Ewe Nafsi Mche Mola Wako
‘Abdun-Naaswir Hikmany
Ewe nafsi mche Mola wako kabla ya kufika mbele ya Hisabu. Utataka ardhi ipasuke ujifukie wala hutaweza, utahitaji kuitenganisha nafsi na umbo lako hutapatiwa nafasi hiyo na wala hutaonja mauti wala uhai. Ni adhabu juu ya adhabu.
Nafsi huwezi kuhimili vishindo vya siku hiyo, basi ni kwanini unamuasi Mola wako? Ni kwa neema gani ambayo Mola wako kakunyima? Nafsi tubu kabla ya siku isiyoshikika wala isiyo na msamaha haijakufikia.
Nafsi unahadaika na dunia? Ni kwa kipi ambacho kinakuhadaa ndani ya dunia hii? Vyote hivyo ni pumba zitakazokuja kupeperushwa, sio
Ewe nafsi, utakuja kulaumu siku ambayo haitafaa lawama, umshike Ibilisi na akakuruka mita alfu juu. Nafsi tubia kwa Mola wako kabla ya kaburi halijakubinya, mbavu zako za kushoto na kulia zikakutanishwa pamoja!
Rehema za Mola zisizo na kifani kutwa zakumurika, nazo ndizo zinazokupelekea kutomuasi Mola wake. Ewe nafsi unapojiweka mbali na rehema hizi, naye Muumbaji Anajiweka mbali na wewe, ni hasara iliyoje kujiweka mbali na rehema za Yule Ambaye nafsi yako imo Mikononi Mwake.
Ndani ya Suratu-Yuusuf tunakutana na kisa maarufu cha mke wa Mheshimiwa kumhadaa Nabii Yuusuf, naye mwisho alikiri kwamba nafsi ndiyo iliyompotosha isipokuwa ile ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Ameirehemu. Tafsiri ya aya hiyo ni
{{Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu, isipokuwa ile ambayo Mola wangu Aliyoirehemu.}} [Suratu-Yuusuf: 53]
Nafsi zote ni zenye kukosa, na mbora wa mwenye kukosa ni yule ambaye atarudi kwa Mola wake. Ikamate nafsi yako na uzungumze nayo asubuhi, mchana na usiku. Hiyo ni nafsi ambayo itakuja kuwa ni adui yako namba moja Siku ya Qiyaamah.
Basi elekea kwa Mola wako na muombe msamaha wa makosa ya nafsi yako
{{Mola wetu! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu! Usitubebeshe mzigo
((Ee Allaah! Wewe ni Mola wangu, hapana mola Apasaye kuabudiwa kwa haki ila Wewe, Umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najilinda Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa Kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba Unisamehe kwani hasamehe madhambi ila Wewe.))
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
