Nyama Ya Ng'ombe Ya Kukaanga Na Mboga

Nyama Ya Ng'ombe  Ya Kukaanga Na Mboga 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Nyama  (Beef Pasande)  - 1 LB

(Isiyo na mafupa iliyokatwa

vipande vyembamba vya duara)

Kitunguu saumu(thomu) na Tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Sosi ya Soya (soy sauce)  - 2 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Karoti  - 1

Maharage ya kijani (spring beans)  - 1 kikombe

Pilipili mboga kijani - 1

Kabeji -  2 vikombe

Vitunguu vya kijani  - 2 miche

Mafuta - ½ kikombe 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

1)    Katakata nyama vipande virefu vidogo vidogo.

2)    Roweka Nyama kwa chumvi, thomu na tangawizi, pilipili manga, sosi ya soya kwa muda kama saa.

3)    Katakata karoti vipande virefu virefu vidogo kiasi.

4)    Katakata pilipili mboga

5)    Kata Kabeji nyembamba kiasi.

6)    Weka mafuta katika karai kaanga nyama mpaka iwive.

       (Karai nzuri kutumia ni ya inayoitwa 'wok' lakini sio lazima)

7)    Weka karoti na maharage ya kijani (spring beans) endelea kukaanga kwa dakika chache tu.

8)    Usiwache mboga zikawiva sana. 

9)    Tia kabeji na pilipili mboga na ukaange kwa dakika moja tu.

10)  Katia vitunguu vya kijani.

11)  Epua na tayari kuliwa. 

 

 

Share