Skip navigation.
Home kabah

Sandwichi Za Soseji

 

Vipimo 

Mikate Yake:

Soma maelezo katika upishi ufuatao:

Sandwichi Za Mkate Wa Pita Na Nyama

 

Soseji                                                                    8 -12

Kabeji iliyokatwa nyembamba                                2 vikombe                        

Karoti                                                                    1  

Vitunguu vya kijani                                                 1 msongo

Slesi za achari ya matango

(zilorowekwa katika siki)                                       8 - 12

Chumvi                                                                 kiasi

Pilipili manga                                                          1 kijiko cha chai

Sosi ya haradali (mustard sauce)                            kiasi ya kunyunyuzia

 

 

Namna Ya Kutayarisha  

  1. Chemsha soseji kiasi unachotaka kufanya sandwichi weka kando.

  1. Katika bakuli, katakata kabeji nyembamba kiasi ifikie vikombe viwili.

  1. Ikune karoti ikatike nyembamba, changanya pamoja katika bakuli.

  1. Katakata vitunguu vya majani, (au kitunguu cha kawaida) tia chumvi, pilipili manga, changanya na slesi za matango.

  1. Fungua mkate kama ilivyo maelezo ujaze mchanganyiko.

  1. Nyunyizia sosi ya haradali (mustard sauce)

  1. Weka soseji juu yake, panga katika sahani zikiwa tayari.

  

Kidokezo:

 

  1. Ukipenda  nyunyizia pia kechapu ya nyanya (tomato ketchup) na sosi ya pilipili yoyote upendayo.

  1. Ukipenda pia tia slesi ya jibini (cheese)