Anaweza Kufunga Swawm Za Sunnah Katika Mwezi Wa Shawwaal?

SWALI:

assalam alaikum warahmatu llahi wabarakatuhu,je inafaa kufunga sunna ya jumatatu na alhamisi katika mwezi huu washawwali?

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Unaweza kufunga Sunnah za Jumatatu na Alkhamiys na hata Ayyaamul-baydhw (tarehe 13, 14, 15 ).Na unaweza kufunga siku hizo pamoja na Sitta Shawwaal ikiwa umeshamaliza kulipa deni lako la Ramadhaan hivyo utakuwa unapata thawabu za Sitta Shawwaal  na za siku hizo Insha Allaah.

 

Na Allah Anajua zaidi

 

 

 


Share