Keki Ya Jibini Ya Matunda Ya Peach

Keki Ya Jibini Ya Matunda Ya Peach

                         

Vipimo

Malai ya jibini (cream cheese) -  2 Pakiti za 450g

Sukari -  ½ Kikombe cha chai

Mayai -  2

Unga wa ngano - 1 Kijiko cha chai

Mtindi (yogurt) -  ½ Kikombe cha chai

Ukoko wa tayari (ready crust) -  2

Matunda ya Peach ya kopo - 1

Unga wa kastadi - 1 Kijiko cha chai 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Washa oveni moto wa 350°F.
  2. Katika bakuli la mashine, changanya vizuri malai ya jibini, sukari, mtindi na halafu kijiko cha unga.
  3. Kisha tia mayai na uendele kuchanganya.
  4. Halafu mimina juu ya ule ukoko (crust) na utandaze vizuri hadi pembeni.
  5. Vumbika (bake) kwenye oveni kwa muda wa dakika 15, Kisha badilisha moto kwa kuweka 300°F na uendele kuchoma kwa muda wa saa moja.
  6. Ikishaiva iache ipoe na huku tayarisha sosi yake.
  7. Katika sufuria, tia juisi ya peach utakayoitoa kwenye kopo pamoja na kastadi na uweke moto mdogo huku unakoroga mpaka iwe nzito kiasi.
  8. Kisha mimina juu ya ile jibini iliyopoa na upange peach kwa mpango mzuri.
  9. Iweke kwenye firiji ipate ubaridi na kisha itakuwa tayari kwa kuliwa - kata vipande upendavyo.

Share