054-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila ya Kulia Kutokana na Kumuogopa Allaah na Shauku Kwake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل البكاء من خشية الله تَعَالَى وشوقاً إِليه

054-Mlango Wa Fadhila ya Kulia Kutokana na Kumuogopa Allaah na Shauku Kwake

 

Alhidaaya.com 

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩﴿١٠٩﴾

Na wanaporomoka kifudifudi huku wanalia na inawazidishia unyenyekevu. [Al-Israa: 109]

 

أَفَمِنْ هَـٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ ﴿٥٩﴾ وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ ﴿٦٠﴾

Je, mnastaajabu kwa Al-Hadiyth hii (ya Qur-aan)? Na mnacheka na wala hamlii? [An-Najm: 59-60]

 

 

 

Hadiyth – 1

وعن ابن مسعود رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ لِي النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم: (( اقْرَأْ عليَّ    القُرْآنَ )) قلت : يَا رسول اللهِ ، أقرأُ عَلَيْكَ ، وَعَلَيْكَ أُنْزِلَ ؟! قَالَ : (( إِنِّي أُحِبُّ أنْ أسْمَعَهُ مِنْ غَيرِي )) فَقَرَأْتُ عَلَيْهِ سورةَ النِّسَاءِ ، حَتَّى جِئْتُ إِلى هذِهِ الآية :( فَكَيْفَ إِذَا جِئْنَا مِنْ كُلِّ أُمَّةٍ بِشَهيدٍ وَجِئْنَا بِكَ عَلَى هؤُلاءِ شَهيداً) [ النساء : 41 ] قَالَ : (( حَسْبُكَ الآنَ )) فَالَتَفَتُّ إِلَيْهِ فإذا عَيْنَاهُ تَذْرِفَان . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uud (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Nisomee Qur-aan." Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! nikusomee Qur-aan na juu yako imeteremshwa?" Akasema: "Mimi napenda niisikie kwa mwingine Hivyo nikamsomea Suwrah an-Nisaa' mpaka nikafika katika ayah hii: "Basi itakuwaje Tutakapoleta kutoka kila Ummah shahidi, na Tukakuleta (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa shahidi juu ya hawa?" [An-Nisaa: 41]. Akasema: "Inatosha sasa." Tahamaki macho yake yanabubujika machozi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 2

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : خطب رسول الله صلى الله عليه وسلم خُطْبَةً مَا سَمِعْتُ مِثْلَهَا قَطُّ ، فقال : (( لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أعْلَمُ ، لَضَحِكْتُمْ قَليلاً وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيراً )) قَالَ : فَغَطَّى أصْحَابُ رسول الله صلى الله عليه وسلم وُجُوهَهُمْ ، وَلَهُمْ خَنِينٌ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas ambaye amesema: "Alituhutubia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hotuba ambayo sijawahi kusikia mfano wake kabisa, akasema: 'Lau nyinyi mgejua ninayoyajua basi mgecheka kidogo na kulia sana.' Hapo Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) waliokuwepo walifunika nyuso zao na kuanza kumamia (kulia) kwa kwikwi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( لا يَلِجُ النَّارَ رَجُلٌ بَكَى مِنْ خَشْيَةِ اللهِ حَتَّى يَعُودَ اللَّبَنُ في الضَّرْعِ ، وَلاَ يَجْتَمِعُ غُبَارٌ في سبيلِ اللهِ وَدُخَانُ جَهَنَّمَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حَسنٌ صحيحٌ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hataingia Motoni mtu ambaye Amelia kwa kumuogopa Allaah mpaka maziwa yarudi katika matiti yake na pia vumbi liliopatikana kwa mtu kufanya Jihadi katika njia ya Allaah na moshi wa Jahanam haziungani pamoja." [At-Tirmidhiy, na alisema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم: (( سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ في ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ : إمَامٌ عَادِلٌ ، وَشَابٌ نَشَأَ فِي عِبَادَةِ اللهِ تَعَالَى ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ بِالمَسَاجِدِ ، وَرَجُلاَنِ تَحَابّا في الله اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وتَفَرَّقَا عَلَيْهِ ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ، فَقال: إنِّي أَخَافُ الله، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُه مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً ففاضت عَيْنَاهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kwa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Saba, Allaah atawafunika chini ya kivuli Chake Siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa kivuli Chake: Imamu (kiongozi) muadilifu, na kijana aliyeinukia katika kumuabudu Allaah Ta'aalaa, na mtu ambaye moyo wake umetundikwa katika Msikiti, na watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah, wanakuwa pamoja na kufarikiana kwa ajili Yake, na mtu ambaye ameitwa na mwanamke mzuri na mwenye kuvutia (kuzini naye), akasema: 'Mimi namwogopa Allaah.' na mtu aliyetoa swadaqah kwa kuificha sana mpaka mkono wake wa kushoto usijue kilichotolewa na mkono wa kuume, na mtu ambaye amemkumbuka Allaah peke yake na macho yake yakabubujika na machozi." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

وعن عبد الله بن الشِّخِّير رضي الله عنه ، قَالَ : أتيتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُصَلِّي ولِجَوْفِهِ أَزِيزٌ كَأَزِيزِ المِرْجَلِ مِنَ البُكَاءِ . حديث صحيح رواه أَبو داود والترمذي في الشمائل بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillah bin Ash-Shikhayr (Radhwiyah Allaah 'anhu) ambaye amesema: Nilikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye alikuwa anaswali. Nilisikia sauti ya kilio kutoka katika kifua chake ambacho kilikua kama sauti ya chungu kinacho chemka." [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy katika "Shamaa'il" na Isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم لأُبَي بن كعب رضي الله عنه: (( إنَّ الله (عزّ وجلّ أَمَرَنِي أنْ أقْرَأَ عَلَيْكَ :( لَمْ يَكُنِ الَّذِينَ كَفَروا ... )قَالَ : وَسَمَّانِي ؟ قَالَ : (( نَعَمْ )) فَبَكَى أُبَيٌّ . متفقٌ عَلَيْهِ .وفي رواية : فَجَعَلَ أُبَيٌّ يَبْكِي .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Ubayy bin Ka'b: "Hakika Allaah ('Azza wa Jalla), ameniamuru nikusomee: "Lam Yakunil Ladhiina Kafaruu..." [Al-Bayyinah]." Ubayy akauliza: "Allaah amenitaja mimi kwa jina?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ndio." Ubayy akawa alilia." [Al-Bukhaariy na Muslim]. Na katika riwaayah: "Ubayy akawa analia."

 

 

Hadiyth – 7

وعن أنس رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ أَبو بكر لِعُمَرَ ، رَضِيَ اللهُ عنهما ، بعد وفاة رسول الله صلى الله عليه وسلم: انْطَلِقْ بِنَا إِلى أُمِّ أيْمَنَ رضي الله عنها نَزورُهَا ، كَمَا كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَزُورُها ، فَلَمَّا انْتَهَيَا إِلَيْهَا بَكَتْ ، فقالا لها : مَا يُبْكِيكِ ؟ أمَا تَعْلَمِينَ أنَّ مَا عِنْدَ الله تَعَالَى خَيرٌ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم! قالت : مَا أبْكِي أَنْ لاَ أَكُونَ أَعْلَمُ أنَّ مَا عِنْدَ اللهِ خَيْرٌ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم، وَلكِنِّي أبكِي أَنَّ الْوَحْيَ قَد انْقَطَعَ مِنَ السَّمَاءِ ؛ فَهَيَّجَتْهُما عَلَى البُكَاءِ ، فَجَعَلا يَبْكِيَانِ مَعَهَا . رواه مسلم.

Kutoka kwa Anas (Radhwiyah Allaahu 'anhu) amesema: Abu Bakr alimwambia 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) baada ya kufa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Twende kumzuru Ummu Ayman (Radhwiyah Allaahu 'anhaa), kama alivyokuwa Rasuli wa Allaah anamzuru." Tulipofika kwake akalia. Wakamwambia: "Nini kinachokuliza?, kwani hujui yalio kwa Allaah ni bora kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?" Akasema: "Mimi najua nami silii kwa sababu hiyo bali nalia kukatika wahyi toka mbinguni." Hili liliwafanya Swahaaba wawili watukufu (Abu Bakr na 'Umar Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) walie pamoja naye." [Muslim]

 

 

 

Hadiyth – 8

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمَّا اشْتَدَّ برسول الله صلى الله عليه وسلم وَجَعُهُ ، قِيلَ له في الصَّلاَةِ ، فقال : (( مُرُوا أَبَا بَكْرٍ فَلْيُصَلِّ بِالنَّاسِ )) فقالت عائشة رضي الله عنها : إنَّ أَبَا بَكْرٍ رَجُلٌ رَقِيقٌ ، إِذَا قَرَأَ القُرْآنَ غَلَبَهُ البُكَاءُ ، فقال :  (( مُرُوهُ فَليُصَلِّ )) .

وفي رواية عن عائشة ، رضي الله عنها ، قالت : قلت : إنَّ أَبَا بَكْرٍ إِذَا قَامَ مَقَامَكَ لَمْ يُسْمِعِ النَّاسَ مِنَ البُكَاءِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiyah Allaahu 'anhummaa) amesema: "ugonjwa wa Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ulipozidi aliulizwa nani aswalishe watu. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Muamrisheni Abu Bakr aswalishe watu." 'Aaisha (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) alisema: "Hakika Abu Bakr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) moyo wake ni mwema (laini) na hivyo anaposoma Quraan huanguka kilio (hulia)." Akasema: "Muamuruni (yeye Abu Bakr) aswalishe." 

Na katika riwaayah kutoka kwa 'Aisha (Radhwiyah Allaahu 'anhaa) ambaye amesema, nikasema: "Hakika Abu Bakr anaposimama (Imamu) watu hawatamsikia kwa sababu ya kulia." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

وعن إبراهيم بن عبد الرحمان بن عوف : أنَّ عبد الرحمان بن عوف رضي الله عنه أُتِيَ بطعام وكان صائِماً ، فقال : قُتِلَ مُصْعَبُ بن عُمَيْر رضي الله عنه، وَهُوَ خَيْرٌ مِنِّي ، فَلَمْ يوجَدْ له مَا يُكَفَّنُ فيهِ إِلاَّ بُرْدَةٌ إنْ غُطِّيَ بِهَا رَأسُهُ بَدَتْ رِجْلاهُ ؛ وَإنْ غُطِّيَ بِهَا رِجْلاَهُ بَدَا رَأسُهُ ، ثُمَّ بُسِطَ لَنَا مِنَ الدُّنْيَا مَا بُسِطَ – أَو قَالَ : أُعْطِينَا مِنَ الدُّنْيَا مَا أُعْطِينَا – قَدْ خَشِينا أنْ تَكُونَ حَسَنَاتُنَا عُجِّلَتْ لَنَا ، ثُمَّ جَعَلَ يَبكِي حَتَّى تَرَكَ    الطعَام . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwake Ibraahiym bin 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf kwamba 'Abdir-Rahmaan bin 'Awf (Radhwiyah Allaahu 'anhu) aliletewa chakula akiwa ameamefunga, akasema: "Mus'ab bin 'Umayr (Radhwiyah Allaahu 'anhu) aliuliwa naye ni bora kuliko mimi na hakukupatikana kitu cha kumkafini isipokuwa kitambara kilichokuwa kifupi sana. Akifinikwa kichwa miguu kichwa hubaki wazi. Baada ya hapo tukafunguliwa dunia au alisema: 'Tukapatiwa katika dunia kile tulichopatiwa (tukapatiwa mali nyingi).' Tunaogopa isiwe malipo yetu tumepatiwa mapema (yaani katika hii dunia). Kisha akaanza kulia mpaka akaacha chakula." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 10

وعن أَبي أُمَامَة صُدَيِّ بن عجلان الباهلي رضي الله عنه، عن النبي صلى الله عليه وسلم، قَالَ : (( لَيْسَ شَيْءٌ أحَبَّ إِلى اللهِ تَعَالَى مِنْ قطْرَتَيْنِ وَأثَرَيْنِ : قَطَرَةُ دُمُوع مِنْ خَشْيَةِ    اللهِ ، وَقَطَرَةُ دَمٍ تُهَرَاقُ في سَبيلِ اللهِ. وَأَمَّا الأَثَرَانِ : فَأَثَرٌ في سَبيلِ اللهِ تَعَالَى، وَأَثَرٌ في فَريضةٍ مِنْ فَرائِضِ الله تَعَالَى )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديثٌ حسنٌ )) .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Umamah Swudayyi bin 'Ajlaan Al-Baahiliy (Radhwiyah Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna kitu kinachompendeza Allaah Ta'aalaa kama matone mawili na alambili. Ama matone ni machozi yanayobubujika kwa kumuogopa Allaah na damu inayotoka katika njia ya Allaah. Na alama mbili, alama katika njia ya Allaah Ta'aalaa na alama inayopatikana katika kutekeleza faradhi miongoni mwa faradhi miongoni mwa faradhi alizoamrisha Allaah Ta'aalaa." [At-Tirmidhiy, na alisema ni Hadiyth Hasan]

 

 Hadiyth – 11

حديث العرباض بن سارية رضي الله عنه، قَالَ : وعظنا رسول الله صلى الله عليه وسلم مَوعظةً وَجلَتْ منها القُلُوبُ ، وذرِفت منها الْعُيُونُ . وقد سبق في باب النهي عن البدع.

Amehadithia al-'Irbaadh bin Saariyah kwamba: "Alituaidhia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mawaidha yaliyozifanya nyoyo zikaingia hofu na macho yakatokwa na machozi." Hii ni sehemu tu ya Hadiyth ndefu iliyotangulia kutajwa katika Mlango wa Amri ya kuhifadhi Sunnah na Adabu Zake.

 

 

 

 

Share