Kutumia Kitu Kujitoa Matamanio Nini Hukmu Yake
SW
asalam alaikum ndugu waislamu, nimetumwaga na mwislamu niwaulize, je mtu akiwa mbali na mchumba wake, alafu akatamani kufanya tendo la ndoa, alafu akachukua kitu akaweka katikati ya miguu kwenye tupu lake bila kuingiza ndani, mpaka akahisi ile haja yakufanya tendo la ndoa ina malizika na akatokwa na manii; hicho kitendo ni haramu? na anatakiwa kuoga janaba?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako
Kuhusu mas-ala haya Allaah Aliyetukuka Anatuambia:
"Na ambao tupu zao wanazilinda. Isipokuwa kwa wake zao au kwa wanawake wale iliyowamiliki mikono
Aayah ya saba inayosema:
"Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka (ya Allaah)" ni ibara ya jumla ambayo inajumlisha kutekeleza matamanio kinyume na ile njia ya ndoa (yaani mume kufanya kitendo cha ndoa na mkewe kwa njia ile moja. Inaingia hapa zinaa, liwati na kujichua au njia nyingine mfano ni ile uliyoitaja.
Kuhusu hili Sa'iyd bin Jubayr, ambaye ni Tabii' mcha Mungu, mwanachuoni amesema: "Allaah Atauadhibu Ummah kwa kuchezea nyuchi zao (tupu za mbele". Na imepokewa pia: "Watu saba Allaah Hatawaangalia … akawahesabu miongoni mwao: mwenye kuoa mkono wake (kupiga punyeto" (Sh. Muhammad al-Haamid, Ruduud 'alaa Abaatwyil, uk. 40).
Kwa muhtasari ni kuwa kitendo hicho unachofanya ni haramu katika Uislamu. Kwa hiyo, nasaha yetu kwako ni kuwa ni wajibu kwako kuoa au kuolewa. Hakika ibara uliyoitumia niko mbali na mchumba wangu ina utata kwani katika Uislamu huwezi kufanya tendo la ndoa na mchumba wako kwani hajakuwa ni mkeo au mumeo. Ila ikiwa umemaanisha kwa ibara mchumba ni kuwa tayari umemuoa au umeolewa naye, na ni wako wa halali. Na ikiwa ni mkeo au mumeo wa halali basi ni vyema pale ulipo umchukue mumeo au mkeo ili usipate shida uliyo nayo.
Ama ikiwa umefanya kitendo hicho cha madhambi mwanzo unatakiwa umuombe msamaha Allaah Aliyetukuka, ujute na uazimie kutorudia tena. Na lau katika kufanya kitendo hicho utatokwa na manii basi itabidi ili uweze kufanya Ibaadah tofauti uoge josho la janaba.
Pia soma katika kiungo hiki upate kuyajua masuala hayo kwa upana zaidi:
Nini Hukumu Ya Kujichua Sehemu Za Siri Au Kujisaga?
Tunatumai kuwa umeelewa mas-ala hayo vizuri.
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


