Alhidaaya.com
Published on Alhidaaya.com (http://www.alhidaaya.com/sw)

Ukurasa Wa Kwanza > Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

Swalah [1]

 

 

 

 

 

 

IMEELEZEWA  

Kutoka mwanzo mpaka mwisho kama kwamba unaiona 

 

((Swalini Kama Mlivyoniona Nikiswali)) 

[Al-Bukhaariy]

 

 

Sifa Ya Swalaah Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

Kutoka Takbiyra Ya Kufunga Swalaah Hadi Kumalizika Salaam Kama Vile Unaiona    

"صفة صلاة النبي صلى الله عليه وآله وسلم"

من التكبير إلى التسليم كأنك تراها

Swifatus Swalaat An-Nabbiy (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

Minat Takbiyr Ilaat Tasliym Kaannaka Taraaha

  

Imeandikwa na: Shaykh Muhammad Naaswirud Diyn Al-Albaaniy 

Imetafsiriwa na: Muhammad Baawaziyr (Abu 'Abdillaah)

 

Share [2]

001-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Utangulizi Wa Mfasiri

Utangulizi Wa Mfasiri

 

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Hakika shukurani ni Zake Allaah (سبحانه وتعالى), tunamshukuru Yeye, na kumtaka msaada, na tunamuomba Yeye msamaha. Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atulinde na shari za nafsi zetu na ubaya wa matendo yetu. Anayeongozwa na Allaah (سبحانه وتعالى) hakuna wa kumpoteza, na anayepotezwa na Allaah (سبحانه وتعالى) basi hakuna wa kumuongoza.

 

Na nashuhudia kuwa hakuna apasaye kuabudiwa ila Allaah (سبحانه وتعالى), Ni Mmoja tu Asiye na mshirika. Na nashuhudia kuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mja Wake na ni Mjumbe Wake. Swalah na Salaam za Allaah zimshukie yeye, jamaa zake, Swahaba zake, na wote waliotangulia kwa wema hadi siku ya mwisho.

 

Ama ba’ad,

Namshukuru tena Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuniwezesha kukamilisha kazi hii kwa Lugha ya Kiswahili, kazi ambayo naamini sana kuwa itawanufaisha sana Waislam wazungumzaji wa lugha hii na kuweza kuwasaidia kupata mafunzo sahihi ya 'Ibaadah hii adhimu ambayo itakuwa ni jambo la kwanza kabisa kwa mja kuulizwa kwalo siku ya Hesabu.

 

Umuhimu wa kitabu hiki ni mkubwa sana, haswa kwa kuwa ni kitabu kilichoelezea ‘Ibaadah hii ya Swalah kwa mapana na marefu na kwa dalili sahihi zilizothibiti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Ni kitabu kwa mwenye kutaka kujua ilivyokuwa Swalah ya kipenzi chetu (صلى الله عليه وآله وسلم) kama alivyosema: ((Swalini kama mlivyoniona nikiswali)) [Al-Bukhaariy]. Basi anapaswa kuwa nacho kwenye nyumba yake.

 

Hiki ni kitabu cha Swalah kilichoenea na kuuzika kwa wingi sana labda kuliko vitabu vyote vya Swalah vilivyowahi kuandikwa. Ni kitabu chenye mauzo makubwa katika nchi za Kiarabu kwa mujibu wa wachapishaji wa kitabu hicho. Hali kadhalika kimetafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza na kimeuzwa na kinaendelea kuuzika kwa wingi katika nchi za Ulaya na haswa Uingereza. Nimeonelea manufaa hayo yasiwaenee tu wenye kuzungumza Kiarabu na Kiingereza pekee, bali na jamii yetu ya wazungumzao Kiswahili.

 

Swalah ina fadhila kubwa sana, hivyo kukosa kuswali ni kosa kubwa. Swalah ni 'amali ya kwanza itakayokaguliwa Siku ya Qiyaamah na ndio ufunguo wa Pepo. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

((’Amali ya mwanzo atakayoulizwa Muislamu Siku ya Qiyaamah kuwa kaitekeleza–na kaitekeleza vilivyo–ni Swalah. Ikiwa aliitekeleza vilivyo basi kunatarajiwa atafaulu. Ikiwa hakuitekeleza au kaitekeleza, lakini sivyo ndivyo, basi itatazamwa Swalah za Sunnah, kama alizitekeleza vilivyo. Ama ikiwa hana hata Sunnah au kaitekeleza sivyo ndivyo, basi keshapata khasara)) [Ahmad, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy na Ibn Maajah].

Amesema tena (صلى الله عليه وآله وسلم):

((Funguo za kufungulia milango ya Peponi ni Swalah)) [Muslim].

 

Ubaya wa kuacha Swalah ni mkubwa sana kwani Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلاَةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا  

((Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Swalah, na wakafuata matamanio. Basi watakuja kuta adhabu ya moto)) [19: 59].

 

Na kadhalika Anasema tena Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutaja habari za wasioswali pindi watakapoulizwa sababu yao ya kuwepo motoni:

 

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ  . قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ  

 

((Ni nini kilichokupelekeni motoni? Waseme: Hatukuwa miongoni waliokuwa wakiswali))  [74: 42 -43].

 

Na Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

((Kizuizi kilichoko baina ya mtu na ukafiri ni Swalah)) [Muslim].

 

Kadhalika akaeleza ubaya wa mtu kutokuswali na kumfananisha na kafiri:

((Tofauti baina yetu Waislamu na wasio Waislamu ni Swalah)) [Abu Daawuud, an-Nasaaiy na Ibn Maajah].

 

Baada ya kujua masuala hayo muhimu kutoka katika Kitaab na Sunnah, ndivyo vilevile tutaona umuhimu wa kuijua ‘Ibaadah hiyo vilivyo ili tuweze kuitekeleza ipasavyo. Na kwa mintarafu hiyo, tutaona kuna ulazima wa kupata mafunzo hayo kutoka katika chanzo kilichokamilika kwa dalili thaabit kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake. Na ndio nikakichagua kitabu hiki kukitafsiri ili kumuwezesha Muislam mwenye kusoma Kiswahili anufaike na aweze kuinoa na kuiboresha Swalah yake ili aweze kufikia makusudio yaliyotajwa katika Aayah na Hadiyth mbalimbali nilizotanguliza hapo juu, na pia ili aweze kuepukana na sifa na adhabu nilizotangulia kutaja.

 

Nisiwe mbakhili wa fadhila na mchache wa shukurani kwa wale waliotoa mchango wao mkubwa kabisa katika kazi hii tukufu. Nawaombea wote malipo kamili kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى) yanayotokana na kazi hii, bila kukosa thawaab za wale wote watakaonufaika kutokana na ‘amali hii.

 

Shukurani zangu za dhati na du’aa zangu ni kwa dada yangu Ummu Iyyaad ambaye kwa juhudi zake zisizo mithali kazi hii imeweza kukamilika na pia ushirikiano wake mkuu wa dhati. Pia Al-Akh 'Abdullaah Mu'awiyyah na Al-Akh Fayswal ‘Abdul-‘Aziyz, kwa kujitolea wakati mkubwa kuipitia kazi hii. Pamoja na ndugu yangu mpenzi Sa’iyd Baawaziyr kwa kupitia vilevile na kuchangia maoni mbalimbali. Bila kusahau mchango mkubwa wa upitiaji na mawazo wa Al-Akh Muhammad Faraj As-Sa’ay. Hali kadhalika Al-Ukht Ummu ‘Abdir-Rahmaan kwa mchango wake.

 

Na shukurani nyingi kwa tashji’i kubwa na uvumilivu wa hali ya juu kutoka kwa mke wangu Ummu ‘Abdillaah ambaye amenisaidia kwa kiasi kikubwa na amenipa fursa ya kutosha ya kushughulika na majukumu haya matukufu bila kuchoshwa wala kuvunjika moyo. Namuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Amlipe yeye na wote duniani na Akhera. Aamiyn

 

 

Abu ‘Abdillaah Muhammad Baawaziyr

Swafar 1429 H – Februari 2008 M

 

Share [3]

002-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Historia Fupi Ya Mwandishi Wa Kitabu

 

 

Historia Fupi Ya Shaykh Al-Albaaniy

 

 

(Historia hii fupi ya Shaykh nimeitoa katika kitabu nilichoandika kuhusu maisha ya Shaykh kiitwacho Shaykh Al-Albaaniy – Mwanachuoni Wa Karne Ambacho kinapatikana katika tovuti ya www.alhidaaya.com [4] na karibuni kitachapishwa in shaa Allaah)

 

Abu ‘Abdillaah Muhammad Saalim Sa’iyd Baawaziyr

 

Al-Imaam, Al- Muhadith, Shaykh Muhammad Naaswirud-Diyn Al-Albaaniy

1332 H-1420 H – 1914 M-1999 M 

  

Jina Lake: Muhammad Naaswir-ud-Diyn bin Nuuh An-Najaatiy

Nasaba Yake: Al-Albaaniy (Kajulikana kwa jina la Al-Albaaniy kwa sababu asili yake ni mtu wa Albania)

Kun-Yah Yake: Abu ‘Abdir-Rahmaan (Baba ya ‘Abdur-Rahmaan’)

Wake Zake: Alioa wake wanne; watatu wa mwanzo walimzalia watoto, na wa nne ‘Ummu Al-Fadhwl’ hakujaaliwa kuzaa, na ndiye aliyeishi naye hadi alipofariki dunia.

Watoto Wake: Aliruzukiwa watoto 13; 7 wa kiume na 6 wa kike. Wa kiume ni: ‘Abdur-Rahmaan, ‘Abdul-Latwiyf, ‘Abdur-Razzaaq, ‘Abdul-Muswawwir, ‘Abdul-Muhaymin, Muhammad na ‘Abdul-A’alaa. Wa kike ni: Aniysah, Aasiyah, Salaamah, Hassaanah, Sakiynah na HibatuLlaah.

 

Mwanachuoni Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn bin Nuuh An-Najaatiy Al-Albaaniy ni mmoja kati ya Ma’ulamaa wakubwa wa Kiislam katika zama hizi. Anahesabika kuwa ni Mwanachuoni wa Hadiyth maarufu kabisa katika fani ya elimu ya Jarh na Ta’adiyl.[1]

Shaykh Al-Albaaniy vilevile ni hoja katika elimu ya Mustwalahul-Hadiyth.[2] Na Wanachuoni wamemsifu na kuelezea kwamba kwa elimu yake hiyo, karejesha kumbukumbu za zama za kina Imaam Ibn Hajr Al-‘Asqalaaniy, Ibn Kathiyr na Wanachuoni wengine wakubwa wa fani hiyo.

 

Alikuwa na kumbukumbuku ya hali ya juu katika kuhifadhi vitu kichwani na mengine mengi. Kumbukumbu inayotukumbusha wema waliotangulia kama kina Ibn ‘Abbaas, Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliofuatia kama Imaam Al-Bukhaariy, Imaam Ash-Shaafi’y, Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah, Imaam Ibn Kathiyr, Imaam An-Nawawiy na wengine (Allaah Awarehemu wote).

 

 

 

Kuzaliwa Na Kukua Kwake

 

 

Alizaliwa mwaka 1332 H – 1914 M katika mji wa Ashkodera ambao kwa wakati huo ulikuwa mji mkuu wa Albania huko Ulaya Mashariki na ukoo wake ulikuwa maskini. Baba yake aliyeitwa Shaykh Nuuh An-Najaatiy alihitimu katika chuo cha Shari’ah huko Istanbul, Uturuki, na kurejea kwao akiwa Mwanachuoni. Lakini baada ya mfalme Ahmad Zogo kutwaa madaraka ya nchi na kuendesha utawala wa nchi hiyo kikomunisti ikabidi baba yake (Shaykh Al-Albaaniy) ahamie Damascus, Syria. Wakati huo Shaykh Al-Albaaniy alikuwa na umri wa miaka tisa.

 

Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy alianza masomo yake ya awali katika madrasah ya Al-Is’aaf Al-Khayriyah hapo Damascus na kuendelea hadi alipomaliza na kuwa msimamizi wa chuo hicho hadi yalipoanza mapinduzi dhidi ya Ufaransa nchini humo. Madrasah hiyo ikakumbwa na maafa ya moto yaliyosababishwa na vurugu na machafuko katika vita hivyo. Baba yake akaamua kumuachisha masomo na akaanza kumsomesha yeye mwenyewe. Alimwekea ratiba kali ya masomo ambayo ni; Qur-aan, Tajwiyd, Swarf, Fiqh (ya Kihanafi, yaliyokuwa madhehebu ya baba yake aliyekuwa Mwanachuoni mkubwa wa madhehebu hayo). Shaykh Al-Albaaniy alijifunza pia masomo mbalimbali ya Dini na lugha kutoka kwa Wanachuoni wakubwa na Mashaykh waliokuwa marafiki wa baba yake kama vile Shaykh Sa’iyd Al-Burhaaniy ambaye alimsomesha masomo ya balaaghah na lugha.

 

 

 

Kujifunza Kwake Elimu Ya Hadiyth

 

 

Alitunukiwa shahada ya juu ya elimu ya Hadiyth kutoka kwa Shaykh Raaghib At-Twabbaakh, Mwanachuoni mkubwa wa Halab katika wakati huo. Hapo ni wakati alipokutanishwa naye kupitia Shaykh Muhammad Al-Mubaarak ambaye alimjulisha Shaykh At-Twabbaakh umahiri wa kijana huyo (Al-Albaaniy) katika elimu ya Hadiyth. Baada ya Shaykh At-Twabbaakh kumjaribu na kuthibitisha hilo mwenyewe, akamtunuku shahada (Ijaazah). Shahada hiyo si pekee, bali pia alipata kwa Wanachuoni wengine wakubwa wa Hadiyth kama Shaykh Bahjatul Baytaar (ambaye isnaad yake inafika hadi kwa Imaam Ahmad bin Hanbal).[3]

 

Aliingia kwenye fani ya Hadiyth akiwa na umri wa miaka ishirini. Aliathirika sana na tafiti mbalimbali za Muhammad Rashiyd Ridhwaa, Mwanachuoni wa Misr wakati huo. Tafiti hizo zilikuwa katika jarida la Al-Mannaar. Anasema Imaam Al-Albaaniy: “Nilichokimulika mwanzo miongoni mwa vitabu, ni vile vya visa vya lugha ya kiarabu, kama vile; Adhw-Dhwaahir, ‘Antarah, Maalik as-Sayf na vinginevyo kama hivyo. Kisha nikazama katika vitabu vya visa vya kijasusi vilivyotarjumiwa katika lugha ya Kiarabu. Siku moja nikapita katika vibanda vya kuuza vitabu na macho yangu yakaangaza kwenye jarida moja liitwalo Al-Mannaar na katika kupekuapekua ndani yake nikakutana na makala ya kitafiti ya Rashiyd Ridhwaa akikielezea kitabu cha ‘Ihyaa ‘Uluum ad-Diyn’ cha Abu Haamid al-Ghazaaliy, akitaja mazuri yaliyomo ndani ya kitabu hicho na kasoro zake. Kwa mara ya kwanza nikakutana na aina kama hii ya uchambuzi wa kielimu. Nilivutika sana na uchambuzi sampuli hiyo na ukanifanya nisome toleo zima la makala hiyo. Kisha nikawa nafuatilizia maudhui za uchambuzi wa Hadiyth wa Mwanachuoni Al-Haafidh Al-‘Iraaqiy alioufanya kwa Hadiyth zilizomo ndani ya kitabu ‘Ihyaa ‘Uluum ad-Diyn’. Sikutosheka hadi ikabidi nimuombe muuza duka aniazime jarida hilo kwa kuwa sikuwa na uwezo wa fedha wa kulinunua!

 

Hapo ndipo ilipoanza safari ndefu ya kusoma vitabu mbalimbali. Nikatoa nakala ya maudhui hiyo iliyofanyiwa uchambuzi wa kina katika jarida hilo”

 

Shaykh Al-Albaaniy alijifunza pia kwa baba yake elimu ya kutengeneza saa hadi akawa fundi mzuri maarufu kwa kazi hiyo. Ikawa ndiyo kazi iliyompatia rizki yake. Alikuwa fundi na hapo hapo mtafutaji elimu. Hali hiyo ikaendelea hivyo hadi alipoamua kutenga siku mbili tu za kufanya kazi ya kutengeneza saa, na siku zote zilizobaki zikawa ni za kutafuta elimu. Elimu hiyo alikuwa akiichukulia katika maktaba kubwa ya mji huo wa Damascus iliyoitwa Adhw-Dhwaahiriyah ambapo alikuwa akitumia siku nzima kusoma na kutafiti. Alishughulishwa mno na kusoma hadi akawa anasahau hata kula. Kilichokuwa kinakatisha utafiti na masomo yake ni vipindi vya Swalah tu. Mwishowe, wahusika wa maktaba hiyo wakamuamini na kuamua kumpa funguo zake awe anatumia maktaba wakati wa ziada, na akawa daima ni mtu wa mwisho kutoka na kufunga mwenyewe.

 

Hadiyth za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zilikuwa zina athari kubwa sana katika maisha ya Shaykh kielimu na kiutendaji. Zikamuelekeza katika Manhaj (Njia, mwenendo) Sahihi; ambao ni kuchukua kutoka kwa Allaah (Qur-aan) na Mtume Wake (Sunnah) tu. Akipata usaidizi wa ufahamu wa vyanzo hivyo viwili vikuu kutoka kwa Maimaaam Wanachuoni katika wema waliotangulia (As-Salafu as-Swaalih) bila kuwa na ta’aswub (kasumba) ya kumshabikia yeyote miongoni mwao au kumponda yeyote, bali msimamo wake ulikuwa ni kuchukua haki popote ipatikanapo na kutoka kwa yeyote.

 

Kwa sababu hiyo, aliyaacha na kuyaweka pembeni madhehebu ya Kihanafi aliyokulia nayo na aliyosomeshwa na baba yake. Baba yake (Allaah Amrehemu), alikuwa akivutana naye sana juu ya masuala hayo ya kimadhehebu, kwani baba yake alikuwa ameshikilia kwa nguvu sana msimamo wa Kihanafi na hataki kusikia mingine hata iliyokuwa sahihi katika masuala mengine. Shaykh alijaribu sana kumfahamisha baba yake kuwa anapaswa kufanyia kazi Hadiyth za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) endapo itathibiti usahihi wake, na kuacha ya wengine wote kama hayawafikiani na maneno ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

 

Wanafunzi Wake Maarufu

 

Wanafunzi wake ni wengi sana na walio maarufu katika Mashaykh ni hawa ambao baadhi yao wako hai hadi leo:

Shaykh Muqbil bin Haadiy Al-Waadi’iy (Yemen)

Dkt. ‘Umar Sulaymaan Al-Ashqar (Jordan)

Shaykh Saalim Al-Hilaaliy (Palestina)

Shaykh Hamdiy ‘Abdul-Majiyd

Shaykh Muhammad ‘Iyd ‘Abbaasy

Shaykh Muhammad Ibraahiym Shaqrah (Jordan)

Shaykh ‘Aliy Khushshaan

Shaykh Muhammad Jamiyl Zaynuu (Saudi Arabia)

Shaykh ‘Abdur-Rahmaan ‘Abdus-Swamad

 

 

 

Vitabu Vyake

 

Maktaba za Kiislam zimeneemeka kwa vitabu vingi vya Shaykh hususan vile vikubwa vyenye mijalada mingi vya ‘Silsilatul Ahaadiyth Asw-Swahiyhah’ na ‘Silsilat al-Ahaadiyth adhw-Dhwa’iyfah wal-Mawdhuw’ah’ na kitabu chake cha Swalah kiitwacho ‘Swiftatus Swalaatin Nabbiy’[4] ambacho kimepokelewa kwa nguvu sana na wasomaji pande zote za ulimwengu, haswa vijana. Ni mojawapo ya vitabu vizuri na muhimu sana katika mafunzo ya Swalah kama ilivyoswaliwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Kadhaalika, Shaykh ana vitabu maarufu sana vya Hadiyth vyenye kuvifanyia sharh, tahkiki, na hata kubainisha yale ya sahihi na ya dhaifu ndani ya vitabu hivyo, kama alivyofanya kwenye vitabu Sunan At-Tirmidhy, Sunan Ibn Maajah, Sunan Abi Daawuud n.k. Vilevile ana mijalada mingi ya vitabu kama tutakavyoona hapo chini kwenye orodha fupi. Vilevile ameweza kutoa vitabu vya kufafanua na kusahihisha vitabu maarufu vya Wanachuoni wakubwa wa karibuni kama vitabu ‘Tamaamul-Minnah Fiyt-Ta’aliyq ‘Alaa Fiqhis-Sunnah’ kilichokuwa ni masahihisho ya Hadiyth zisizo sahihi katika kitabu cha Shaykh Sayyid Saabiq kitwacho ‘Fiqhus-Sunnah’, na ana kitabu cha ‘Ghaayatul-Maraam Fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal wal Haraam’ ambacho ni usahihisho wa Hadiyth zilizomo katika kitabu cha Dr. Yuusuf Al-Qaraadhwaawiy kiitwacho ‘Al-Halaal Wal Haraam Fiyl Islaam’.

 

Kazi zake za uandishi kuhusu masuala ya Hadiyth zinazidi zaidi ya mia.

 

Baadhi Ya Vitabu Vyake Vilivyoenea Sana Ni:

 

1- Silsilatul Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (Mijalada 1-11)

 

2- Silsilatul Ahaadiyth Adhw-Dhwa’iyfah wal Mawdhuw’ah (Mijalada 1-14)

 

3- Al-Irwaa Al-Ghaliyl (Mijadala 1-9)

 

4- At-Targhiyb wa At-Tarhiyb (Mijalada 1-4)

 

5- Swahiyh wa Dhwa’iyf Sunan Abi Daawuud (Mijalada 1-4)

 

6- Swahiyh wa Dhwa’iyf Sunan At-Tirmidhiy (Mijalada 1-4)

 

7- Swahiyh wa Dhwa’iyf Sunan Ibn Maajah (Mijalada 1-4)

 

8- Mukhtaswar Swahiyh Al-Bukhaariy

 

9- Mukhtaswar Swahiyh Muslim

 

10- Sharhu Al-‘Aqiydah Atw-Twahaawiyah

 

11- Ahkaam Al-Janaaiz

 

12- At-Tawaswul: Anwa’uhu wa Ahkaamuhu

 

13- Kitaabu As-Sunnah

 

14- Swalaatu At-Taarawiyh (Qiyaamu Ramadhwaan)

 

15- Tamaamul-Minnah Fiyt-Ta’aliyq ‘Alaa Fiqhis-Sunnah

 

16- Ghaayatul-Maraam Fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal wal-Haraam

 

17- Adaabu Az-Zafaaf[5]

 

18- Swifatu Asw-Swalaatin-Nabiy[6]

 

 

 

 

 

 

 

Fadhila Na Mema Yake

 

 

 

Shaykh Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu) alikuwa ni mwenye kufuata mwenendo wa wema waliotangulia (Salafus-Swaalih), akifuata mwenendo wao na tabia zao, na yakawa macho yake yanafuata kilichosemwa na Allaah (سبحانه وتعالى) na Mtume Wake (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Alikuwa hastahi katika haki, akiitangaza haki katika vitabu na mihadhara yake. Hii ni sifa ya nadra sana kuipata katika ulimwengu wa leo, ambao wengi hawapendi kusema haki kwa kuchelea kuwaudhi wengine au kupoteza kukubalika. Shaykh alikuwa akijirudi pindi alipokutana na dalili sahihi inayokwenda kinyume na kauli yake, na aliacha kauli yake na kufuata dalili hiyo iliyosihi bila kuangalia imetoka kwa nani. Kuna baadhi ya Hadiyth alizokuwa akiitakidi kuwa sahihi kwa elimu yake, na baadaye zikambainikia au akatanababishwa kuwa si sahihi, akawa anajirudi haraka na kukubali na kuzitaja katika vitabu vyake.

 

 

 

 

 

 

 

Elimu Yake Na Athari Yake Kwa Watu

 

 

 

Shaykh alikuwa katika daraja ya Al-Haafidh (Mwanachuoni wa Hadiyth aliyehifadhi Hadiyth laki moja (100,000) pamoja na mnyororo wa wapokezi wake na ‘mutuun’ zake (maneno ya kila Hadiyth). Hayo yanaelezwa na Shaykh ‘Ashiysh aliyemuuliza suala hilo na Shaykh akakataa kumjibu kwa unyenyekevu na kutotaka kujifakharisha, alichojibu baada ya kukazaniwa sana swali hilo, alijibu kwa Aayah hii: ((Na neema yoyote mliyonayo inatoka kwa Allaah)) [An-Nahl: 56].[7]

 

 

 

Katika wasia wake Shaykh alitoa hadiya maktaba yake ya vitabu na kazi zake za uandishi kukitunuku Chuo Kikuu Cha Madiynah Al-Munawarah kama alivyosema katika wasia wake: “Nimeiachia maktaba yangu – vyote vilivyomo, vikiwa ni vilivyochapishwa tayari, au nakala, au kazi nilizoziandaa kuchapishwa; kwa maandishi ya mkono wangu, au ya mwengine aliyeniandikia – kwa kuipa maktaba ya Jaami’atul-Islaamiyah (Chuo Cha Kiislam) kilichopo katika mji wa Madiynah. Kwa sababu ni kumbukumbu nzuri kwa chuo hicho wakati nilipokuwa huko nikifundisha, kwa kulingania kwake kwa msingi wa Kitaab (Qur-aan) na Sunnah kwa kufuata mwenendo (Manhaj) wa wema waliotangulia (Salafus-Swaalih)”.[8]

 

 

 

Alikuwa mtu wa kawaida sana, mnyenyekevu asiye na makuu na asiyetofautishwa na watu wengine ila kwa vitendo na maongezi yake ya kielimu.

 

 

 

Katika kipindi cha maisha yake, alifanya tafiti nyingi na kuzichambua taqriban silsilah 30,000 za wasimulizi wa Hadiyth (isnaad), akiwa ametumia kiasi cha miaka 60 ya umri wake kusoma na kupitia vitabu vya Sunnah na kuwa karibu navyo kwa muda wote huo, na mawasiliano ya nyanja hiyo, na pia kuwa karibu na Ma’ulamaa wa elimu hiyo.[9]

 

 

 

 

 

 

 

Sifa Njema Walizotoa Ma’ulamaa Kwa Mujaddid Wa Zama Hizi Shaykh Muhammad Naaswir-Ud-Diyn Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Bin Baaz [Aliyekuwa Mufti Wa Saudi Arabia] (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Sikumuona mtaalamu wa Hadiyth za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika enzi yetu ya leo chini ya qubah la mbingu kama Mwanachuoni mkubwa Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy. Aliulizwa kuhusu Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) isemayo:

 

((Allaah Hutuma kwa Ummah huu Mwanachuoni katika kila miaka mia mtu wa kupiga msasa mambo ya dini Yake)).[10] Aliulizwa ni nani mpiga msasa wa karne hii? Akajibu: Ninadhani Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy, ndiye mpiga msasa wa zama hizi. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.

 

 

 

 

 

Mwanachuoni Shaykh Muhammad Ibn Swaalih Al-‘Uthaymiyn (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Yale niliyoyajua kuhusu Shaykh na ambayo ni kidogo wakati nilipokuwa nakutana naye, ni kuwa yeye ana shime ya hali ya juu ya kutumia Sunnah na kupiga vita bid’ah; sawasawa katika ‘Aqiydah au matendo. Ama kwa kusoma kwangu vitabu vyake, hakika nimemjua vyema kwa hayo. Ana elimu kubwa ya Hadiyth kwa upande wa Riwaayah na Diraayah. Allaah Amewanufaisha watu wengi kutokana na yale aliyoyaandika kwa upande wa elimu, mfumo na mwelekeo katika taaluma ya Hadiyth. Hii ni faida kubwa sana kwa Waislam. Himdi ni za Allaah. Ama kwa upande wa uhakiki wake wa kitaaluma katika fani ya Hadiyth, basi hayo hayasemeki. 

 

 

 

 

 

Mwanachuoni Mfasiri Shaykh Muhammad Al-Amiyn Ash-Shanqiytwiy (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Al-Haddaah anasema:

 

“Hakika Mwanachuoni mkubwa Ash-Shanqiytwy anamtukuza Shaykh Al-Albaaniy utukuzo wa kushangaza. Anapomuona anapita nailhali yeye yuko katika darsa yake katika Msikiti wa Madiynah, kasha husimamisha darsa lake, husimama na kumsalimia kwa ajili ya kumuheshimu”.

 

 

 

 

 

Shaykh ‘Abdul-Muhsin Al-’Abaadiy (Allaah Amhifadhi)

 

 

 

Bila shaka Shaykh Al-Albaaniy, alikuwa ni katika Ma’ulamaa wa kipekee walioumaliza umri wao katika kuitumikia Sunnah, kuitungia vitabu, kulingania kwa Allaah Mtukufu, kuinusuru ‘Aqiydah ya kisalafiya, kuipiga vita bid'ah, na kutetea Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Yeye ni katika Ma’ulamaa wazuri wenye sifa za kipekee. Sifa zake zimeshuhudiwa na watu maalumu na wa kawaida. Hakuna shaka kwamba kumpoteza Mwanachuoni kama huyu, ni katika misiba mikubwa inayowapata Waislamu. Allaah Amlipe kheri nyingi kutokana na juhudi zake kubwa na Amweke katika Pepo Yake pana.

 

 

 

 

 

Mufti Wa Zamani Wa Saudia Mwanachuoni Shaykh Muhammad Bin Ibraahiym Aal Shaykh (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Amesema kuhusu Shaykh Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu): “Yeye ni mwana Sunnah, mpiganiaji haki, na mwenye kupambana na watu wasiofuata haki”.

 

 

 

 

 

Mwanachuoni Shaykh Muqbil Al-Waadi'iy (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Hakika katika taaluma ya Hadiyth, hakuna mtu kama Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy. Na Allaah Amenufaisha kwa elimu yake na vitabu vyake mara nyingi zaidi kuliko yale wanayoyafanya wale wenye hamasa na Uislam pasi na elimu ya kutosha, na wasio na msimamo. Ninaloliamini na ambalo ni deni kwangu mbele ya Allaah ni kuwa, Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy, ni katika waipigao msasa Dini na wanasadikishwa na neno la Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

((Allaah Hutuma kwa Ummah huu mwanzoni mwa kila miaka mia mtu wa kupiga msasa mambo ya Dini Yake)).[11]

 

 

 

 

 

Mwanachuoni Wa Hadiyth India, Shaykh ‘Abdus-Swamad Sharafud-Diyn (Allaah Amrehemu)

 

 

 

Katika moja ya barua walizokuwa wakiandikiana na Shaykh Al-Albaaniy katika masuala ya kitafiti ya Hadiyth, alikiri kuwa Shaykh Al-Albaaniy alikuwa Mwanachuoni mkubwa wa Hadiyth.

 

 

 

 

 

Waziri Wa Masuala Ya Kiislamu, Al-Awqaaf, Ulinganio Na Uongozi Shaykh Swaalih Bin ‘Abdil-‘Aziyz Bin Muhammad Aali Shaykh

 

 

 

Alisema: “Shukrani ni za Allaah kwa hukumu Zake na uwezo Wake ((Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea)).[12] Hakuna shaka kwamba kumpoteza Mwanachuoni Mkubwa Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn Al-Albaaniy, ni msiba. Yeye ni katika Wanachuoni wakubwa wa Ummah na mabingwa wa Hadiyth. Kwa Ma’ulamaa hao (Shaykh Al-Albaaniy), Allaah Mtukufu Ameilinda Dini hii na Akaieneza Sunnah kupitia kwao…”

 

 

 

 

 

 

 

Kipindi Cha Mwisho Cha Maisha Yake Na Kifo Chake

 

 

 

Shaykh (Allaah Amrehemu) hakutulia kutafuta elimu hadi umri wa miaka 86, akisoma, akifundisha, akielimisha, akiandika vitabu, akiandika barua kwa Wanachuoni wenzake kuwapongeza, kuwanasihi, kuwakosoa makosa ya vitabuni mwao au fatwa zao. Hadi umri huo hakuwa akiacha kutafiti masuala ya Hadiyth, akipangua sahihi na dhaifu na za kutungwa, aliweza kugawa vitabu vingi vikubwa vya Hadiyth kama vya Maimaam Abu, Dawuud, Ibn Maajah, At-Tirmidhy, An-Nasaaiy na wengineo, akaweza kuvigawa Sahihi zake na Dhaifu zake na kuwasaidia kuwarahisishia wenye elimu na wanafunzi katika uandishi na tafiti zao.

 

 

 

Shaykh anakumbukwa sana kwa kazi hiyo iliyosaidia Ummah leo hii, na kuuamsha kujua Hadiyth sahihi na dhaifu na pia kuwafanya wengi wawe karibu na kuifuatilizia elimu ya Hadiyth na sayansi yake.  Aliyafanya yote hayo – kwa sababu moyo wake ulikuwa umefungamana nayo hayo kwa mapenzi ya juu – na hakuacha hadi taqriban miezi miwili ya mwisho ya maisha yake, alipokuwa dhaifu akiugua kitandani. Pamoja na magonjwa mazito yaliyomdhoofisha sana na kutotoka kitandani, hakuacha kusoma wala hakupoteza kumbukumbu zake, akiwa anamjua kila aliyekwenda kumtazama, akimuita kila mmoja kwa jina lake! Hadi Allaah (سبحانه وتعالى) Alipoirejesha roho yake na akamfisha katika nyakati za mwisho za Alasiri, siku ya Jumamosi, tarehe 22 katika mwezi wa Jumaadah Al-Aakhirah, mwaka 1420 H sawa na 10-02-1999 M huko ‘Ammaan, Jordan.

 

Wanachuoni, watafuta elimu, wanafunzi, na watu wa kawaida wote waliathirika sana na kifo cha Shaykh. Taarifa za kifo chake zilipowafikia Waislam, majonzi yalienea pote na wengi kuhisi kuwa ile elimu na yule ‘Mujaddid’ (Mkarabati wa Dini) wa zama hayupo nao tena. Mwaka huo ulikuwa ni mwaka wa huzuni, kwa kutanguliwa na kifo cha Mwanachuoni mkubwa wa zama hizo hizo ambaye alikuwa Mufti wa Saudia wa wakati huo, Shaykh Al-‘Alaamah ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdullaah bin Baaz, na baada yao kufuatiwa na kifo cha Mwanachuoni Shaykh Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn, Mashaykh wengine wakubwa waliofariki katika mwaka huo ni, Shaykh Swaalih bin 'Aliy Ghaswuun, Shaykh 'Aliy Twantwawiy, Dkt. Mustwafaa Az-Zarqaa, Shaykh Mana'a Al-Qahtwaan na Shaykh 'Atwiyah bin Muhammad Saalim (Allaah Awarehemu wote hao na Awaweke katika pepo Yake Tukufu).

 

 

 

Abu ‘Abdillaah (1432 H – 2011 M)

 

 

 

 

 

 

[1] Ni fani ya Hadiyth inayohusiana na uaminifu wa wasimulizi wa Hadiyth na inakusanya habari zao zinazothibitisha uaminifu au udhaifu wa hao wasimulizi.

[2] Sayansi ya Hadiyth

[3] Hayaatul Al-Albaaniy, Muhammad Ash-Shaybaaniy. Al-Albaaniy mwenyewe anayaeleza hayo pia kwenye vitabu vyake ‘Mukhtaswar Al-’Uluww’ na ‘Tahdhiyrus-Saajid’.

[4] Kitabu hiki kimeshatafsiriwa na mwandishi kwa lugha ya Kiswahili na kinapatikana maeneo mbalimbali kwa jina “Sifa Ya Swalah Ya Mtume ”.

[5] Kitabu hiki kilishatafsiriwa na mwandishi wa Historia hii ya Shaykh na kinapatikana kwa jina “Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotwaharika.” Chapa za mwanzo kimetawanywa bure na shukurani zote ni Zake Allaah.

[6] Kitabu hiki kimeshatafsiriwa na mwandishi kwa jina “Sifa Ya Swalah Ya Mtume” na chapa za mwanzo zimetawanywa bure na himidi zote Anastahiki Allaah.

[7] Shaykh Husayn Al-’Awaaishah, Swafahaat Baydhwaa Min Hayaati Shaykhina Al-Albaaniy, uk. 40.

[8] Samiyr bin Amiyn Az-Zuhayriy, Muhadith Al-’Aswr, uk.78.

[9] Abu Hudhayfah: 20 Points Regarding Shaykh al-Albaanee

[10] Imepokewa na Abu Daawuud, na imeelezewa kuwa ni sahihi na Al-’Iraaqiy na wengineo.

[11] Imepokewa na Abu Daawuud, na imeelezewa kuwa ni sahihi na Al-’Iraaqiy na wengineo.

[12] Al-Baqarah: 156.

 

 

Share [5]

003-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Utangulizi Wa Kitabu

 

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

 

UTANGULIZI WA KITABU

 

 

Sifa njema zote ni za Allaah Aliyefanya Swalah kuwa ni fardhi kwa waja Wake na kuwaamrisha kuitekeleza ipasavyo; Aliyeambatanisha kufaulu na furaha kutokana na unyenyekevu katika Swalah; Aliyefanya kuwa ni kigezo cha Iymaan na kufr; na aliyeifanya ni kizuizi cha mambo machafu na vitendo viovu.

 

Swalah na Salaam zimshukie Mtume Muhammad ambaye Amefunuliwa na maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ 

((Nasi Tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao, wapate kufikiri))

 Na ambaye ametekeleza kikamilifu kazi hii. Swalah ilikuwa ni jambo muhimu kabisa aliyowaeleza watu kwa kauli na vitendo, hata aliwahi kuswali mara moja katika minbar akisimama, akirukuu na kusujudu, kisha akasema: ((Nimefanya hivi ili mnifuate na mjifunze Swalah yangu)). Ametuwajibisha tumfuate anavyoswali kwa kusema: ((Swalini kama mlivyoniona nikiswali)). Amebashiria pia kuwa atakayeswali kama anavyoswali, atakuwa katika ahadi ya Allaah kwamba Atamuingiza katika Pepo, akisema: ((Swalah tano ambazo Allaah (عزوجل) Amezifaradhisha. Atakayefanya wudhuu wake vizuri, akaziswali kwa wakati wake, na kutimiza rukuu zake, sujudu zake na unyenyekevu, ana dhamana kutoka kwa Allaah kwamba Atamsamehe, lakini asiyetekeleza hana dhamana kutoka kwa Allaah, Akipenda Atamsamehe au Akipenda Atamuadhibu))

 

Swalah na amani pia ziwafikie jamaa zake na Maswahaba zake Waswalihina waliotuletea ‘Ibaadah yake (صلى الله عليه وآله وسلم), na Swalah, kauli na vitendo vyake  na wakavifanya hivyo kuwa ni madhehebu na mfano bora kwao wa kufuata; na wale watakaofuata nyayo zao hadi siku ya Qiyaama.  

 

Nilipomaliza kusoma kitabu cha Swalah katika At-Targhiyb wat-Tarhiyb cha Al-Haafidhw Al-Mundhiry (رحمه الله) na kuwafundisha ndugu zetu miaka minne iliyopita, ilidhihirika kwetu umuhimu wa nafasi ya Swalah katika Uislamu; na thawabu, neema na fadhila zinazowasubiri watakaoitekeleza na kuiswali sawa sawa; na kwamba yote inatofautiana, kutegemea ukaribu wa Swalah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Hii ndivyo ilivyoashiriwa katika usemi wake: ((Hakika mja huswali Swalah ambayo haandikiwi kitu ila sehemu ya kumi, au ya tisa, ya nane, ya saba, ya sita, ya tano, robo, thuluthi au nusu yake)). Hivyo nikawakumbusha ndugu kwamba haiwezekani kutekeleza Swalah ipasavyo au hata kuikaribia ila tutambue maelezo ya sifa ya Swalah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), ikijumuisha namna ya kuiswali, mfumo wake, du'aa na adkhkaar zake, kisha tufanye jitihada kutumia elimu hiyo katika utekelezaji kwa makini, hapo ndipo tutaweza kuwa na tamaa kwamba Swalah zetu zitatuzuia na mambo machafu na vitendo viovu na ndipo tutaandikiwa thawabu na baraka zilizotajwa katika usimulizi mbali mbali.

 

Lakini, maelezo kwa urefu juu ya vipengele vyote hivi vya Swalah sio wepesi kutekelezwa na watu wengi siku hizi, hata Maulamaa wengi kwa sababu ya kujihusisha na kujiwekea mipaka ya madhehebu fulani. Lakini kwa yeyote mwenye kujali na kusaidia katika ukusanyanji na utafiti wa Sunnah zilizotakasika, atajua kwamba katika kila madhehebu kuna Sunnah ambazo hazipatikani katika madhehebu mengine; juu ya hivyo, katika kila dhehebu kuna usemi na vitendo ambavyo havipatikani dalili za usahihi wake kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).  Mengi hayo hupatikana katika usemi tu wa Maulamaa waliofuatia, wengi wao tunaona kwamba wanahusisha haya kwa Mtume. Ndio maana Maulamaa wa Hadiyth (Allaah Awalipe wote vyema) wametoa vitabu vya Takhriyj kuhusu vitabu maarufu vya Maulamaa waliofuatia, wakielezea daraja ya kila Hadiyth iliyotolewa humo: mfano kama ni 'Swahiyh' au 'Dhaifu', au 'Imezushwa'. Mifano ya vitabu hivi vya Takhriyj ni: 'Al-‘Inaayah fiy Ma'rifah Al-Ahaadiyth Al-Hidaayah na At-Twuruq wal-Wasaail fiy Takhriyj Ahaadiyth Khulaaswah Ad-Dalaail cha Shaykh 'Abdul-Qaadir bin Muhammad Al-Qurayshiy Al-Hanafiy; Naswb Ar-Raaayah li Ahaadiyth Al-Hidaayah cha Haafidwh Zayla'iy, na mukhtasari yake ya Ad-Diraayah cha Haafidhw Ibn Hajr Al-Asqalaaniy ambaye pia ameandika Talkhiys Al-Habiyr fiy Takhriyj Ahaadiyth Ar-Raafi'iy Al-Kabiyr;  kuna vingi vingenvyo, kuvitaja vyote vitazidisha urefu wa maelezo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

[1] Suratun-Nahl: 16: 44

[2] Al-Bukhaariy na Muslim – itafuatia baadaye kikamilifu

[3] Al-Bukhaariy na Ahmad

[4] Maalik, Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ibn Hibbaan. Hadiyth Swahiyh iliyobainishiwa kuwa Swahiyh na Maimamu wengi. Nimeitoa takhriyj yake katika Swahiyh Abi Daawuud (451, 1276)

[5]  Swahiyh – Imekusanywa na Ibn Al-Mubaarak katika Az-Zuhd (10/21/1-2), Abu Daawuud na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad nzuri; Nimetoa takhriyj yake katika Swahiyh Abi Daawuud (761).

 

[6] Abul-Hasanaat Al-Laknawiy kasema katika An-Naafi' Al-Kabiyr Liman Yutwaali' Al-Jaami' As-Swaghiyr (Uk. 122.3) baada ya kuvikadiri vitabu vya Fiqh ya Hanafiy na kutaja vipi vya kutegemea na vipi visitegemewe: "Yote hayo tuliyosema kuhusu daraja zinazohusika za ukusanyaji huu unahusiana na yaliyomo katika mas-ala ya Fiqhi; lakini ama yaliyomo kuhusu Hadiyth za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hazihusiki kwani vitabu vingi ambavo Mafuqahaa wanatagemea vimejaa uzushi wa Hadiyth, achilia mbali hukmu za Maulamaa. Ni dhahiri kwetu kutokana na uchambuzi mpana kwamba ingawa waandishi wake walikuwa ni mahodari lakini hawakuwa makini katika kunukuu usimulizi".

 

Si Maulamaa wa Hadiyth wala hawakutoa hizi Hadiyth kutoka kwa wakusanyaji wa Hadiyth".

Ash-Shawkaaniy pia alitaja Hadiyth hii katika Al-Fawaaid Al-Majmuu'ah Fil Ahaadiyth Al-Mawdhwuu'ah ikiwa na maneno yaliyofanana, kisha akasema (Uk. 54): "Hii imezushwa bila shaka – sijaipata hata katika mkusanyo wa Hadiyth za Uzushi! Bali imekuwa ni maarufu baina ya wanafunzi wa Fiqh katika mji wa San'aa katika karne yetu, na wengi wameanza kuitekeleza. Sijui nani aliyewazushia. Allaah Awahizi waongo".

 

[7] Maneno ya Imaam An-Nawawiy (رحمه الله) katika Al-Majmuu' Sharh Al-Muhadhdhab (1/60) yanaweza kujumuishwa kama ifuatavyo: "Maulamaa watafiti wa Hadiyth na wengineo wamesema kwamba ikiwa Hadiyth ni dhaifu, haitotajwa kuwa: 'Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم)kasema/katenda/kaamrisha/kakataza….' Au ibara yoyote nyingine inayotaja uhakika, bali itasemwa: 'Imeripotiwa/imenukuliwa/imesimuliwa kutoka kwa…' au ibara zingine zinazodokeza shaka. Wanasema kuwa ibara za uhakika huwa ni Swahiyh na Hadiyth Hasan na ibara zenye shaka huwa ni nyinginezo. Hii ni kwa sababu ibara zinazotaja uhakika zina maana kwamba yanayofuatia ni Swahiyh, hivyo zinatumika kwa hali ya Usahihi pekee, au sivyo itakuwa ni kumzulia (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

Jambo hili limepuuzwa na Mafuqahaa wengi wa zama zetu, bali Maulamaa wengi wa nidhamu yoyote, isipokuwa Muhaddithiyn wenye ujuzi. Huu ni uzembe wa kuchukiza kabisa, kwani mara nyingi hutaja Hadiyth Swahiyh: 'Imeripotiwa kutoka kwake kwamba…' Na kuhusu Hadiyth dhaifu: 'Amesema' na: 'Fulani na Fulani ameripoti...' Hivi sio sawa kabisa". 

 

Laknawiy akaendelea kusema: "Kutegemea Hadiyth hii ambayo inapatikana katika vitabu vya uradi na du’aa ni uzushi, nimeandika insha fupi ya kitaalamu na dalili inayoitwa 'Kuwakanusha Ndugu Kutokana Na Uzushi Wa Ijumaa Ya Mwisho Ya Ramadhaan'. Humo nimetoa nukta ambazo zitamulika akili na zitazibua masikio, hivyo isome, kwani ni ya thamani katika maudhui hii na ni ya ubora wa hali ya juu.

 

Marudio ya Hadiyth za uongo kama hizo katika vitabu vya Fiqhi vimeharibu uaminifu wa Hadiyth nyinginezo ambazo hazikunukuliwa kutoka katika vitabu vya Hadiyth vinvayotegemewa. Maneno ya 'Aliy Al-Qaariy yameashiria haya. Muislamu lazima apokee Hadiyth kutoka kwa watu ambao ni wataalamu katika fani hii, kama usemi wa zamani wa Kiarabu unavyosema: "Watu wa Makkah wanajua njia za milima yao vizuri" na "Mwenye kumiliki anajua vyema vilivyomo nyumbani mwake".

 

[8] Tanbihi ya Mchapishaji

Katika mlango huu, kuna kazi ya mwalimu wetu pia mwandishi wa Irwaa' Al-Ghaliyl Fiy Takhriyj Manaar As-Sabiyl katika Mijalada 9, na Ghaayah Al-Maraam fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal wal-Haraam, takhriyj ya Ahaadiyth zinazopatikana katika kitabu cha Dkt. Yuusuf Qaradhwaawiy 'Halali Na Haramu Katika Uislamu' (ambacho kina Hadiyth nyingi dhaifu).

 

Share [6]

004-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Sababu Za Kuandika Kitabu Hiki

 

Sababu Za Kuandika Kitabu Hiki Na Baadhi Ya Vipengele Vyake

 

 

Kwa vile sijapata kuona kitabu chenye maarifa mengi kuhusu maudhui hii, nimehisi imeniwajibikia kutoa kitabu ambacho kitakusanya sifa nyingi za Swalah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili ya manufaa ya ndugu zangu Waislamu wapendao kufuata uongofu wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika ibada zao, hadi iwe wepesi kwa yeyote mwenye kumpenda kweli  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aweze kutumia kitabu hiki kutimiza amri yake: ((Swalini Kama Mlivyoniona nikiswali)).

 

Hivyo nikaianza kazi hii ngumu, na kufanya utafiti wa Hadiyth zinazohusika kutoka vyanzo mbali mbali za Hadiyth hadi kitabu hiki kilichokuwa sasa mikononi mwako kuwa ni matokeo yake yote. Nikajiwekea masharti nafsini mwangu kwamba nitaziweka Hadiyth zilizokuwa na isnaad Swahiyh pekee kutokana na kanuni za msingi na sheria ya Sayansi ya Hadiyth. Nimepuuza Hadiyth yoyote ambayo imetegemewa na msimulizi asiyejulikana au dhaifu ikiwa imehusianina na maelekezo ya nje, adhkhaar, ubora n.k. wa Swalah. Hii ni kwa sababu naamini kwamba Hadiyth Swahiyh[1] zinatosheleza, na hakuna haja ya zilizo dhaifu kwani zilizo dhaifu hazizidishi kitu isipokuwa dhana (makisio, mashaka) na makisio yasiyo sahihi ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه و تعالى):

 

  وَإِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا

 

((Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki))[2]

 

Na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kasema: ((Tahadharini na dhana kwani dhana ni kauli ya uongo))[3]

 

Kwa hiyo hatuwezi kumuabudu Allaah kwa kufuata Hadiyth zisizo Swahiyh, bali Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ametukataza akisema: ((Jiepusheni na kusema yanayonihusu isipokuwa muyajuayo))[4]. Kwa vile ametukaza kusimulia masimulizi dhaifu, basi pia haipasi kuzitekeleza.

 

Nimekigawa hiki kitabu katika sehemu mbili; kubwa na ndogo, matini kuu na matini ya kisaidizi/matini ndogo.

 

Matini kuu imejumuisha matini ya Hadiyth au ibara ilivyochukuliwa humo, pamoja na maneno yanayolingana kuunga pamoja ili kukifanya kitabu chepesi tokea mwanzo hadi mwisho. Nimekuwa makini kuibakisha matini ya kila Hadiyth kama ilivyopatikana katika vitabu vya Sunnah; ambako Hadiyth ilikuwa na meneno tofauti na nimechagua maelezo yaliyo bora kabisa yanayowafikiana na ufasaha, wepesi n.k.. Lakini nimekusanya maneno mengine pamoja; hivyo: "(katika usemi kadha na kadhaa…..)" au "(katika usimulizi kadhaa na kadhaa …)". Sikumtaja Swahaba aliyesimulia Hadiyth ila kwa nadra tu nimefanya hivyo, wala sikumtaja Imaam gani wa Hadiyth aliyekusanya Hadiyth, ili kufanya wepesi usomaji na marejeo.

 

Ama matini ya kisaidizi/ndogo ni maelezo kutokana na matini kuu. Humo nimefuatilia Hadiyth kutoka asili yake nikifumbua maelezo mbali mbali na njia za usimulizi. Pamoja nayo, nimetoa maelezo katika isnaad zao na usimulizi unaotilia nguvu, pamoja na tanbihi Swahiyh na zenye kutezwa kwa wasimulizi, ikiwa ni Swahiyh au dhaifu kutokana na hukumu za Sayansi ya Hadiyth. Aghlabu njia ya usimulizi moja huwa na nyongeza ya maneno ambayo hayapatikani katika njia nyingine, hivyo nimezitia hizi katika Hadiyth ya asili zilizotajwa katika matini kuu kila ilipowezekana bila ya kuharibu ufasaha, nikiweka nyongeza katika mabano ya mraba […]. bila ya kutaja chanzo gani kilichonacho nyongeza hiyo. Hii imefanywa ikiwa Hadiyth asili yake imetoka kwa Swahaba mmoja, au sivyo nimeitoa peke yake; mfano katika Du'aa za kufungulia n.k. Nyongeza hii ya maneno ziada ni manufaa makubwa ambayo hutoyapata katika vitavu vingi – Sifa njema zote ni za Allaah Ambaye Kwa Neema Zake Mema hutimia.

 

Kisha, nikataja katika matini ya kisaidizi/matini ndogo Madhehebu ya Maulamaa kuhusu Hadiyth tulizozitoa na dalili zake kila moja pamoja na hoja zake na kubainisha uzito wake na udhaifu wake. Kisha tukachagua rai iliyo sahihi ambayo tumeiweka katika matini kuu. Pia katika matini ya kisaidizi tumetoa baadhi ya mas-ala ambayo hakuna matini katika Sunnah, lakini imehitaji Ijtihaad, na haikuja chini ya maudhui ya kitabu hiki.

 

Kwa vile kuchapishwa kitabu kuwekwa matini kuu na matini ya kisaidizi haiwezekani sasa kwa sababu mbali mbali, tumeamua kukichapisha kikiwa na matini kuu ya kitabu (pamoja na tanbihi fupi) kwa uwezo wa Allaah, na kukiita 'Swiffatus-Swalat 'An-Nabiyy'   (صلى الله عليه وآله وسلم)Min At-Takbiyr ilaa At-Tasliym Kaannaka Taraaha' (Sifa ya Swalah ya  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuanzia Takbiyra Ya Mwanzo hadi Kumalizika kwa Salaam Kama Kwamba Unaiona)"

 

 

Namuomba Allaah Ajaalie kazi hii iwe khaswa kwa ajili Yake, na iwasaidie ndugu zangu katika Iymaan kunufaika nayo kwani Yeye ni Mwenye Kusikia Aliye Karibu.

 

 

 

 

 

[1] Istilahi ya 'Hadiyth Swahiyh' inajumuisha Swahiyh na Hasan mbele ya macho ya Muhaddithiyn, ikiwa ni Hadiyth Swahiyh lidhaatihi au Swahiyh lighayrihi, au Hasan lidhaatihi au Hasan lighayrihi.

 

[2] An-Najm: 53: 28

[3] Al-Bukhaariy Na Muslim

[4] Swahiyh – imekusanywa na At-Tirmidhiy, Ahmad na Ibn Abi Shaybah.

 

 

 


Share [7]

005-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuatwa Rai Zao

 

KAULI ZA MAIMAAM WANNE KUHUSU KUSHIKAMANA NA SUNNAH NA KUACHA KUFUATA RAI ZAO

 

Itakuwa ni manufaa makubwa ikiwa tutazieleza baadhi ya kauli zao hapa, kwani labda hii itamuonya mtu au itawakumbusha wale ambao wanafuata rai za Maimaam au madhehebu maalum, bali wanaofuata kwa upofu wale Waalimu au Mashaykh na wale walio chini ya daraja ya hao Maimaam wanne wakubwa[1] wakishikilia madhehebu yao au rai zao kama kwamba zimeteremeshwa kutoka mbinguni! Na hali Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 ((اتَّبِعُواْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلاَ تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاء))

((Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake))[2]     

 

 

WASEMAVYO MAIMAAM

 

1) ABU HANIYFAH (رحمه الله)

Wa kwanza wao ni Abu Haniyfah Nu'maan bin Thaabit.

Wafuasi wake wamesimulia kauli zake mbali mbali pamoja na maonyo tofauti ambayo yote lengo lake ni moja, nalo ni: Wajibu wa kuikubali Hadiyth na kuachilia mbali kufuata rai za Maimaam ambazo zinakhitilafiana nayo.

  1. "Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu"[3]    
  2. "Hairuhusiwi[4] kwa mtu yeyote kukubali rai zetu ikiwa hawatojua wamezipata kutoka wapi"[5]     

Katika usimulizi mwengine:"Imekatazwa[6]  mtu ambaye hajui dalili zangu kutoa hukmu[7]   kutokana na maneno yangu"

Usimulizi mwengine imeongezwa: "…Kwani sisi ni wanaadamu, tunasema jambo siku moja na kulirudisha (kulikataa) siku ya pili yake".

Na katika usimulizi mwengine: "Ole Ewe Ya'quub![8]Usiandike kila kitu unachosikia kutoka kwangu kwani huwa natoa rai moja leo na kesho huikataa. Au hutoa rai moja kesho na kuikataa keshokutwa".[9]    

  1. "Ninaposema jambo linalokhitilafiana na kitabu cha Allaah (سبحانه وتعالى) au yaliyosimuliwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi mpuuze kauli yangu".[10]        

 

 

2) MAALIK BIN ANAS (رحمه الله)

Imaam Maalik bin Anas yeye amesema:

  1. "Hakika mimi ni mwanaadamu: Ninafanya makosa (mara nyingine) na ninakuwa sahihi (mara nyingine). Kwa hiyo, tazameni rai zangu: zote ambazo zinakubaliana na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, zikubalini; na zote ambazo hazikubaliani na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, basi zipuuzeni". [11]

 

  1. "Kila mmoja baada ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), atakuwa na kauli yake itakayokubaliwa na kukataliwa, isipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)" [12]   

 

  1. Ibn Wahb amesema: "Nilimsikia Maalik akiulizwa kuhusu takhliyl ya vidole vya miguu (kuvichanganua vidole ili kupitisha maji) wakati wa wudhuu. Akasema: "Watu si lazima kufanya hivyo". Sikumkaribia hadi zogo la watu lilipopunguka. Nilipomwambia: "Tunajua kuwa ni Sunnah kuhusu jambo hilo". Akasema: "Jambo gani hilo? Nikasema: "Layth bin Sa'd, Ibn Lahiy'a na 'Amr bin Al-Haarith wamesimulia kwetu kutoka kwa Mustawrid bin Shaddaad Al-Quraishiy ambaye amesema: "Nilimuona Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisugua baina ya vidole vyake vya miguu kwa kidole chake kidogo". Akasema: "Hadiyth hii ni Hasan (njema); sikuwahi kuisikia abadan ila leo". Kisha baadaye nikamsikia akiulizwa kuhusu jambo hili hili, naye akaamrisha kufanya takhliyl ya vidole vya miguu"[13] 

  

 

3) ASH-SHAAFI'IY (رحمه الله)

Ama kutoka kwa Imaam Ash-Shaafi'iy, kauli zake zilizonukuliwa ni nyingi na nzuri mno.[14] na wafuasi wake walikuwa ni bora kabisa katika kufuata.

 

  1. "Sunnah za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zinamfikia na kumkwepa kila mmoja wetu. Kwa hiyo kila ninapotaja rai yangu au nikiunda sheria, na ikiwa ipo dalili kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), inayopinga rai yangu, basi rai iliyo sahihi ni aliyosema Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na hiyo ndio rai yangu"[15]   

 

  1. "Waislamu wamekubaliana pamoja kwamba ikiwa Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) imebainishwa dhahiri kwa yeyote, hairuhusiwi[16]  kwake kuiacha kwa kufuata kauli ya mwengine yeyote[17]  

 

  1. "Ukiona katika maandishi yangu jambo ambalo ni tofauti na Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi zungumza kwa kurejea Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na acha niliyoyasema mimi". Katika usimulizi mwengine: "…basi ifuate (Sunnah) na usitazame tena pembeni kufuata kauli ya mwengine yeyote"[18]    

 

  1. Hadiyth ikipatikana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu"[19]    

 

  1. "Wewe (Imaam Ahmad)[20] ni mwenye elimu zaidi kuhusu Hadiyth kuliko mimi. Kwa hiyo Hadiyth ikiwa ni Swahiyh basi nijulishe, ikiwa ni kutoka Kufah, Basrah au Syria, ili nichukue rai ya Hadiyth madamu tu ni Swahiyh"[21] 

 

  1. "Katika kila jambo, ambako wenye kusimulia wakipata ripoti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo ni kinyume na niliyoyasema, basi narudisha kauli yangu nyuma, ikiwa wakati wa maisha yangu au hata baada ya kufa kwangu"[22]   

 

  1. "Ukinisikia nasema kitu, na kinyume chake ni Hadityh Swahiyh kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi tambua kuwa akili yangu imetoweka"[23]   

 

  1. "Kwa kila ninalosema, ikiwa upo usimulizi ulio Swahiyh, basi Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) inakuja mwanzo, kwa hiyo usifuate rai yangu"[24]   

 

  1. "Kila kauli kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni rai yangu pia, japokuwa hujaisikia kutoka kwangu"[25]    

 

 

4) AHMAD BIN HANBAL (رحمه الله)

 

Imaam Ahmad alikuwa wa mbele miongoni mwa Maimaam kukusanya Sunnah na kuzishikilia sana hadi   alichukizwa kuona kinaandikwa kitabu kilichokusanya mambo yaliyogeuzwa na mambo yaliyotegemea rai zaidi[26]  kwa hilo akasema:   

 

  1. Msifuate rai yangu, wala msifuate rai ya Maalik, au Ash-Shaafi'iy au ya Awzaa’iy, wala Ath-Thawriy, lakini chukueni kutoka kule  walikotoa"[27]  

Katika usimulizi mmoja: "Msiige dini yenu kutoka kwa mtu yeyote katika hawa, bali chochote kilichotoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake, chukueni, kisha kwa At-Taabi'iyn (Waliofuata) ambako mtu ana khiari".

Mara moja kasema: "Kufuata[28] ina maana kwamba mtu anafuata yaliyokuja kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake, ama baada ya  At-Taabi'iyn (Waliofuata) anayo khiari" [29]   

  1. "Rai ya Awzaaiy, rai ya Maalik, rai ya Abu Haniyfah, zote ni rai, na ni sawa katika macho yangu. Lakini, dalili ni yale masimulizi kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake"[30]  

 

  1. "Yeyote atakayekanusha kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) basi yumo katika ukingo wa kuangamia"[31]            

Hizi ndizo kauli za wazi kabisa za Maimaam, Allaah (سبحانه وتعالى) Awe radhi nao, kuhusu kushikamana na Hadiyth na kukataza kufuata rai zao bila ya kuwa na dalili iliyo dhahiri kabisa.

Kwa hiyo, yeyote aliyeshikamana na lolote la Sunnah ambayo imeshuhudiwa kuwa ni Swahiyh hata kama imepinga kauli ya baadhi ya Maimaam, hatokuwa anapingana na madhehebu yao, wala hatopotoka katika njia zao, bali mtu huyo atakuwa anawafuata wote na atakuwa amekamata kile kilichoaminiwa zaidi akishika mkono ambao hautavunjika. Lakini hii haitakuwa hali ya yule anayeziweka kando Sunnah Swahiyh kwa sababu tu zimepingana na rai za Maimaam, bali mtu huyo atakuwa sio mtiifu kwao na amepingia kauli zao hizo za juu. Na tunaona Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

((فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيمًا))

((La! Naapa kwa Mola! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.))[32]  

((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))

((Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo))[33]

 

Haafidhw Ibn Rajab Al-Hanbali (رحمه الله) amesema: "Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu yeyote anayesikia amri ya Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) au kuijua, kuielezea kwa Ummah, kuwapa nasaha ya dhati na kuwaamrisha kufuata amri zake japo kama itakuwa ni kinyume na rai ya mtu mkubwa. Hii ni kwa sababu hukmu ya Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) ina haki zaidi kuheshimiwa na kufuatwa kupita rai za mtu yeyote mkubwa aliyekwenda kinyume bila ya kujua na amri za Mtume katika jambo lolote. Ndio maana Maswahaba na waliofuatia walimpinga yeyote aliyekwenda kinyume na Sunnah Swahiyh, mara nyingine wakiwa wakali katika kuwapinga kwao[34], sio kutokana na kumchukia huyo mtu, bali alikuwa ni mpenzi wao na mwenye kuheshimiwa, lakini kwa sababu Mjumbe wa Allaah alikuwa mpenzi wao zaidi na amri zake zilikuwa juu ya amri za viumbe wengine. Hivyo inapokuwa amri ya Mtume na ya mtu mwengine zinapingana, amri ya Mtume huwa ndiyo ipasayo kutiliwa nguvu na kutekelezwa. Hakuna katika hili lingeliwazua wasimheshimu mtu waliyempinga kwa sababu wamejua kuwa atasamehewa[35] , bali aliyetajwa mwisho hatojali amri zake kupingwa itakapokuwa amri za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zimeonyesha dhahiri kuwa ni kinyume chake [36]

Vipi wachukiwe hayo ikiwa wamewajibisha wafuasi wa kama ilivyo, na kama tulivyoona, kuwa wameamrisha waziache kando rai zao zinazokwenda kinyume na za Sunnah. Bali Imaam ash-Shaafi'iy (رحمه الله) aliwaambia Maswahaba zake kuzihusisha kwake Sunnah zilizo Swahiyh pia, japo kama hakuzitekeleza  au katekeleza zilizo kwenda kinyume nazo. Hivyo mhakiki Ibn Daqiyq alipokusanya pamoja katika mjalada mzito, mas-ala ambayo kila mmoja katika kauli za madhehebu ya Maimaam wanne kuwa yamekwenda kinyume na Hadiyth Swahiyh, kama alivyaondika mwanzoni mwake: "Imekatazwa kuhusisha majibu haya kwa Maimaam waliojitahidi na ni fardhi kwa wanasheria wanaofuata rai zao kujua hizi ili wasije kuzinukuu wakawazulia"[37]

 

Wafuasi Wa Maimaam Kuacha Rai Zao Ikiwa Zinapingana na Sunnah

 

 

Kutokana na yote tuliyotaja, wafuasi wa Maimaam,  ((Fungu kubwa katika wa mwanzo Na wachache katika wa mwisho))[38] hawakubali rai za Imaam wao, bali wanazipuuza nyingi wanapotambua kuwa zinakenda kinyume na za Sunnah. Hata Maimaam wawili Muhammad Ibn Al-Hasan na Bu Yuusuf (رحمها الله) walikhitilafiana na Shekhe wao Abu Haniyfah 'Fiy Nahw thuluth al-madhhab'[39]kama vitabu vya masaail vinavyothibitisha. Imesemwa hivyo hivyo kuhusu Imaam Al-Muzaniy[40] na wafuasi wengineo wa Ash-Shaafi'iy na Maimaam wengine. Tungelianza kutoa mifano majadiliano yangeliendelea kuwa marefu na tungelitoka nje ya makusudio katika mas-ala utangulizi huu, hivyo tutajiwekea mipaka kwa mifano miwili:

 

1.     Imaam Muhammad amesema katika Muwattwa yake[41] (Uk. 158). "Ama Abu Haniyfah hakuona kuwa kuna Swalah ya kuomba mvua, lakini kauli yetu ni kwamba Imaam anaswali Rakaa mbili na anaomba du'aa na anashika shuka yake…"

 

2.     Tunaye 'Iswaam bin Yuusuf Al-Balkhiy mmoja wa wafuasi wa Imaam Muhammad[42]  na mtumishi wa Imaam Abu Yuusuf[43] ambaye akitoa hukmu kinyume na Imaam Abu Haniyfah kwa sababu hakujua ushahidi wake na ushahidi mwingine ulijitokeza kwake wenyewe hivyo alikuwa akiutolea hukmu:[44]. Hivyo alinyanyua mikono katika rukuu (kwenye Swalah) na anaponyanyuka[45] kama ilivyo mutawaatir Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) bali Maimaam wake watatu (yaani Abu Haniyfah, Abu Yuusuf na Muhammad) wamesema vinginevyo na hawakumzuia kutekeleza Sunnah. Huu ni mfano ambao kila Muislamu inampasa kuwa nao kwani tumeshaona kutokana na ushahidi wa Maimaam wanne na wengineo huko juu.

 

 

 

 


 

[1]   Hii ni aina ya taqliyd (kufuata kwa upofu [kiujinga]) ambayo Imaam At-Twahaawiy alihusisha aliposema: "Hafuati rai ila ni mtu mkaidi au mjinga" (kufuata kama kipofu)

[2]   Al-A'raaf:3

[3]    Ibnul-'Aabidiyn katika al-Haashiyah (1/63) na katika inshaa yake   Rasm al-Mufti (1/4 kutoka Mkusanyiko wa Inshaa za Ibnul-'Aabidyin). Shaykh Swaalih Al-Fulaaniy katika al-Iyqaadhw al-Himaam (uk.62) na wengineo. Ibnul-'Aabidiyn amenukuu kutoka Sharh al-Hidaayah ya Ibn Al-Shahnah Al-Kabiyr, mwalimu wa Ibn Al-Himaam, kama ifuatavyo:

"Ikiwa Hadiyth iliyo kinyume na Madhehebu imeonekana kuwa ni Swahiyh basi mtu atende kwa kufuata hiyo Hadiyth na aifanye kuwa ni madhehebu yake. Kuifanyia kazi Hadiyth hakutombatilisha mtu kuwa sio mfuataji wa madhehebu ya Hanafi, kwani imeripotiwa kuwa Abu Haniyfah alisema: "Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu". Na hii imeelezewa na Imaam Ibn 'Abdil-Barr kutoka kwa Abu Haniyfah na kutoka kwa Maimaam wengine".

Hii ni sehemu ya ukamilifu wa elimu na uchaji Allaah wa Maimaam, kwani wameonyesha kwa kusema kwamba wao hawakuwa na maarifa (elimu) kamili ya Sunnah zote. Na Imaam Ash-Shaafi'iy amefafanua wazi wazi (tazama mbele). Hutokea wanapokwenda kinyume na Sunnah huwa ni kwa sababu hawakuitambua. Ndipo walipotuamrisha tushikilie Sunnah na tuizingatie kuwa ni sehemu ya madhehebu yao. Allaah Awashushie Rahma Yake kwao wote.

[4]    Sio halaal

[5]   Ibn 'Abdil-Barr katika Al-Intiqaa' fiy Fadhwaail Ath-Thalaathah Al-Aimmah Al-Fuqahaa (uk.145), Ibn Al-Qayyim katika 'I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/ 309), Ibn 'Aabidiyn katika tanbihi zake kwenye Al-Bahr Ar-Raa'iq (6/ 293) na katika Rasm Al-Mufti (uk. 29, 32) na Sha'raaniy katika Al-Miyzaan (1/ 55) pamoja na usimulizi wa pili. Usimulizi wa mwisho ulikusanywa na 'Abbaas Ad-Dawriy katika At-Taariykh ya Ibn Ma'iyn (6/ 77/1) ikiwa na Isnaad Swahiyh kutoka kwa Zafar, mwanafunzi wa Imaam Abu Haniyfah. Usimulizi uliofanana upo kutoka kwa wafuasi wa Abu Haniyfah; Zafar, Abu Yuusuf na 'Aafiyah bin Yaziyd; taz. Al-Iyqaadhw (uk. 52). Ibn Al-Qayyim alithibitisha kwa nguvu usahihi wake kutoka kwa Abu Yuusuf katika I'laam Al-Muwaqi'yn (2/ 344). Nyongeza ya usimulizi wa pili unarejewa na mwandishi wa Al-Iyqaadhw (uk. 65) kwa Ibn 'Abdil-Barr, Ibn Al-Qayyim na wengineo.

     Ikiwa hivi ndivyo wanavyosema kwa mtu asiyejua dalili zao, jibu lao litakuwa nini kwa yule anayetambua kuwa dalili zinapingana na kauli yao, lakini bado anatoa hukumu iliyopinga dalili? Kwa hiyo, fuata usemi huu, kwani pekee unatosheleza kuvunja ufuataji rai kwa ujinga. Ndio maana nilipomlaumu mmoja wa Mashaykh (Muqallid) wa madhehebu katika kutoa fatwa (hukm) kwa kutumia maneno ya Abu Haniyfah bila ya kujua dalili, aligoma kuamini kuwa hiyo ni kauli ya Abu Haniyfah!

 

[6]    Haraam

[7]     Fatwa

[8]  Mwanafunzi mashuhuri wa Imaam Abu Haniyfah, Abu Yuusuf  (رحمه الله)

[9]  Hii ni kwa sababu Imaam kawaida hutoa rai yake kutokana na Qiyaas (analojia). Kisha tena hupata analojia iliyo na nguvu zaidi, au Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) humfikia. Kwa hiyo huikubali hiyo na kuipuuza rai yake ya nyuma. Maneno ya Sha'araaniy katika Al-Miyzaan (1/62) yamewekwa kwa mukhtasari kama ifuatavyo:

     "Imani yetu na ya kila mtafiti wa Imaam Abu Haniyfah (رحمه الله) ni kwamba, aliishi hadi iliporikodiwa Sharia. Na safari za wahifadhi wa Hadiyth katika miji mbali mbali na mipakani kwa ajili ya kukusanya na kuzipata. Angeliipokea na kupuuza analojia zote ambazo alizozitumia, idadi za Qiyaas katika madhehebu yake zingelikuwa kidogo kama zilivyo katika madhehebu mengine. Lakini kwa vile dalili za Sharia zimetapakaa kwa Waliotangulia na waliowatangulia, na haizikukusanywa wakati wa maisha yake, ilihitajika kuwepo Qiyaas nyingi katika madhehebu yake kulingana na Maimaam wengine. Maulamaa wa baada ya hapo, kisha wakafanya safari kutafuta na kukusanya Hadiyth kutoka nchi mbali mbali na miji na wakaziandika. Hivyo baadhi ya Hadiyth za Sharia zimeelezea nyingine. Hii ni sababu ya kuweko idadi kubwa ya qiyaas katika madhehebu yake wakati kwenye madhehebu mengine ilikuwa ni idadi ndogo"

     Abul-Hasanaat Al-Laknawiy amenukuu maneno yake kikamilifu katika An-Naafi' Al-Kabiyr (uk. 135) akiandika na kupanua tanbihi zake. Kwa hiyo yeyote anayependa kutafuta maelekezo yake afanye humo.

     Kwa vile hii ni uthibitishaji kuwa kwa nini Abu Haniyfah mara nyingine alikhitilafiana na Hadiyth zilizokuwa Swahiyh bila ya kukusudia na ni sababu barabara ya kukubaliwa, kwani Allaah Haikalfishi nafsi kwa yale isiyoweza kubeba. Hairuhusiwi kumtukana kwa sababu hiyo kama walivyofanya watu wajinga. Bali ni wajibu kumheshimu, kwani yeye ni mmoja wa Maimaam wa Waislamu ambao wameihifadhi hii dini hadi ikafikishwa kwetu kutoka katika kila matawi yake. Na kwa vile yeye analipwa (Na Allaah سبحانه وتعالى) kwa hali yoyote ile; ikiwa kapata au amekosea kwa kutokusudia. Wala hairuhusiwi kwa wafuasi wake wapenzi kuendelea kushikilia kauli zake ambazo zinakhitilafiana na Hadiyth zilizo Swahiyh kwani kauli hizo sio madhehebu yake kama kauli zake hapo juu zilivyosema. Kwa hiyo hii ni mipaka miwili; ukweli na uongo katika yake. ((Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala Usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu)) [Al-Hashr 59:10]

[10] Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw Al-Himaam (uk.50), ikifuatilia kwa Imaam Muhammad na kisha kusema: "Hii haimhusu Mujtahid, (mwenye kujitahidi kwa elimu yake na kutoa hukmu) kwa vile hakujifunga katika rai zao, bali inamhusu Muqallid (mwenye kufuata).

 

[11] Ibn 'Abdil-Barr katika Jaami'ul Bayaan Al-'Ilm (2/32), Ibn Hazm   akinukuu kutoka kwake katika Uswuul-Al-Ahkaam (6/149) na hali kadhaalika Al-Fulaaniy (uk. 72).

 

[12]  Hii inajulikana sana miongoni mwa Maulamaa wa baadaye kuwa ni kauli ya Maalik. Ibn 'Abdil-Haadiy alikiri kuwa ni Swahiyh katika Irshaad As-Saalik (227/1); Ibn 'Abdil-Barr katika Jaami'ul-Bayaan Al-'Ilm (2/91) na Ibn Hazm katika Uswuul Al-Ahkaam (6/145, 179) alisimulia kama ni kauli ya Al-Hakam bin 'Utaybah na Mujaahid; Taqiyud-Diyn As-Subki alisimulia  katika Al-Fataawa (1/148) kama ni kauli ya Ibn 'Abbaas akishangazwa kwa uzuri wake kisha akasema: "Haya maneno yameanzia kwa Ibn 'Abbaas na Mujaahid, na Maalik (رحمه الله) aliyachukua, na akawa mashuhuri kwayo". Inavyoelekea kwamba Imaam Ahmad kisha akachukua kauli hii kutoka kwao, kama Abu Daawuud alivyosema katika Masaail ya Imaam Ahmad (uk 276). "Nilimisikia Ahmad akisema: Kila mmoja anapokelewa na anakatiliwa katika rai zake, isipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)"

 

[13]  Kutoka kwa Utangulizi wa Al-Jarh wat-Ta'diyl ya Ibn Abi Haatim (uk. 31-32)

 

[14]    Ibn Hazm anasema katika Uswuul al-Ahkaam (6/118)

"Hakika, Mafuqahaa wote ambao rai zao zilikuwa zikifuatwa zilipingwa kwa taqliyd na waliwakataza wafuasi wao kufuata rai zao kijinga. Aliyekuwa mkali kabisa miongoni mwao ni Ash-Shaafi'iy (رحمه الله), kwani yeye alirudia kutilia mkazo zaidi kuliko yeyote mwengine kufuata usimulizi ulio Swahiyh na kukubali dalili yoyote iliyoamriwa. Vile vile alidhihirisha wazi na kujitenga kuwa hana hatia ikiwa atafuatwa yeye tu pekee na aliwatangazia hayo wale waliokuwa naye. Tunaomba hii imnufaishe mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) na thawabu zake ziwe za juu kabisa kwani alikuwa ni sababu ya mema mengi".

[15] Imesimuliwa na Al-Haakim ikiwa ina isnaad ya kuendelea hadi kwa Ash-Shaafi'iy kama ilivyo katika Taariykh Dimashq ya Ibn 'Asaakir (15/1/3), I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/363,364) na Al-Iyqaadhw (uk. 100)

[16] Halaal

[17] Ibn al-Qayyim (2/361) na Al-Fulaaniy (uk. 68)

[18] Al-Haraawiy katika Dhamm Al-Kalaam (3/47/1) Al-Khatiyb katika Al-Ihtijaaj bi Ash-Shaafi'iy (8/2), Ibn 'Asaakir (15/9/10), An-Nawawiy katika Al-Majmuu' (1/ 63), Ibn al-Qayyim (2/ 361), na Fulaani (uk. 100) usimulizi wa pili ni kutoka Hilyah Al-Awliyaa ya Abu Nu'aym.

 

[19] An-Nawawiy katika Al-Majmuu' (1/ 63), Sha'raaniy (1/ 57), akitoa chanzo chake kama Al-Haakim na Al-Bayhaqiy na Al-Fulaaniy (uk. 107). Ash-Sha'raaniy kasema: "Ibn Hazm kasema: "Kwamba imeonekana ni Swahiyh naye au kwa Imaam mwengine". Kauli yake nyingine imethibitisha ufahamu huu.

     An-Nawawiy amesema: "Wafuasi wetu walitenda kutokana na hili katika mambo ya tathwiyb (mwito wa Swalah baada ya adhana), shuruti za kutoka katika ihraam kwa ajili ya ugonjwa, na mambo mengine yaliyojulikana vyema katika vitabu vya madhehebu. Miongoni wafuasi wetu ambao wameripotiwa kuwa walitoa hukumu kutokana na chanzo cha Hadiyth (yaani kuliko kuchukua kauli ya Ash-Shaafi'iy) ni Abu Ya'quub Al-Buwiity na Abul-Qaasim Ad-Daarikiy. Wafuasi wa Muhaddithiyn (Wakusanyao Hadiyth), Imaam Abu Bakr Al-Bayhaqiy na wengineo walitenda kwa kufuata kauli hii. Wafuasi wengi wetu wa zamani, walipokumbana na jambo ambalo ilikuweko Hadiyth na madhehebu ya Ash-Shaafi'iy yalikuwa ni kinyume nalo, basi walitenda  kwa kufuata Hadiyth na kutowa fatwa (hukmu) pia wakisema: "Madhehebu ya Ash-Shaafi'iy ni kila kinachokubaliana na Hadiyth". Shaykh Abu 'Amr (Ibn Asw-Swalaah) alisema: "Yeyote miongoni mwa Ash-Shaafi'iy akiona Hadiyth inayopinga madhehebu yake, alichukulia kama alitimiza shuruti za Ijtihaad kwa kawaida, au katika maudhui au jambo lile khaswa ambalo alikuwa huru kutenda kwa kufuata Hadiyth; kama sio. Lakini hata hivyo aliona vigumu kupingana na Hadiyth baada ya utafiti zaidi, hakuweza kupata uthibitishaji wa kukinaisha wa kupinga Hadiyth. Kwa hiyo, alibakia kutenda kwa kufuata Hadiyth ikiwa Imaam mwengine mwenye kujitegemea mbali na Ash-Shaafi'iy, basi alitenda kuifuata. Na hii huwa ni kithibitisho chake cha kuacha madhehebu ya Imaam wake katika jambo hilo". Alichosema (Abu 'Amr) ni Swahiyh na lililokubalika. Na Allaah Anajua zaidi.

     Kuna uwezekano mwingine ambao Ibn As-Swalaah alisahau kutaja: Afanyeje mtu ikiwa hakumpata mtu yeyote ambaye alitenda kwa kufuata Hadiyth? Hii imejibiwa na Taqiyud-Diyn As-Subkiy katika makala yake 'Maana Ya Kauli ya Ash-Shaafi'iy: Ikiwa Hadiyth ikipatikana kuwa ni Swahiyh, basi ndio madhehebu yangu' (uk. 102, Mjalada 3). "Kwangu, lililo bora kabisa ni kufuata Hadiyth. Mtu na awaze kwamba yuko mbele ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kama vile ameisikia kutoka kwake, je, atakwenda demani (kufuata mweleko wa upepo) acheleweshe kutenda kwa kuifuata? Hapana! WaLLaahi, na kila mmoja anabeba jukumu kutokana na ufahamu wake".

     Mjadala wake uliobakia umetolewa kuchambuliwa  katika I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/ 303, 370)  na katika kitabu cha Al-Fulaaniy, (Kichwa cha habari kamili) Al-Iyqadhw Himam Uwl Al-Abswaar, Lil-iqtidaa Bisayyid Al-Muhaajiriyn Wal-Answaar, wa Tahdhiyrihim 'An Al-Ibitidaa' Ash-Shaai' fit-Quraa Wal-Amswaar, Min Taqlyid Al-Madhaahib Ma'a Al-Hamiyyat Wal-'Aswabiyyat Bayna Fuqahaa Al-A'swaar"

     Kitabu hicho ni cha pekee katika maduhui hii, ambacho kila mpenda haki akisome kwa ufahamu na kutafakari.

[20]  Akimwambia Imaam Ahmad bin Hanbal (رحمه الله)

[21] Imesimuliwa na Ibn Abi Haatim katika Aadaabu Ash-Shaafi'iy (uk. 94-5), Abu Nu'aym katika Hulya Al-Awliyaa (9/ 106), Al-Khatwiyb katika Al-Ihtijaaj Bish-Shaafi’iy (8/1) na kutoka kwake Ibn 'Asaakir (15/ 9/1), Ibn 'Abdil-Barr katika Al-Intiqaa' (uk. 75), Ibn Al-Jawziy katika Manaaqib Al-Imaam Ahmad (uk. 499) na Haraawiy (2/ 47/2) katika njia tatu kutoka kwa 'Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal kutoka kwa baba yake kwamba Ash-Shaafi'iy alimhusisha nayo katika I'laam (2/325) kama alivyofanya Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw (uk. 152) na kisha akasema: "Al-Bayhaqiy amesema: "Hii ndio maana yeye, yaani Ash-Shaafi'iy alitumia Hadiyth sana, kwa sababu alikusanya elimu kutoka kwa watu wa Hijaaz, Syria, Yemen na Iraq. Kwa hiyo alikubali yote aliyoona kuwa ni Swahiyh bila ya kutegemea au kuangalia yale yaliyokuwa nje ya madhehebu ya watu wa nchi yake, wakati ukweli ulipodhihirika kwake kutoka sehemu nyingine. Wengineo kabla yake, walijiwekea mipaka kwa waliyoyakuta katika madhehebu ya watu wa nchi yao bila ya kujaribu kuhakikisha usahihi wa yale yaliyokuwa kinyume nayo. Allaah Atusamehe sote"   

[22] Abu Nu'aym (9/ 107), Harawiy (47/ 1), Ibn al-Qayyim katika I'laam Al-Muwaqqi'iyn (2/ 363) na Fulaani (uk. 104)

[23] Ibn Haatim katika Al-Adaab (Uk. 93), Abul-Qaasim Samarqandi katika Al-Amaal, kama katika uchaguzi kutoka kwa Abu Hafsw al-Mu'addab (234/ 1), Abu Nu'aym (9/ 106), na Ibn 'Asaakir (15/ 10/1) ikiwa ni sanad Swahiyh.

 

[24]    Ibn Abi Haatim, Abu Nu'aym na Ibn 'Asaakir (15/ 9/2)

[25]    Ibn Abi Haatim (uk. 93-4)

[26]    Ibn Al-Jawziy katika Al-Manaaqib (uk. 192)

[27]    Al-Fulaaniy (Uk. 113) na Ibn Al-Qayyim katika I'laam

[28]    Ittibaa'

[29]    Abu Daawuud katika Masaail ya Imam Ahmad (uk. 276-7)

[30]     Ibn 'Abdil-Barr katika Jaami' Bayaan Al-'Ilm

[31]     Ibn Al-Jawziy (uk. 182)

 

[32]    An-Nisaa:4:65

[33]    An-Nuur: 24:63

[34]    Japokuwa ni dhidi ya baba zao na walimu wao, kama Atw-Twahaawiy katika Sharh Ma'aaniy Al-Aathaar (1/ 372) na Abu Ya'laa katika Musnad yake (3/ 1317) wamesimulia, ikiwa na isnaad ya watu walioaminika kutoka kwa Saalim bin 'Abdillaah bin 'Umar (رحمه الله) ambaye amesema:

"Nilikuwa nimekaa na Ibn 'Umar (رضي الله عنه) msikitini siku moja, alikuja mtu kutoka Syria na akamuuliza kuhusu kuendeleza 'Umrah pamoja na Hajj (Inayojulikana kama ni Hajj At-Tamaattu'). Ibn 'Umar akajibu: 'Ni vizuri na jambo jema'. Kisha mtu akasema: 'Lakini baba yako (yaani 'Umar bIn Al-Khattwaab) alikuwa akikataza' Basi Akasema,' Ole wako! Ikiwa baba yangu alikuwa akikataza kitu ambacho Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم)alikuwa akifanya na kuamrisha, je, utakubali rai ya baba yangu au amri ya Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم)?' Akajibu: 'Amri ya Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم)' Akasema: 'Basi nenda zako mbali na mimi' Ahmad (Namba 57000) amesimulia kama hivyo kama alivyosimulia At-Tirmidhiy (2/ 82) na amekiri kuwa ni Swahiyh.

 

[35]   Bali atalipwa thawabu kwa sababu ya kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Qaadhi akipitisha hukmu, akifanya juhudi (ijtihaad) na hukmu ikawa Swahiyh atapata thawabu mbili. Akifanya juhudi (ijtihaad) na akahukumu kimakosa, atapata thawabu moja)) [Imesimuliwa na Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]

[36]   Imenukuliwa katika tanbihi za 'Iyqaadhw al-Himam (Uk. 93)

[37]   Fulaaniy (Uk. 99)

[38]   Suratul Al-Waaqi'ah 56: 13-14

[39]   Ibn 'Aabidiyn Katika 'al-Haashiyah (1/ 62) na Al-Laknawiy kaipa chanzo chake kutoka katika An-Naafi' al-Kabiyr (Uk. 93) ya Al-Ghazaaliy.

[40]   Yeye mwenyewe amesema katika mwanzo wa 'Mukhtaswar Fiy Fiqhis-Shaafi'iy' (iliyochapishwa katika pembizo ya 'Al-Umm') "Kitabu hiki ni uchaguzi kutoka elimu ya Muhammad bin Idriys Ash-Shaafi'iy (رحمه الله) na kutokana na maana ya kauli zake kumsaidia yeyote anayekitaka akiwa anajua makatazo ya kufuata rai yake au ya yoyote mwengine ili mtu azingatie dini yake"

[41]   Ambako ameelezea kumpinga Imaam wake katika masaail ishirini (Namba 42, 44, 103, 120, 158, 169, 172, 173, 228, 230, 240, 244, 274, 275, 284, 314, 331, 338, 355, 356 kutoka Ta'liyq Al-Mummajjid 'alaa Muwattwa' Muhammad (Tanbihi muhimu ya Muwattwa ya Muhammad)

[42]   Ibn 'Aabidiyn amemtaja miongoni katika 'Al-Haashiyah' (1/ 74) na katika 'Rasm Al-Muftiy (1/17). Qurayshi amemtaja katika 'Al-Jawaahiyr Al-Madhwiyyah fiy Twabaqaat Al-Haniyfah' (uk. 347) na akasema: "Alikuwa ni msimulizi wa Hadiyth wa kutegemewa. Yeye na kaka yake Ibraahiym walikuwa Mashaykh wawili wa Al-Balakh katika zama zao".

[43]   Al-Fawaaid Al-Bahiyyah Fiy Taraajim Al-Hanafiyyah (uk. 116)

[44]   Al-Bahr Ar-Raaiq (6/ 93) na Rasm Al-Muftiy (1/ 28)

[45]   Al-Fawaaid … (uk. 116) kisha muandishi akaongeza tanbihi yenye faida:

"Kutokana na hii inawezekana kutambulika ubatilifu wa usimulizi wa Makhuul kutoka kwa Abu Haniyfah: 'Kwamba mwenye kunyanyua mikono yake katika Swalah, Swalah yake itakuwa batili' ambayo Amiyr mwandishi wa al-Itqaaniy alivyohadaiwa kama ilivyotajwa kaitka historia yake. 'Iswaam Ibn Yuusuf, mfuasi wa Abu Yuusuf alikuwa akinyanyua mikono yake.  

 

Share [8]

006-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuelekea Ka'abah Na Kusimama Kwenye Swalah

 

KUELEKEA QIBLAH

 

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa anasimama kuswali Swalah zote za Fardhi na za Sunnah alikuwa anaelekea upande wa Ka'abah[1]

 

Naye Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliliamrisha hilo kwa kumwambia "mtu aliyeswali vibaya”[2]: ((Unaposimama kuswali, fanya wudhuu sawasawa, kisha elekea Qiblah na upige Takbiyr))[3].

 

"Wakati yuko safarini, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalah za Sunnah na Swalah ya Witr na huku amepanda mnyama popote alipoelekea. (Mashariki au Magharibi)[4]

 

 

Hilo ni kwa Neno Lake Allaah Mtukufu:

 

 فَأَيْنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجْهُ ٱللَّهِ  ... 

((Basi kokote mnakoelekea, huko kuna wajihi wa Allaah))

[Al-Baqarah: 115]

 

Kauli hii inahusiana na Hadiyth hiyo[5] .

 

“Wakati mwengine alipokuwa anataka kuswali Swalah zisizo za fardhi juu ya ngamia wake, alikuwa akimwelekeza Qiblah, kisha akisema Takbiyr na akiswali kuelekea popote kule msafara unapoelekea.”[6].

 

"Alikuwa akifanya rukuu na sujuud huku amempanda mnyama kwa kuinamisha kichwa chake, na akiinamisha kichwa zaidi chini katika sujuud kuliko alivyoinamisha katika rukuu.”[7]

 

"Alipotaka kuswali Swalah za fardhi alikuwa akiteremka kutoka kwa mnyama na akielekea Qiblah.”[8]

 

Ama katika Swalah ya mtaharuki wa vita vilivyopamba moto, Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم) aliweka kwa ummah wake kanuni ya kuswali "wakiwa wamesimama na kutembea kwa miguu yao, au wakiwa wamepanda mnyama, wakielekea Qiblah au kutokuelekea”[9]. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: ((Wanapokutana majeshi Swalah ni Takbiyr na kuashiria kwa kichwa))[10]

 

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  pia alikuwa akisema ((Kilichokuweko baina ya Mashariki na Magharibi ni Qiblah))[11] [9]

 

Jaabir (رضي الله عنه) amesema,

"Mara moja tulikuwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  katika msafara au kikosi cha jeshi, na kulikuwa na mawingu, tukajaribu kutafuta Qiblah lakini tulikhtilafiana, kwa hiyo kila mmoja wetu akaswali kuelekea upande tofauti na kila mmoja wetu alichora mstari mbele yake ili kuweka alama mahali pake. Ilipofikia asubuhi, tukazitazama tukaona kwamba hatukuswali kuelekea Qiblah. Kwa hiyo tukamuelezea Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)  lakini hakutuamrisha tuirudie (Swalah) na akasema:

((Swalah yenu imetosheleza)).[12] [10]

 

Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kuelekea Bayt Al-Maqdis (na Ka'abah ikiwa mbele yake) kabla ya kuteremshwa Aayah ifuatayo:

 

قَدْ نَرَىٰ تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِي ٱلسَّمَاء فَلَنُوَلّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلّ وَجْهَكَ شَطْرَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمْ شَطْرَهُ ...

((Kwa yakini tukiona unavyo geuza geuza uso wako mbinguni. Basi Tutakuelekeza kwenye Qiblah ukipendacho. Basi elekeza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu; na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu upande huo…)) [Al-Baqarah, 2: 144]

 

Ilipoteremshwa Aayah hii alielekeza uso wake Ka'abah.  Walikuwa watu katika msikiti wa Qubaa' wakiswali Swalah ya Alfajiri, alipokwenda mtu kuwaambia "Hakika Mtume wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameteremshiwa Aayah jana usiku na ameamrishwa kuelekeza uso wake Ka'bah. Basi jueni na elekeeni huko". Nyuso zao zilikuwa zimeelekea Shaam kwa hiyo wakageuka (na Imaam wao akageuza uso kuelekea Qiblah pamoja nao).[13] [11]

 

 

 

KUSIMAMA KATIKA SWALAH

 

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali kwa kusimama katika Swalah zote mbili za fardhi na za Sunnah kwa kufuata maamrisho ya Allaah 

 

وَقُومُواْ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ  

((…na simameni kwa ajili ya Allaah nanyi ni kuqunuti (kunyenyekea)) [Al-Baqarah, 2: 238]

 

 

Ama katika safari alikuwa akiswali Swalah za Sunnah na huku amempanda (mnyama).

 

Ameweka kanuni kwa ummah wake kuswali wakati wa khofu kubwa kwa kusimama juu ya mnyama. Na hili ni kwa Neno Lake Allaah Mtukufu:

 

حَـٰفِظُواْ عَلَى ٱلصَّلَوٰتِ وٱلصَّلَوٰةِ ٱلْوُسْطَىٰ وَقُومُواْ لِلَّهِ قَـٰنِتِينَ   فَإنْ خِفْتُمْ فَرِجَالاً أَوْ رُكْبَانًا فَإِذَا أَمِنتُمْ فَٱذْكُرُواْ ٱللَّهَ كَمَا عَلَّمَكُم مَّا لَمْ تَكُونُواْ تَعْلَمُونَ 

 

 ((Zilindeni Swalah, na khasa Swalah ya katikati,[14] [12] na simameni kwa ajili ya Allaah nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea))) 

 

 ((Ikiwa mnakhofu (Swalini) na hali mnakwenda kwa miguu au mmepanda. Na mtakapokuwa katika amani, basi mkumbukeni Allaah kama Alivyokufunzeni yale mliyokuwa hamyajui)) [Al-Baqarah, 2: 238-239]

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali kwa kukaa wakati alipokuwa akiumwa hata akafariki[15] [13]. Vile vile aliswali kwa kukaa kwa mara nyingine kabla ya hivyo wakati alipojeruhiwa, na watu waliokuwa nyuma yake waliswali kwa kusimama, akawaashiria wakae nao, wakakaa (na kuswali).  Alipomaliza, akasema, Mlikuwa mnataka kufanya kama wanavyofanya wa-Fursi na Warumi wanavyofanya, wanawasimamia wafalme wao waliokuwa wanakaa. Kwa hiyo msifanye hivyo tena, kwani Imaam ni kwa ajili ya kumfuata, anapofanya rukuu fanyeni rukuu, anaposimama simameni, anaposwali kwa kukaa na nyinyi swalini kwa kukaa (nyote).[16] [14]

 

 

[1] [15] Jambo hili halina shaka yoyote kutokana na mlolongo wa umashuhuri wake (tawaatur). Kwa hiyo, halihitaji maelezo zaidi ingawa baadhi ya dalili zitafuata.

 

[2] [16] Tazama Kiambatisho 3.

 

[3] [17] Imekusanywa na Al-Bukhaariy, Muslim na Siraaj.

 

[4] [18] Imekusanywa na Al-Bukhaariy, Muslim na Siraaj. Takhriyj yake imetolewa katika “Irwa'a Al-Ghaliyl” (289 na 588).

 

[5] [19] Muslim. At-Tirmidhiy amekiri kuwa ni Hadiythi Swahiyh.

 

[6] [20]Abu Daawuud na Ibn Hibbaan katika “Ath-Thiqaat” (1/12) na Adh-Dhiyaa  katika “Al-Mukhtaarah” ikiwa na sanad hasan. Ibn As-Sukn amekiri kuwa ni Swahiyh na pia Ibn al-Mulaqqin katika “Khulaaswat Al-Badr Al-Muniyr” (22/1) na kabla yao, ‘Abdul-Haqq Al-Ishbiyli katika “Ahkaamuh” (Namba 1394 kwa uhakiki wangu). Ahmad ameitumia kama ni uthibitisho kama alivyoripoti Ibn Haani kutoka kwake katika “Masaailuh” (1/67).

 

[7] Ahmad na At-Tirmidhiy ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh.

 

[8] Al-Bukhaariy na Muslim.

 

[9] [21] Al-Bukhaariy na Muslim.

 

[10] [22] Al-Bayhaqiy na Sanad inayoelekeana na mahitajio ya Al-Bukhaariy na Muslim.

 

[11] [23] At-Tirmidhiy na Haakim wamekiri kuwa ni Swahiyh. Nimeitowa katika “Irwaa  Al-Ghaliyl fiy takhriyj Ahaadiyth manaar As-Sabiyl” (292).  Uchapisho wake Allaah (سبحانه وتعالى ) Ameufanya wepesi.

 

[12] [24] Ad-Daara Qutniy, Al-Haakim, Al-Bayhaqiy, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na At-Twabaraaniy.  Imetolewa katika “Al-Irwaa” (296).

 

[13] [25] Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad, As-Siraaj, At-Twabaraaniy (3/108/2) na Ibn Sa'ad (1/243).  Pia iko katika “Al-Irwaa” (290).

 

[14] [26] Yaani Swalah ya 'Alasiri kutokana na usemi ulio Swahiyhi wa Maulamaa wengi. Miongoni mwao ni Abu Haniyfah na wanafunzi wake wawili.   Kuna Hadiyth kuhusu kauli hii ambayo Ibn Kathiyr ameiweka katika Tafsiyr yake ya Qur-aan.

 

[15] [27] At-Tirmidhiy ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Ahmad.

 

[16] [28] Muslim na Al-Bukhaariy na imetolewa katika kitabu changu Irwaa' Al-Ghaliyl katika Hadiyth 394.

 

Share [29]

007-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Swalah Ya Mgonjwa Na Swalah Ya Kwenye Meli

 

SWALAH YA MGONJWA KATIKA HALI YA KUKAA

 

'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه) alisema: "Nilikuwa naumwa ugonjwa wa bawasili (futuru), nikamuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akasema:

((Swali kwa kusimama, ikiwa huwezi, swali kwa kukaa, ikiwa huwezi swali kwa kulala ubavu))”. [1] [30]

 

'Imraan bin Huswayn pia amesema, "Nilimuuliza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Swalah ya mtu anayeswali kwa kukaa, akasema:

((Anayeswali kwa kusimama ni bora, na anayeswali kwa kukaa, thawabu zake ni nusu ya anayeswali kwa kusimama, na anayeswali  kwa kulala (na katika riwaya nyingine kwa kulala chali), basi atapata thawabu nusu ya yule mwenye kuswali kwa kukaa)).[2] [31]

 

Makusudio hapa ni mtu mgonjwa, kwani Anas amesema: "Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka mbele ya watu waliokuwa wakiswali kwa kukaa kwa sababu ya ugonjwa, akasema:

((Hakika Swalah ya mwenye kukaa ni (sawa) na nusu ya Swalah ya mwenye kuswali kwa kusimama)).[3] [32]

 

Siku moja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtembelea mgonjwa na akamuona anaswali (huku ameegemea) juu ya mto. Akauchukua na akautupa (pembeni). Kisha mgonjwa akachukua kipande cha mti ili akiegemee katika Swalah yake. (Mtume) akakichukua akakitupa (pembeni) na akasema:

((Swali juu ya ardhi ukiweza, na kama huwezi, basi fanya harakaati kwa kichwa chako kwa kufanya sujuud iwe ya kuinama chini zaidi ya rukuu)).[4] [33]

 

 

 

SWALAH YA KWENYE MELI (CHOMBO CHA BAHARINI)

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu Swalah katika meli, akasema:   ((Swali ukiwa umesimama ila ukiogopa kuzama)).[5] [34]

 

Alipokuwa mzee mtu mzima, alijiwekea kiguzo katika sehemu ya kuswali ili kukiegemea.[6] [35]

 

 


 


 

[1] [15] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na Ahmad.

 

[2] [16] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud na Ahmad. Al-Khatwaabiy amesema: "Makusudio ya Hadiyth ya 'Imraan ni mgonjwa wa kukisiwa anayeweza kuchechemea na kusimama kwa tabu, na kwa hivyo, thawabu za mwenye kukaa zimefanywa nusu ya mwenye kusimama kwa ajili ya kumpa msukumo asimame ingawa inajuzu kwake kukaa.” Al-Haafidhw Ibn Hajr amesema katika Fat-h Al-Baariy (2/468): “Nayo ni makisio yenye kukubalika.”

 

[3] [17] Ahmad na Ibn Maajah kwa sanad Swahiyh.

 

[4] [18] At-Twabaraaniy, Al-Bazzaar, Ibn As-Samaak katika “Hadiythih” (2/67) na Al-Bayhaaqiy. Sanad yake ni Swahiyh kama nilivyoeleza katika Silisilah Al-Ahaadiyth As-Swahiyhah (323).

 

[5] [19]  Al -Bazzaar (68), Ad-Daaraqutniy na Abdul-Ghaaniy Al-Maqdisi katika “As-Sunan” (2/82). Na Al-Haakim amekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy ameikubali.

 

[6] [20] Abu Daawuud na Al-Haakim ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh kama alivyokiri Adh-Dhahabiy. Nimeiweka katika “As-Swahiyhah” (319) na “Al-Irwaa” (383).

 

Share [36]

008-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kukaa Na Kusimama Katika Swalah Ya Usiku (Tahajjud)

 

 

KUKAA NA KUSIMAMA KATIKA SWALAH YA USIKU (TAHAJJUD)

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa (mara) akiswali usiku mrefu akiwa amesimama na (mara nyingine) akiswali usiku mrefu kwa kukaa. Na alikuwa anaposoma kwa kusimama, hurukuu kwa kusimama, na anaposoma kwa kukaa, hurukuu kwa kukaa.[1]

 

Na wakati mwengine, alikuwa anaswali kwa kukaa, na husoma hivyo hivyo huku amekaa. Na inapobakia katika kisomo chake kiasi cha Aayah thalathini au arubaini hivi, husimama na kuzisoma kwa kusimama, halafu hurukuu na kusujudu. Kisha hufanya hivyo hivyo katika Raka'ah ya pili.[2]

 

 

Bali aliswali Asw-Swubha (Swalah ya Asubuhi)[3] kwa kukaa chini katika siku za mwisho za maisha yake alipokuwa katika umri mkubwa, na na hilo lilikuwa kabla ya kufariki kwake kwa mwaka mmoja.[4]

 

Vile vile alikuwa akikaa kwa kukunja miguu (mkao wa chuoni).[5]

 

 



[1] Muslim na Abu Daawuud.

[2] Al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Ni Swalah ya Sunnah (usiku au jioni) imeitwa hivyo kutokana na yaliyokuwemo humo ya tasbiyh (Kumtukuza Allaah).

[4] Muslim na Ahmad.

[5] An-Nasaaiy, Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/107/2), 'Abdul-Ghaaniy Al-Maqdisi katika Sunan yake (80/1) na al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy amekubali.

Share [37]

009-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Swalah Kwa Kuvaa Viatu Na Swalah Juu Ya Minbar

 

 

SWALAH KWA KUVAA VIATU NA MAAMRISHO YA KUFANYA HIVYO

 

"Alikuwa akisimama (katika Swalah) bila ya viatu wakati mwingine na kuvaa viatu wakati mwingine"[1]

 

Ameruhusu kufanya hivyo kwa Ummah wake na kusema:

((Mmoja wenu anaposwali, basi avae viatu vyake au avivue baina ya miguu yake, na wala asimkere mtu kwa viatu hivyo)).[2]

 

Aliwasisitizia kuswali na viatu wakati mwingine, na kusema:

((Kuweni tofauti na Mayahudi, kwani wao hawaswali na viatu vyao wala na khufu [soksi za ngozi] zao)).[3]

 

Mara moja moja alikuwa anavivua wakati anaswali na kisha akiendelea na Swalah yake kama alivyosema Abu Sa'iyd Al-Khudriy:

 

"Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha siku moja, na alipokuwa yumo katika Swalah, alivua viatu vyake na akaviweka upande wa kushoto kwake. Watu walipoona hivyo, nao pia wakavua viatu vyao.  Alipomaliza kuswali alisema: ((Kwa nini mmevua viatu vyenu?)) Wakajibu: "Tumekuona wewe unavua viatu vyako  na sisi pia ndio tukavua viatu vyetu". Akasema:

((Hakika Jibriyl alinijia na kunijulisha kwamba kulikuwa na uchafu)) au kasema (kulikuwa na) kitu cha madhara)).  Katika riwaya nyingine ((uchafu/ Najsi)) katika viatu vyangu, kwa hiyo nikavivua. Kwa hivyo, mmoja wenu anapokuja msikitini, basi atazame viatu vyake. Akiona vina uchafu, au kasema kitu chenye madhara, na (katika riwaya nyingine) najsi, basi avifute kisha aswali navyo)).[4]

 

"Alipokuwa akivivua, alikuwa akiviweka upande wa kushoto kwake.”[5]

 

Na pia alikuwa akisema: ((Mmoja wenu anaposwali, asiweke viatu vyake upande wa kulia wala kushoto kwake, ambako vitakuwa katika upande wa kulia wa mwenzake, isipokuwa kama kutakuwa hakuna mtu upande wa kushoto, lakini aviweke baina ya miguu yake)).[6]

 

 

 

SWALAH KATIKA MINBAR

 

Mara moja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali katika Minbar (na katika riwaya nyingine: iliyokuwa na daraja (vijingazi) tatu[7]). Hivyo (akasimama juu yake na akapiga Takbiyr (akasema 'Allaahu Akbar') na watu nyuma yake wakapiga Takbiyr wakati yuko juu ya Minbar), (kisha akarukuu juu ya Minbar), halafu akainuka na kushuka kinyume nyume mpaka akasujudu katika kitako cha Minbar. Kisha akarudi (na akafanya kama alivyofanya katika raka'ah ya mwanzo) mpaka akamaliza Swalah yake. Kisha akageuka kwa watu na kusema: ((Enyi watu! Nimefanya hivyo ili mnifuate na mjifunze Swalah yangu))[8].

 

 



 

[1] Abu Daawuud na Ibn Maajah. Ni Hadiyth yenye mapokezi mengi (Mutawaatir) kama alivyotaja  atw-Twahaawiy.

 

[2] Abu Daawuud na Bazzaar (53, Az-Zawa'id), al-Haakim amekiri kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy amekubali.

 

[3] Abu Daawuud na Bazzaar.

 

[4] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah na al-Haakim ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh na adh-Dhahabiy na an-Nawawiy wamekubali. Ya kwanza imetolewa katika Irwaa.

 

[5] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah na al-Haakim.

 

[6] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah (1/110/2) na kwa Sanadi iliyo Swahiyh.

 

[7] Hii ni Sunnah kuhusu Minbar, kwamba iwe na daraja tatu, na sio zaidi. Kuwa na zaidi ya daraja tatu ni bid'ah iliyoanzishwa na Bani Umayyah. Ni mara nyingi safu hukatika. Na kuliepuka hilo kwa kuiweka pembezoni mwa upande wa Magharibi wa Msikiti au wa Mihraab, ni bid'ah nyingine. Vile vile ni (bid’ah) kuipandisha katika ukuta wa kusini kama roshani ambako mtu hupanda kwa ngazi zilizoshikanishwa na ukuta! Na uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم) ). Tazama Fat-h Al-Baariy (2/331).

 

[8] Al-Bukhaariy na Muslim. Riwaya nyingine ni yake Muslim na Ibn Sa'd (1/253).  Imetolewa katika “Al-Irwaa” (545).

 

Share [38]

010-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Sutrah Na Yanayokata (Yanayotengua) Swalah

 

 

 

 

SUTRAH[1] NA KUWAJIBIKA KWAKE

 

"Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisimama karibu na sutrah, ili iweko (umbali wa) dhiraa tatu baina yake na ukuta”[2] na "baina ya sehemu ya sujuud na ukuta (kulikuweko) nafasi ya kuweza kupita kondoo”[3].

 

Alikuwa akisema,

((Msiswali isipokuwa mbele ya Sutrah, na msimuachie mtu kupita mbele yenu, lakini kama mtu akiendelea (kujaribu kupita) basi mzuwieni kwani yuko pamoja na rafiki)) (yaani Shaytwaan).[4]

 

Alikuwa akisema,

((Mmoja wenu akiswali mbele ya Sutrah, basi awe karibu yake ili Shaytwaan asiweze kuivunja Swalah yake)).[5]

 

 

Mara nyingine "Alikuwa anaswali mbele ya nguzo ya msikiti.”[6]

 

Alipokuwa anaswali (kwenye sehemu ya wazi ambako kulikuwa hakuna kitu cha kutumia kiwe Sutrah) alikuwa akiuchomeka mkuki ardhini mbele yake kisha akiswali kuuelekea na watu wakiwa nyuma yake.[7] Mara nyingine "alikuwa akiweka kipando chake (mnyama) kisha akiswali kukielekea kipando chake.[8] Lakini hii sio sawa na Swalah katika sehemu ya mapumziko ya ngamia[9] ambayo "ameikataza”[10] na mara nyingine "alikuwa akichukua tandiko lake (la ngamia) akiliweka kwa urefu kisha akiswali kuelekea nchani mwake.”[11]

 

Na alikuwa akisema,

((Mmoja wenu akiweka mbele yake kitu kama fimbo nchani (mwishoni) mwa tandiko la mnyama, basi aswali na asijali mtu yeyote atakayepita mbele yake)).[12]

 

Mara moja "Aliswali akiuelekea mti”[13] na wakati mwengine "Alikuwa akiswali mbele ya kitanda ambacho Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa amelala (akiwa amejifunika shuka).”[14]

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa haachii kitu chochote kupita baina ya Sutrah yake, kwa hiyo mara moja "alikuwa anaswali na kondoo alipokuja na kukimbia mbele yake alimkimbiza mpaka akalibonyeza tumbo lake katika ukuta (kisha akapita nyuma yake).”[15]

 

 

Vile vile mara moja "wakati anaswali Swalah ya fardhi, alikunja ngumi yake. Na alipomaliza (kuswali) watu walimwambia, "Ewe Mjumbe wa Allaah, kuna jambo limetokea wakati wa Swalah?" Akasema, ((Hapana isipokuwa Shaytwaan alitaka kupita mbele yangu, nikamkaba mpaka nikahisi ubaridi wa ulimi wake katika mkono wangu. Naapa kwa Allaah! Ingelikuwa sio ndugu yangu Sulaymaan kunitangulia[16]. Ningelimfunga (Shaytwaan) katika nguzo moja ya msikiti ili watoto wa Madiynah waweze kutembea mbele yake. (kwa hiyo yeyote atakayeweza kuzuwia kitu kumuingilia baina yake na Qiblah afanye hivyo).”[17]

 

Pia alikuwa akisema,

 

((Mmoja wenu anaposwali mbele ya kitu kama Sutrah baina yake na watu na mtu akitaka kupita mbele yake, basi amsukume kwa shingo yake)) (na amfukuze kadiri anavyoweza) (katika riwaya nyingine, ((amzuie mara mbili na akikataa (akishikilia kutaka kupita mbele) basi agombane naye kwani hakika huyo ni Shaytwaan)).[18]

 

Vile vile alikuwa akisema,

((Ikiwa mtu aliyepita mbele ya mtu mwenye kuswali amejua (kuwa ni dhambi) juu yake (kufanya hivyo), basi ingelikuwa ni bora kwake kusubiri arubaini kuliko kupita mbele)). Na nyongeza katika riwaya nyingine yasema, (Abu An-Nadr kasema, "Sikumbuki khaswa kama alisema ni siku arubaini, au miezi au miaka").[19]

 

 

 

YANAYOKATA (YANAYOVUNJA) SWALAH

 

Alikuwa akisema,

((Swalah ya mtu inavunjika (inakuwa baatwil) kunapokuwa hakuna kitu kama ncha ya tandiko (la mnyama) mbele yake (vitu vitatu) mwanamke (baleghe)[20] punda au mbwa mweusi)) Abu Dharr akasema, "Nilisema, Ewe Mjumbe wa Allaah, kwa nini mbwa mweusi na sio mwekundu?" Akasema, ((Mbwa mweusi ni Shaytwaan)).[21]

 

 



[1] Sutrah – "Kinga ya kuzuia" katika Swalah, inakusudia kitu cha kuwekwa mbele ya sehemu ya kusujudu kukinga ili asipite mtu au chochote mbele yake kama ilivyoelezewa katika somo hili.

[2] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[3] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[4] Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/93/1) na Isnaad iliyothibitika.

[5] Abu Daawuud, Bazzaar (ukurasa 54 Zawaaid) na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy na An-Nawawiy wameikubali.

[6] Al-Bukhaariy.  Sutrah ni lazima kuweko kwa Imaam au mtu anayeswali peke yake hata katika msikiti mkubwa.  Ibn Haani amesema katika Masaa'il yake kutoka Imaam Ahmad (1/66) "Abu 'Abdillaah (Imaam Ahmad Ibn Hanbal) aliniona siku moja wakati naswali bila ya Sutrah mbele yangu na nilikuwa katika (Swalah ya) Jama'ah (kubwa) msikitini, kwa hiyo akaniambia, "Weka kitu kama Sutrah".  Nikamchukua mtu kama Sutrah. Hii inaonyesha kwamba Imaam Ahmad hakutofautisha baina ya msikiti mkubwa au mdogo katika mas-ala ya Sutrah. Na hii hakika ni sahihi, lakini hili ni jambo ambali limedharauliwa na watu wengi pamoja na ma-Imaam wa misikiti katika kila nchi nliyotembea pamoja  na nchi za Arabuni ambazo nimeweza kutembea katika mwezi wa Rajab wa mwaka huu (1410).  Kwa hiyo ma-Ulamaa waambie watu na kuwanasihi jambo hili, na kuwafahamisha sheria yake na kwamba pia inahitajika kuweko katika misikiti miwili mitukufu.

[7] Al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Maajah.

[8] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[9] Yaani ni sehemu yao ya kupiga magoti.

[10] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[11] Muslim, Ibn Khuzaymah (92/2) na Ahmad.

[12] Muslim na Abu Daawuud.

[13] An-Nasaaiy na Ahmad kwa Isnaad Swahiyh.

[14] Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Ya'laa (3/1107).

[15] Ibn Khuzaymah katika Swahihy yake (1/95/1) At-Twabaraaniy (3/140/3) na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy kaikubali.

[16] Inakusudiwa Du'aa ifuatayo ya Nabii Sulaymaan (عليه السلام) ambayo alijibiwa na Allaah (سبحانه وتعالى) kama ilivyo katika Qur-aan.  ((Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji)) ((Basi Tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika)) ((Na tukayafanya mashaytwaan yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi))   ((Na wengine wafungwao kwa minyororo)) [Swaad, 38: 35-38].

[17] Ahmad, Daaraqutniy na At-Twabariy kwa Isnaad ya Swahiyh na iliyo na maana kama hii ni Hadiyth inayopatikana katika Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo kutoka kwa mapokezi ya Maswahaba mbali mbali.  Na mojawapo ya Hadiyth ambayo kundi la Maqadiyani hawaiamini kwani hawaamini (ulimwengu wa) majini ambao wametajwa katika Qur-aan na Sunnah.  Desturi yao ni kukanusha maandishi yaliyo mashuhuri sana. Kama kutoka kwenye Qur-aan wanabadilisha maana yake mfano, maneno ya Subhaana Wa Ta’ala ((Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza)) [72:1] wanasema kwamba ina maana "kikundi cha binaadamu" na kulifanya neno la 'majini' kuwa inakaribia na maana ya 'binaadamu'. Kwa hiyo wanacheza na lugha na dini.  Na kama kutoka katika Sunnah basi kama inawezeka kwao kubadilisha kwa tafsiyr ya uongo wanafanya hivyo, au sivyo wanaona ni wepesi  kukiri kuwa ni uongo hata kama Maimaam wa Hadiyth wote  na Ummah mzima kabla yao wamekubaliana na usahihi wake, (tunawaambia kuwa hilo wanalilikataa hapo) kuwa hapana, hiyo ni mutawaatir (imekuja kwa mapokei mengi haina shaka yoyote).  Allaah Awahidi.

 

[18] Al-Bukhaariy na Muslim na riwaya zaidi ni kutoka kwa Ibn Khuzaymah (1/94/1).

[19] Al-Bukhaariy na Muslim.

[20] Ina maana baleghe, na maana ya 'inavunjika' ni kuwa 'haifai tena' (baatwil).  Ama kuhusu Hadiyth "Hakuna kinachovunja Swalah" hiyo ni Hadiyth dhaifu na nimeionyesha katika Tamaam Al-Minnah (Ukurasa 306).

[21] Muslim, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah (1/95/2).

Share [39]

011-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Swalah Kulielekea Kaburi, Nia, Takbiyr, Kunyanyua Mikono Na Kufunga Mikono Wa Kulia Juu Ya Kushoto

 

 

 

SWALAH KULIELEKEA KABURI

 

Alikuwa akikataza kuswali kwa kuyaelekea makaburi akisema:

((Msiswali kuelekea makaburi na msiyakalie)).[1]

 

 

 

NIA[2]

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema:

((Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia)).[3]

 

 

TAKBIYR

 

Kisha Yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akianza Swalah kwa kusema:

‘Allaahu Akbar’.[4]

 

Alimuamrisha 'mtu aliyeswali vibaya' afanye kama ilivyotajwa na akamwambia: ((Hakika Swalah ya mtu haikamiliki hadi awe ametawadha kwa wudhuu uliyokamilisha viungo vya mwili kisha akasema Allaahu Akbar)).[5]

 

Pia alikuwa akisema:

((Ufunguo wa Swalah ni Twahara, inaharamishwa (inaanzwa) na Takbiyr na inahalalishwa (inamalizikia) na Tasliym)).[6]

 

Pia "alikuwa akipandisha sauti yake kutamka Takbiyr hadi walio nyuma yake walimsikia"[7]. Lakini "anapoumwa, Abu Bakr alikuwa akipandisha sauti yake kutamka Takbiyr kwa niaba ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).[8 ] [40]

 

Alikuwa akisema pia:

((Imamu anaposema: Allaahu Akbar, basi sema: Allaahu Akbar)).[9]

 

 

KUNYANYUA MIKONO

 

Alikuwa mara nyingine akinyanyua mikono pamoja na Takbiyr.[10] Mara nyingine baada ya Takbiyr[11] na mara nyingine kabla yake.[12]

 

Alikuwa akiinyanyua kwa kuvinyosha vidole vyake (sio kwa kuvitawanya wala kuvibana pamoja)[13] na "alikuwa akiiweka (mikono) sambamba na mabega yake"[14] ingawa kwa nadra, "alikuwa akiinyanyua hadi ifikie sawa na (ncha ya juu ya) masikio yake".[15]

 

 

KUWEKA (KUFUNGA) MKONO WA KULIA JUU YA MKONO WA KUSHOTO NA KUAMRISHWA KWAKE

 

"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto"[16] na alikuwa akisema:

((Sisi, Mitume, tumeamrishwa kukimbilia kufungulia Swawm, kuchelewa (kula) daku na kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika Swalah)).[17]

 

Vile vile: "alimpitia mtu aliyekuwa akiswali aliyeweka mkono wake wa kushoto juu ya mkono wa kulia, akamvuta kuondosha kisha akauweka wa kulia juu ya kushoto"[18]

 

 

 



[1] Muslim, Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah.

[2] An-Nawawiy amesema katika Radhwah Atw-Twaalibiyn (1/224 iliyochapishwa na Maktab Al-Islaamiy): "Nia ni kusudio, kwa hiyo mtu anayetaka kuswali, hutia akilini tayari hiyo Swalah pamoja na yanayohusika nayo ya sifa zake, mfano kama ni Swalah ya kipindi kipi, je, ni Swalah ya faradhi n.k. ndipo huleta hivi vyote katika nia yake pamoja na Takbiyr ya mwanzo".

[3] Al-Bukhaariy na Muslim na wengineo. Imetolewa pia katika Al-Irwaa (Namba: 22).

[4] Muslim na Ibn Maajah. Hadiyth inaashiria kwamba hakuwa akianza (Swalah) kwa maneno ya baadhi ya watu: "Nawaytu Uswalliy… n.k" ambayo imekubalika kuwa ni bid'ah (uzushi). Bali wamekhitilafiana kama ni bid'ah njema au mbaya ambayo tunasema: Hakika bid'ah zote katika ibada ni upotofu, kutokana na kauli (صلى الله عليه وآله وسلم) ((…na kila bid'ah ni upotofu na kila upotofu ni motoni)). Lakini hapa sipo mahali pa maelezo marefu ya mas-ala haya.

[5] Atw-Twabaraaniy ikiwa na isnadi Swahiyh.

[6] Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na Al-Haakim ambao wamekiri usahihi wake na Adh-Dhahaabiy amekubali. Imetolewa katika Al-Irwaa (Namba: 301). Maana hasa ya 'inaharamishwa na Takbiyr', ni vitendo vyote ambayo Allaah Ameviharamisha wakati huo. 'na inahalalishwa na Tasliym' ni yote yaliyoruhusiwa nje ya Swalah. Kama vile Hadiyth ilivyothibitsha kuwa mlango wa Swalah umefungwa, hakuna mwenye kuabudu anaweza kufungua isipokuwa kwa Twahara, imethibitisha pia kuwa Swalah haiwezi kufunguliwa (kuanzishwa) isipokuwa kwa Takbiyr na haiwezi kumalizika bila ya Tasliym. Hii ni rai iliyokubalika kwa wengi wa Maulamaa.

[7] Ahmad, Al-Haakim ambao wamekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana.

[8] Muslim na An-Nasaaiy.

[9] Ahmad na al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy.

[11] Al-Bukhaariy na An-Nasaaiy.

[12] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[13] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/62/2, 64/1), Tammaam Na Al-Haakim ambao wamekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy amekubaliana.

[14] Al-Bukhaary na An-Nasaaiy.

[15] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[16] Muslim Na Abu Daawuud, pia imetolewa katika Al-Irwaa (352).

[17] Ibn Hibbaan na Adh-Dwiyaa ikiwa na isnaad Swahiyh.

[18] Ahmad Na Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh.

 

Share [41]

012-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuweka Mikono Juu Ya Kifua, Kutazama Mahali Pa Kusujudu, Na Khushuu (Unyenyekevu) Katika Swalah

 

KUWEKA MIKONO JUU YA KIFUA

 

"Alikuwa akiweka mkono wa kulia nyuma ya kitanga cha mkono wa kushoto, kiwiko na kigasha"[1] "na aliwaamrisha Maswahaba wake kufanya hivyo"[2] na (mara nyingine) "akiushika mkono wa kushoto kwa mkono wake wa kulia"[3]

 

"Alikuwa akiiweka juu ya kifua chake"[4]

 

Pia, alikuwa akikataza mtu kuweka mkono juu ya kiuno wakati wa Swalah na aliweka mkono wake juu ya kiuno (kuonyesha makosa hayo)[5] Na hii ndio swilb aliyokuwa akikataza.[6]

 

 

 

KUTAZAMA MAHALI PA KUSUJUDU NA KUSHUU (UNYENYEKEVU)

 

"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiinamisha kichwa chake wakati wa Swalah na kukongomeza (kuyaelekeza) macho yake katika ardhi[7]

"Alipoingia katika Kaabah, hakuacha jicho lake kutazama sehemu ya kusujudu hadi alipotoka nje"[8]  na alisema: ((Haipasi kuweko na kitu chochote katika Nyumba kitakachomshawishi mwenye kuswali))"[9]

 

"Alikuwa akikataza kuinua macho kutazama mbinguni"[10] na alishikilia makatazo haya sana hadi alisema: ((Watu lazima waache kutazama juu mbinguni katika Swalah au macho yao hayatorudi kwao)) [na katika riwaaya nyingine] ((…au macho yao yatapofushwa))[11]

 

Katika Hadiyth nyingine: ((Mnaposwali msiangaze huku na kule kwani Allaah Huelekeza Uso Wake mbele ya uso wa mja Wake madamu mja hatoangaza kwengine)).[12] Akasema pia kuhusu kuangaza huku na kule: ((Ni kunyakuliwa ambako Shaytwaan hunyakuwa katika Swalah ya mja anaposwali))[13]

 

Akasema pia (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Allaah Haachi kuelekea kwa mja katika Swalah madamu tu mja haangazi huku na kule, anapogeuza uso wake mbali, Allaah Hugeuka mbali naye))[14] na "Akakataza mambo matatu; kudonoa kama jogoo, kuchutama kama mbawa na kuangaza kama fisi",[15] vile vile alikuwa akisema: ((Swalini Swalah ya kuaga (dunia) kama kwamba mnamuona Yeye (Allaah) na kama hamumuoni, hakika Yeye Anakuoneni))[16], na (akisema), ((Mtu yeyote anayefikwa na Swalah ya fardhi akatawadha vizuri, akakamilisha khushuu (unyenyekevu) zake, na rukuu zake, hakika itakuwa ni kafara ya dhambi alizotenda kabla ya Swalah hiyo madamu hajatenda dhambi kubwa, hali hiyo ni kwa mwaka wote))[17]

 

Mara moja yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali katika khamiysah[18] (na alipokuwa akiswali) alizitazama alama zake. Alipomaliza akasema: ((Ipelekeeni khamiysah hii yangu kwa Abu Jahm na nileteeni (badala yake) anbijaaniyyah[19] kwani imenipotezea umakini wangu katika Swalah)) [katika usimulizi mmoja] ((…kwani nimetazama alama zake wakati wa Swalah ilikaribia kunitia katika mtihani))[20]

 

Pia Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa na kitambaa cha picha kilichotandazwa mbele ya sahwah[21] ambayo Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali mbele yake, akasema: ((Iondoshelee mbali, [kwani picha zake hazikuacha kunishawishi katika Swalah]))[22]

Alikuwa akisema pia: ((Hakuna kuswali chakula kinapokuwa tayari, wala mtu anapotaka kukidhi haja kubwa na ndogo))[23]

 





[1] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na Ibn Khuzaymah (1/54/2) ikiwa na isnaad Swahiyh na Ibn Hibbaan amekiri usahihi wake (485).

[2] Maalik, Al-Bukhaariy na Abu 'Awaanah.

[3] An-Nasaaiy na Ad-Daraqutwniy ikiwa na isnaad Swahiyh. Katika Hadiyth hii kuna ushahidi kwamba kuishikilia ni Sunnah na katika Hadiyth nyingine, kuwekea tu, hivyo yote ni Sunnah. Ama kuunga baina ya kuweka na kushikilia ambayo baadhi ya Mahanafi waliotangulia wameona ni vizuri, hivyo ni bid'ah; mfumo wake ni kama walivyotaja kuwa ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto, kushikilia kiwiko kwa kidole kidogo na cha gumba, na kuviweka bapa vidole vitatu vengine, kama ilivyoelezewa katika tanbihi za Ibn 'Aabidiyn kwenye Durr Al-Mukhtaar (1/454) kwa hiyo usibabaike na wasemayo.

[4] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/54/2) Ahmad na Abu Shaykh katika Taariykh Iswbahaan (Uk.125), At-Tirmidhiy amekiri moja ya isnaad ni hasan (njema) na maana yake inapatikana katika Al-Muwattwaa na Swahiyh Al-Bukhaariy ikichukuliwa kwa makini. Nimenukuu isnaad kamili ya Hadiyth hii katika kitabu changu Ahkaam al-Janaaiz (Uk. 118).

 

TANBIHI:

Kuiweka katika kifua ndivyo ilivyothibiti katika Sunnah, na kinyume chake ni aidha dhaifu au haina msingi. Na Imaam Is-haaq Ibn Raahawayh alifanya Sunnah hii kama alivyosema Al-Marwazy katika Masaail (Uk. 222). "Is-haaq alikuwa akiswali Witr pamoja na sisi … alikuwa akinyanyua mikono yake katika Qunuut na akileta Qunuut kabla ya kurukuu na kuweka mikono yake kifuani mwake au chini yake". Ni sawa na usemi wa Qaadhwiy 'Iyaadh Al-Maalikiy katika Mustahabbaat As-Swalah kitabu chake Al-I'laam (Uk. 15, chapa ya 3, Ar-Rabaatw) "Mkono wa kulia uwekwe juu ya mkono wa kushoto sehemu ya juu ya kifua". Na karibu na hii ni kama alivyohusisha 'Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal katika Masaail yake (Uk. 62): "Niliona wakati wa kuswali, baba yangu akiweka mikono yake mmoja juu ya mwenziwe juu ya kitovu (chini ya kifua kidogo)" Tazama Kiambatisho 4.

 

 

[5] Al-Bukhaariy na Muslim.

[6] Abu Daawuud, An-Nasaaiy na wengineo.

[7]  Al-Bayhaaqiy na al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh kama alivyosema. Pia ina Hadiyth iliyotilia nguvu iliyoripotiwa na Maswahaba kumi: iliyosimuliwa na Ibn 'Asaakir' (17/202/2) Taz. Al-Irwaa (354).

 

TANBIHI:

Hadiyth hizi mbili zinaonyesha kwamba Sunnah ni kukaza macho yake mtu mahali pa kusujudu ardhini, hivyo kufunga macho katika Swalah kama wafanyavo baadhi ya watu ni ukosefu ya uchaji Mungu, kwani uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).

 

[8]  Al-Bayhaaqiy na al-Haakim.

[9] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa ni isnaad ya Swahiyh (Al-Irwaa 1771); iliyokusudiwa hapa 'Nyumba' ni Kaabah kama inavyoonyesha yaliyomo katika Hadiyth.

[10]  Al-Bukhaary Abu Daawuud.

[11] Al-Bukhariy, Muslim na Siraaj.  

[12] [24]  At-Tirmidhiy na al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh – (Swahiyh At-Targhiyb Namba: 353).

[13] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[14] Imesimuliwa na Abu Daawuud na wengineo. Ibn Khuzayma na Ibn Hibbaan wamekiri usahihi wake. Taz. Swahiyh At-Targhiyb (Namba 555).

[15] Ahmad na Abu Ya'laa. Taz Swahiyh At-Targhiyb (Na,ba 556)

[16]  Al-Mukhlisw katika Ahaadityh Muntaqaa, At-Twabaraaniy, Ar-Ruuyaaniy, Adh-Dwiyaa katika Al-Mukhtaarah, Ibn Maajah, Ahamd na Ibn 'Asaakir. Al-Hayatamy amekiri ni Swahiyh kaitka Asnan Al-Matwaalib

[17] Muslim.

[18]  Nguo ya sufi iliyo na alama.

[19]  Nguo ya kukwaruza isiyo na alama.

[20] Al-Bukhaariy, Muslim na Maalik imetolewa katika Al-Irwaa (376)

[21] Chumba kidogo kilichobanwa kidogo katika ardhi kama chemba au kabati. (Nihaayah)

[22] Al-Bukhaariy, Muslim na Abu 'Awaanah. Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuamrisha kufutwa au kuchana picha bali aliziondosha kwa sababu. Na Allaah Anajua zaidi- hazikuwa ni picha zenye roho. Ushahidi wa hili ni kwamba yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alichana picha nyinginezo kama ilivyothibiti katika usimulizi mwingi katika Al-Bukhaariy na Muslim na yeyote apendaye kutafiti zaidi atazame Fat-h Al-Baariy (10/321) na Ghaayah Al-maraam fiy Takhriyj Ahaadiyth Al-Halaal wal-Haraam (Namba: 131-145).

[23]Al-Bukhaariy na Muslim.

 

Share [42]

013-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Du'aa Za Kufungulia Swalah

 

 

DU'AA ZA KUFUNGULIA

 

Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akianza kusoma kwake kwa aina nyingi za du'aa ambazo akimsifu na kumtukuza na kumuadhimisha Allaah (سبحانه وتعالى). Alimuamrisha "mtu aliyeswali vibaya" afanye hivyo akimwambia: ((Swalah ya mtu haikamiliki hadi atamke Takbiyr, amsifu Allaah (سبحانه وتعالى), amtukuze na amuadhimishe asome iliyo nyepesi katika Qur-aan…..))[1] .

 

Alikuwa akisoma du'aa zozote katika hizi zifuatazo:

 

 1.

 

 

 

"Ee Allaah! Niweke mbali na madhambi yangu kama Ulivyoweka mbali baina ya Mashariki na Magharibi, Ee Allaah! Nitakase na madhambi yangu kama vile inavyotakaswa nguo nyeupe na uchafu, Ee Allaah!  Nisafishe na madhambi yangu kwa theluji na kwa maji na kwa barafu"[2]

(Na alikuwa akisema katika swala za fardhi):

2.

 

 

 

“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule Ambaye Ameumba mbingu na ardhi hali ya kumtakasia yeye dini yangu, na sikuwa mimi ni katika washirikina, hakika Swalah yangu na kuchinja  kwangu na uhai wangu, na kufa kwangu ni kwa Allaah Bwana wa viumbe vyote, Hana mshirika, na kwa hilo nimeamrishwa, nami na mimi ni wa kwanza waliojisalimisha.[3]  Ee Allaah! Wewe ndiye Mfalme, hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe, Wewe ndiye Bwana wangu na mimi ni mtumwa (mja) Wako[4] Nimedhulumu nafsi yangu, na nimekiri madhambi yangu kwa hivyo nisamehe madhambi yangu yote, hakika hasamehe madhambi, ila Wewe. Na niongoze kwenye tabia nzuri, kwani haongozi kwenye tabia nzuri ila Wewe. Na Niepushe na tabia mbaya, kwani hakuna wa kuniepusha na tabia mbaya ila Wewe. Naitikia mwito Wako, na nina furaha kukutumikia.[5] Kheri zote ziko mikononi Mwako, na shari haitoki Kwako[6], Na ameongoka yule Uliyemuongoa, mimi nimepatikana kwa ajili Yako, hapana penye uokovu wala wa pa kukimbilia isipokuwa Kwako, umetakasika, na umetukuka, nakutaka msamaha na ninarejea Kwako (kwa kutubia).”

 

Alikuwa akisema hivyo katika Swalah za fardhi na za Sunnah[7]

 

 

 

3. Hii du’aa ni kama iliyo juu bila ya:

 

 

 

 

“Wewe Ni Mola wangu nami ni mja Wako…”

 

Hadi mwishoni pamoja na nyongeza ifuatayo:

 

 

 

 

 

“Ee Allaah, Wewe Ni Mfalme, hapana apasaye kuabudiwa isipokuwa Wewe, Kutakasika ni Kwako na Sifa njema zote ni Zako”[8]

 

 

4- Kama na Namba 2 hadi,

 

 

 

 

 

“…nami ni Muislamu wa mwanzo,

 

Na akiongeza,

 

 

 

 

 

 

Ewe Allaah, niongoze kwenye tabia njema (nzuri) na vitendo vyema haongozi kwenye uzuri wake ila Wewe. Niepushe na tabia mbaya na vitendo vibaya hakuna mwenye uwezo wa kupesuha??? ubaya wake ila Wewe [9].

 

 

5-

 

 

 

 

 

Kutakasika ni Kwako[10] Ee Allaah, na sifa njema zote ni Zako[11], na limetukuka Jina Lako[12], na Utukufu ni Wako[13], na hapana apasae kuabudiwa kwa haki, asiyekuwa Wewe[14]

Alisema (صلى الله عليه وآله وسلم) pia: ((Hakika maneno yanayopendwa kabisa na Allaah ni mja Wake anaposema: (سبحانك اللهم) Umetukuka Ewe Allaah…”[15]

 

 

6- Kama ilivyo juu kwa kuongeza katika Swalah za usiku:

 

 

 

                                                               

 

 

“Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah”

 

Mara tatu na

 

 

 

 

“Allaah ni Mkubwa”

 

 

Mara tatu

 

 

7-

 

 

 

 

 

“Allaah Ni Mkubwa, Na sifa njema ni za Allaah kwa wingi, Ametakasika Allaah asubuhi na jioni.”

 

 

 

 

 

Mmoja wa Maswahaba alifungua Swalah yake kwa du’aa hiyo, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: ((Imenipendeza hiyo (du'aa) kwani kwayo milango ya Pepo imefunguliwa))[16]

 

 

8- 

 

 

 

 

 

“Sifa njema ni za Allaah, sifa nyingi, nzuri, zenye Baraka”

 

Mtu mwengine alifungua Swalah yake kwa du’aa hiyo, kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Nimewaona Malaika kumi na mbili wakishindana nani atakayeipeleka juu))[17]

 

 

9-

 

 

“Ee Allaah ni Zako sifa njema, Wewe ndiye nuru[18] ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na ni Zako sifa njema. Wewe ndiye Mwenye kuzisimamia[19] mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, [na ni Zako sifa njema, Wewe ni Mfalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake],  na sifa njema ni Zako, Wewe ni Haqq, na ahadi Yako ni ya Haqq, na neno Lako ni Haqq, na kukutana Nawe ni Haqq, na Pepo ni Haqq, na Moto ni Haqq, na Sa’ah (Qiyaamah) ni Haqq, na Mitume ni Haqq, na Muhammad ni Haqq, Ee Mola Kwako nimeweka imani yangu, na Kwako nimetegemea, na Kwako ndio nakurejelea, nimepigana kwa ajili Yako, na kwa hukumu Zako ndio nazifuata zinihukumu, [Wewe ndiye Mola wetu na Kwako ndio tunaishia, nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha  na niliyoyatangaza], [Na yote unayoyajua kutoka kwangu] Wewe ndiye mwenye kutanguliza na ndiye mwenye kuchelewesha, [Wewe ni Mola wangu] hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Wewe[20]; 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema hivi katika Swalah ya usiku alipokuwa akisoma du'aa ifuatayo[21]:

 

10-

 

 

 

 

“Ewe Mwenyezi Mungu  Mola wa Jibiriyl na Mikaaiyl na Israafiyl, Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa mambo yaliojificha na yaliyowazi, Wewe unahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitofautiana, niongoze mimi kwenye  haki katika yale waliyotafautiana kwa ruhusa Yako.  Hakika Wewe unamuongoza umtakae kwenye njia iliyonyoka[22]”

 

 

11- Alikuwa akisema Takbiyr, Tahmiyd, Tasbiyh, Tahliyl na Istighfaar mara kumi kila moja na akisema:

 

 

 

 

 

“Ee Allaah, nighufurie na niongoze na niruzuku [Na Nisamehe madhambi yangu]” mara kumi kisha akisema:

 

 

 

 

 

“Ee Allaah, Najikinga Kwako na dhiki za Siku ya Hisabu”[23]

 

Mara kumi

 

 

 

12-

 

 

 

 

“Allaah ni Mkubwa [mara tatu] Mwenye Ufalme, Nguvu, Ufakhari na Utukufu”[24]

 

 





[1] [15] Al-Bukhaariy, Muslim na Ibn Abi Shaybah (12/110/2) imetolewa katika Al-Irwaa (Namba 8)

[2] [16] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana.

 

[3] [17]  Imesimuliwa katika usimulizi mwingi, katika mwengine, 'Wa Anaa Minal-Muslimiyn’ (Mimi ni miongoni wa Waislamu). Inaweza kuwa ni kutokana na makosa ya usimulizi mmojawapo, na ushahidi mwingine unaelekeza hapo, kwa hiyo mwenye kuswali aseme: ‘Wa Anaa Awwalul-Muslimiyn’ (Nami ni Muislamu wa mwanzo). Hakuna makosa hivyo, kinyume na watu wanavyosema kwa uoni kwamba inamaanisha "Mimi ni Muislamu wa kwanza mwenye sifa hii, na watu wengine hawana sifa hii". Lakini sio hivyo, ibara hii inaashiria kushindana katika kutekeleza amri. Hii ni sawa na ((Sema: Ingelikuwa ar-Rahmaan ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu)) [Az-Zukhruf, 43: 81] na kauli ya Muusa ('Alayhis-Salaam) ((na mimi ni wa kwanza wa Waumini)) [Al-A'raaf 7: 143].

[4] [18]  Al-Azhariy amesema kwamba, "Siabudu chochote kingine isipokuwa Wewe"

[5] [19]  Labbayk: Niko thabiti na daima niko katika utiifu Wako. Sa'dayk: Furaha kubwa kuwa katika amri Yako na kufuata kwa dhati dini Uliyoichagua.

[6] [20]  Yaani, Uovu haunasibishwi kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa sababu hakuna chochote kibaya katika vitendo Vyake, kwani vyote ni vyema vikianzia kutoka uadilifu, fadhila na hikma vyote ambayo ni kheri na havina shari ndani yake bila ya kuwa na shari ndani yake. Kwa sababu shari imekuwa shari kwa sababu hauwezi kurudia kwa Allaah. Ibn Al-Qayyim (Rahimahu-Allaah) amesema: "Yeye ni Muumba wa mema na maovu, lakini maovu yako katika baadhi ya viumbe Vyake, na sio katika kuumba Kwake na sio katika vitendo Vyake. Kwa ajili hiyo Ametakasika na dhulma ambayo asili yake ni kuweka kitu katika sehemu nyingine isiyopasa. Haweki kitu isipokuwa katika mahali panapostahiki ili yote yawe mema. Lakini uovu ni kuweka kitu mahali pasipostahiki. Kinapowekwa katika mahali panapostahiki, huwa si kiovu, kwa hiyo jua kuwa uovu hautoki Kwake.  Lakini ikisemwa: Kwa nini Ameumba maovu? Nitasema: Ameumba, na vitendo Vyake ni vizuri sio viovu kwani kuumba na vitendo vinasimama na Allaah, haiwezekani uovu kufanywa au kuhusishwa na Allaah. Chochote kilichokuwa kiovu hakiwezi kurudishwa kwa Allaah, ama vitendo na Alivyoviumba vinaweza kuhusishwa Naye, na vinakuwa ni vyema". Majadiliano muhimu yaliyobakia na kimalizio chake kitapatikana katika kitabu chake Shifaa Al-'Aliyl fiy Massail al-Qadhwaa wal-Qadar wat-Ta'liyl – taz (uk. 178-206).

[7] [43] Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud, An-Nasaaiy, Ibn Hibbaan, Ahmad, Ash-Shaafi'iy na At-Twabaraaniy. Walioeleza kuwa ni Swalah za Sunnah wamekosea.

[8] [44]  An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[9] [21]  An-Nassaiy na Ad-Daaraqutwniy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] [22]  Nakutukuza ina maana kwamba nazingatia kuwa Umetakasika na kasoro yoyote. Na ‘Sifa njema’ maana yake ni kuwa tumezijua vizuri sifa Zako. Na ‘Kutakasika’ maana yake ni wingi wa kutakasika kwa jina Lako, kwa sababu kila la kheri linapatikana katika kulitaja jina Lako. ‘limetukuka Jina Lako’ maana yake ni kuwa limenyanyuka juu jina Lako (utukufu wako).

[11] [23]  Tumeshikamana katika kukusifu.   

[12] [24]  Baraka za Jina Lako ni kubwa, kwani makubwa yaliyo mazuri hutokana na kukumbuka Jina Lako.

[13] [25]  Utukufu na Nguvu Zako.

[14] [26]  Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana. 'Uqayl amesema (Uk. 103) "Hii imesimuliwa kupitia njia mbalimbali kwa isnaad Swahiyh". Imetolewa katika Al-Irwaa (Namba 341) Imesimuliwa na Ibn Mandah katika At-Tawhiyd (123/2) kwa isnaad Swahiyh na An-Nasaaiy katika Al-Yawm wal-Laylah ikiwa ni mawquuf na marfuu'  kama katika Jaami' Al-Masaaniyd ya Ibn Kathiyr (Mj. 3 Kifungu 2. Uk. 235/2)

 

[15] [27] Abu Daawuud na Atw-Twahaawiy kwa isnaad Swahiyh.

[16] [28] Muslim Na Abu Awaanah; At-Tirmidhiy kasema ni Swahiyh. Kadhalika Abu Na’iym ameisimulia katika ‘Akhbaar Aswbahaan’ (1/210) kutoka kwa Jubayr bin Mutw-am ambaye alimsikia Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma kwenye Swalah ya Sunnah.

[17] [45] Muslim na Abu 'Awaanah

[18] [46] Wewe Ndiye Mwenye kuzipa mwanga na Kwayo ndio Wanaopata uongofu kutoka Kwako.

[19] [47] Mwenye kuhifadhi na Mchungaji wao.

[20] [48]  Al-Bukhaariy na Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud, Ibn Nasr na Ad-Daarimiy.

[21] [49]  Ingawa inapaswa kusomwa katika Swalah za fardhi pia, isipokuwa kwa Imaam kwa khofu ya kurefusha Swalah kwa Maamuma.

[22] [50] Muslim na Abu 'Awaanah.

[23] [51]   Ahmad, Ibn Abi Shaybah (12/119/2), Abu Daawuud na At-Twabaraaniy katika Mu'jam al-Awswatw (62/2) ikiwa na isnaad moja Swahiyh na nyingine Hasan.

[24] [52]   At-Twayaalisiy na Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh.

Share [53]

014-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Katika Swalah, Na Kusoma Aayah Moja Moja

 

KISOMO (TILAAWAH)

 

Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akijikinga kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kusema:

 

A’udhu bil Llaahi minash Shaytwaanir Rajiiymi Min Hamzihii Wa Nafkhihii Wa Nafathihi

“Najilindia na Allaah kutokana na Shaytwaan aliyefukuzwa, najilinda na (kutokana na) wazimu wake[1] na kiburi chake, na ushairi [kutabana] wake[2]

Mara nyingine huongeza kwa kusema,

A’udhu bil Llaahis Samiy’il ‘Aliymi Minash Shaytwaanir…

Najikinga kwa Allaah, Mwingi wa Kusikia, Mwenye Ujuzi, kutokana na Shaytwan…[3]

Kisha husoma,

Bismi-Llaahir Rahmaanir Rahiym

Kwa Jina la Allaah,Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.

Hakuwa akinyanyua au kupaza sauti[4]

 

 

 

KUSOMA AAYAH MOJA MOJA

 

Kisha alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Suratul-Faatihah na akigawanya (kisomo chake,) kwa kuisoma Aayah moja moja; kama hivi:

 

 

BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym

[Kisha hupumua/husimama, kisha husema:]

AlhamduliLlaahi Rabbil ‘Aalamiyn

[Kisha hupumua/husimama, kisha husema:]

Ar-Rahmaanir-Rahiym

[Kisha hupumua/husimama, kisha husema:]

Maaliki Yawmid Diyn

Kisomo chake kilikuwa kama hivyo, hadi mwisho wa Surah. Na hivyo hasa ndivyo ilivyokuwa kisomo chake chote, kila anaposoma huwa anasimama/anapumua mwisho wa Aayah na wala haiunganishi na Aayah inayofuatia[5].

mara nyingine alikuwa akiisoma bila ya kuivuta/bila ya kutia madda[6] (alisoma):

Malik Yawmid Diyn

Mfalme wa Siku Ya Qiyaamah

 

(badala ya

Maaliki Yawmid Diyn

 

Mwenye kumiliki Siku Ya Qiyaamah)

 

 

 





[1]  Maneno matatu ya Kiarabu; hamz, nafkh na nafth yamefasiriwa na baadhi ya wapokezi kuwa hamz ni aina ya wazimu, na nafkh ni kiburi, na nafth ni ushairi; yametafsiriwa hivyo hivyo na msimulizi; tafsiyr zote tatu zimepokewa (zimerudiwa pia) marfuu’an kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa isnaad Swahiyh Mursal (Ni hadiyth katika isnaad yake hakutaja Swahaba, bali kataja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)). Na kusudio la (kwa) 'ushairi' [kutabana] hapa ni mashairi yasiyokubalika/yasiyo na heshima/yenye kudharauliwa (ina maana kwa majaribio yasiyo na mafanikio) kwani Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika katika baadhi ya ushairi kuna (ni) hikma)) [Al-Bukhaariy)

[2] Abu Daawuud Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwny na Al-Haakim ambaye pamoja na Ibn Hibban na Adh-Dhahaabiy wamesema ni Swahiyh. Imetolewa pamoja  na inayofuatia katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl (342)

 

[3]   Abu Daawuud na At-Tirmidhiy kwa isnaad nzuri. Ahmad ameinukuu katika Massail ya Ibn Haaniy 1/50

[4]   Al-Bukhaariy, Muslim, Abu 'Awaanah, At-Twahaawiy na Ahmad.

 

[5]Abu Daawuud na Sahmiy (64-65); Al-Haakim amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amakubaliana naye. Imetolewa katika Al-Irwaa (343). Na ameipokea Abu 'Amr Ad-Daaniy katika Al-Muktafaa (5/2) na kasema: Hadiyth hii ina njia nyingi na ndiyo tegemeo katika mlango huu, kisha akasema: (na) Kundi la Maimamu wengi waliotangulia na Maqurraa (wasomaji wa Qur-aan) waliopita walikuwa wakipendelea kusimama katika kila Aayah hata kama (Aayah nyingine) itakuwa imefungamana  katika maana na Aayah ijayo") Nasema: Sunnah hii imepuuzwa na Maqurraa (wasomaji wa Qur-aan) wengi wa nyakati hizi, achilia mbali wengineo ambao si Maqurraa.

[6] Tamaam Ar-Raaziy katika Al-Fawaaid, Ibn Abu Daawuud katika Maswaahif (7/2), Abu Nu'aym katika Akhbaar Aswbahaan (1/104) na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekuliana naye, qiraa/kisomo hichi  ‘Malik’ ni mutawaatir pia kama kilivyo kile qiraa cha kwanza ‘Maalik’.

Share [54]

015-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Ulazima Wa Kusoma Suratul Faatihah Na Fadhila Zake

 

 

ULAZIMA (UFARADHI) WA AL-FAATIHA NA FADHILA ZAKE

 

Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akitilia mkazo na kusisitiza kuhusiana na (Alisisitiza mno) umuhimu wa Surah hii, alikuwa akisema: ((Hakuna Swalah kwa asiyesoma [ndani yake] Ufunguo wa Kitabu))[1]

 

Na Katika usemi mwengine: ((Swalah haitimii mtu asiposoma ndani yake Ufunguo wa Kitabu))[2]

 

Na wakati mengine anasema: ((Mwenye kuswali Swalah yoyote ile bila ya kusoma ndani yake Ufunguo wa Kitabu basi hiyo Swalah ni khiddaaj[3], ni khiddaaj, ni khiddaaj, haikukamilika))[4]

 

Na anasema (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Amesema: "Nimegawa Swalah[5] baina Yangu na mja Wangu (katika) sehemu mbili; nusu ya kwanza ni Yangu na nusu nyengine iliyobaki ni ya mja Wangu, na mja Wangu atapata alichokiomba" (Kisha) Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Someni: Mja anasema: "Al-hamdu Llillaahi Rabbil ‘Alaamiyn”, Allaah (سبحانه وتعالى) Husema "Mja Wangu amenisifu" Mja akisema: "Ar-Rahmaanir Rahiym”, Allaah Husema: "Mja Wangu amenitukuza" Mja akisema: "Maalik/Malik”,Allaah Husema: Mja Wangu Ameniadhimisha" Mja akisema: "Iyyaaka na’budu wa iyyaaka nasta’iyn”, [Husema]: "Hii ni baina Yangu na Mja Wangu, na Mja wangu atapata atachoomba". Mja akisema: "Ih-dinaas swiraattal mustaqiym, swiraattal Laadhiyna An’amta ‘alayhim ghayril maghdhuubi ‘alayhim wala-dhwaaliyn”, [Husema] Yote haya ni ya Mja Wangu na Mja Wangu atapata aliyoyaomba"[6]

 

Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah Aliyetukuka hakuteremsha katika Tawraat wala katika Injiyl chochote kile chenye kufanana na Ummul Qur-aan -Mama wa Qur-aan-, nayo Ni Aayah Saba zisomwazo mara kwa mara[7] [Na Qur-aan Tukufu niliyopewa])[8]

 

Alimuamrisha (صلى الله عليه وآله وسلم) "Mtu aliyeswali vibaya" aisome hiyo Faatihatul Kitaabu katika Swalah yake"[9](Lakini) na kwa yule asiyeweza kuihifadhi alimuambia (aliyeisahau): Sema:

 

Subhaana Llaah, Wal-Hamdu Lillaah, wala ilaaha illa Llaahu, wa Allaahu Akbar, wala Hawla wala Quwwata ila bi Llaah

 

Ametakasika Allaah  na sifa njema ni za Allaah  na hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, na Allaah  ni Mkubwa na Hakuna uwezo wala nguvu ila za Allaah[10]

 

 

Na (Pia) alimuambia "aliyeswali kimakosa": ((Ikiwa umehifadhi cho chote kile katika Qur-aan basi isome, vyenginevyo msifu Allaah, kiri Ukubwa Wake, na kiri kwamba hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye))[11]

 





 



[1] Al-Bukhaairy, Muslim, Abu 'Awaanah na Al-Bayhaqiy. Imetolewa katika Al-Irwaa (302)

[2] Ad-Daaraqutwniy, ambae amesema kuwa ni Swahiyh, na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake. Pia katika Al-Irwaa (302)

[3] Kwa maana kuwa ni kasoro, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri kwa kusema: haikutimilia

[4] Muslim na Abu 'Awaanah.

[5] Ina maana kuwa ni Suratul Faatihah, ni katika mifano ya kutaja kitu chote lakini kinachokusudiwa ni baadhi tu ya kitu hicho, kwa kusisitiza umuhimu/utukufu wake.

[6] Muslim, Abu 'Awaanah na Maalik, na inayo yenye kuipa nguvu –shaahid- kutokana na Hadiyth ya Jaabir iliyothibiti kwa As-Sahmiy katika Taariykh Jurjaan (144)

[7] Al-Baajiy amesema: "Anakusudia maneno ya سبحانه وتعالى: ((Na tumekupa Aayah saba zinazosomwa mara kwa mara, na Qur-aan Tukufu)) [Al-Hijr: 15:87]. Imeitwa 'saba', kwa sababu ni Aayah saba, na al-Mathaaniy (inayosomwa mara kwa mara') kwa sababu inarudiwa katika kila rakaa, na sababu ya kuitwa (Imeitwa) 'Qur-aan Tukufu' kubainisha jina hili kwa ajili yake khaswa, japokuwa kila sehemu ya Qur-aan ni Tukufu. Kama inavyosemwa kuhusiana na Ka'abah kuwa ni 'Nyumba ya Allaah' japokuwa kuwa nyumba zote ni Zake Allaah, lakini hivi ni kwa njia ya kuibainisha umahsusi na utukufu wake"

[8]  An-Nassaiy na Al-Haakim ambae amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy amekubaliana nayo.  

[9] Al-Bukhaariy katika makala yake 'Kusoma nyuma ya Imaam’ kwa isnaad Swahiyh.

[10] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/80/2), Al-Haakim, At-Twabaraaniy na Ibn Hibbaan ambae pamoja na Al-Haakim, wamesema ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana nayo. Imo katika Al-Irwaa (303)

[11] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambae amesema ni nzuri; isnaad yake ni Swahiyh. (Swahiyh Abu Daawuud Namba. 807)

Share [55]

016-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kufutwa Kisomo Nyuma Ya Imaam Katika Swalah Za Sauti, Na Kuwajibika Katika Swalah Za Kimya

 

 

KUFUTWA KISOMO NYUMA YA IMAAM KATIKA SWALAH ZA JAHRIYYAH (SWALAH ZA KUNYANYUA SAUTI)

 

Alikuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ameruhusu kwa wale waliokuwa ma-amuma kuisoma Suratul-Faatihah nyuma ya Imaam katika Swalah za jahriyyah, na mara moja alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم), "Akiswali Alfajiri na kisomo kikawa kigumu kwake. Alipomaliza alisema: ((Labda mnasoma nyuma ya Imaam wenu!)). Tukasema: "Ndio hadhdhan[1] Ewe Mjumbe wa Allaah". Akasema: ((Basi Msifanye hivyo isipokuwa [kwa kusoma mmoja wenu] Ufunguo wa Kitabu, kwani hakuna Swalah kwa asiyeisoma))[2]

 

Kisha aliwakataza kusoma katika Swalah za jahriyyah kabisa, na hilo lilitokea wakati,

 

"Alipomaliza Swalah ambayo alikuwa akisoma kwa sauti [katika usimulizi (mmoja) ilikuwa Swalah ya Alfajiri] basi akauliza: ((Je, kuna (yeyote) aliyekuwa akisoma pamoja nami hivi sasa?)) Mtu mmoja akajibu: "Ndio, mimi Ewe Mjumbe wa Allaah". Akasema: ((Mimi Nasema: sasa kwa nini naingiliwa kati katika kisomo changu][3] [Abu Hurayrah alisema]: (Hivyo) watu wakaacha kusoma pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kila anapokuwa anasoma kwa sauti baada ya kusikia hivyo kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) [wakawa wanaendelea kusoma kimya kimya kila anapokuwa Imaam haisomi kwa sauti][4]

 

Pia Akaufanya (صلى الله عليه وآله وسلم) ukimya katika kisomo cha Imaam kuwa ni sehemu katika kukamilisha kumfuata Imaam, kwa kusema: ((Kwa hakika amewekwa Imaam ili apatwe kufuatwa, hivyo anapoleta takbiyr, na nyinyi leteni takbiyr, na anaposoma kaeni kimya))[5] kama alivyofanya kumsikiliza Imaam kuwa kunatosheleza na kisomo nyuma yake, kwa kusema (aliposema): ((Mwenye kuwa na Imaam, basi kisomo cha Imaam huyo ni kisomo chake))[6]. Hii inahusu Swalah za jahriyyah.

 

 

 

 

 

KUWAJIBIKA KUSOMA KATIKA SWALAH ZA SIRRIYYAH (SWALAH ZA KIMYA)

 

Ama katika Swalah za kimya kimya, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaachilia waendelea kusoma humo. Jaabir alisema: "Tulikuwa tukisoma katika (Swalah ya) Adhuhuri na 'Aswr nyuma ya Imaam katika Rakaa mbili za mwanzo Suratul-Faatihah na Surah nyingine, na katika mbili za mwisho Suratul-Faatihah[7]

 

Lakini, alichukizwa kwa tashwishi na kubabaishwa, kwa kisomo chao pale aliposwali Adhuhuri na Maswahaba akauliza: ((Nani katika nyinyi aliyesoma: "Sabbihisma Rabbikal A’laa" [Suratul-A'laa, 87:1])). Mtu mmoja akajibu: "ni mimi" [sikuwa na kusudio lo lote lile kwa kuisoma ila kheri] Akasema: ((Nilijua kuwa kuna mtu anavutana na mimi kwayo))[8]

 

Na Katika Hadiyth nyingine: "Walikuwa wakisoma nyuma ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), hivyo akasema: ((Mmenibabaisha katika kisomo changu))[9]

 

Akasema: ((Anayeswali huwa ananongo’na na Mola wake, basi aangalie cha kumnongo’neza, wala msisome Qur-aan pamoja wote kwa sauti))[10] 

 

Pia alikuwa akisema: ((Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allaah atapata hasanah (jema) moja, na kila hasanah moja ni sawa na thawabu kumi, (wala) sisemi 'Alif-Laam-Miym' ni herufi moja, bali Alif ni herufi moja na Laam ni herufi moja na Miym ni herufi moja)) [11]

 

 





[1] Hadhdhan:  kusoma haraka haraka, kwa kukimbilia au kuharakiza.

[2] Al-Bukhaariy katika kijarida, Abu Daawuud na Ahmad. At-Tirmidhy na Ad-Daaraqutwniy wamesema ni nzuri.

[3] Amesema al-Khattabiy: maana yake ameingilia kisomo changu, pia yawezekana ikawa ushindani kwa maana ya kushirikiana na kubadilishana, na maana ya pili ndio iliyokusudiwa hapa kwa sababu ya kuacha Swahabah (رضي الله عنهم) kusoma moja kwa moja, na kama ingelikuwa kusudio ni maana ya kwanza, basi wesingeliacha kusoma, lakini inaonyesha kuwa ni kuingilia kati tu kama ilivyodhihiri.

[4] Maalik, Humaydy, Al-Bukhaariy katika kijarida chake, Abu Daawuud na Mahaamaliy (6/139/1) At-Tirmidhiy amesema ni nzuri, Abu Haatim Ar-Raaziy, Ibn Hibbaan na Ibn Qayyim wamesema kuwa ni Swahiyh, na hadiyth yenye kuipa nguvu –shaahid- katika Hadiyth ya ‘Umar ambayo mwisho wake: sasa kwa nini nashindaniwa Qur-aan?! Haimtoshelezeshi mmoja wenu kisoma cha Imaam wake?! Kwa hakika amewekwa Imaam ili apatwe kufuatwa, basi ataposoma kaeni kimya. Imepokewa na al-Bayhaaqiy katika kitabu ulazima wa kisomo katika Swalah, kama ilivyo katika al-Jaami’ al-Kabiyr (3/344/2)

[5] Ibn Abi Shaybah (1/97/1), Abu Daawuud, Muslim, Abu 'Awaanah na al-Ruwayaaniy katika musnad yake, (24/119/1). Imetolewa katika Al-Irwaa (332,394).   

[6] Ibn Abi Shaybah (1/97/1), Ad-Daraaqutwniy, Ibn maajah, At-Twahaawiy na Ahmad kutoka njia mbali mbali, musnad na mursal. Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema kuwa ina nguvu kama katika Al-Furuu' ya Ibn 'Abdil-Haadiy (48/2). Al-Buswayriy amesema kuwa baadhi ya isnaad zake kuwa ni Swahiyh. Nimeijadili Hadiyth hii kwa kirefu na kuzitafiti njia zake (mbali mbali) za usimulizi katika maandishi kisha katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl (Namba. 500)

[7] Ibn Maajah kwa isnaad Swahiyh. Imetolewa katika Al-Irwaa (506)   

[8] Muslim, Abu 'Awaanah na Siraaj.

[9] Al-Bukhaariy katika makala yake, Ahmad na Siraaj kwa isnaad nzuri.

[10] Maalik na al-Bukhaariy katika Af'aal al-'Ibaad kwa isnaad Swahiyh.

 

TANBIHI:

Rai ya uthabiti wa kusoma nyuma ya Imaam katika Swalah za Sirriyah na sio za Jahriyyah, imetolewa na Imaam Ash-Shaafi'y mwanzo, na Muhammad mwanafunzi wa Abu Haniyfah katika usimulizi kutoka kwake ambao umependelewa (zaidi) na Shaykh 'Aliy al-Qaariy na baadhi ya Mashaykh (wengine) wa madhehebu. Pia (ulikuwa) ni msimamo wa Imaam Az-Zuhriy, Maalik, Ibn Al-Mubaarak, Ahmad bin Hanbal, na kundi la Muhaddithiyn na wengineo, na ni mapendeleo ya Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah.

[11] At-Trimidhiy na Ibn Maajah kwa isnaad Swahiyh. Imesimuliwa pia na Aajuriy katika Aadaab Hamalat al-Qur-aan. Ama Hadiyth: "Mwenye kusoma nyuma ya Imaam mdomo wake utajazwa moto" ni Hadiyth ya uzushi (mawdhwuu) na hii imelezewa katika Silsilat al-Ahaadiyth Adh-Dhwa'iyfah (Namba. 569) Taz. Kiambatisho 5.

Share [56]

017-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Aamiyn - Imaam Kunyanyua Sauti Yake Anapoileta

 

 

AAMIYN, IMAAM KUNYANYUA SAUTI YAKE ANAPOILETA

 

 

Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anapomaliza kusoma Al-Faatihah husema:


‘Aamiyn’

 

kwa sauti na huku akiirefusha sauti yake[1]

 

 

Pia alikuwa akiwaamrisha wenye kumfuata Mamuumiyn waseme Aamiyn, kwa kusema: ((Imaam ataposema:

 

“Ghayril Magh-dhuubi ‘alayhim waladh dhwaaaaaalliyyyyyyn”

 

“Sio waliokasirikiwa wala waliopotea”

 

basi semeni: ‘Aamiyn’ [kwani Malaika na wao pia huwa wanasema: ‘Aamiyn’ na hakika Imaam anasema: 'Aamiyn']))

 

Katika usemi mwengine: ((Imaam atakaposema ‘Aamiyn’ basi na nyinyi semeni: ‘Aamiyn’ - kwani itakayeafiki ‘Aamiyn’ yake na ‘Aamiyn’ ya Malaika - [katika usemi mwengine] ((Anaposema Mmoja wenu katika Swalah ‘Aamiyn’ na Malaika mbinguni wakasema ‘Aamiyn’, zikaafikiana moja na nyingine, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia))[2]

 

Na Katika Hadiyth nyingine, ((Semeni: Aamiyn, Allaah Atakujibuni))[3]

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Mayahudi hawakuoneeni choyo kwa jambo lo lote lile zaidi kama wanavyoona choyo kwa kutoleana saalam na kuitikia Aamiyn [nyuma ya Imaam]))[4]



[1] Al-Bukhaairy katika Juz' Al-Qiraah na Abu Daawuud kwa isnaad Swahiyh.

[2] Ash-Shaykhaan na An-Nasaaiy na Ad-Daarimy. Maneno yaliyozidi yameripotiwa na wawili wa mwisho na ni dalili kuwa Hadiyth hii haiwezi kuthibitisha kuwa Imaam hasemi ‘Aamiyn’ kama ilivyoripotiwa na Maalik, hivyo Ibn Hajar anasema katika Fat-h Al-Baariy: "Inaonyesha dhahiri kwamba Imaam anasema ‘Aamiyn’ ". Ibn 'Abdil Barr anasema katika Tamhiyd (7/13), "Ni rai ya Waislamu wengi pamoja na Maalik kama watu wa Madiynah walivyosimulia kutoka kwake, kwani ni Swahiyh kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah (ambayo ni hii) na ile ya Waail Ibn Hujr (yaani ya nyuma yake)"

 

[3] Muslim na Abu Aawaanah.

[4] Al-Bukhaariy katika Al-Adaab Al-Mufrad, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah, Ahmad na Siraaj kwa isnaad mbili na zote ni Swahiyh.

TANBIHI:

‘Aamiyn’ ya Maamuumiyn nyuma ya Imaam inakuwa kwa sauti na inakuwa inaletwa pamoja na ‘Aamiyn’ ya Imaam, na wala hawamtangulii kama wafanyavyo waswaliji wengi, na wala hawaicheleweshi na ‘Aamiyn’ ya Imaam. Hii ndio iliyokuwa Raajih (na nguvu kwangu) kama nilivyoihakiki katika baadhi ya vitabu vyangu; miongoni mwake ni ‘Silsilat al-Ahaadityh Adh-Dhwa'iyfah’ (Namba. 952 Mjalada 2) ambayo imechapishwa kwa Fadhila Zake Allaah, na Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (1.205). Taz. Kiambatisho 6.   

Share [57]

018-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Baada Ya Al-Faatihah

 

 

KISOMO CHAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) BAADA YA AL-FAATIHAH

 

Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah nyingine baada ya al-Faatihah, na alikuwa akikirefusha hicho kisomo mara nyingine, na mara nyingine akikifupisha kwa sababu ya safari, au kikohozi, au maradhi au kilio cha mtoto.

 

Kama alivyosema Anas Ibn Maalik (رضي الله عنه): "Alifupisha[1] Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) siku moja katika Swalah ya Alfajiri" (Na Katika Hadiyth nyingine, "Aliswali (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalah ya Asubuhi akasoma Surah mbili zilizo fupi sana katika Qur-aan)". Pakaulizwa: "Ewe Mjumbe wa Allaah, kwa nini umefupisha?" Akasema: ((Nimesikia kilio cha mtoto hivyo nimehisi kwamba mama yake yu pamoja na sisi anaswali, kwa hiyo nikataka kumpa wasaa mama yake kwa ajili yake))[2]

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika mimi huingia katika Swalah hali ya kuwa ninataka kuirefusha, ninaposikia kilio cha mtoto, hufupisha Swalah yangu kwa kuelewa machungu makubwa ya mama yake kwa kilio chake))[3]

 

"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akianza kusoma kutoka mwanzo wa Surah, na aghlabu huimaliza"[4]    

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Ipeni kila Surah sehemu yake katika Rukuu na Sujuud))[5]

 

Katika usemi mwengine: ((Kwa Kila Surah Raka’ah))[6]

 

Mara nyingine huigawa Surah katika Rakaa mbili[7] na mara nyingine huirudia yote nzima katika Raka’ah ya pili.[8]

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunganisha katika Rakaah baina  Surah mbili au zaidi.[9]

 

Mtu Mmoja katika Answaar alikuwa akiswalisha katika Msikiti wa Qubaa, na alikuwa kila anapoanza kuwasomea Surah[10] katika Swalah baada ya al-Faatihah, huanza kwa ‘Qul Huwa Llaahu Ahad’ [Suratul-Ikhlaasw: 112] hadi mwisho, kisha anasoma Surah nyingine pamoja nayo, na alikuwa akifanya hivyo katika kila Raka’ah. wenzake walimuuliza kwa kusema: "Unaanza na Surah hii, kisha huoni kama inakutosheleza mpaka unasoma nyingine, basi chagua moja; isome hiyo pekee au iache na uisome nyingine". Akasema: "Sitoiacha, ikiwa mtapenda mimi nikuswalisheni (niwe Imaam wenu) kwayo, nitaendelea, lakini ikiwa mtachukiwa, sitokuswalisheni tena", na walikuwa wakimuona kuwa yeye ni mbora miongoni mwao, na pia hawakuwa wanapendekezewa kuswalishwa na mwenginewe. Na pindi alipokuja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuelezea habari hiyo, Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Ewe fulani, kipi kinachokuzuia kutekeleza wanayokuomba watu wako? Na Kipi kinachokupelekea kuwa lazima uisome Surah hii katika kila Raka’ah?)) Akasema: "Hakika Naipenda Surah hii" akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Mapenzi yako kwayo yatakuingiza Peponi))[11]

 

 

 



[1] Alifupisha Swalah kwa maana kuwa hakuirefusha, na katika Hadiyth hii na nyingine kama hii zinaonyesha kuruhusiwa watoto wadogo kuingia Misikitini. Ama Hadiyth iliyozagaa na kueleweka na wengi hadi kufikia kuwa inasemwa na kila mtu: "Watengeni mbali watoto wenu na Misikiti… "ni hadiyth dhwa'iyf na haiwezi kuwa ni dalili kabisa kwa mawafikiano yaliyopo. Na Miongoni mwa walisema kuwa ni dhwa'iyf ni: Ibn Al-Jawziy, Al-Mundhiriy, Al-Haythamiy, Ibn Hajar Al-'Asqalaaniy na Al-Buuswiyriy. Na akasema 'Abdul-Haqq Al-Ishbiyliy: "Haina asili"

[2] Ahmad kwa isnaad Swahiyh. Na Hadiyth nyingine imepokelewa na Ibn Abi Daawuud katika al-Maswaahif (4/14/2).

[3] Al-Bukhaariy Na Muslim   

[4] Linathibitishwa hili na Hadiyth nyingi zilizotajwa mbele.

[5] Ibn Abi Shaybah (1/100/1), Ahmad na 'Abdul-Ghaniy Al-Maqdisiy katika Sunan (9/2) kwa isnaad Swahiyh.

[6] Ibn Naswr na At-Twahaawiy kwa isnaad Swahiyh. Maana ya Hadiyth kwangu ni: Jaaliyeni kwa kila Rakaa Surah kamili, ili Rakaa iwe na hadhi yake kamili kwa hiyo Surah! Amri hii ni pendekezo na sio lazima utekelezaji wake kutokana na dalili inayofuatia.

[7] Ahmad na Abu Ya'ala kutoka njia mbili. Pia tazama "kisomo katika Swalah ya Alfajiri'

[8] Kama alivyofanya katitka Swalah ya Alfajiri, kama itakavyofuatia.

[9] Maelezo yake na vyanzo vyake vitafuatia karibuni.

[10] Yaani miongoni mwa Surah baada ya al-Faatihah.

[11] Al-Bukhaairy ameipokea ta'liyqan (ni hadiyth inayoondoshwa mwanzo wa isnaad yake Msimulizi mmoja au zaidi kwa mfululizo); na At-Tirmidhiy ameipokea Mawswuulan (ni hadiyth inayoungana isnaad yake, iwe imemalizika kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) au kwa Swahaba), na At-Tirmidhiy akasema: ni Swahiyh.

Share [58]

019-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuchanganya Kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) Baina Ya Surah Zinazofanana Na Nyinginezo Katika Rakaa

 

KUCHANGANYA KWAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) BAINA YA SURAH ZINAZOFANANA NA NYINGINEZO KATIKA RAKAA

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunganisha baina ya An-Nadhwaair([1])  miongoni mwa Surah za Mufasswal([2]), hivyo basi alikuwa akisoma jozi mojawapo za Surah zifuatazo katika Rakaa moja([3]):

 

Ar-Rahmaan (55: 78) ([4]) na An-Najm (53: 62).

Al-Qamar (54: 55) na Al-Haaqqah (69: 52).

At-Twuur (52: 49) na Adh-Dhaariyaat (51: 60).

Al-Waaqi'ah (56: 96) na Al-Qalam (68: 52).

Al-Ma'arij (70:44) na An-Naazi'aat (79:46).

Al-Mutwaffifiyn (83: 36) na 'Abasa (80: 42).

Al-Muddaththir (74: 56) na Al-Muzzammil (73: 20).

Ad-Dahr (76: 31) na Al-Qiyaamah (75: 40).

An-Nabaa (78: 40) na Al-Mursalaat (77: 50).

Ad-Dukhaan (44: 59) na At-Takwiyr (81: 29).

 

Mara nyingine alikuwa akiunganisha baina ya Surah kutoka Sab'at-Twiwaal (Surah Saba ndefu); kama al-Baqarah, an-Nisaa na aal-'Imraan katika Rakaa moja kwenye Swalah ya usiku kama itakavyokuja. Na alikuwa akisema:

((Swalah bora kabisa ni yenye kisimamo kirefu)).([5])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposoma:

 

((أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَى))

 

Alaysa dhaalika biqaadirin ‘alaa-an Yuhyiyal Mawtaa

 

((Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu)). [Al-Qiyaamah 75: 40)

 

Husema:

 

Sub-haanak fabalaa

Utukufu ni Wako Ndio hapana shaka

 

Na anaposoma:

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

 

Sabb-hisma Rabbikal A’laa

((Litakase Jina la Mola wako Mlezi Aliye juu kabisa)). [Al-A'laa 87: 1)

 

Husema:

Sub-haana Rabbiyal A’laa

Ametakasika Mola wangu Aliye juu([6]).

 

 

 

 





[1] "An-Nadhwaair": Ni Surah zilizofanana katika maana. Ni kama zile ambazo zote zina nasaha, maamrisho au visa.

[2] Mufasswal, hizi zimekubalika kuwa zinazomalizia Qur-aan mwisho, na mwanzo wake ni Surat Qaaf (Namba 50) kwa rai iliyo sahihi zaidi.

[3] Al-Bukhaary na Muslim.

[4] Namba ya mwanzo inamaanisha Surah, na ya pili ni idadi ya Aayah za hiyo Surah. Na namba zenye kumaanisha Surah, zimetuwekea wazi kuwa  hakuwa

(صلى الله عليه وآله وسلم) akifuata katika kuunganisha baina ya Surah nyingi za An-Nadhwaair utaratibu wa Surah ulivyo katika Msahafu. Hivyo inaonyesha kuwa ni jambo lenye kuruhusiwa. Hali kama hiyo itaonekana katika Swalah ya Usiku, japokuwa ni bora zaidi kufuata mpangilio wa Qur-aan.

[5] Muslim na Atw-Twahaawiy.

[6]  Abu Daawuud na al-Bayhaqiy kwa isnaad Swahiyh. Hadiyth hii ni ya kawaida, hivyo inajumuisha kisomo kwenye Swalah na nje ya Swalah, au Swalah hiyo iwe ni ya Sunnah au ya Faradhi.  Ibn Abi Shaybah (2/132/2) amesimulia kutoka kwa Abu Muusa Al-Ash'ariyy na Al-Mughiyrah kwamba wao wawili walikuwa wakisema hivyo katika Swalah ya Faradhi. Na ameipokea kutoka kwa 'Umar na 'Aliy bila ya maelezo hayo.      

 

Share [59]

020-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Ruhusa Ya Kusoma Al-Faatihah Pekee

 

RUHUSA YA KUSOMA AL-FAATIHAH PEKEE

 

Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) alikuwa akiswali 'Ishaa (ya mwisho) pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha akirudi huwaswalisha wenzake. Usiku mmoja, aliporudi aliwaswalisha, na akaswali kijana mmoja katika watu wake [wa Banu Salamah aliyeitwa Sulaym], lakini (Swalah) ilipokuwa ndefu kwa yule kijana, [alijiondokea] na akaswali [pembezoni mwa Msikiti]. Kisha akatoka na kushika ungwe za ngamia wake na akajiondokea. Mu'aadh (رضي الله عنه) Alipomaliza kuswali alielezwa yaliyotokea, akasema: "Bila shaka ana baadhi ya unafiki! Nitamweleza Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyofanya". Na yule kijana naye akasema: "Nami nitamweleza Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyofanya". Kulipopambazuka, walikuja kwa Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi Mu'aadh akamweleza yale aliyoyafanya yule kijana. Kijana akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Yeye hukaa na wewe muda mrefu, kisha anarudi na kuturefushia". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Je, wewe ni mfitini ewe Mu'aadh?!)). Na akasema kumwambia yule kijana([1]): ((Vipi  unafanya unaposwali ewe mtoto wa ndugu yangu?)) Akamjibu: "Nasoma Kifungulio cha Kitabu, kisha namuomba Allaah Pepo, na najikinga Kwake kutokana na moto. Na hakika mimi sielewi dandanah([2]) yako wala dandanah ya Mu'aadh!" Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Hakika Mimi na Mu'aadh tuko katika hayo hayo mambo mawili, au mfano wake)).  Msimulizi alisema: "Yule Kijana akasema: "Lakini Mu'aadh ataelewa watakapokuja watu wakapewa habari kwamba adui wamefika". Msimulizi akasema: "(Hivyo) Adui wakaja na yule kijana akafa shahidi. Baada ya hapo, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema kumwambia Mu'aadh: ((Amefanya nini yule aliyejadiliana nami na wewe?)). Akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Amemsadikisha Allaah, nami sikuwa mkweli, amekufa shahidi".([3])

 





[1]  Asili ni 'Yule Kijana".  

[2] "Dandanah" ni mtu anaposema maneno kwa madaha na kusikiwa mvumo wa maneno yake lakini hayafahamiki. Ni karibu kidogo na kunong'ona. (An-Nihaayah)

[3]  Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1634) na Al-Bayhaqiy kwa isnaad Swahiyh. Na pahala penye ushahidi kutokana na Hadiyth pako katika Abu Daawuud (Namba 758, Swahiyh Abu Daawuud) na asili ya kisa chenyewe kipo katika as-Swahiyhayn (Al-Bukhaary na Muslim). Nyongeza ya mwanzoni iko katika usimulizi wa Muslim. Ya pili iko katika Ahmad (5/74), na ya tatu na ya nne katika Al-Bukhaary. Pia mlango wa hizi, ni Hadiyth iliyotolewa na Ibn 'Abbaas kwamba Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali Rakaa mbili ambazo hakusoma ndani yake isipokuwa Kifungulio cha Kitabu (Al-Faatihah) pekee". Imesimuliwa na Ahmad (1/282), Al-Haarith bin Abi Usaamah katika musnad yake (Uk. 38 kutoka zawaaiyd yake) na Al-Bayhaqiy (2/62) kwa isnaad dhwa'iyf. Nilikuwa nimesema kuwa Hadiyth hii ni nzuri katika chapa  zilizopita, kisha ikanibainikia kuwa nilikuwa nimekwenda kombo, kwa sababu Hadiyth  yenyewe inazunguka kwa Handhwalah Ad-Dawsiy ambaye anaeleweka kuwa ni dhaifu, na sielewi kwa nini sikuweza kugundua hili?! Huenda nilifikiri kuwa ni mtu mwengine. Hata hivyo, Sifa zote ni Zake Allaah Aliyeniongoza kuweza kufikia kutambua kosa langu, na ndio maana nikakimbilia kuisahihisha katika chapa. Kisha Allaah Akanisawazisha kwa kuniruzuku Hadiyth hii bora ya Mu'aadh ambayo inahusisha yaliyoashiriwa katika Hadiyth ya Ibn 'Abbaas. Sifa zote ni Zake Allaah Ambaye kwa Neema Zake yanatimia mema.

Share [60]

021-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kunyanyua Sauti Na Kusoma Kimya Katika Swalah Tano Na Swalah Nyinginezo

 

KUNYANYUA SAUTI NA KUSOMA (KISOMO CHA) KIMYA KIMYA KATIKA SWALAH TANO NA NYINGINEZO

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa sauti katika Swalah ya Asubuhi na katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalah ya Magharibi na 'Ishaa, na akisoma kimya kimya katika Swalah za Adhuhuri, Alasiri na Rakaa ya tatu ya Swalah ya Magharibi na Rakaa mbili za mwisho za Swalah ya 'Ishaa.([1])

 

Walikuwa wakiweza kuelewa kuwa anasoma kimya kimya kutokana na mtikisiko wa ndevu zake([2]) na kwa kuwasikilizisha Aayah mara nyingine([3]).

 

Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa sauti katika Swalah ya Ijumaa na Swalah za 'Iyd mbili([4]), na Swalah ya kuomba mvua([5]), na Swalah ya kupatwa([6]) jua au mwezi.

 

 

 

KUNYANYUA SAUTI NA KUSOMA KIMYA KATIKA SWALAH YA USIKU([7])

 

Ama katika Swalah ya usiku, mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma kimya kimya na mara nyingine kwa sauti([8]), na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposoma hali ya kuwa yuko nyumbani kwake, humsikia kisomo chake aliyeko barazani mwake([9]).

 

Huenda mara moja moja akapandisha sauti yake zaidi ya hivyo hadi akaisikia aliyelala([10]).  (Yaani nje ya baraza/uwa).

 

Na hivyo ndivyo alivyowaamrisha Abu Bakr na 'Umar (رضي الله عنهم) wakati alipokuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) ametoka nje usiku mmoja akatahamaki kumuona Abu Bakr (رضي الله عنه) anaswali huku akiishusha sauti yake chini. Na akampitia ‘Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) aliyekuwa akiswali kwa kunyanyua sauti yake juu. (Baadaye,) walipokutana pamoja kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: ((Ewe Abu Bakr! Nilikupitia na hali ukiwa unaswali kwa kushusha sauti yako)). Akasema: "Nimemsikilizisha niliyekuwa nanong’ona Naye ewe Mjumbe wa Allaah".  Akamwambia 'Umar: ((Nilikupitia na hali ukiwa unaswali kwa kupaza sauti yako)). Akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Nilikuwa naondosha usingizi na namkimbiza Shaytwaan". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ewe Abu Bakr! Pandisha sauti yako kidogo. Na akasema kumwambia 'Umar: ((Ewe 'Umar! punguza sauti yako kidogo))([11]).

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Mwenye kusoma Qur-aan kwa kunyanyua sauti, ni kama mfano wa mwenye kutoa sadaka kwa kuonekana na watu, na mwenye kusoma Qur-aan kimya kimya kwa kushusha sauti yake, ni kama mwenye kutoa sadaka kwa siri))([12]).

 





[1] Katika hili kuna Ijmaa ya Waislamu iliyopokewa na Khalaf kutoka kwa Salaf pamoja na Hadiyth Swahiyh ambazo zinathibitisha hayo kama alivyosema An-Nawawiy. Na zitafuatia baadhi yake. Tazama pia Al-Irwaa (345).  

[2] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[3] Al-Bukhaariy na Muslim.

[4] Tazama kisomo (sehemu ya TILAAWAH) chake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah ya Ijumaa na Swalah za 'Iyd mbili.

[5] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim.

[7] 'Abdul-Haqq alisema katika Tahajjud (90/1):

"Ama Swalah za Sunnah za mchana, hakikusihi chochote Swahiyh kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) chenye kuonyesha (kuhusu) kuswali kimya au kwa sauti katika Swalah hizo, Na kinachoelekea (inavyoelekea) zaidi ni kwamba alikuwa akisoma kimya kimya katika hizo Swalah. Imeripotiwa kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba mara moja (wakati wa mchana,) alimpitia 'Abdullaah Ibn Hudhaafa ambaye alikuwa akiswali mchana na kusoma kwa sauti, akamwambia: Ewe 'Abdullaah, Amesikia (mwache) Allaah (Asikie), na wala usitusikilizishe (sio) sisi)). Lakini Hadiyth hii haina nguvu"

[8]  Muslim na Al-Bukhaariy katika Af'aal Al-'Ibaad. 

[9] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy katika Shamaail ikiwa na isnaad nzuri. Hadiyth ina maana kwamba yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa yu katikati baina ya ukimya na kupaza sauti.   

[10] An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy katika Shamaail na Al-Bayhaqiy katika Dalaail ikiwa na isnaad nzuri. 

[11] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[12] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

Share [61]

022-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Alivyokuwa Akisoma (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Mbalimbali. 1 - Swalah Ya Alfajiri

 

ALIYOKUWA AKISOMA (صلى الله عليه وآله وسلم) KATIKA SWALAH (MBALI MBALI)

 

Kuhusu Surah gani na Aayah gani aliyokuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisoma katika Swalah, hilo linatofautiana kwa kutofautika kwa Swalah tano na Swalah nyenginezo. Basi chukua maelezo ya upambanuzi wake kwa kuanzia na Swalah ya kwanza katika Swalah tano:

 

 

1-   SWALAH YA ALFAJIRI

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah([1]) ndefu za mufasswal([2])  hivyo alikuwa (wakati mwengine) akisoma Al-Waaqi'ah (56: 96) na mfano wake katika Rakaa mbili.([3])

 

Alisoma kutoka Surat-Twuur (52: 49) katika Hijjatul-Wadaa’ (Hijjah ya Kuaga).([4])

 

Mara nyingine, alikuwa akisoma Surat Qaaf [50: 45] na mfano wake [katika Rakaa ya mwanzo].([5])

 

Mara nyingine alikuwa akisoma Surah fupi za mufasswal kama:

 

((إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ))

 

((Jua litakapokunjwa)) [At-Takwiyr 81: 29)).([6])

 

Na mara moja alisoma:

((إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا))

 

 

((Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!)). [Az-Zilzalah 99: 8)

 

katika Rakaa zote mbili, jambo lililomfanya msimulizi kusema: "Sielewi kama Mjumbe wa Allaah alisahau au aliisoma kwa makusudi.([7])

 

Alisoma mara moja akiwa safarini:

 

((قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ))

 

 

((Sema: Najikinga kwa Mola Mlezi wa mapambazuko)). [Al-Falaq 113: 5]

 

na

 

 ((قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ))

 

 

((Sema: Najikinga kwa Mola wa wana Aadam)). [An-Naas 114: 6][8]

 

Akasema kumwambia 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه): ((Soma Al-Mu'awwidhatayn([9])katika Swalah zako, kwani hakuna mwenye kutafuta kinga kama hiyo))([10]).

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma zaidi ya hivo, kwani alikuwa akisoma Aayah sitini (60) au zaidi([11] [62]). Baadhi ya wasimulizi wake wamesema: " Sielewi kama ilikuwa katika moja ya Rakaa mbili au katika zote mbili."

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surat Ar-Ruum [30: 60]([12] [63]) na mara nyingine akisoma Surat Yaasiyn [36: 83)([13] [64]).

 

Mara moja aliswali Swalah ya Alfajiri Makkah, akaanza kusoma Suratul-Mu-minuun [23: 118] hadi alipofikia kutajwa Muusa na Haaruun au kutajwa 'Iysa([14] [65]) -Msimulizi mmoja hakuwa na hakika- alianza kukohoa hivyo akarukuu([15] [66]).

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwaswalisha katika Swalah ya Alfajiri kwa kusoma Suratu Asw-Swaaffaat [77: 182]([16] [67])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiiswali Swalah ya Alfajiri siku ya Ijumaa kwa kusoma Surat As-Sajdah [32: 30] (katika Rakaah ya mwanzo na Rakaa ya pili) Surat Ad-Dahr [76: 31].([17])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akirefusha Rakaa ya kwanza na kufupisha Rakaa ya pili.([18] [68])

 

 

KISOMO KATIKA SUNNAH YA ALFAJIRI

 

Kisomo chake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Rakaa mbili za Sunnah ya Alfajiri, kilikuwa chepesi mno([19] [69]) hadi 'Aaishah رضي الله عنها) ) alikuwa akijiuliza kwa kusema: "Je, amesoma ndani yake Kifungulio cha Kitabu (Suratul Faatihah)?"([20] [70]).

 

Mara nyingine alikuwa akisoma baada ya al-Faatihah katika Rakaa ya mwanzo ya hizo mbili Aayah hii:

 

((قُولُواْ آمَنَّا بِاللّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا ...))

 

((Semeni nyinyi: Tumemwamini Allaah na yale tuliyoteremshiwa sisi…)). [Al-Baqarah 2:136) mpaka mwisho wa Aayah.

 

 

(katika Rakaa ya kwanza,) na katika ya pili alikuwa akisoma Aayah:

 

 

((قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْاْ إِلَى كَلَمَةٍ سَوَاء بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ ...)) 

 

((Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi…)) [Al-'Imraan 3: 64] ([21] [71]) mpaka mwisho wa Aayah.

 

Mara nyingine husoma badala ya Aayah ya pili:

 

((فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَى مِنْهُمُ الْكُفْرَ))

 

(('Iysaa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri)) [Al-'Imraan 3:52]([22] [72]) mpaka mwisho wa Aayah.

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Suratul-Kaafiruun [109 -6] katika Rakaa ya kwanza, na Suratul-Ikhlaasw [112-4] katika Rakaa ya pili.([23] [73])

 

Pia alikuwa akisema: ((Hizi ni jozi bora kabisa za Surah (hizi)).([24] [74])

 

Alimsikia mtu akisoma Surah ya mwanzo - Suratul-Kaafiruun - katika Rakaa ya kwanza, akasema: ((Huyu mja amemwamini Mola wake)). Kisha mtu huyo akasoma Surah ya pili - Suratul-Ikhlaasw - katika Rakaa nyengine, akasema: ((Huyu mja amemwelewa Mola wake)).([25] [75])

 

 

[1] An-Nasaaiy na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[2] Sehemu ya saba ya mwisho ya Qur-aan, kuanzia Surah Qaaf (Namba 50) kama ilivyo rai yenye nguvu kabisa kama ilivyotangulia.

[3] Ahmad, Ibn Khuzaymah (1/69/1) na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubaliana naye.        

[4] Al-Bukhaariy na Muslim.

[5] [76] Muslim na At-Tirmidhiy. Imetolewa pamoja na inayofuatia katika Al-Irwaa (345).

[6] [77] Muslim na Abu Daawuud.

[7] [78] Abu Daawuud na Al Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Kinachodhihiri ni kuwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya hivyo kwa makusudi ili kuthibitisha kujuzu kwake.

[8] [79] Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/76/1), Ibn Bushraan katika Al-Amaaliy na Ibn Abi Shaybah (12/176/1). Al-Haakim amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubaliana naye.

[9] [80] Surah mbili za kujikinga; yaani Surah mbili za mwisho katika Qur-aan, zote zinaanzia na Qul-A'udhu…. (Sema najikinga….).

[10] [81] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[11] [82] Al-Bukhaariy na Muslim.

[12] [83] An-Nassaaiy, Ahmad na Al-Bazzaar kwa isnaad nzuri.

[13] [84] Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[14] [85] Muusa ametajwa katika Aayah ya 45: ((ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَى وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ)) na 'Iysa ametajwa katika Aayah ya 50: ((وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَى رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ))

[15] [86] Muslim na Al-Bukhaariy katika Ta'aliyqan, nayo ni Hadiyth inayoondoshwa mwanzo wa isnaad yake msimulizi mmoja au zaidi kwa mfululizo kama ilivyoelezwa nyuma. Imetolewa katika Al-Irwaa (397).

[16] [87] Ahmad na Abu Ya'laa katika Musnad zao, na Al-Maqdisiy katika Al-Mukhtaarah.

[17] [88] Al-Bukhaariy na Muslim.

[18] [89] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. 

[19] [90] Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[20] [91] Al-Bukhaariy na Muslim.

[21] [92] Muslim, Ibn Khuzaymah na Al-Haakim.

[22] [93] Muslim na Abu Daawuud.

[23] [94] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[24] [95] Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah.

[25] [96] Atw-Twahaawiy, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake na Ibn Bushraan. Ibn Hajar amesema kuwa ni nzuri katika Al-Ahaadiyth Al-'Aaliyaat (Namba, 16).

Share [97]

023-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Alivyokuwa Akisoma (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Mbalimbali. 1 - Swalah Ya Adhuhuri

 

1-   SWALAH YA ADHUHURI

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo Suratul-Faatihah na Surah mbili, hurefusha ya kwanza kuliko ya pili.([1])

 

Mara nyingine alikuwa akiirefusha urefu ambao ilikuwa inaweza kufika kuqimiwa kwa Swalah ya Adhuhuri, na aliweza mtu kwenda Al-Baqiy' kukidhi haja yake, [kisha aende nyumbani kwake], kutawadha, kisha aje hali ya kuwa Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa bado yuko katika Rakaa ya mwanzo, kwa namna alivyokuwa akiirefusha([2]).

 

(Pia) walikuwa wakidhania kwamba alikuwa akifanya hivyo ili watu waweze kuidiriki Rakaa ya mwanzo.([3])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika kila Rakaa ya hizo Rakaa mbili, kadiri ya Aayah thelathini, kiasi cha kusoma As-Sajdah [32-30] na ikiwemo al-Faatihah.([4]) (na kufuatia As-Sajdah [32-30])

 

Mara nyingine alikuwa akisoma:

((وَالسَّمَاء وَالطَّارِقِ))

 

((Naapa kwa mbingu na kinachokuja usiku!)) [At-Twaariq: 86-17], na

 

 

((وَالسَّمَاء ذَاتِ الْبُرُوجِ))

 

((Naapa kwa mbingu yenye Buruji!)) [Al-Buruuj: 85-22], na

 

((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))

 

((Naapa kwa usiku unapo funika!)) [Al-Layl: 92-21], na mfano wa Surah zilizofanana na hizi.([5])

 

Na huenda akasoma

 ((إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ))

 

((Itapochanika mbingu)) [Al-Inshiqaaq: 84-25], na mfano wake.([6])

 

Walikuwa wakiweza kuelewa kwamba alikuwa anasoma katika Adhuhuri na Alasiri kutokana na mtikisiko wa ndevu zake.([7])

 

 

 

[1]   Al-Bukhaariy na Muslim.

[2]   Muslim na Al-Bukhaariy katika Juz-u Al-Qiraat (Makala ya Tilaawah).

[3]   Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh na Ibn Khuzaymah (1/165/1).

[4]   Ahmad na Muslim.

[5]  Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na Ibn Khuzaymah (1/67/2). Wawili wa mwisho wamesema kuwa ni Swahiyh.

[6]   Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1/67/2).

[7]   Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

Share [98]

024-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Cha Aayaat Baada Ya Al-Faatihah Katika Rakaa Mbili Za Mwisho

KISOMO CHAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) CHA AAYAAT BAADA YA AL-FAATIHAH KATIKA RAKAA MBILI ZA MWISHO

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akizifanya Rakaa mbili za mwisho fupi zaidi kulinganisha na Rakaa mbili za mwanzo kiasi cha nusu yake, kiasi cha Aayah kumi na tano,([1]) na pengine alifupisha katika Rakaa mbili za mwisho kwa kusoma al-Faatihah pekee.([2])

 

Alikuwa mara nyingine akiwasikilizisha Aayah.([3]) Na walikuwa wakisikia kutoka kwake mvumo wa kisomo chake:

 

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

 

((Litakase jina la Mola Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87-19],

na

 

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

 

((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [Al-Ghaashiyah 88-26].([4])

 

 

Mara nyingine husoma:

 

((وَالسَّمَاء ذَاتِ الْبُرُوجِ))

 

((Naapa kwa mbingu yenye Buruji!)) [Al-Buruuj 85-22], na

 

((وَالسَّمَاء وَالطَّارِقِ))

 

((Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku!)) [Atw-Twaariq 86-17], na Sura nyinginezo mfano wa hizi mbili.([5])

 

Mara nyingine alikuwa akisoma:

 

((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))

 

((Naapa kwa usiku unapofunika!)) [Al-Layl 92-21], Na mfano wake.([6])

 

 

[1] Ahmad na Muslim. Katika Hadiyth hii, kuna dalili kwamba kusoma Surah zaidi ya Suratul-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho ni Sunnah, na Maswahaba wengi walifanya hivyo. Miongoni mwao ni Abu Bakr (رضي الله عنه). (Pia) na ni rai ya Imaam Ash-Shaafi'iy, na ni sawa tu kama itakuwa katika Adhuhuri au katika Swalah nyinginezo. Maulamaa waliofuatia, Abul-Hasanaat Al-Laknawiy katika ((At-Ta’aliyq Al-Mummajad ‘Alaa Muwattwa Muhammad)) (Uk. 102) (akasema:"Na baadhi ya wafuasi wetu wamekuja na rai ya ajabu, kwani waliwajibisha Sajdatus-Sahw (Sajda ya kusahau) kwa kusoma Surah katika Rakaa mbili za mwisho. Na kwa hakika wamejibiwa na wenye kutoa maelezo/ sharh ya Al-Maniyyah; Ibraahiym Al-Halabiy na Ibn Amiyr Haaj na wengineo, wamejibiwa majawabu mazuri mno. Bila shaka wale waliosema hivyo haikuwafikia Hadiyth iliyotaja hayo, na lau kama imewafikia wasingelisema hivyo"

[2] Al-Bukhaariy Na Muslim.

[3] Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1.67/2) na Adh-Dhiyaa Al-Maqdsiy katika Al-Mukhtaarah ikiwa na isnaad Swahiyh.

[4] Al-Bukhaariy katika Makala ya Tilaawah, na At-Tirmidhiy ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh.

[5]   Muslim na At-Twayaalisiy.

[6]   Al-Bukhaariy na Muslim.

Share [99]

025-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Za Alasiri, Maghrib Na 'Ishaa

 

1-   SWALAH YA ALASIRI

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo al-Faatihah na Surah mbili, hurefusha Rakaa ya kwanza kuliko ya pili([1]) na walikuwa wakidhani kuwa alikuwa akifanya hivyo ili watu waweze kuidiriki Rakaa ya mwanzo.([2])

 

Alikuwa akisoma kadiri ya Aayah kumi na tano katika kila Rakaa mbili za mwanzo, kiasi cha nusu ya kisomo alichokuwa akisoma katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalah ya Adhuhuri, na alikuwa akizifupisha Rakaa mbili za mwisho kiasi cha nusu ya urefu wa Rakaa mbili za mwanzo.([3])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma al-Faatihah katika Rakaa mbili za mwisho.([4])  Alikuwa akiwasikilizisha Aayaah (au zaidi) mara nyingine([5]), na alikuwa akisoma Surah tulizozitaja hapo nyuma katika Swalah ya Adhuhuri.

 

 

 

2-   SWALAH YA MAGHRIB

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma katika Swalah hii – baadhi ya nyakati -Surah fupi za Mufasswal([6]), kiasi cha “wao wanapomaliza kuswali naye, huondoka mmoja wao, na hakika mtu (angeweza kuutupa na) kuona sehemu iliyoangukia mshale wake.”([7]).

 

Na (Mara moja), alipokuwa safarini alisoma:

 

((وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ))

 

((Naapa kwa tini na zaytuni!)) [At-Tiyn 95:8) katika Rakaa ya pili.([8])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) mara nyingine akisoma Surah ndefu za Mufasswal na za wasitani, hivyo alikuwa akisoma:

 

الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ

 

((Waliokufuru na wakazuilia njia ya Allaah)). [Muhammad 47: 1].([9])

 

Mara nyingine akisoma Suratu-Twuur [52: 49]([10])

 

Na mara nyingine akisoma Suratul-Mursalaat [77: 50] ambayo aliisoma katika Swalah (yake) ya mwisho aliyoiswali (صلى الله عليه وآله وسلم).([11])

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma moja kati ya Surah mbili ndefu (atw-Twuwlayayn)([12]);  [Al-A'araaf 7: 206] (katika Rakaa mbili).([13])  Na mara nyingine akisoma Al-anfaal [8: 75] katika Rakaa mbili.([14])

 

 

 

KISOMO KATIKA SUNNAH (BAADA YA SWALAH) YA MAGHARIBI

 

Ama katika Sunnah ya baada (al-ba’diyyah) ya Maghrib, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma:

 

((قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ))

((Sema: Enyi makafiri!)). [Al-Kaafiruun 109: 6], na

 

 

((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))

((Sema: Yeye Allaah ni wa Pekee)). [Al-Ikhlaasw 112: 4].([15])

 

 

 

3-   SWALAH YA 'ISHAA

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah za kati na kati za Mufasswal katika Rakaa mbili za mwanzo([16]), hivyo alikuwa mara nyingine akisoma:

 

 

((وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا))

((Naapa kwa jua na mwangaza wake!)) [Ash-Shams 91: 15] na Surah nyingine zilizofanana na hiyo([17]).

 

Na mara nyingine alikuwa akisoma:

 

((إِذَا السَّمَاء انشَقَّتْ))

 

((Itapochanika mbingu)) [Al-Inshiqaaq 84: 25), na alikuwa akileta Sajdah humo([18]).

 

Pia mara moja alipokuwa safarini alisoma:

 

((وَالتِّينِ وَالزَّيْتُونِ))

((Naapa kwa tini na zaytuni!)) [At-Tiyn 95:8) (katika Rakaa ya mwanzo).([19])

 

 

Alikataza (صلى الله عليه وآله وسلم) kurefusha kisomo katika 'Ishaa, katazo hili lilikuja wakati Mu'aadh bin Jabal alipowaswalisha watu wake Swalah ya 'Ishaa akaifanya ndefu, akajiondoa mtu mmoja katika Answaar na kuswali pekee. Mu'aadh akaelezwa habari ya mtu huyo akasema: "Hakika yeye ni mnafiki". Mtu yule ilipomfikilia taarifa, alikwenda kwa Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumweleza vile alivyosema Mu'aadh. Basi hapo Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم)akamwambia Mu'aadh: ((Je, unataka kuwa mfitini ewe Mu'aadh? Utaposwalisha watu basi soma:

 

 

((وَالشَّمْسِ وَضُحَاهَا))

((Naapa kwa jua na mwangaza wake!)) [Ash-Shams 91: 15], na

 

 

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

 

((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], na

 

 

((وَاللَّيْلِ إِذَا يَغْشَى))

 

((Naapa kwa usiku unapofunika!)) [Al-Layl 92: 21] [Bila ya shaka huswali nyuma yako watu wazima, wagonjwa na wenye haja zao].[20])

 

 

[1]   Al-Bukhaariy na Muslim.

[2]   Abu Daawuud ikiwa na isnaad Swahiyh na Ibn Khuzaymah.

[3]   Ahmad na Muslim.

[4]   Al-Bukhaariy na Muslim.

[5]   Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[6]   Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[7]   An-Nasaaiy na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[8]   Atw-Twayaalisy na Ahmad katika isnaad Swahiyh.

[9]  Ibn Khuzaymah (1/166/2), Atw-Twabaraaniy na Al-Maqdisiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[10] Al-Bukhaariy na Muslim.

[11] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[12] At-twuulayayn ni Al-A'raaf [7] kwa makubaliano, na Al-an'aam [6] kutokana na kauli iliyo sahihi zaidi kama ilivyotajwa katika Fat-h al-Baariy.

[13] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud, Ibn Khuzaymah (1/68/1), Ahmad, Siraaj na Mukhlisw.

[14] Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr ikiwa na isnaad Swahiyh.

[15] Ahmad, Al-Maqdisiy, An-Nasaaiy, Ibn Naswr na Atw-Twabaraaniy.

[16] An-Nasaaiy na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[17] Ahmad na At-Tirmidhy ambaye amekiri ni nzuri.

[18]   Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy.

[19]   Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[20]   Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Imetolewa pia katika Al-Irwaa (295).

 

Share [100]

026-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Usiku - Sifa Ya Swalah Ya Mtume

 

1.    SWALAH YA USIKU  

 

Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)mara nyingine akifupisha ([1]) kisomo katika hiyo Swalah ya usiku, na mara nyingine hukirefusha, na wakati mwengine hukirefusha sana, mpaka ikampelekea 'Abdullaah bin Mas'uud kusema: "Usiku mmoja niliswali pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi aliendelea kusimama (kwa) muda mrefu sana mpaka nikawaza jambo baya. Pakaulizwa: "Uliwaza nini"? Akajibu: "Nilifikiria kukaa chini na kumuacha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)!([2]).    

 

Hudhayfah bin Al-Yamaan pia alisema:

"Usiku mmoja niliswali na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi alianza kusoma Suratul Al-Baqarah (2: 286). Nikasema (moyoni): "Atarukuu baada ya Aayah mia". Lakini aliendelea, nikawaza kuwa huenda ataimaliza Surah katika [rakaa mbili]. Lakini aliendelea na nikasema: "Atarukuu atakapoimaliza." Kisha akaanza kusoma Suratun-Nisaa (4: 176), akaisoma yote. Kisha akaanza kusoma Suratul-'Imraan (3: 200)([3]), akaisoma yote. Alikuwa akisoma polepole, anapopita kwenye Aayah zenye kumtukuza Allaah humtukuza, na anapopita kwenye Aayah zenye maombezi huomba, na anapopita kwenye Aayah za kujikinga hujikinga. Kisha akarukuu…" (Hadi mwisho wa) Hadiyth.([4])

 

Pia usiku mmoja alipokuwa akiumwa, alisoma Surah saba ndefu.([5])

 

Pia alikuwa akisoma moja ya Surah hizi saba ndefu katika kila rakaa.([6])

 

Haikupata kutokea kuwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma Qur-aan nzima katika usiku mmoja [abadani]([7]), na wala hakumkubalia hivyo 'Abdullaah bin 'Amru (رضي الله عنه) wakati alipomwambia: ((Soma Qur-aan nzima kila mwezi)). Akasema: Nikamwambia: "Ninao uwezo wa kufanya zaidi ya hivyo". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Isome katika masiku ishirini)). Akasema: Nikamwambia: "Ninao uwezo wa kusoma zaidi". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Basi isome katika siku saba na wala usipunguze zaidi ya hapo)).([8])

 

Kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimruhusu kuisoma Qur-aan nzima katika siku tano.([9])

 

Kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alimruhusu kuisoma Qur-aan nzima katika siku tatu.([10])

 

Kisha Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akamkataza kuisoma Qur-aan nzima chini ya hivyo([11]) na akatoa sababu kwayo kwa kumwambia: ((Yeyote atakayesoma Qur-aan nzima chini ya siku tatu, hatoweza kuifahamu))([12]). Na katika riwaaya nyingine: ((Hawezi kufahamu mwenye kuisoma Qur-aan nzima chini ya siku tatu)).([13])

 

Kisha alimwambia: ((Kwa hakika kila mwenye kuabudu huwa ana muda wa shirrah([14]),  na kila shauku ina kipindi cha kupunguka, aidha ielekee kwenye Sunnah au kwenye bid'ah. Hivyo basi mwenye kuwa upungufu wake umeelekea kwenye Sunnah, huyo basi amepata uongofu, na mwenye kuwa upungufu wake umeelekea kwenye kinyume cha hivyo, basi ameangamia))([15]).

 

Kwa sababu hii, akawa  (صلى الله عليه وآله وسلم) hasomi Qur-aan nzima chini ya siku tatu.([16])

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayeswali katika usiku na akasoma Aayah mia mbili, basi huandikwa miongoni mwa watiifu wenye kumtakasia Allaah )).([17]) 

 

Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surat Bani Israaiyl (17: 111) na Surat Az-Zumar (49: 75) katika kila usiku([18]). Na alikuwa akisema: ((Atakayeswali katika usiku na akasoma Aayah mia, basi hatoandikwa miongoni mwa walioghafilika))([19]). Mara nyingine alikuwa akisoma katika kila Rakaa kiasi cha Aayah khamsiyn au zaidi([20]), na mara nyingine akisoma kiasi cha Suratul Al-Muzammil (73: 20).([21])

 

Na wala hakuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akiswali usiku mzima([22]), isipokuwa kwa nadra, kwani mara moja ‘Abdullaah bin Khabbaab bin al-Arat - ambaye alishuhudia vita vya Badr pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) – alimpeleleza Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) usiku mzima, na katika riwaaya nyingine: katika usiku alioupitisha kwa kuswali usiku mzima hadi ikawa pamoja na Afajiri. Alipoimaliza Swalah yake, Khabbaab alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Kwa heshima zote za baba yangu, nakupa wewe na heshima zote za mama yangu!

 

"Usiku wa leo umeswali Swalah sikuwahi kukuona kuswali mfano wake".

 

Akasema   (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Ndio, ilikuwa Swalah ya shauku na khofu, (na mimi kwa hakika) nilimuomba Mola Wangu عزوجل  mambo matatu, Amenipa mawili, na Amenikatalia moja. Nilimuomba Mola wangu Asituangamize kwa kile Alichowaangamizia Ummah za kabla yetu [na katika riwaaya nyingine]: ((Asiuangamize Ummah wangu kwa njaa) Akanipa hilo, Nikamuomba Mola wangu عزوجل Asitusalitishe na adui asiye kuwa miongoni mwetu, Akanipa hilo, na nilimuomba Mola wangu Asituvurunge vurunge mpaka tukawa makundi yasiyopatana kwa mfarakano, (lakini) Amenikatalia hili)).([23]) 

 

Na usiku mmoja alisimama (صلى الله عليه وآله وسلم) (katika Swalah) akawa akikariri Aayah moja hadi alfajiri. Aayah yenyewe ni:

 

(( إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ))

 

((Ukiwaadhibu, basi hao ni waja Wako. Na Ukiwasamehe, basi Wewe Ndiye Mwenye nguvu na Mwenye hikmah)). [Al-Maaidah 5: 121]

 

[kwayo karukuu nayo, na kwayo kasujuduia na kwayo kaomba], [Kulipopambazuka, Abu Dharr (رضي الله عنه) alimwambia: "Ewe Mjume wa Allaah! Hukusita kuisoma Aayah hii hadi kumepambazuka, umerukuu nayo, umesujudu nayo] [na umeomba nayo] [hali ya kuwa Allaah Amekufundisha Qur-aan nzima], [lau (ingelikuwa) mmoja wetu amefanya hivi, tungelimkemea]. [Akasema: ((Hakika nimemuomba Mola wangu عزوجل kuwashufaia Ummah wangu, Akanipa hilo, na Uombezi huo utapatikana Allaah Akipenda kwa yeyote asiyemshirikisha Allaah na kitu cho chote kile)).([24])

 

Mtu alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Mimi ninaye jirani anayesimama kuswali usiku na hasomi isipokuwa:

 

((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))

((Sema: Yeye Allaah ni wa Pekee)) [Al-Ikhlaasw 112: 4],

(anaikariri) [haongezei nyingine] kama kwamba anaiona kuwa hadhi yake ni ndogo". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake, hakika hiyo ni sawa na thuluthi ya Qur-aan)).([25])

 

 

[1]  An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[2]  Al-Bukhaariy na Muslim.

[3] Hivi ndivyo ilivyopokelewa kutangulizwa Suratun-An-Nisaa (4) kabla ya Al-'Imraan (3), na hiyo ni dalili kwamba inaruhusiwa kusoma kwa kuacha kufuatilia mpangilio wa Msahafu wa 'Uthmaan katika kusoma. Umekwishapita mfano kama huu.

[4]   Muslim na An-Nasaaiy.

[5]  Abu Ya'laa na Al-Haakim ambae amesema kuwa ni Swahihy, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye. Ibn Al-Athiyr amesema: “….Surah saba ndefu ni: Al-Baqarah (2), Al-'Imraan (3), An-Nisaa (4), Al-Maaidah (5), Al-An'aam (6), Al-A'raaf (7) na At-Tawbah (9)".

[6]   Abu Daawuud na An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh.

[7]   Muslim na Abu Daawuud.

[8]  Al-Bukhaariy na Muslim.

[9] An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh.

[10] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[11] Ad-Daarimiy na Sa’iyd ibn Masnuur katika Sunan yake kwa isnaad Swahiyh.

[12] Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

[13] Ad-Daarimiy na At-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh.

[14] "Shirrah" ni msisimko, hamu, shauku, nguvu. Na Shirrah ya vijana mwanzo wake ni bidii, nguvu, hamasa na raghba. Imaam Atw-Twahaawiy amesema: "Ni bidii na hamasa katika vitendo ambavyo wanavitaka Waislamu kutokana na nafsi zao wenyewe katika ‘amali zao ambazo wanajikurubisha kwazo kwa Mola wao عزوجل. Na kwa hakika Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) anapenda zaidi kutoka kwao hivyo, na sio vile vitendo walivyovianza kutokana na shauku na hamasa ambayo hawana budi isipokuwa watakuwa na upungufu na kuachana navyo na kushikamana na kinyume chake. Kwa hiyo, aliwaamrisha waendelee kushikamana na vitendo vyema ambavyo wataweza kuviendeleza na kudumu navyo hadi watakapokutana na Mola waoعزوجل . Katika kulifafanua hili, imesimuliwa kutoka kwake  (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba amesema: ((Vitendo vipendezavyo kwa Allaah, ni vile vyenye kudumishwa japo kuwa ni vichache)).

Nasema: "Hadiyth hii ambayo ameitoa kwa njia ya kuonyesha kuwa  msimulizi wake hajulikani (Majhuul) kama linavyomaanisha neno "imesimuliwa", ni Swahiyh na ni waliyowafikiana kwayo Al-Bukhaariy na Muslim kutokana na Hadiyth ya Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها).

[15]  Ahmad na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake.

[16] Ibn Sa'ad (1/376) na Abu-Ash-Shaykh katika Akhlaaq An-Nabiyy (صلى الله عليه وآله وسلم) (281).

[17]   Ad-Daarimy na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[18] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[19] Ahmad na Ibn Naswr kwa isnaad Swahiyh.

[20] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[21] Ahmad na Abu Daawuud kwa isnaad Swahiyh.

[22] Muslim na Abu Daawuud. Nimesema: "Kwa Hadiyth hii na nyingine, inaonyesha kuwa ni makruuh kukesha usiku mzima kila siku au aghlabu, kwani ni kinyume na mwenendo wake (صلى الله عليه وآله وسلم), na lau ingelikuwa kukesha usiku mzima ni bora, basi hilo lisingelimpita  Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Na uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Na wala usidanganyike na yaliyosimuliwa kuhusu Abu Haniyfah kwamba yeye alikuwa akiswali Swalah ya al-Fajr kwa wudhuu wa 'Ishaa kwa miaka arubaini!! [Maelezo ya Mfasiri: Taz. Tabliygh An-Nisaab: Fadhila za Swalaah kilichoandikwa na Maulana Zakariyyah Kandhalvi kwa mifano ya dai kama hili]. Kwani usimulizi huu kutoka kwake, hauna msingi wo wote ule, bali 'Allaamah Al-Fairuuz ‘Abaadi amesema katika Ar-Radd 'alaa al-Mu'taridh (44/1): "Usimulizi huu ni miongoni mwa uongo uliowazi ambao haupaswi kuambatanishwa na Imaam, kwani hakuna fadhila yenye kutajwa katika kufanya hivyo. Na ilikuwa ni vyema kwa mfano wa Imaam kama huyu, kufanya yaliyo bora zaidi, na hakuna shaka yoyote ile kwamba kutawadha upya (Tajdiydul Wudhuu) kwa kila Swalah, ndilo linalopendeza zaidi, ndio ukamilifu na ndio bora zaidi. Hii kama itathibiti kuwa ilikuwa kweli kwamba yeye alikuwa akikesha usiku kwa miaka arubaini mfululizo! Jambo hili linaelekea kuwa kama jambo lisilowezekana, nalo ni katika simulizi za kale zilizozushwa na washabiki wajinga wavukao mipaka waliosema hivyo kuhusu Abu Haniyfah na wengineo, na yote ni uongo mtupu".

[23] An-Nasaaiy, Ahmad na Atw-Twabaraaniy (1/187/2). At-Tirmidhiy amesema ni Swahiyh.

[24] An-Nasaaiy, Ibn Khuzaymah (1/70/1), Ahmad, Ibn Naswr na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[25] Ahmad na Al-Bukhaariy.

Share [101]

027-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Witr - Sifa Ya Swalah Ya Mtume

 

7-   SWALAH YA WITR

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma katika Rakaa ya mwanzo:

 

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19],

na katika Rakaa ya pili:

 

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ

((Sema: Enyi makafiri)) [Al-Kaafiruun 109: 6],

na katika Rakaa ya tatu.([1])

 

((قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ))

((Sema: Yeye Allaah ni wa Pekee)) [Al-Ikhlaasw 112: 4].

 

Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiongeza katika Rakaa ya mwisho kwa kusoma:

 

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ

 

((Sema: Najikinga kwa Mola wa mapambazuko)) [Al-Falaq 113: 5],

na

 

قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ

((Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wana Aadam)) [An-Naas 114: 6] ([2]).

 

Na mara nyingine alisoma katika Rakaa ya tatu Aayah mia kutoka katika Suratun-Nisaa [4: 176] ([3]).

 

Ama zile Rakaa mbili baada ya Witr([4]), alikuwa kaisoma ndani yake:

 

إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا

((Itakapotetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake)) [Az-Zilzalah 99: 8], na

 

 

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ

((Sema: Enyi makafiri)) [Al-Kaafiruun 109: 6]([5])

 

 

 

 

[1] An-Nasaaiy na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh.

[2] At-Tirmidhiy, Abul-'Abbaas Al-Aswam katika Hadiyth yake (Mjalada 2 Namba 117) na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[3] An-Nasaaiy na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

[4] Zimethibiti Rakaa mbili hizi katika Swahiyh Muslim na wengineo kama ni desturi ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Na kuthibiti kwa Rakaa mbili hizi, kunapingana na kauli yake (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Ifanyeni Swalah yenu ya mwisho usiku kuwa ni Witr)). Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim. Maulamaa wamekhitilafiana katika kuoanisha baina ya Hadiythi hizi mbili, kwa maono, fikra na mitazamo tofauti. Na hakuna hata mtazamo mmoja katika mitazamo yote hiyo ulionikinaisha. Na ni busara kuziacha Rakaa mbili hizi kwa mujibu wa amri ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Anajua zaidi.

Kisha nikakutana na Hadiyth Swahiyh ambayo ndani yake iko amri ya kuswali Rakaa mbili baada ya Witr. Kwa hiyo amri ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) imewafikiana na kitendo chake, na ikathibiti amri ya kuswali Rakaa mbili kwa watu wote. Na amri ya kwanza inaweza kuwa ni mapendekezo, hivyo basi hakuna kinachozikanusha Rakaa mbili. Hadiyth hiyo nimeiweka katika Silsilatul-Ahaadiyth Aswahiyhah (1193). Taz. Kiambatisho 7.

[5] Ahmad, Ibn Naswr na Atw-Twahaawiy (1/202), na Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan ikiwa na isnaad Hasan Swahiyh.

Share [102]

028-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Ijumaa - Sifa Ya Swalah Ya Mtume

 

8-   SWALAH YA IJUMAA

 

 

Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma mara nyingine katika Rakaa ya mwanzo Suratul-Jumu'aa [62: 11]:

 

 يُسَبِّحُ لِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴿١﴾

((Vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi vinamtukuza Allaah, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikmah)),

na katika Rakaa ya pili:

 

إِذَا جَاءكَ الْمُنَافِقُونَ

((Wanapokujia wanaafiki)) [63: 11]([1]),

 

na mara nyingine - badala yake([2])- alikuwa akisoma:

 

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26],

na mara nyingine akisoma:

 

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

((Litakase Jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], katika Rakaa ya mwanzo na:

 

 

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26],

katika Rakaa ya pili([3]).

 

 

[1] Muslim na Abu Daawuud. Imetolewa katika Al-Irwaa (345).

[2] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[3] Muslim na Abu Daawuud.

Share [103]

029-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Za 'Iyd Mbili - Sifa Ya Swalah Ya Mtume

 

9-   SWALAH ZA 'IYD MBILI

 

"Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم)akisoma (mara nyingine) katika Rakaa ya kwanza

 

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى

 

((Litakase jina la Mola wako Aliye juu kabisa)) [Al-A'laa 87: 19], na katika Rakaa ya pili:

 

هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ

 

((Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?)) [88: 26] [1].  Na mara nyingine "alikuwa akisoma katika hizo Rakaa mbili:

 

ق وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ

 

((Qaaf, Naapa kwa Qur-aan Tukufu))[Qaaf 50: 45], na

 

اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ

 

((Saa imekaribia na mwezi umepasuka)) [Al-Qamar 54: 55][2].

 

 

 


[1]  Muslim na Abu Daawuud.

[2]  Muslim na Abu Daawuud.

Share [104]

030-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Swalah Ya Janaazah

 

10- SWALAH YA JANAAZAH

 

"Sunnah ni kusoma Suratul Faatihah[1] [na sura nyingineyo][2]. Pia "Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa  kimya kwa muda baada ya Takbiyr ya kwanza"[3]

 

 

KUSOMA KISOMO VILIVYO NA KUITENGENEZA SAUTI UNAPOSOMA

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma - kama Alivyoamrishwa na Allaah - Qur-aan vilivyo – kama inavyotakiwa kusomwa, mtu anatakiwa achunge hukumu za kuisoma-, bila ya kwenda mbio wala kuharakiza, bali kisomo cha "Uchambuzi/ufafanuzi chenye kupelekea kubaini herufi baada ya herufi"[4] (sana) hadi "alikuwa akisoma Surah mpaka inakuwa ndefu mno kulinganisha na Surah iliyo refu na hiyo anayoisoma (kwa kadiri inavyowezekana).[5]

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Itasemwa kwa mwenye kusoma Qur-aan (siku ya Qiyaamah): Soma na upande; soma (pole pole kwa mahadhi) kama ulivyokuwa ukisoma duniani; makaazi yako kwenye Aayah ya mwisho usomayo))[6]

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) "akirefusha kisomo chake (kwenye herufi za kurefushwa), alikuwa akirefusha Bismi Llaahi, na akirefusha Ar-Rahmaan na akirefusha Ar-Rahiym"[7]  na katika "nadhiyd" [Qaaf 50: 10][8] na mfano wa (kama) hizo.

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisimama mwisho wa kila Aayah kama ilivyoelezwa kabla.

 

Mara nyingine "alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma kwa sauti ya kuvutia ya kutetema[9] kama alviyofanya siku ya kufunguliwa kwa Makkah hali ya kuwa yuko juu ya ngamia wake, anasoma Suratul-Fat-h [48: 29] [kwa suatinyororo][10] na 'Abdullaah bin Mughaffal amesimulia hii sauti ya kuvutia : aaa"[11]

 

Alikuwa akiamrisha kuipamba sauti katika kusoma Qur-aan, alikuwa akisema: ((Ipambeni Qur-aan kwa sauti zenu (kwani sauti nzuri huzidisha kuipamba Qur-aan))[12]

 

Na alikuwa akisema: ((Hakika mwenye sauti bora miongoni mwa watu katika kusoma Qur-aan ni yule ambaye mnapomsikia akiisoma, mtamdhania ni mwenye kumkhofu Allaah))[13]

 

Alikuwa pia akiamrisha kusoma Qur-aan kwa sauti ya kupendeza, alikuwa akisema: ((Jifunzeni kitabu cha Allaah, dumisheni kuisoma, ithibitisheni (kuhifadhi), na isomeni kwa (sauti ya) kughani, kwani Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, inakimbia haraka kuliko ngamia anavyochopoka katika kamba))[14]

 

 

Alikuwa pia akisema: ((Sio miongoni mwetu mwenye kuisoma Qur-aan bila ya kughani [kupendezesha sauti]))[15]

 

Na akisema:

((Allaah Hakuwahi kusikiliza kitu chochote zaidi ya jinsi ya kusikiliza [katika riwaaya nyingine: ((Kama Anavyomsikiliza))] Mtume (kwa shauku) ((kwa sauti ya kupendeza))], na [katika riwaaya nyingine: anavyosoma Qur-aan kwa sauti nzuri[16]  ((ananyanyua sauti kwako))[17]

 

Alimuambia Abu Muusa Al-Ash'ariyy (رضي الله عنه) ((Lau ungeliniona nilipokuwa nasikiliza kisomo chako usiku wa jana, kwa Hakika umepewa mzumari[18] katika mizumari ya aila ya Daawuud!)) Hivyo Abu Muusa akasema: "Lau ningelijua kuwa uko, ningelizidi kuitengeneza na kuipendesha sauti yangu kwa ajili yako"[19]

 

 

 

[1] Hii ni kauli ya Imaam Ash-Shaafi'y, Ahmad na Is-haaq, na pia ni rai ya baadhi ya watafiti wa Mahanafi waliokuja baadaye. Ama kuhusu kusoma Surah baada yake, huu ni mtazamo wa baadhi ya Ma-Shaafi'y na ni mtazamo Swahiyh.

[2] Al-Bukhaariy, Abu Daawuud, An-Nassaiy na Ibn Al-Jaaruud.  Na wala hii ziada sio ya pekee (haina mwenzake) (kitu kimoja hakina mwenzake hapa sio ajabu) kama At-Tuwayjiriy anavyodai.

[3] An-Nasaaiy na At-Twahaawiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[4] Ibn Al-Mubaarak katika Az-Zuhd (162/1 kutoka Al-Kawaakib 575), Abu Daawuud na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

[5] Muslim na Maalik.

[6] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambaye amesema Swahiyh.

[7] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[8] Al-Bukhaariy katika Af'aal al 'Ibaad kwa isnaad Swahiyh.

[9] Inatokana na neon Tarjiy', Ibn Hajar ameeleza: kuwa ni sauti ya kutetema na asli yake ni at tardiyd, watarjiy’ sauti: ni kuikariri kutoka kwenye halq. Al-Manaawiy kasema, "Inakuja aghlabu kwa kuwa na hisia ya shangwe na furaha ambayo alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)siku  ya Ushindi wa Makkah".

[10] Al-Bukhaariy na Muslim.

[11] Al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Hajar amesema katika maelezo kuhusu "aaa (آآآ) "hii ni hamzah ikiwa na fat-haa, ikifuatia na alif ya kimya, ikifuatia na hamzah nyingine". Shaykh 'Aliy Al-Qaariy amenukuu kama hiyo kutokana na wengine na akasema: "Ni dhahiri kuwa hizi ni Alif tatu zenye kuvutwa (ndefu)"

[12] Al-Bukhaariy ta'aliyq (kiambatisho), Abu Daawauud, Ad-Daarimiy, Al-Haakim na Tamaam Ar-Raazi kwa isnaad mbili Swahiyh.

[13] Hadiyth ni Swahiyh, imesimuliwa na Ibn Al-Mubaarak katika Az-Zuhd (162/1 kutoka Al-Kawaakib 575), Ad-Daarimiy, Ibn Naswr, At-Twabaraaniy, Abu Nu'aym katika Akhbaar Aswbahaan na Adh-Dwhiyaa katika Al-Mukhtaarah.

[14] Ad-Daarimiy na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

TANBIHI: Hadiyth ya kwanza imegeuzwa na msimulizi mmoja, hivyo ameisimulia: ((Pambeni sauti zenu kwa (kwenye) Qur-aan)). Haya ni makosa katika usimulizi na ufahamu, na yeyote mwenye kusema ni Swahiyh basi huyo amezama zaidi katika makosa, kwani inapingana na Simulizi Swahiyh zilizofafanuliwa katika mlango huu. Bali ni mfano bora katika Hadiyth Maqluub (iliyogeuzwa) na maelezo zaidi ya hii (tanbihi) yamo katika Silisilatul-Ahaadiyth Ad-Dhwa'iyfah (Namba 5328).

[15] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh na Adh-Dhahaabiy amekubaliana naye.        

[16] Amesema Al-Mundhiriy ‘taghannaa’ inamaanisha kuisoma kwa sauti ya kupendeza; Sufyaan bin 'Uyaynah na wengineo wamechukua rai kwamba ni kufanya istighnaa (yaani Qur-aan kumfanya mtu ajitenge na mapambo ya dunia) lakini hii imekanushwa.

[17] Al-Bukhaariy, Muslim, At-Twahaawiy na Ibn Mandah katika Tawhiyd (81/1)

[18] Maulamaa wamesema kuwa mizumari hapa inamaansiha: sauti nzuri, na asili ya az-zumar ni al-ghinaa: kuimba, na kwamba aila ya Daawuud inakusudiwa Daawuud mwenyewe, na aila fulani hutumika na humaanisha khaswa ya mtu mwenyewe. Daawuud (عليه السلام) alikuwa na sauti nzuri mno. Hii ameitaja An-Nawawy katika maelezo yake ya Swahiyh Muslim.

[19] 'Abdur-Razzaaq katika Al-Amaaliy (2/44/1), Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Naswr na Haakim.

Share [105]

031-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kumsahihisha Imaam Na Kujikinga Na Shaytwaan

 

 

KUMSAHIHISHA IMAAM

 

Ametoa  (صلى الله عليه وآله وسلم)mfano katika kumsahihisha Imaam anapobabaika au anapochanganyikiwa na kisomo chake. Mara moja aliswali, akasoma ndani yake kisomo, akasahau. Alipomaliza alimwambia Ubayy: ((Uliswali na sisi?)). Alijibu: "Ndio". Akasema: ((Hivyo nini kilichokuzuia [kunisahihisha]?))([1]).

 

 

 

KUJIKINGA NA SHAYTWAAN NA KUTEMA MATE KIDOGO WAKATI WA SWALAH ILI KUONDOSHA WASIWASI

 

'Uthmaan bin Abil-Aasw (رضي الله عنه) alimwambia: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Shaytwaan ameingia baina yangu na baina ya Swalah yangu na kisomo changu, ananibabaisha katika kisomo changu!" Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Huyo ni Shaytwaan anayeitwa Khinzab, hivyo utakapomuhisi jikinge kwa Allaah naye, na tema mate kidogo([2]) upande wa kushoto kwako mara tatu)). Akasema: "Nikafanya hivyo, na Allaah Akamuondoshelea mbali nami".([3]).

 

 





[1] Abu Daawuud, Ibn Hibbaan, Atw-Twabaraaniy, Ibn 'Asaakir (2/296/2) na Adhw-Dhwiyaa katika Al-Mukhtaarah kwa isnaad Swahiyh.

[2] "At-Tafl" ni mpulizo ikiwa na mate kidogo, hivyo ni zaidi ya kupuliza.  (An-Nihaayah).

[3] Muslim na Ahmad. An-Nawawiy (رحمه الله) amesema: "Hadiyth hii ina mapendekezo ya kujikinga na Shaytwaan anaposhawishi, pamoja na kutema mate upande wa kushoto mara tatu".

 

Share [106]

032-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kurukuu, Sifa Na Ulazima Wa Kutulia Katika Rukuu

 

KURUKUU

 

Baada ya kumaliza kisomo chake   (صلى الله عليه وآله وسلم), alikuwa akinyamaza kinyamazo kidogo([1]

), kisha huinua mikono yake(

[2]

) kwa namna zilizotangulia kuelezwa katika 'Takbiyr Ya Kufungulia, akaleta Takbiyr(

[3]

) na akarukuu.(

[4]

).

 

Na pia alimuamrisha mambo mawili hayo aliyeswali vibaya kwa kumwambia: ((Hakika Swalah ya mmoja wenu haitotimia mpaka akamilishe wudhuu vizuri kama Allaah Alivyoamrisha… kisha alete Takbiyr, amsifu na kumtukuza Yeye, na asome kiasi kinachosahilika tu kwake katika Qur-aan miongoni mwa Aliyofunzwa na Allaah (kwa kiasi cha wepesi) na uwezo wake, kisha alete Takbiyr na arukuu [na aweke mikono yake miwili juu ya magoti yake mawili] mpaka viungo vyake vitulie na vipumzike…))(

[5]

).

 

 

 

SIFA YA RUKUU

 

Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)akiweka viganja vyake juu ya magoti yake(

[6]

) na alikuwa akiwaamrisha kufanya hivyo(

[7]

) kama alivyomuamrisha mtu aliyeswali vibaya, kama ilivyoelezwa nyuma.

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiimakinisha mikono yake barabara na magoti yake (kama kwamba akiyashikilia](

[8]

), na alikuwa akivichanua vidole vyake(

[9]

), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kama hivyo, kwa kumwambia: ((Utakaporukuu, weka viganja vya mikono yako juu ya magoti yako, na kisha vichanue vidole vyako, kisha bakia (hivyo) hadi kila kiungo kitue  mahali pake))(

[10]

).

 

Alikuwa akijitawanya (sio kujigandamiza mkao mmoja) na akitenganisha viwiko vya mikono na ubavu wake.(

[11]

)

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaporukuu, hutandaza mgongo wake na kuusawazisha(

[12]

) kiasi kwamba kama ungelimwagiwa maji, basi yangelitua (

[13]

). Na pia alimwambia aliyeswali vibaya: ((Utakaporukuu, weka viwiko vyako juu ya magoti yako, na tawanya mgongo wako na makinisha madhubuti rukuu yako)).(

[14]

)

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) hainamishi kichwa chake wala hakinyanyui (zaidi ya mgongo wake),(

[15]

) bali kilikuwa baina yake.(

[16]

)

 

 

ULAZIMA WA KUTULIA KATIKA RUKUU

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitulia kwenye rukuu yake, na alimuamrisha awe hivyo aliyeswali vibaya, kama ilivyotajwa katika mlango wa rukuu.

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Kamilisheni rukuu na sujudu, kwani naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hakika mimi nakuoneni nyuma yangu(

[17]

) mnaporukuu na mnaposujudu)).(

[18]

)

 

Alimuona mtu anaswali bila ya kukamilisha rukuu yake sawa sawa, akidonoa katika sujuud yake, akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Lau atakufa mtu huyu katika hali yake hii, basi atakuwa amekufa katika Mila isiyokuwa ya Muhammad, [anadonoa katika Swalah yake kama adonoavyo kunguru damu]. Mfano wa yule asiyekamilisha rukuu yake na akadonoa katika sujudu yake, ni kama mfano wa mwenye njaa anayekula tende moja au tende mbili, ambazo hazitomfaidisha kitu chochote))(

[19]

)

 

Abu Hurayrah (رضي الله عنه) alisema: "Rafiki yangu mpenzi  (صلى الله عليه وآله وسلم) amenikataza kudonoa katika Swalah yangu mdonowo wa  jogoo na kugeuka geuka kama ageukavyo mbweha, na kuchuchumaa kama achuchumaavyo tumbili"(

[20]

).

 

Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema: ((Mwizi muovu kabisa miongoni mwa wevi ni yule anayeiba katika Swalah yake)). Wakasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Vipi anaiba katika Swalah yake"? Akasema: ((Hatimizi rukuu yake na sujuud yake))(

[21]

)

 

Mara moja, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiswali, na alitupa jicho kwa mtu ambaye hakusawazisha uti wa mgongo wake katika rukuu na sujuud. Alipomaliza alisema: ((Enyi Waislamu! Hakika hakuna Swalah kwa yule asiyesawazisha uti wake wa mgongo katika rukuu na sujuud)).(

[22]

)

 

Akasema katika Hadiyth nyingine: ((Swalah ya mtu haihesabiwi hadi asawazishe mgongo wake katika rukuu na sujuud)).(

[23]

)

 



[1]

Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[2]

Al-Bukhaariy na Muslim. Huku kuinua mikono ni jambo lililothibiti kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa njia ya mutawaatir (Iliyopokelewa na idadi kubwa -ya watu- yenye kuwa muhali katika kawaida kukubaliana kusema uongo) kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Na vile vile imethibiti kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa njia hiyo hiyo ya mutawaatir, kuinua mikono wakati wa kunyanyuka -wakati wa kuitadili - kutoka kwenye rukuu mpaka alingane sawa hali ya kusimama. Na hivi ndivyo walivyokwenda Maimaamu watatu; Maalik, Ash-Shaafi'iy na Ahmad, na wengineo katika kundi kubwa la Maulamaa wa Hadiyth na Maulamaa wa Fiqh. Na ndio mwenendo alioshikamana nao Imaam Maalik (رحمه الله) hadi kufa kwake kama ilivyoripotiwa na Ibn 'Asaakir (15/78/2). Baadhi ya Mahanafi wamechagua kufanya hivyo. Miongoni mwao ni 'Iyswaam bin Yuusuf Abu 'Aswmah Al-Balkhiy (aliyefariki 210) ambaye ni mwanafunzi wa Imaam Abu Yuusuf (رحمه الله), kama ilivyoelezewa katika utangulizi. 'Abdullaah bin Ahmad ameripoti kutoka kwa baba yake katika Masaail yake (Uk. 60).

"Imesimuliwa kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir kwamba amesema kuhusiana na kunyanyua mikono miwili katika Swalah: "Anapata mema kumi kwa kila anapoinyanyua". Nikasema: Yana ushahidi - maneno ya ‘Uqbah - wenye nguvu kutokana na Hadiythul-Qudisy isemayo: ((…mwenye kutia nia ya kitendo chema na akakitekeleza, Allaah Atamuandikia mema kumi hadi mia saba)). Imesimuliwa na Ash-Shaykhaayn. Taz. Swahiyh At-Targhiyb Namba 16.

[3]

Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[4]

Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.   

[5]

Abu Daawuud na An-Nasaaiy. Al-Haakim amesema ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[6]

Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[7]

Al-Bukhaariy na Muslim.

[8]

Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[9]

Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh. Adh-Dhahabiy na Atw-Twayaalisy wamekubaliana naye. Imetolewa katika Swahiyh Abu Daawuud (809).

[10]

Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika Swahiyh zao.

[11]

At-Tirmidhiy ambaye amesema ni Swahiyh, na Ibn Khuzaymah.

[12]

Al-Bukhaariy na Al-Bayhaqiy kwa isnaad Swahiyh.

[13]

Atw -Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr na Mu'jam As-Swaghiyr, 'Abdullaah bin Ahmad katika Zawaaid Al-Musnad na Ibn Maajah.

[14]

Ahmad na Abu Daawuud kwa isnaad Swahiyh.

[15]

Abu Daawuud na Al-Bukhaariy katika Juzuu Al-Qaari'ah kwa isnaad Swahiyh.  Na maana ya hakinyanyui, ni kuwa hakinyanyui kichwa chake mpaka kikawa juu zaidi ya mgongo wake, bali kinakuwa usawa wa mgongo.

[16]

Muslim na Abu 'Awaanah.

[17]

Nasema na kuona huku ni kuona kwa uhakika wake kimaumbile, na ni miongoni mwa miujiza yake (صلى الله عليه وآله وسلم), nako ni katika Swalah basi. Na hakuna dalili ya kuona kwa ujumla.

[18]

Al-Bukhaariy na Muslim.

[19]

Abu Ya'alaa katika Musnad yake (340/3491/1), Al-Aajuriy katika Al-Arba'iyn, Al-Bayhaqiy, Atw-Twabaraaniy (1/192/1), Adhw-Dhwiyaa katika Al-Muntaqaa (276/1), Ibn 'Asaakir (2/226/2, 414/1, 8/14/1, 76/2) kwa isnaad nzuri. Na Ibn Khuzaymah amesema ni Swahiyh (1/82/1). Ibn Batwtwah katika Al-Ibaanah (5/43/1) anao usimulizi Mursal -Hadiyth mwisho wa isnad yake ameangushwa Swahaba- unaounga mkono sehemu ya mwanzo ya Hadiyth ukitoa ziada katika Al-Ibaanah (5/43/1).

[20]

Atw-Twayaalisy, Ahmad na Ibn Abi Shaybah. Ni Hadiyth Hasan, kama nilivyoielezea katika tanbihi zangu kwenye Al-Ahkaam (1348) ya 'Abdul-Haqq Ishbiyliy (1348). 

[21]

Ibn Abi Shaybah (1/89/2), Atw-Twabaraaniy na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[22]

Ibn Abi Shaybah (1/89/1), Ibn Maajah na Ahmad kwa isnaad Swahiyh.

[23]

Abu 'Awaanah, Abu Daawuud na As-Sahmiy (61). Ad-Daaraqutwniy amesema ni Swahiyh.

Share [107]

033-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Adhkaar Za Rukuu

 

ADHKHAAR ZA RUKUU

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nguzo hii akisoma namna mbali mbali za adhkaar na du'aa. Alikuwa akibadilisha katika kusoma kwake; mara nyingine husema hii na mara nyingine husema hii miongoni mwa zifuatazo:

 

1.

Sub-haana Rabbiyal ‘Adhiym

 

“Ametakasika Mola wangu Aliye Mtukufu, mara tatu”([1]). Na mara nyingine alikuwa akiikariri zaidi ya hivyo.([2]) 

 

Mara moja, katika Swalah ya usiku, aliikariri sana hadi rukuu yake ikawa inakaribiana na kisimamo chake, alichokuwa amesoma ndani yake Surah tatu katika Surah ndefu; Al-Baqarah, An-Nisaa na Al-'Imraan. Ndani yake (Swalah hii) kulijaa du'aa na kuomba Maghfirah, kama ilivvyotajwa katika '(Kisomo Katika) Swalah Ya Usiku (Tahajjud).

 

 

2.

Sub-haana Rabbiyal ‘Adhiym wabihamdihi

 

“Ametakasika Mola wangu Aliye Mtukufu Na Sifa Njema Zote Ni Zake, mara tatu”.([3])

 

 

3.

Subuuhun Qudduusun Rabbul Malaaikati war Ruuhi

 

“Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu([4]), Mola wa Malaika na Jibriyl”.([5])

 

 

4.      

Sub-haanaka Allaahumma wa Biham-dika Allaahumma gh-fir-liy

 

“Kutakasika ni Kwako, Ee Mola wangu, na sifa njema zote ni Zako, Ee Mola Nisamehe". Alikuwa akiileta kwa wingi hii katika rukuu yake na sujuud zake, alikuwa akitekeleza amri ya Qur-aan.”([6])

 

 

5.

Allaahumma laka Raka’tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, [Anta Rabbiy] Khasha’a laka sam’iy, wabaswariy, wamukh-khiy, wa’adhwmiy, [wa ‘idhwaamiy] wa’aswabiy, [wamas-taqallat bihii Qadamiy Lillaahi Rabbil ‘Alamiyn]

 

“Ee Allaah! Kwako Wewe nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na Kwako Wewe nimejisalimisha, (Wewe Mola wangu) umenyenyekea  Kwako usikizi wangu, na uoni wangu, na ubongo wangu, na mfupa wangu, (katika riwaaya mifupa yangu) na hisia zangu, (na ambacho kimesimama juu ya miguu yangu([7]) kwa ajili ya Mola Wa viumbe vyote.”([8])

 

 

6.

Allaahumma laka Raka’tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, wa’alayka tawakkaltu, Anta Rabbiy, Khasha’a laka sam’iy, wabaswariy, wadamiy, walahmiy, wa‘adhamiy, wa’aswabiy, Lillahi Rabbil ‘Alamiyn

 

“Ee Allaah! Kwako nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimejisalimisha, Kwako nimekutegemea, Wewe Mola wangu,  umenyenyekea  Kwako usikizi wangu, na uoni wangu, na damu yangu, na nyama yangu, na mfupa wangu, na ubongo wangu kwa ajili ya Mola Wa viumbe vyote”.([9])

 

 

7.

Subhaana dhil Jabaruuti wal Malakuuti wal Kibriyaau wal ‘Adhamati

 

“Ametakasika Mwenye Utawala, na Ufalme, na Ukubwa, na Utukufu”, Hii alikuwa akiisoma katika Swalah ya usiku.([10])

 

 

[1] Ahmad, Abu Daawuud, Ibn Maajah, Ad-Daaraqutwniy, Atw-Twahaawiy, Al-Bazzaar na Atw-Twabaraany katika Mu'jam Al-Kabiyr, kutokana na Maswahaba saba. Ndani yake kuna jibu kwa wale waliokataa ujio wa kutozidi mara tatu katika kuleta Tasbiiyhaat, kama Ibn Al-Qayyim na wengineo.

[2] Inapatikana hii kutokana na Ahaadityh zilizoweka wazi kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifanya kisimamo chake, na rukuu yake na sujuud zake sawa sawa kwa urefu, kama itakavyotajwa katika mlango ufuatao.

[3] Hadiyth Swahiyh. Imesimuliwa na Abu Daawuud, Ad-Daaraqutwniy, Ahmad, Atw-Twabaraaniy na Al-Bayhaqiy.

[4] Abu Is-haaq amesema: "Subuuh" ina maana ya Aliyetakasika na makosa yoyote, na "Qudduus" ina maana ya Mwenye Baraka au Aliyetwaharika". Ibn Saydah: "Subbuuh Qudduus" ni sifa za Allaah عزوجل kwa sababu Anatukuzwa na Kutakaswa". (Lisaanul-'Arab).

[5] Muslim na Abu 'Awaanah.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim. Na maana ya “yata-awwalul Qur-aan” ni kuwa anatekeleza yale aliyoamrishwa ndani yake katika maneno Yake Allaah:

((فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا)).

((Zitakase sifa za Mola wako, na umwombe msamaha, hakika Yeye Ndiye Anayepokea tawbah)) [An-Naswr 110: 3]

[7] Ina maana niliyoyabeba, kutokana na neno "al-istiqlaal" lenye maana "al-irtifaa’". Ni ujumla (ta’miym) baada ya ukhusuusi (takh-swiys), kwa maana imekuja –niliyoyabeba- baada ya khusuus -kutaja kiungo kimoja kimoja- katika viungo vya mtu).

[8]    Muslim, Abu 'Awaanah, Atw-Twahaawiy na Ad-Daaraqutwniy.

[9] An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh.

  

[10]Abu Daawuud, An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh. 

 

FAIDA

Je, inakubalika kuchanganya baina ya hizi adhkaar (mbili au zaidi) katika rukuu moja au haikubaliki? Maulamaa wametofautiana katika hili. Ibn al Qayyim hakuwa na msimamo kuhusu hili katika Zaad Al-Ma'aad, na An-Nawawiy amechagua uwezekano wa mwanzo katika Al-Adhkaar, akisema: "Na lililo bora ni kuchanganya baina ya hizi adhkaar zote ikiwezekana. Na hivi ndio inavyotakikana iwe katika adhkaar za milango yote. Abu Atw-Twayyib Swiddiyq Hasan Khan katika Nuzuul Al-Abraar (84) hakukubaliana naye kwa kusema: "Alete adhkaar hizi mara hii, na alete adhkaar nyingine mara nyingine, wala sioni dalili ya kuchanganya. Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   hakuwa akizichanganya kwa mpigo mmoja, lakini alikuwa mara akisema hii, na mara nyingine akisema nyingineyo. Na kufuata ni bora kuliko kuzusha". (Rai ya mwisho hii ni rai iliyo sahihi,) na hivi ndio haki Insha Allaah. Lakini imethibitika katika Sunnah kuirefusha nguzo hii na nyingine pia (kurukuu huku), kama itakavyokuja ufafanuzi wake, hadi iwe inakaribia urefu wa kisimamo. Hivyo, mwenye kuswali akipenda kumfuata Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Sunnah hii, basi hatoweza kufanya hivyo, isipokuwa kwa njia ya kuzichanganya tu (adhkaar) ambayo amekwenda/ameifuata An-Nawawiy, na Ibn Naswr ameipokea katika Qiyaamul-Layl (76) kutoka Ibn Jurayj kutokana na 'Atwaa, -haitowezekana- isipokuwa kwa njia ya kukariri iliyotaja katika baadhi ya hizi adhkaar. (moja ambayo inayo maandiko ya kukariri,) na hivi ndivyo karibu na Sunnah Na Allaah Anajua zaidi.

Share [108]

034-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuirefusha Rukuu Na Kukatazwa Kusoma Qur-aan Katika Rukuu

 

KUIREFUSHA RUKUU

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya rukuu yake, kisimamo chake baada ya rukuu, na sujuud yake na kikao baina sajda mbili, karibu sawa kwa urefu.([1])

 

 

 

KUKATAZWA KUSOMA QUR-AAN KATIKA RUKUU

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)  akikataza kusoma Qur-aan katika rukuu na sujuud.([2])

 

Alikuwa akisema: ((Hakika mimi nimekatazwa kusoma Qur-aan hali ya kuwa nimerukuu au nimesujudu. Hivyo basi katika rukuu mtukuzeni Mola (عزوجل), na (ama) katika sujuud, jitahidini kwa du'aa, kwani ni karibu kukubaliwa humo)).([3])

 

 





[1] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Irwaa Al-Ghaliyl (331).      

[2] Muslim na Abu 'Awaanah. Makatazo ni ya ujumla, hivyo inahusisha Swalah za Faradhi na Sunnah. Ziada ya Ibn 'Asaakir (17/299/1): "Ama Swalah za Sunnah, hakuna ubaya", ni (aidha) shaadhah au munkar. Ibn 'Asaakir ameashiria dosari humo, hivyo haijuzu kufanyiwa kazi.

[3] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

Share [109]

035-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kusimama (Kuitadili) Kutoka Katika Rukuu Na Anachokisema Ndani Yake

 

 

KUSIMAMA (KUITADILI) KUTOKA KATIKA RUKUU NA ANACHOKISEMA NDANI YAKE

 

Kisha, alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunyanyua mgongo wake kutoka rukuu huku akisema:

 

 

Sami’a Allaahu liman Hamidah

Allaah Amemsikia mwenye kumsifu([1])

 

 

Alimuamrisha pia aliyeswali vibaya kufanya hivyo alipomwambia: ((Swalah ya mtu haitimii hadi… amesema Takbiyr … kisha akarukuu …. Kisha akasema 'Allaah Amemsikia mwenye kumsifu' hadi asimame kwa kunyooka sawa sawa))([2]).

 

Aliponyanyua kichwa chake, alikuwa akisimama wima na kunyooka sawa sawa hadi kila pingili ya uti imerudi sehemu yake.([3])

 

 

Kisha alikuwa akisema huku akiwa amesimama wima:

 

 

Rabbanaa Walakal-Hamdu

Ee Mola Wetu! Na Zako Sifa njema na shukrani za dhati.([4])

 

 

Aliwaamrisha wanaoswali wote sawasawa wakiweko nyuma ya Imaam au wasiweko nyuma ya Imaam kufanya hivyo, wanapoinuka kutoka rukuu kwa kusema: ((Swalini kama mlivyoniona nikiswali)).([5])

 

Alikuwa akisema pia: ((Imaam amewekwa kwa ajili ya kufuatwa …, anaposema ' Sami’a Allaahu liman Hamidah’ (Allaah Amemsikia mwenye kumsifu), basi semeni: '[Allaahumma] Rabbanaa Walakal-Hamd'. Allaah Atakusikilizeni, kwani hakika Allaah (تبارك وتعالى) Amesema katika ulimi wa Mtume Wake, (صلى الله عليه وآله وسلم), Allaah Anamsikiliza mwenye kumsifu)).([6])

 

Pia ametoa sababu ya kuamrisha hivi katika Hadiyth nyingine kwa kusema: ((... kwani mwenye kuwafikiana kauli yake na kauli ya Malaika, ataghufuriwa madhambi yake yaliyotangulia)).([7])

 

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)  akiinua mikono yake katika huku kusimama([8])  kwa namna zilizotangulia kuelezwa katika 'Takbiyra Ya Kufungulia', na husema hali ya kuwa amesimama - kama ilivyotajwa kabla- :

 

1.      

 

Rabbanaa Walakal-Hamd'

Ewe Mola Wetu! Na Zako sifa njema na shukrani za dhati([9]). Na mara nyingine husema:

 

2.

 

Rabbanaa Lakal-Hamd'

Ewe Mola Wetu! Ni Zako sifa njema na shukrani za dhati([10]). Na mara nyingine huongezea matamshi mawili haya tamshi:

Allaahumma

Ee Allaah!([11])

 

 

3.

 

 

 

Allaahumma Rabbanaa Walakal-Hamd'

Ee Allaah! Mola Wetu! Na Zako sifa njema na shukrani za dhati.

 

 

 

4.

 

 

 

 

 

 

Allaahumma Rabbanaa Lakal-Hamd'

Ee Allaah! Mola Wetu! Ni Zako sifa njema na shukrani za dhati.

 

 

Alikuwa akiamrisha (wengine) kufanya hivi kwa kusema: ((Imaam anaposema 'Sami'a Allaahu Liman Hamidah' semeni: 'Allaahumma, Rabbanaa Lakal-Hamd', kwani mwenye kuwafikiana kauli yake na ya Malaika ataghufuriwa madhambi yake yaliyopita)).([12])

                                                                     

Mara nyingine alikuwa akiongeza:

 

5.

 

 

Mil-as Samaawaati, wamil- al Ardhi, wamil-a maa shi-ita min shayin ba’du

Zimejaa mbingu, na zimejaa ardhi, na zimejaa (sifa Zako) kwa Ulichokitaka baada yake.([13])

 

 

Au:

 

6.

 

 

 

Mil-as Samaawaati, [wamil-a]l Ardhi, wamaa baynahumaa, wamil-a maa shi-ita min shayin ba’du

Zimejaa mbingu na (zimejaa) ardhi na vilivyomo ndani yake sifa Zako, na zimejaa (sifa Zako) kwa Ulichokitaka baada yake.([14])

 

Mara nyingine aliongeza zaidi:

 

7.

 

 

Ahlath – thanaai wal Majdi, laa maani’a limaa a’twayta, wala mu’twiya lima mana’ta, walaa yanfa’u dhal jaddi minkal jaddu

Wewe ni Mstahiki wa sifa na Utukufu, hapana anayeweza kukizuia Ulichokitoa, na wala kutoa Ulichokizuia, na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani kwao Wewe ndio utajiri.([15])

 

Au mara nyingine ziada ilikuwa:

 

8.

 

 

Mil-as Samaawaati, wamil-al Ardhi, wamaa baynahumaa, wamil-a maa shi-ita min shayin ba’du, ahlath-thanaai wal Majdi, ahaqqu maa qaalal ‘abdu, wakullunaa laka ‘abdun, [Allaahumma] laa maani’a lima a’twayta, [wala mu’twiya lima mana’ta], walaa yanfa’u dhal jaddi minkal jaddu

Zimejaa mbingu na zimejaa ardhi na vilivyomo ndani yake sifa Zako, na zimejaa (sifa Zako)  kwa Ulichokitaka baada yake, Wewe ni Mstahiki wa Sifa na Utukufu, ni kweli aliyoyasema mja Wako, na sote ni waja Wako, (Ee Allaah)  hapana anayeweza kukizuia Ulichokitoa, (na wala kutoa Ulichokizuia), na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako Wewe ndio utajiri.([16])

 

Mara nyingine alikuwa akisema katika Swalah ya usiku:

 

9.

 

LiRabbiyl Hamdi, li Rabbiyl Hamdu,

Kwa Mola wangu Sifa zote, Kwa Mola Wangu Sifa zote na shukrani za dhati.

 

Akikariri hadi kisimamo chake kilikuwa kirefu kama rukuu yake ambayo ilikuwa inakaribiana kwa urefu na kisimamo chake cha mwanzo, na alikuwa amesoma ndani yake Suratul-Baqarah.([17])

 

 

10.

 

 

Rabbanaa walakal Hamdu, Hamdan Kathiyran Twayyiban Mubaarakan fiyh [Mubaarakan ‘alayhi, kamaa Yuhibbu Rabbunaa Wayar-dhwaa]

Ee Mola wetu! Ni zako sifa njema sifa nyingi, nzuri, zenye Baraka (Baraka juu yake kama Anavyopenda Mola wetu na Kuridhika)([18])

 

 

Matamshi haya aliyasoma mtu aliyekuwa akiswali nyuma yake   (صلى الله عليه وآله وسلم). Aliyasoma baada ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kunyanyua kichwa chake kutoka kwenye rukuu na alisema: 'Sami'a Allaahu Liman Hamidah'. Alipomaliza Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم) kuswali, alisema: ((Nani aliyesema hivi sasa?)) Yule mtu akasema: "Ilikuwa ni mimi ewe Mjumbe wa Allaah!" Hivyo Mjumbe wa Allaah  (صلى الله عليه وآله وسلم)akasema: ((Nimewaona Malaika zaidi ya thelathini wanakimbilia kuwa wa kwanza kuyaandika)).([19])

 

 





[1] Al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[3] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. "Al-Faqaar" ni uti – "mifupa inayounda uti wa mgongo kutoka mwanzo wa shingo hadi kitokono" kama ilivyo katika Kamusi. Taz. pia Fat-h Al-Baariy (2/308).

[4] Al-Bukhaariy na Ahmad.

[5] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[6] Muslim, Abu 'Awaanah, Ahmad na Abu Daawuud.

 

TANBIHI: Hadiyth hii haithibitishi kwamba Maamuma hawashirikiani na Imaam katika kusema: 'Sami'a Allaahu Liman Hamidah'. Pia haithibitishi kuwa Imaam hashirikiani na Maamuuma wanaosema: 'Rabbanaa Walakal-Hamd', yote kwa kuwa Hadiyth hii haikuja kubainisha yale khaswa ambayo Imaam na Maamuma wanapaswa kuyasema katika nguzo hii, bali imekuja kueleza kwamba tahmiyd (Rabbana Walakal-Hamd) ya Maamuma inatakiwa isemwe baada ya tasmiy' (Sami'a Allaahu Liman Hamidah) ya Imaam. Hii imetiliwa nguvu kutokana na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema tahmiyd hali ya kuwa yeye ni Imaam, na pia kwa ujumla wa kauli yake: ((Swalini kama mnavyoniona nnaswali)) ambayo inaonyesha kwamba Maamuuma waseme anayoyasema Imaam kama (Sami'a Allaahu Liman Hamidah) na mengineo. Wale ndugu waheshimiwa waliorejea kwetu kuhusu mas-ala haya watilie maanani haya, labda katika tuliyotaja kuna yenye kukinaisha. Na yeyote atakayetaka kujadii zaidi mas-ala haya arejee katika makala ya Al-Haafidh As-Suyuutwiy katika mas-ala hii kwenye kitabu chake Al-Haawy lil Fataawa (1/529).

 

[7] Al-Bukhaariy na Muslim. At-Tirmidhiy amesema ni Swahiyh.

 

[8] Al-Bukhaariy na Muslim. Huku kunyanyua mikono ni mutawaatir kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), na ni kauli ya Maulamaa wengi na baadhi ya Mahanafi. Taz. Tanbihi za nyuma katika (mlango wa) Rukuu.   

[9] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[10] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[11] Al-Bukhaariy na Ahmad. Na kwa hakika Ibnul-Qayyim (رحمه الله) alikosea (katika nukta hii,) pale alipokanusha katika Zaad Al-Ma'aad usahihi wa riwaayah hii yenye kukusanya baina ya 'Allaahumma' na 'wa' pamoja na kuwepo kwake katika Swahiyh Al-Bukhaariy, Musnad Ahmad, An-Nasaaiy na Ahmad tena kupitia njia mbili (za usimulizi) kutoka kwa Abu Hurayrah, na katika Ad-Daaraimiy kutokana na Hadiyth ya Ibn 'Umar, na katika Al-Bayhaqiy kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudhriyy, na katika An-Nasaaiy tena kutokana na Hadiyth ya Abu Muusa Al-Ash'ariyy.

[12] Al-Bukhaariy na Muslim. At-Tirmidhiy amesema ni Swahiyh.

[13] Muslim na Abu 'Awaanah.

[14] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[15] Jadd: Bahati, Utajiri, Utukufu, nguvu, yaani Mwenye mali, watoto, cheo, uwezo na nguvu katika dunia hii. Hatoweza kunufaika navyo mbele Yako; Anavyomiliki havitomuokoa kutoka Kwako, lakini kitachomnufaisha na kumuokoa ni amali njema pekee.

[16] Muslim na Abu 'Awaanah.

[17] Muslim, Abu 'Awaanah na Abu Daawuud.

[18]    Abu Daawuud na An-Nasaaiy kwa isnaad Swahiyh. Imetolewa katika Al-Irwaa (335).

[19]    Maalik, Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

Share [110]

036-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kurefusha Kisimamo Hiki Na Wajibu Wa Kutulia Ndani Yake

 

 

KUREFUSHA KISIMAMO HIKI NA WAJIBU WA KUTULIA NDANI YAKE 

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akikifanya kisimamo chake hiki kuwa kirefu, (kama) unaokaribiana na urefu wa rukuu yake kama ilivyotajwa; bali, alikuwa akisimama mara nyingine mpaka msemaji husema: "Amesahau" [kutokana na kusimama kwake muda mrefu]".([1])

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiamrisha (wafanye) utulivu humo. Alimwambia aliyeswali vibaya ((…kisha nyanyua hadi unyooke sawa sawa hali ya kuwa umesimama (kila mfupa urudi mahali pake) [katika riwaaya nyingine] Unapoinuka nyoosha uti wako na nyanyua kichwa chako hadi mifupa irudi katika viungo vyake))([2]). Pia alimkumbusha kwamba: ((Swalah ya mtu haitimii kama hajafanya hivyo)).

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Allaah عزوجل Hatazami Swalah ya mja asiyenyosha uti wake wa mgongo barabara baina ya rukuu zake na sijda zake)).([3])

 

 

 





[1] Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad. Imetolewa katika Al-Irwaa (namba 307).

[2] Al-Bukhaariy, Muslim, Ad-Daraamiy, Al-Haakim, Ash-Shaafi'iy na Ahmad.

TANBIHI: Maana ya Hadiyth hii iko dhahiri na wazi, nayo ni utulivu katika kusimama huku. Ama utumiaji wa Hadiyth hii unaofanywa na baadhi ya ndugu zetu katika watu wa Hijaaz na kwengineko kama ni dalili ya kuthibitisha kuweka mkono wa kulia juu ya kushoto katika kusimama, bila shaka iko  mbali sana na  riwaaya nyingi za Hadiyth. Bali ni hoja ni batili, kwani uwekaji uliotajwa, haukuja utajo wake katika kisimamo cha kwanza katika usimulizi wowote ule wa Hadiyth na katika matamshi yake (Hadiyth). Basi inakuaje kupelekea kutafsiri "mifupa irudi sehemu yake" iliyotajwa katika Hadiyth kuwa ni mkono wa kulia kuukumata mkono wa kushoto kabla ya rukuu?! Hii ingelitumika kama matamshi yote ya Hadiyth yangeasiriwa kumaanisha hivi. Basi vipi kuhusu wanavyohusisha maana iliyobainisha maana tofauti kabisa? Bali kuweka kwake hakuwezi kufahamika kutoka katika Hadiyth kabsia, kwa vile iliyokusudiwa 'mifupa' ni mifupa ya uti wa mgongo, kama ilivyothibitishwa katika Sunnah, "…alikuwa akisimama kwa kunyooka barabara hadi kila mfupa ulirudi sehemu yake."

 

Mimi binafsi, sina shaka kwamba kuweka mikono juu ya kifua katika kusimama ni uzushi unaopotoa, kwani haikutajwa katika Hadiyth zozote za Swalah juu ya kwamba ni nyingi mno. Ingelikuwa kutendeka huko kuna asili, ingelitufikia japo katika usimulizi mmoja. Juu ya hivyo, hakuna hata Salaf mmoja aliyefanya hivyo, wala hakutaja hata mmoja wa Maulamaa wa Hadiyth nijuavyo.

 

Hii hailingani na alivyonukuu Shaykh At-Tuwayjiriy katika Makala yake (Uk. 18-19) kutoka kwa Imaam Ahmad (رحمه الله), "Akipenda mtu, anaweza kuacha mikono yake pembeni, au akipenda anaweza kuweka kifuani mwake", kwani Imaam Ahmad hakuhusisha hii kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), bali alisema kutokana na ijtihaad  na rai yake mwenyewe. Na rai inaweza kuwa imekosewa. Inapopatikana dalili sahihi dhidi ya uzushi inafuatwa na kuachwa hiyo ya uzushi, mfano kama hii, hivyo kauli ya Imaam yenye mapendekezo yake haikanushi uzushi wake kama alivyoandika Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyah (رحمه الله). Bali naona haya maneno yake ni ishara kwamba Imaam Ahmad hakuchukulia kuwekwa kulikotajwa juu kama ni kumethibitika katika Sunnah, kwani ameruhusu uchaguzi baina ya kutenda na kuacha kutenda. Je, anadhani Shaykh Mheshimiwa kwamba Imaam aliruhusu pia uchaguzi kuhusu uwekaji wa mikono kabla ya rukuu? Hivyo imethibitika kwamba kuweka mikono kifuani katika kusimama baada ya rukuu sio katika Sunnah. Haya ni majadiliano mafupi ya mas-ala haya  ambayo yanaweza kujadiliwa katika maelezo zaidi kwa upana, lakini kutokana na uchache wa sehemu hapa, inatosha, na badala yake, ni ubainisho wangu dhidi ya Shaykh (At-Tuwayjiriy) katika Chapa ya tano (Uk. 30) chapa mpya.

 

     

[3]    Ahmad na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr ikiwa na isnaad Swahiyh.

Share [111]

037-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kusujudu, Kwenda Chini Kusujudu Kwa Kutanguliza Mikono

 

 

KUSUJUDU

 

Kisha alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)akileta Takbiyr na kuporomoka chini kwa kusujudu([1]), na alimuamrisha aliyeswali vibaya afanye hivyo akimwambia: ((Swalah ya mtu ye yote haikamiliki hadi … aseme: 'Sami'a Allaahu Liman Hamidah' na mpaka anyooke sawa sawa, kisha aseme: 'Allaahu Akbar' kisha asujudu mpaka viungo vyake (vitulizane))).([2])

 

Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anapotaka kusujudu, huleta Takbiyr, (akitenganisha mikono yake mbali na ubavu wake) kisha ndio husujudu)([3])

 

Mara nyingine alikuwa akiinua mikono yake anaposujudu.([4])

 

 

KWENDA CHINI KUSUJUDU KWA (KUTANGULIZA) MIKONO

 

Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitanguliza mikono yake ardhini kabla ya magoti yake.([5])

 

Alikuwa akiamrisha hivyo kwa kusema: ((Anaposujudu mmoja wenu, basi asiiname kama anavyoinama ngamia, bali atangulize mikono yake kabla ya magoti yake)).([6])

 

Na alikuwa pia akisema: ((Hakika mikono miwili inasujudu kama uso unavyosujudu, basi anapoweka mmoja wenu uso wake, aweke mikono yake na anapoinuka aiinue )).([7])

 

 

Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) viganja vyake (akivitanua)([8]) , akibana vidole vyake pamoja([9]) na kuvielekeza Qiblah.([10])

 

Na pia alikuwa akiviweka viganja vya mikono yake usawa na mabega yake([11]), na mara nyingine usawa na masikio yake([12]).  Alikuwa akiimakinisha pua yake na kipaji chake na ardhi.([13])

 

Alimuambia aliyeswali vibaya: ((Unaposujudu, makinisha sijda yako))([14]).  Na katika usimulizi mwingine: ((Unaposujudu, makinisha uso wako na mikono yako, hadi mifupa yako yote itulie mahali pake)).([15])

 

Na alikuwa pia akisema: ((Hakuna Swalah kwa ye ote yule isiyegusa pua yake ardhi kama kinavyogusa kipaji cha uso)).([16])

 

Alikuwa pia akimakinisha chini magoti yake na vidole vya miguu yake([17]), na akielekeza ncha za vidole vya mikono yake Qiblah([18]). Aliweka visigino vyake pamoja([19]). Aliweka miguu yake sawa sawa([20]) na aliamrisha hivyo.([21])

 

Hivi ni viungo saba ambavyo   (صلى الله عليه وآله وسلم) alisujudia; viganja viwili vya mikono, magoti mawili, miguu miwili, kipaji cha uso na pua.

 

Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم)  alivihesabu viungo viwili vya mwisho kama ni kiungo kimoja katika kusujudu kwani alisema: ((Nimeamrishwa kusujudu (katika riwaaya nyingine: Tumeamrishwa kusujudu juu ya viungo saba): Juu ya kipaji cha uso na akaashiria kwa mkono wake([22]), kwenye pua, na mikono, [katika riwaaya nyingine: viganja vya mikono], magoti na vidole vya miguu, na wala tusikunje([23]) nguo na nywele)).([24])

 

Alikuwa akisema: ((Mja anaposujudu, husujudu pamoja nae viungo saba: uso wake, viganja vya mikono yake, magoti yake, na miguu yake)).([25])

 

Na kuhusiana na mtu aliyeswali akiwa kafunga nywele zake([26]) kwa nyuma, Mtume  (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: ((Mfano wake hakika ni kama mfano wa mtu anayeswali huku amefunga mikono yake [nyuma ya mgongo wake]))([27]).  Akasema pia: ((Hiyo ni tandiko la Shaytwaan)), yaani anapokaa Shaytwaan, akikusudia mafundo ya nywele zake.([28])

 

Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)  hailazi mikono yake([29]), bali alikuwa akiinyanyua mbali na ardhi na kuiweka mbali na mbavu zake kiasi kwamba weupe wa kwapa zake huonekana nyuma yake([30]), na pia kiasi kwamba lau mbuzi mchanga angelitaka kupita chini ya mikono yake angelipita.([31])

 

Alikuwa akifanya hivyo sana kiasi cha kwamba baadhi ya Swahaba zake walisema: "Tulikuwa tunahisi vibaya kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu ya vile anavyoweka mikono yake mbali na mbavu zake anaposujudu.([32])

 

Alikuwa  (صلى الله عليه وآله وسلم)akiamrisha hivyo kwa kusema: ((Unaposujudu, weka viganja vyako (ardhini), na inua viwiko vyako ([33]). Na akisema: Kuweni sawa katika sujuud, na wala asitawanye mmoja wenu mikono yake mtawanyo wa [na katika riwaaya nyingine: kama anavyoitawanya] mbwa))([34]).

Na katika tamshi jingine na Hadiyth nyingine: ((Na wala asilaze mmoja wenu mikono yake kama mlazo wa mbwa))([35]). 

Alikuwa pia akisema: ((Msitandaze mikono yenu [kama mtandazo wa mbuai (mnyama wa kuwinda). Lazeni mikono na tandazeni mikono mbali, kwani ufanyapo hivyo, huwa kila kiungo chako kinasujudu nawe)).([36])

 

 

 





[1] Al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amewafikiana.

[3] Abu Ya'laa katika Musnad (284/2) ikiwa na isnaad nzuri na Ibn Khuzaymah (1/79/2) ikiwa na isnaad tofauti iliyo Swahiyh.

[4] An-Nasaaiy, Ad-Daaraqutwniy na Mukhlisw katika Al-Fawaaid (1/2/2) ikiwa na isnaad mbili Swahiyh. Kunyanyua mikono huku kumeripotiwa na Maswahaba kumi na Masalaf wengi wameona ni muono Swahiyh. Miongoni mwao ni Ibn 'Umar, Ibn 'Abbaas, Hasan Al-Baswriy, Twaawuus, mtoto wake 'Abdullaah, Naafi' mtumwa wa Ibn 'Umar aliyeachwa huru, Saalim mtoto wa Ibn 'Umar, Qaasim bin Muhammad, 'Abdullaah bin Diynaar na ‘Atwaa. Vile vile 'Abdur-Rahmaan bin Mahdi kasema: "Hii ni kutokana na Sunnah". Imefanywa na Maimamu wa Sunnah; Ahmad bin Hanbal, na imenukuliwa kutoka kwa Maalik na Ash-Shaafi'y.

[5] Ibn Khuzaymah (176/1), Ad-Daaraqutwniy na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Hadiyth zote zinazopinga hii sio Swahiyh. Namna hii kumeidhinishwa  na Maalik, na ripoti kama hiyo  kutoka kwa Ahmad katika At-Tahqiyq ya Ibn Al-Jawzi (108/2). Al-Marwaz pia amenukuu kwa isnaad Swahiyh. Imaam Al-Awazaa'iy katika Masaail yake (1/47/1) akisema: "Nimewaona watu wakitanguliza mikono kabla ya magoti".

[6] Abu Daawuud, Tamaam katika Al-Fawaaid, na An-Nasaaiy katika Sunan As-Sughraa na Sunan Al-Kubraa (47/1) ikiwa na isnaad Swahiyh. 'Abdul-Haqq amekiri ni Swahiyh katika Al-Ahkaam (54/1) na akaendelea kusema katika Kitabu At-Tahajjud (56/1), "Ina isnaad madhubuti kuliko ya nyuma yake". Yaani Hadiyth ya Waail ambayo ni kinyume (magoti kabla ya mkono). Bali Hadiyth ya mwisho, pamoja nakuwa inapinga Hadiyth hii Swahiyh na iliyotangulia, sio Swahiyh katika isnaad wala katika maana, kama nilivyoelezea katika ‘Silsilatul-Ahaadiyth Adh-Dhwa'iyfah’ (Namba. 929) na katika Al-Irwaa (357).

Itambulikane kwamba njia ya kutofautisha na ngamia ni kutanguliza mikono kabla ya magoti kwa sababu ngamia anaanza kutanguliza magoti kwanza; magoti ya ngamia yako katika miguu yake ya mbele kama ilivyobainishwa katika Lisaan Al-'Arab na vitabu vingine vya Kiarabu, na kama ilivyotajwa na Atw-Twahaawiy katika Mushkil Al-Athaar  na Sharh Ma'aani Al-Athaar. Pia Imaam Qaasim As-Saraqutwniy (رحمه الله) katika Ghariyb Al-Hadiyth (2/70/1-2), ikiwa na isnaad Swahiyh, kauli ya Abu Huraryah, "Asipige magoti mtu kama afanyavyo ngamia anayekimbia". Akasema Imaam, "Hii ni katika sajdah. Anasema kwamba mtu asijitupe chini kama anavyojitupa ngamia anayekimbia (asiyefugwa) kwa haraka na bila ya utulivu, bali aende polepole chini akitanguliza kuweka mikono yake kwanza, kisha yafuatie magoti. Na maelezo ya Hadiyth marfuu' imesimuliwa kuhusu jambo hili". Kisha akataja Hadiyth za juu.

 

Ama kauli ya ajabu ya Ibnul-Qayyim, "Maneno haya hayaeleweki na hayafahamiki na mabingwa wa lugha", inajibiwa na vyanzo tulivyovitaja pamoja na vingi vinginevyo ambavyo maelekezo yanaweza kutafutwa. Nimelezea pia kuhusu hii katika kubainisha uongo dhidi ya Shaykh At-Tuwayjiriy ambayo imechapichwa.

 

[7] Ibn Khuzaymah (1/79/2), Ahmad na Siraaj. Al-Haakim amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy ameikubali. Imetolewa katika Al-Irwaa (313).

[8] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.

[9] Ibn Khuzaymah, Al-Bayhaqiy na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahaby amekubali.

[10] Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Ibn Abi Shaybah (1/82/2) na Siraaj wamehusisha kuelekeza vidole vya mguu katika usimulizi mwingine.

[11] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh, kama alivyokiri Ibn Al-Mulaqqin (27/2). Imetolewa katika Al-Irwaa (309).

[12] Abu Daawuud na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[13] Abu Dawuud na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh kama alivyokiri Ibn Al-Mulaqqin (27/2). Imetolewa katika Al-Irwaa (309).

[14]  Abu Daawuud na Ahmad ikiwa na isnaad Swahiyh.

[15] Ibn Khuzaymah (1/10/1) ikiwa na isnaad nzuri.

[16] Ad-Daaraqutwniy, Atw-Twabaraaniy (3/140/1) na Abu Nu'aym katika Akhbaar Isbahaan.

[17] Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh, Ibn Abi Shaybah (1/82/2) na Siraaj. Wamehusisha nia kuelekeza vidole vya mguu katika usimulizi mwingine.

[18] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Ibn Sa'd (4/157) amesimulia kutoka kwa Ibn 'Umar kwamba alipenda kuelekezea Qiblah kila sehemu ya mwili wake awezavyo wakati wa kuswali hata vidole gumba.

[19] Atw-Twahaawiy, Ibn Khuzaymah (Namba 654) na Al-Haakim ambaye amekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahaby amekubali.

[20] Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[21] At-Tirmidhy na Siraaj. Al-Haakim amekiri ni Swahiyh na Adh-Dhahaby amekubali.

[22] Kuashiria huku kwa mkono kumefasiriwa kutokana na sarufi ya matini ya Kiarabu (Fat-h Al-Baariy).

[23] Yaani kuvikusanya na kuvizuia kutawanyika, kwa maana, kukusanya nguo au nywele kwa mikono katika rukuu na sujuud (An-Nihaayah). Makatazo haya sio katika Swalah, bali hata kabla ya Swalah imekatazwa kama walivyoongeza Maulamaa wengi katika makatazo. Hii imetiliwa nguvu zaidi kwa kuwakataza wanaume kuswali wakiwa wamefunga nywele zao, ambayo inafuatia baadaye.

[24] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Al-Irwaa (310).

[25] Muslim, Abu 'Awaanah na Ibn Hibbaan.

[26] Yaani kubanwa juu au kusukwa.

[27] Muslim, Abu 'Awaanah na Ibn Hibbaan. Ibn Al-Athiyr amesema: "Maana ya Hadiyth hii ni kwamba kama nywele zake ingelikuwa zimelegea, zingelianguka ardhini katika sajdah; hivyo mtu atalipwa thawabu za kusujudu nywele. Lakini nywele zikifungwa, zitamaanisha kuwa hazikusujudu, kwani kamlinganisha na mtu ambaye mikono yake imefungwa pingu pamoja, kwa vile haitogusa ardhini kusujudu.

Inaelekea amri hii imewekewa mipaka kwa wanaume pekee na haiwahusu wanawake kama Ash-Shawkaaniy alivyonukuu katika Ibn Al-'Arabi.

[28]  Abu Daawuud na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni nzuri. Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan amekiri ni Swahiyh. Taz. Swahiyh Abu Daawuud (653).

[29]    Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[30]    Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Al-Irwaa (359).

[31]    Muslim, Abu 'Awaanah na Ibn Hibbaan.

[32]   Abu Daawuud na Ibn Maajah ikiwa na isnaad Hasan.

[33]    Muslim na Abu 'Awaanah.

[34]    Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud na Ahmad.

[35]    Ahmad na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh.

[36]   Ibn Khuzaymah (1/80/2), Al-Maqdisy katika Al-Mukhtaarah na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.

Share [112]

038-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Kutulia Katika Sujuud Na Adhkaar Za Sujuud

 

WAJIBU WA KUTULIA KATIKA SUJUDU

 

Alikuwa ( (صلى الله عليه وآله وسلمakiamrisha kutimiza rukuu na sujuud, na akimlinganisha mtu asiyetimiza hivyo kuwa ni kama mtu mwenye njaa anakula tende moja au mbili ambazo hazimsaidii kitu cho chote. Pia akimuambia kuhusiana na asiyetimiza: ((Hakika yeye ni muovu kabisa miongoni mwa watu  wezi)).

 

Vilevile alikuwa ( (صلى الله عليه وآله وسلمakihukumu kubatilika kwa Swalah ya mtu asiyenyoosha mgongo wake sawa sawa katika rukuu na sujudu, kama ulivyotangulia uchambuzi wake katika rukuu, na akamuamrisha aliyeswali vibaya atulie katika sujuud, kama ilivyotangulia katika mlango wa kwanza.

 

 

 

ADKHAAR ZA SUJUDU

 

Alikuwa   (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema katika nguzo hii namna mbali mbali za adhkaar na du'aa zozote, mara hizi na mara nyingine hizi. Kati ya du'aa hizo ni hizi zifuatazo:

 

1.

 

Subhaana Rabbiyal ‘Alaa

Ametakasika Mola wangu Aliye juu. (mara tatu).( [1])

 

 

Mara nyingine aliikariri zaidi ya mara hizo.([2])

 

 

Mara moja aliikariri sana katika Swalah ya usiku hadi sujuud yake ilikuwa inakaribiana na kisimamo chake alichokuwa amesoma ndani yake Surah tatu katika Surah ndefu; Al-Baqarah, An-Nisaa na Al-'Imraan. Ndani yake (Swalah hii) kulijaa du'aa na kuomba maghfirah, kama ilivyotajwa kabla katika Swalah ya Usiku.

 

 

2-

 

 

Subhaana Rabbiyal ‘Alaa wabihamdihii

Ametakasika Mola wangu Aliye juu Na Sifa Njema Ni Zake. (mara tatu)([3]).

 

 

3-

 

Subuuhun Qudduusun Rabbul Malaaikati war Ruuh

Mwingi wa kutakaswa Mtakatifu, Mola wa Malaika na Jibriyl.([4])

 

 

 

 

4-

 

 

Sub-haanaka Allaahumma Rabbanaa wa Biham-dika Allaahumma gh-fir-liy

Kutakasika ni Kwako, Ewe Allaah! Mola wetu, na sifa njema zote ni Zako, Ewe Allaah! Nisamehe.

Alikuwa akiileta kwa wingi hii katika rukuu yake na sujuud zake, alikuwa akitekeleza amri ya Qur-aan.([5])

 

 

5-

 

 

Allaahumma laka Sajad-tu, wabika Aamantu, walaka As-lamtu, [Anta Rabbiy] Sajada wajhiy Li-lladhiy Khalaqahu waswawwarahu, [fa-ahsana swuwarahu] washaqqa sam’ahu wabaswarahu, [fa]tabaaraka Allaahu Ahsanul Khaaliqiyn.

Ee Allaah! Kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimesilimu, (Nawe ni Mola Wangu) umesujudu uso wangu kumsujudia Yule Aliyeuumba na Akautia sura, na Akaupasua usikizi wake na uoni wake, [Basi] Ametukuka Allaah Mbora wa waumbaji.([6])

 

 

6-

 

 

Allaahumma gh-firliy dham-biy kullahu, wa diqqahu, wajillahu, wa awwalahu wa aakhirahu, wa’alaaniyyatahu wasi-rrahu.

Ee Allaah! Nisamehe dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri.([7])