SWALI:
Asalam aleykum. Mimi ni msichana wa miaka 25 lkn bado sijaaliwa nimekua nikipata wachumba mara nyingi lkn ndoa haisimami wanaowa kwingine bila sbb sasa je kuna tatizo kwangu au bado tu rizki? Maana kuna watu wananiambia lbd nina jini mahaba au husda je nifanye nini kwa kweli natamani
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu posa kutofanikiwa. Kupata wachumba kisha wakavunja posa na kwenda kuoa pahali pengine ni moja ya mitihani ambayo huwakumba wasichana au wanawake au pengine pia huwa mwanamme huyo si kheri nawe. Ikiwa ni mtihani inabidi uupite ili upate rehema ya Allaah Aliyetukuka kwa kuwa Anasema:
“Je, watu wanadhania kuwa wataachwa tu kwa kusema kuwa wameamini nao nao hawajajaribiwa. Hakika Tumewajaribu waliokuwa kabla yenu, na kwa yakini Allaah Atawatambulisha wale walio wa kweli na wale walio waongo” (Al-‘Ankabuut: 2-3).
Kushindwa kuupita ni kumaanisha kuwa umepata hasara hapa duniani na Kesho Akhera.
Ama kwa sababu ya pili ni kuwa ikiwa si kheri kwako basi pia unatakiwa uvumilie kwani kwa kuvumilia Allaah Aliyetukuka Hatokuacha bali Atakuletea yule mwenye kheri. Ama uwezekano wa jini hauwi hivyo rahisi kwa kusema tu bali inatakiwa ufanyiwe dawa kujua
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akuweke katika hali njema hata usifikirie kuzini, kwani kufanya hivyo ni kuonyesha kutoogopa kwako Muumba wako. Na zinaa ni dhambi kubwa ambayo tumeagiziwa hata tusiikaribie. Na ama kutamani ni jambo la kawaida kabisa kwa kila mmoja wetu – mvulana au msichana miongoni mwetu. Lile ambalo tunafaa kulitilia maanani ni kujaribu kuyazuia matamanio kadiri tuwezavyo kwani ukitofanya hivyo kunaweza kukuingiza wewe katika zinaa ambayo unaiogopa
Wakati unapojiwa na matamanio kule kushika sehemu zako za siri ndio kunazidisha matamanio. Kwa hiyo, ni vyema ujiepushe na kushika sehemu hizo kwa kujishughulisha na mambo mengine yatakayokunufaisha wewe. Na lau utashika sehemu hizo na ukatokwa na maji ya uzazi (manii) basi itabidi uoge josho la janaba. Na ikiwa si maji ya uzazi bali ni maji yanayoitwa madhii yanayotoka kwa matamanio kabla ya manii, itabidi tu uoshe sehemu zako za siri na kisha uchukue wudhuu kwa ajili ya Swalah.
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akuepushe na hayo matamanio pamoja na ndugu zetu wote katika Uislamu. Na tunamuomba Muumba wetu, Awapatie wake wenye kheri wanaume wasiokuwa na wake na wanaume wa kheri wanawake wasio na waume.
Na Allaah Anajua zaidi
Links
[1] http://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/65
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/1125
[3] https://www.addtoany.com/share#url=http%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F3964&title=Posa%20Zake%20Hazifanikiwi%20%E2%80%93%20Anapata%20Matamanio%20Na%20Kujishika%20Sehemu%20Zake%20Hadi%20Atulie