Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (https://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Puri Za Hamira

Puri Za Hamira

Mikate-Mahamri [1]

Puri Za Hamira

 

Vipimo   

 

Unga mweupe vikombe 4

Baking powder vijiko 2 vya chai

Hamira kijiko 1 cha kulia

Maji kiasi vikombe 1 ½  takriban

Mafuta ya kukaangia katika karai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Tia vitu vyote katika bakuli uchanganye vizuri donge liwe kiasi kama la paratha (mkate wa kusukuma)
  2. Funika kwa karatasi ya plastiki muda wa dakika 20
  3. Weka mafuta katika moto kwenye karai yashike moto.
  4. Changanya unga kidogo ufanye vidonge vidogodogo vya kiasi.

  1. Sukuma vidonge utandaze kiasi tu kisha kaanga katika mafuta huku unageuza mpaka zigeuke rangi ya hudhurungi.
  2. Epua uchuje mafuta kisha panga katika sahani zikiwa tayari.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

Kidokezo:  

 

1-Puri ni nzuri kuliwa na kuku wa kubanika (Grilled) au kuoka (baked). Bonyeza viungo vifuatavyo:

Kuku Wa Kubanika Kwa Sosi Tamu Kali Ya Ukwaju [2]

Kuku Wa Kuokwa (Baked Chicken) [3]

2-Tolea pia na chatine ya ukwaju na mtindi na saladi ya kabeji.  Bonyeza viungo vifuatavyo:

Sosi Ya Ukwaju [4]

Chatine Ya Mtindi Na Nanaa [5]

Saladi Ya Kabeji Na Pilipili Mboga (Hoho) Na Karoti [6]

 

 

Share [7]
www.alhidaaya.com

Source URL: https://www.alhidaaya.com/sw/node/8541

Links
[1] https://www.alhidaaya.com/sw/taxonomy/term/105
[2] http://www.alhidaaya.com/sw/node/8513
[3] http://www.alhidaaya.com/sw/node/1778
[4] http://www.alhidaaya.com/sw/node/2954
[5] http://www.alhidaaya.com/sw/node/2953
[6] http://www.alhidaaya.com/sw/node/7255
[7] https://www.addtoany.com/share#url=https%3A%2F%2Fwww.alhidaaya.com%2Fsw%2Fnode%2F8541&title=Puri%20Za%20Hamira%20