06-Hadiyth: Fadhila Za 'Ilmu Na 'Ulamaa: ‘Ilmu Ni Kama Mfano Wa Ardhi Yenye Rutuba Inayonufaisha Watu

 

Hadiyth: Fadhila Za ‘Ilmu Na ‘Ulamaa

 

Hadiyth Ya 06

 

‘Ilmu Ni Kama Mfano Wa Ardhi Yenye Rutuba Inayonufaisha Watu

 

Alhidaaya.com

 

 

 عَنْ أَبِي مُوسَى، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَثَلُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ مِنَ الْهُدَى وَالْعِلْمِ كَمَثَلِ الْغَيْثِ الْكَثِيرِ أَصَابَ أَرْضًا، فَكَانَ مِنْهَا نَقِيَّةٌ قَبِلَتِ الْمَاءَ، فَأَنْبَتَتِ الْكَلأَ وَالْعُشْبَ الْكَثِيرَ، وَكَانَتْ مِنْهَا أَجَادِبُ أَمْسَكَتِ الْمَاءَ، فَنَفَعَ اللَّهُ بِهَا النَّاسَ، فَشَرِبُوا وَسَقَوْا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَتْ مِنْهَا طَائِفَةً أُخْرَى، إِنَّمَا هِيَ قِيعَانٌ لاَ تُمْسِكُ مَاءً، وَلاَ تُنْبِتُ كَلأً، فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقِهَ فِي دِينِ اللَّهِ وَنَفَعَهُ مَا بَعَثَنِي اللَّهُ بِهِ، فَعَلِمَ وَعَلَّمَ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأْسًا، وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللَّهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ ‏"‏‏.‏ قَالَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ قَالَ إِسْحَاقُ وَكَانَ مِنْهَا طَائِفَةٌ قَيَّلَتِ الْمَاءَ‏.‏ قَاعٌ يَعْلُوهُ الْمَاءُ، وَالصَّفْصَفُ الْمُسْتَوِي مِنَ الأَرْضِ‏.‏

Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia:  Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mfano wa mwongozo na ‘Ilmu Aliyonituma nayo Allaah ni kama mvua nyingi iliyonyesha juu ya ardhi, kukawa katika hiyo ni ardhi safi ilisharaba maji (ilinyonya mvua) na kuotesha mimea na nyasi nyingi. Na sehemu nyingine ilikuwa ngumu ikazuia maji, na Allaah Akawafaidisha nayo watu, na wakayanywa, wakanywesha (wanyama wao) na wakamwagilia mashamba. (Na) mvua ikanyeshea sehemu nyingine iliokuwa jangwa ambao hakuweza kubeba maji wala kuotesha majani. Huo ni mfano wa mtu aliyefahamu Dini ya Allaah na akapata manufaa (kutokana na ‘Ilmu) ambayo Allaah Amenituma nayo, kwa hiyo akajua na kuwafundisha wengine. Na Mfano wa yule ambae hakuinua kichwa chake kwa ajili ya hilo (mwongozo wa Allaah) na wala hakukubali mwongozo wa Allaah ambao nimetumwa nayo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

 

Share