Kuku Wa Kubanika Kwa Sosi Tamu Kali Ya Ukwaju

 

Kuku Wa Kubanika Kwa Sosi Tamu Kali Ya Ukwaju

 

Vipimo 

Kuku 1 mkate mapande manne makubwa

Thomu (kitunguu saumu/garlic) iliyosagwa vijiko 2 vya supu

Ukwaju kamua uwe mzito kikombe cha chai 1

Nyanya kopo vijiko 2 vya kulia

Sosi ya nyanya (tomato ketchup) vijiko 2 vya kulia

Paprika (pilipili tamu ya unga) kijiko 1 cha kulia

Asali vijiko 2 vya kulia

Mafuta vijiko 2 vya kulia

Chumvi  1 kijiko cha chai

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Osha kuku vizuri kwa chumvi na bizari ya manjano atoe harufu kisha mchuje maji
  2. Changanya viungo vyote katika kibakuli kisha paka sosi katika kuku ubakishe kidogo ya kupakia mwishoni
  3. Roweka kuku kwa muda wa saa au zaidi.
  4. Weka kuku katika treya ya kupikia katika oven
  5. Mchome (grill) kwa moto wa kiasi huku unamgeuza.
  6. Anapoiva mpakaze sosi ilobakia kisha mtoe katika oveni uweke katika chombo akiwa tayari.

 Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)  

 

 

Share