Swafar: Uzushi Kuhusu Swalah Maaulum Ya Jumatano Ya Mwisho Mfungo Tano (Swafar)

 

Uzushi Kuhusu Swalah Maaulum Ya Jumatano Ya Mwisho Mfungo Tano (Swafar)

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalamu alaykuom,

 

Nasikia kuna sala ambayo inasaliwa jumatano ya mwisho ya mfungo tano je sheikh ni kweli ipo sala hiyo naomba majibu yenu, la pili

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho 

 

 

Swalaah ni ‘Ibaadah; ina masharti muhimu na ya msingi ambayo yamewekwa na Shariy’ah. Ibaadah yoyote kuwa sahihi na sawa ni lazima yatimize masharti hayo:

 

1.     Niyyah nzuri na Ikhlasi katika kutekeleza ‘Ibaadah yoyote.

 

2.     Ifuate kama alivyofanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Swalaah za faradhi zinaeleweka barabara na vile vile zile Swalaah za Sunnah kutoka katika Hadiyth zilizohifadhiwa na sahihi. Miongoni mwa Swalaah za Sunnah ni zile za kabla ya Swalaah ya faradhi, baada yake, Swalaah ya Adhw-Dhwuhaa, Taraawiyh, Tahajjud, Witri, na kadhalika. Hizi zote zimenukuliwa na Hadiyth zilizo sahihi.

 

 

Ama kuhusu Swalaah hiyo ambayo umeitaja haipo kabisa ima katika zile ambazo hazikusisitizwa au zile ambazo zimehimizwa, wala hakuna dalili yoyote iliyothibiti.

 

 

Hivyo, huo ni uzushi na sisi kama Waislamu hatufai kabisa kufuata mambo ambayo hayamo katika Dini yetu tukufu. Kwa hiyo, hakuna Swalaah kama hiyo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share