05-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: Vikao Vya ‘Ilmu Huteremkiwa Utulivu, Hufunikwa Rahma, Malaika Huwazunguka Na Allaah Huwataja
Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa
Hadiyth Ya 05
Vikao Vya ‘Ilmu Huteremkiwa Utulivu, Hufunikwa Rahma,
Malaika Huwazunguka Na Allaah Huwataja
عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال مَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Abu Huraryah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: Hawajumuiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakasomeshana baina yao ila watateremkiwa na As-Sakiynah (utulivu) na itawafunika rahmah, na Malaika watawazunguka, na Allaah Atawataja kwa walio Naye. [Muslim]
