Sosi Ya Ukwaju
Sosi Ya Ukwaju
 
Vipimo
Ukwaju - 2 Paketi
Chumvi - kiasi
Tende - ¼ kikombe
Pilipili mbichi - 1
Bizari ya jiyrah (Cummin powder) - ¼ kijiko
Namna ya kutayarisha
- Toa kokwa ukwaju, kisha roweka kwenye maji ya moto.
 - Chambua tende utoe kokwa weka kando.
 - Tia vitu vyote katika mashine, saga hadi vitu visagike vyote.
 - Mimina katika bakuli ukiwa tayari kutolewa na aina nyingi ya vyakula upendavyo.
 
Kidokezo:
- Ikiwa huna tenda tumia sukari vijiko 2 viwili vya supu.
 - Inaweza kuliwa na aina nyingi ya vyakula kama; dehii baree, biriani, nyama/kuku wa kuchoma, mishkaki, sambusa, kachori, katlesi viazi vya duara (chops), kababu na vinginevyo vingi.
 
    
    