067 - Al-Mulk

 

 

 

  الْمُلْك

Al-Mulk: 067

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾

1. Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo ufalme, Naye juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ﴿٢﴾

2. Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. Naye Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa Kughufuria.

 

 

الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَـٰنِ مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ﴿٣﴾

3. Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka. Hutaona katika Uumbaji wa Ar-Rahmaan tofauti yoyote. Basi rejesha jicho. Je, unaona mpasuko wowote ule?

 

 

ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ حَسِيرٌ﴿٤﴾

4. Kisha rejesha jicho tena na tena, litakupindukia jicho likiwa limehizika, nalo limenyong’onyea.

 

 

وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا لِّلشَّيَاطِينِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ﴿٥﴾

5. Na kwa yakini Tumeipamba mbingu ya dunia kwa mataa, na Tukazifanya kuwa ni makombora ya kuwavurumishia mashaytwaan, na Tumewaandalia adhabu ya moto uliowashwa vikali mno. 

 

 

وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿٦﴾

6. Na wale waliomkufuru Rabb wao wana adhabu ya Jahannam. Ni ubaya ulioje mahali pa kuishia! 

 

 

إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ﴿٧﴾

7. Watakapotupwa humo, watasikia sauti yake mbaya ya kuchukiza mno, nao huku unafoka.

 

 

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ ۖ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ﴿٨﴾

8. Unakaribia kupasuka kwa ghadhabu. Kila wanapotupwa humo kundi, walinzi wake watawauliza: Je, hajakufikieni mwonyaji yeyote? 

 

 

قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ﴿٩﴾

9. Watasema: Sivyo hivyo! Bali kwa yakini alitujia mwonyaji, lakini tulikadhibisha, na tukasema: Allaah Hakuteremsha kitu chochote, nyinyi si chochote isipokuwa mumo katika upotofu mkubwa.

 

 

وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١٠﴾

10. Na watasema: Lau tungelikuwa tunasikiliza au tunatia akilini, tusingelikuwa katika watu wa motoni. 

 

 

فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ﴿١١﴾

11. Basi watakiri madhambi yao, na (wataambiwa): Tokomeeni mbali watu wa motoni. 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ كَبِيرٌ﴿١٢﴾

12. Hakika wale wanaomkhofu Rabb wao wakiwa pweke mbali na macho ya watu, watapata maghfirah na ujira mkubwa.

 

 

وَأَسِرُّوا قَوْلَكُمْ أَوِ اجْهَرُوا بِهِ ۖ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ﴿١٣﴾

13. Na fanyeni siri kauli zenu, au zidhihirisheni, hakika Yeye Ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.

 

 

 

أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ﴿١٤﴾

14. Kwani Hajui Yule Aliyeumba! Na hali Yeye Ni Mwenye Kudabiri mambo kwa Ulatifu, Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri!

 

 

هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ ۖ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ﴿١٥﴾

15. Yeye Ndiye Aliyeidhalilisha ardhi kwa ajili yenu, basi nendeni katika pande zake na kuleni katika Riziki Yake, na Kwake ndio kufufuliwa.

 

 

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ﴿١٦﴾

16. Je, mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika?

 

 

أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ﴿١٧﴾

17. Au mnadhani mko katika amani na (Allaah) Aliyeko mbinguni kwamba Hatokutumieni tufani ya mawe? Basi mtajua vipi Maonyo Yangu!

 

 

 

وَلَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ﴿١٨﴾

18. Na kwa yakini walikadhibisha wale walio kabla yao, basi ilikuwaje Kukana Kwangu (kwa adhabu ya maangamizi)?!  

 

 

أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَـٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ﴿١٩﴾

19. Je, hawawaoni ndege juu yao, wakiwa wanakunjua na kukunja (mbawa)! Hakuna anayewashikilia isipokuwa Ar-Rahmaan. Hakika Yeye Ni Mwenye Kuona kila kitu.

 

 

أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ الرَّحْمَـٰنِ ۚ إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ﴿٢٠﴾

20. Au ni lipi hilo jeshi lenu linaloweza kukunusuruni badala ya Ar-Rahmaan? Makafiri hawamo isipokuwa katika ghururi.

 

 

أَمَّنْ هَـٰذَا الَّذِي يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُ ۚ بَل لَّجُّوا فِي عُتُوٍّ وَنُفُورٍ﴿٢١﴾

21. Au ni nani huyu ambaye atakuruzukuni ikiwa (Allaah) Atazuia Riziki Yake? Bali wanang’ang’ania kwenye ufidhuli na kukimbilia mbali kwa chuki.

 

 

أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٢٢﴾

22. Je, yule anayekwenda akiwa gubigubi juu ya uso wake ameongoka zaidi, au yule anayekwenda sawasawa kuelekea njia iliyonyooka? 

 

 

قُلْ هُوَ الَّذِي أَنشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۖ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ﴿٢٣﴾

23. Sema: Yeye Ndiye Aliyekuanzisheni, na Akakujaalieni kusikia na kuona na nyoyo za kutafakari. Ni kidogo sana mnayoshukuru.

 

 

قُلْ هُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٢٤﴾

24. Sema: Yeye Ndiye Aliyekutawanyeni kwenye ardhi, na Kwake mtakusanywa.

 

 

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَـٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ﴿٢٥﴾

25. Na wanasema: Ni lini hiyo ahadi (ya kufufuliwa), mkiwa ni wasemao kweli?

 

 

قُلْ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّـهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ﴿٢٦﴾

26. Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Allaah tu. Na hakika mimi ni mwonyaji mwenye kuwabainishia.

 

 

فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَقِيلَ هَـٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَدَّعُونَ﴿٢٧﴾

27. Basi watakapoiona (adhabu ya Qiyaamah) inakaribia, zitadhikika nyuso za wale waliokufuru, na itasemwa: Hii ndio ambayo mlikuwa mkiiomba.

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِيَ اللَّـهُ وَمَن مَّعِيَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن يُجِيرُ الْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٢٨﴾

28. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Je, mnaonaje ikiwa Allaah Ataniangamiza na walio pamoja nami, au Akiturehemu, basi ni nani atakayewakinga makafiri na adhabu iumizayo?

 

 

قُلْ هُوَ الرَّحْمَـٰنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢٩﴾

29. Sema: Yeye Ndiye Ar-Rahmaan tumemwamini, na Kwake tunatawakali. Basi karibuni hivi mtakuja kujua ni nani ambaye yumo katika upotofu wa bayana.

 

 

قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَاؤُكُمْ غَوْرًا فَمَن يَأْتِيكُم بِمَاءٍ مَّعِينٍ﴿٣٠﴾

30. Sema: Mnaonaje yakijakuwa maji yenu yamedidimia, basi ni nani atakayeweza kukuleteeni maji (ya chemchemu) yatiririkayo?

 

 

 

Share