ya%20Taraawiyh%2C%20Qiyaamul-Layl%20Na%20Tahajjud%20%20
[13] http://www.alhidaaya.com/
[14] http://www.binbaz.org.sa/fatawa/1033
[15] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8561&title=09-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Tofauti%20Ya%20Taraawiyh%20Na%20Qiyaam%20Na%20Kurefusha%20Katika%20Siku%20Kumi%20Za%20Mwisho
[16] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8563&title=10-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Kuswali%20Taraawiyh%20Nyumbani%20Ni%20Bora%20Au%20Kuiswali%20Msikitini%3F
[17] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8564&title=11-Imaam%20Ibn%20%27Uthaymiyn%3A%20Tofauti%20Ya%20Swalaah%20Ya%20Taraawiyh%20Na%20Swalaah%20Ya%20Qiyaam
[18] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8565&title=12-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Bid%E2%80%99ah%20Za%20Ramadhwaan%3A%20Kumdhukuru%20Allaah%20Kila%20Baada%20Ya%20Rakaa%20Za%20Tarawiyh
[19] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8566&title=13-Shaykh%20Swaalih%20Al-Fawzaan%3A%20Taraawiyh%20Au%20Qiyaam%20Kuswali%20Baada%20Ya%20%27Ishaa%20Na%20Usiku%20Katika%20Makumi%20Ya%20Mwisho