Alijimai Bila Ya Kujua Kwamba Alfajiri Imeingia Akaendelea Na Swawm
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Alifanya jimai na mkewe katika masaa ya mwisho ya usiku akidhania kuwa wakati wa Alfajiri bado haujaingia. Lakini, baada ya kumaliza, katoka chumbani na kutambua kuwa amefanya kitendo hicho baada ya Alfajiri kuingia. Amesikitika na akaendelea na Swawm. Lakini anahisi kuwa amefanya dhambi na anauliza nini kinachompasa kufanya kuhusu kufanya kitendo hiki baada ya Alfajiri kuingia?
JIBU:
Kama hali ilikuwa kama ilivyotajwa, basi anatakiwa alipe siku hiyo kama ana hakika kuwa alifanya jimai baada ya kutakiwa ajiepushe na mambo yanayovunja Swawm baada ya kuingia Alfajiri. Na akishalipa siku hiyo, anatakiwa aache huru mtumwa mmoja aliye Muumini. Na ikiwa hawezi basi afunge miezi miwili mfululizo (bila ya kupumzika) na ikiwa hawezi basi alishe masikini sitini (60) au watu wanaohitaji kwa sababu ya dharau yake ya kufanya kitendo hicho bila ya kuhakikisha wakati wa Alfajiri kuingia. Na mke naye anatakiwa kulipa hivyo hivyo isipokuwa ikiwa alilazimishwa kufanya kitendo hicho cha ndoa na mumewe.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa 615, Fatwa Namba 612; Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah lil-Buhuwth Al-'Ilmiyyah Wal-Iftaa - Fatwa Namba 10676]
Kafara Ngapi Ikiwa Amejimai Zaidi Ya Mara Moja Kwa Siku Moja Ramadhwaan
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Ikiwa mtu amejimai (kitendo cha ndoa) zaidi ya mara moja katika siku moja ya Ramadhwaan, Je, Anatakiwa alipe kafara mara zile zile sawa na kitendo cha jimai?
JIBU:
Inavyofahamika katika madhehebu ya Imaam Ahmad ni kwamba ikiwa mtu amejimai zaidi ya mara moja kwa siku moja katika Ramadhwaan basi kafara moja tu inatosheleza. Lakini kama kajimai katika siku mbili za Ramadhwaan (au zaidi ya siku mbili) basi inampasa alipe kafara sawa na siku alizojimai kwa sababu kila siku moja ni tofauti na nyingine (kwa hiyo kila siku moja ni kafara moja).
[Imaam Ibn ‘Uthyamiyn - Fataawaa Ramadhwaan - Mjalada 2, Ukurasa 608, Fatwa Namba 601-Fiqh al-'Ibaadaat]
Hukmu Ya Kujimai Mchana Wa Ramadhwaan
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Nini hukmu ya aliyejimai (kitendo cha ndoa) na mkewe mchana wa Ramadhwaan?
JIBU:
Ikiwa wote walikuwa wako katika udhuru wa kutokuwa katika swawm; mfano kama walikuwa safarini, hakuna ubaya hivi hata kama wote walikuwa katika swawm. Lakini ikiwa walikuwa katika hali ya kuwajibika swawm, basi ni haraam kwao wote na wanatakiwa walipe siku hiyo, na juu yake kafara nayo ni kuachia huru mtumwa, na kama hawawezi basi wafunge miezi miwili mfululizo (bila ya kukatiza), na ikiwa hawawezi kufanya hivi basi walishe masikini sitini au watu wanaohitaji.
Kufanya hivyo inawapasa wote wawili kila mmoja afanye sehemu yake. Lakini kama mke alilazimishwa kufanya kitendo hicho basi yeye haimpasi kulipa kafara.
[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn - Fataawa Ramadhwaan – Mjalada 2, Ukurasa 606, Fatwa Namba 597 - Fataawa Imaam Ibn 'Uthaymiyn –Mjalada 1, Ukurasa 541-542]
Mke Alipe Kafara Ikiwa Alijimai Na Mumewe Siku Za Ramadhwaan?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Mtu alijimai (kitendo cha ndoa) na mkewe katika siku ya Ramadhwaan na kwa hivyo akafunga swiyaam kama ni kafara miezi miwili mfululizo. Sasa mkewe anatakiwa kufanya lolote? Allaah Akulipeni.
JIBU:
BismiLLaah. Himdi zote ni za Allaah Pekee.
Yale yale yanayompasa yeye mke ni sawa na yanayompasa mumewe ikiwa alifanya kitendo hicho kwa pendekezo lake mwenyewe na hakulazimishwa.
Na ikiwa ni shida kwake swiyaam ya miezi miwili mfululizo, basi alishe masikini sitini au kuwalisha wanaohitaji. Kila mmoja amlishe pishi moja (sawa na vibaba vinne au 3kg) .
Lakini kama alilazimishwa na kupigwa basi hatakiwi kulipa lolote na dhambi zitakuwa ni za mume pekee. Lakini kama alifanya kwa mapendekezo basi anatakiwa alipe kafara sawa sawa na mumewe.
[Imaam Ibn Baaz - Fataawaa Ramadhwaan – Mjalada 2, Ukurasa 610, Fatwa Namba 605 -Majmuw' Fataawaa libni Baaz - Mjalada 3, Ukurasa 200]
Kula Kusudi Na Kujamiana Mchana Wa Ramadhwaan
Imaam An-Nawawiy (Rahimahu-Allaah)
SWALI:
Je, mtu ambaye anakula kwa kukusudia mchana wa Ramadhwaan ni waajib kwake kulipa kaffaarah?
Je, mtu ambaye kwa kusudi anamuingilia mke wake mchana wa Ramadhwaan alipe kafara? Na kama alimuingilia mara kadhaa wakati wa Ramadhwaan, anapaswa kulipa kaffaraah mara kadhaa?
JIBU:
Kuhusiana na kafara (ya kula kwa makusudi mchana wa Ramadhwaan) halazimiki kulipa kafara. Hata hivyo anapata madhambi na analazimika kulipa siku iliyobaki. Hali kadhalika anapaswa kulipa siku alizofanya hivyo na kufanya tawbah.
Ama kuhusiana masuala ya kumuingilia mke, analazimika kulipa kafara kwa ile mara ya kwanza ya kumuingia mke na si lazima kwa kila mara (kwa siku hiyo aliyofanya tendo hilo).
Na Allaah Anajua zaidi.
[Imaam Abuu Zakariyyah An-Nawawiy - Fataawaa Imaam An-Nawawiy, uk. 55]
Mume Na Mke Wameingiliana Mchana Wa Ramadhwaan Kwa Kuridhiana
Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-‘Abaad (Hafidhwahu-Allaah)
SWALI:
Mwanamke ambaye mumewe amemuingilia (mchana wa) Ramadhwaan naye yuko radhi. Nini hukmu yake mwanamke huyo?
JIBU:
Ni juu yake mwanamke kulipa kafara na mumewe pia mfano wake (alipe kafara).
[Fataawaa Shaykh 'Abdul-Muhsin Al-‘Abaad [10]]
Mwanaume Ambaye Kalazimishwa Kujima Na Mkewe Katika Ramadhwaan
Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiyy (Rahimahu-Allaah)
Ikiwa mwanaume atalazimishwa kujimai, basi Swawm yake inabatilika, na pia Swawm ya mwanamke inavunjinka kwa sababu ya jimai. Swawm ya mwanaume ni aula zaidi kubatilika kwa sababu hiyo hiyo.
Kuhusiana na kafara anasema Al-Qaadhwiy:
"Ni waajib kwake kulipa kafara, kwa sababu haiwezekani (kwa mwanaume) kalazimishwa jimai. Mwanaume hawezi kufanya jimai bila kwanza ya dhakari yake kusimama, na dhakari kusimama inasababishwa na matamanio. Kwa hali hiyo haonelei kabisa kuwa (mwanaume) alilazimishwa.
Abul-Khattwaab anasema: "Kuna mapokezi mawili. Moja inasema kuwa si lazima kwake kulipa kafara."
Hii pia ni kauli ya Ash-Shaafi'iy. Suala zima la kafara ni ili imtakase mtu kwa madhambi yake. Kwa hivyo haihusiani na mtu kulazimishwa, kwa kuwa mtu anakuwa hana makosa. Hata hivyo anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Ummah wangu umesamehewa makosa ya mtu kusahau na kulazimishwa."
Vile vile Shariy'ah haijataja kuwa analazimika kutoa kafara.”
Ibn ‘Aqiyl kasema mwanaume ambaye amelala (huku) dhakari yake imesimama, mke wake akaiingiza tupu wake kwake (kwa mumewe aliyelala): "Hatalazimika kulipa siku hiyo wala kulipa kafara”
[Imaam Ibn Qudaamah Al-Maqdisiyy - Al-Mughniy (4/377)]
Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/261
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/
[3] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8452&title=Fataawaa%3A%20Kafara%20Ya%20Jimai%20Ramadhwaan
[4] http://www.alhidaaya.com/
[5] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8501&title=01-Al-Lajnah%20Ad-Daaimah%3A%20Alijimai%20Bila%20Ya%20Kujua%20Kwamba%20Alfajiri%20Imeingia%20Akaendelea%20Na%20Swawm
[6] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8502&title=02-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Kafara%20Ngapi%20Ikiwa%20Amejimai%20Zaidi%20Ya%20Mara%20Moja%20Kwa%20Siku%20Moja%20Ramadhwaan%20
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8503&title=03-Imaam%20Ibn%20%E2%80%98Uthaymiyn%3A%20Hukmu%20Ya%20Kujimai%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan
[8] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8505&title=05-Imaam%20Ibn%20Baaz%3A%20Mke%20Alipe%20Kafara%20Ikiwa%20Alijimai%20Na%20Mumewe%20Siku%20Za%20Ramadhwaan%3F
[9] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F10015&title=07-Imaam%20An-Nawawiy%3A%20Kula%20Kusudi%20Na%20Kujamiana%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan
[10] http://www.alharamain.gov.sa/
[11] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8508&title=08-Shaykh%20%E2%80%98Abdul-Muhsin%20Al-%E2%80%98Abaad%3A%20Mume%20Na%20Mke%20Wameingiliana%20Mchana%20Wa%20Ramadhwaan%20Kwa%20Kuridhiana
[12] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8509&title=09-Imaam%20Ibn%20Qudaamah%20Al-Maqdisiyy%3A%20Mwanaume%20Ambaye%20Kalazimishwa%20Kujima%20Na%20Mkewe%20Katika%20Ramadhwaan