005 - Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuatwa Rai Zao
KAULI ZA MAIMAAM WANNE KUHUSU KUSHIKAMANA
Itakuwa ni manufaa makubwa ikiwa tutazieleza baadhi ya kauli zao hapa, kwani labda hii itamuonya mtu au itawakumbusha wale ambao wanafuata rai za Maimaam au madhehebu maalum, bali wanaofuata kwa upofu wale Waalimu au Mashaykh na wale walio chini ya daraja ya hao Maimaam wanne wakubwa[1] wakishikilia madhehebu yao au rai zao kama kwamba zimeteremeshwa kutoka mbinguni! Na hali Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
((اتَّبِعُواْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلاَ تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاء))
((Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake))[2]
WASEMAVYO MAIMAAM
1) ABU HANIYFAH (رحمه الله)
Wa kwanza wao ni Abu Haniyfah Nu'maan bin Thaabit.
Wafuasi wake wamesimulia kauli zake mbali mbali pamoja na maonyo tofauti ambayo yote lengo lake ni moja, nalo ni: Wajibu wa kuikubali Hadiyth na kuachilia mbali kufuata rai za Maimaam ambazo zinakhitilafiana nayo.
- "Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu"[3]
Katika usimulizi mwengine:"Imekatazwa[6] mtu ambaye hajui dalili zangu kutoa hukmu[7] kutokana na maneno yangu"
Usimulizi mwengine imeongezwa: "…Kwani sisi ni wanaadamu, tunasema jambo siku moja na kulirudisha (kulikataa) siku ya pili yake".
Na katika usimulizi mwengine: "Ole Ewe Ya'quub![8] Usiandike kila kitu unachosikia kutoka kwangu kwani huwa natoa rai moja leo na kesho huikataa. Au hutoa rai moja kesho na kuikataa keshokutwa".[9]
- "Ninaposema jambo linalokhitilafiana na kitabu cha Allaah (سبحانه وتعالى) au yaliyosimuliwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi mpuuze kauli yangu".[10]
2) MAALIK BIN ANAS (رحمه الله)
Imaam Maalik bin Anas yeye amesema:
- "Hakika mimi ni mwanaadamu: Ninafanya makosa (mara nyingine) na ninakuwa sahihi (mara nyingine). Kwa hiyo, tazameni rai zangu: zote ambazo zinakubaliana na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, zikubalini; na zote ambazo hazikubaliani na Kitabu (Qur-aan) na Sunnah, basi zipuuzeni". [11]
- "Kila mmoja baada ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), atakuwa na kauli yake itakayokubaliwa na kukataliwa, isipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)" [12]
- Ibn Wahb amesema: "Nilimsikia Maalik akiulizwa kuhusu takhliyl ya vidole vya miguu (kuvichanganua vidole ili kupitisha maji) wakati wa wudhuu. Akasema: "Watu si lazima kufanya hivyo". Sikumkaribia hadi zogo la watu lilipopunguka. Nilipomwambia: "Tunajua kuwa ni Sunnah kuhusu jambo hilo". Akasema: "Jambo gani hilo? Nikasema: "Layth bin Sa'd, Ibn Lahiy'a na 'Amr bin Al-Haarith wamesimulia kwetu kutoka kwa Mustawrid bin Shaddaad Al-Quraishiy ambaye amesema: "Nilimuona Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akisugua baina ya vidole vyake vya miguu kwa kidole chake kidogo". Akasema: "Hadiyth hii ni Hasan (njema); sikuwahi kuisikia abadan ila leo". Kisha baadaye nikamsikia akiulizwa kuhusu jambo hili hili, naye akaamrisha kufanya takhliyl ya vidole vya miguu"[13]
3)
Ama kutoka kwa Imaam Ash-Shaafi'iy, kauli zake zilizonukuliwa ni nyingi na nzuri mno.[14] na wafuasi wake walikuwa ni bora kabisa katika kufuata.
- "Sunnah za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zinamfikia na kumkwepa kila mmoja wetu. Kwa hiyo kila ninapotaja rai yangu au nikiunda sheria, na ikiwa ipo dalili kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), inayopinga rai yangu, basi rai iliyo sahihi ni aliyosema Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na hiyo ndio rai yangu"[15]
- "Waislamu wamekubaliana pamoja kwamba ikiwa Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) imebainishwa dhahiri kwa yeyote, hairuhusiwi[16] kwake kuiacha kwa kufuata kauli ya mwengine yeyote[17]
- "Ukiona katika maandishi yangu jambo ambalo ni tofauti na Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi zungumza kwa kurejea Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na acha niliyoyasema mimi". Katika usimulizi mwengine: "…basi ifuate (Sunnah) na usitazame tena pembeni kufuata kauli ya mwengine yeyote"[18]
- Hadiyth ikipatikana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu"[19]
- "Wewe (Imaam Ahmad)[20] ni mwenye elimu zaidi kuhusu Hadiyth kuliko mimi. Kwa hiyo Hadiyth ikiwa ni Swahiyh basi nijulishe, ikiwa ni kutoka Kufah, Basrah au Syria, ili nichukue rai ya Hadiyth madamu tu ni Swahiyh"[21]
- "Katika kila jambo, ambako wenye kusimulia wakipata ripoti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo ni kinyume na niliyoyasema, basi narudisha kauli yangu nyuma, ikiwa wakati wa maisha yangu au hata baada ya kufa kwangu"[22]
- "Ukinisikia nasema kitu, na kinyume chake ni Hadityh Swahiyh kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), basi tambua kuwa akili yangu imetoweka"[23]
- "Kwa kila ninalosema, ikiwa upo usimulizi ulio Swahiyh, basi Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) inakuja mwanzo, kwa hiyo usifuate rai yangu"[24]
- "Kila kauli kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ni rai yangu pia, japokuwa hujaisikia kutoka kwangu"[25]
4) AHMAD BIN HANBAL (رحمه الله)
Imaam Ahmad alikuwa wa mbele miongoni mwa Maimaam kukusanya Sunnah na kuzishikilia sana hadi alichukizwa kuona kinaandikwa kitabu kilichokusanya mambo yaliyogeuzwa na mambo yaliyotegemea rai zaidi[26] kwa hilo akasema:
- Msifuate rai yangu, wala msifuate rai ya Maalik, au Ash-Shaafi'iy au ya Awzaa’iy, wala Ath-Thawriy, lakini chukueni kutoka kule walikotoa"[27]
Katika usimulizi mmoja: "Msiige dini yenu kutoka kwa mtu yeyote katika hawa, bali chochote kilichotoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake, chukueni, kisha kwa At-Taabi'iyn (Waliofuata) ambako mtu ana khiari".
Mara moja kasema: "Kufuata[28] ina maana kwamba mtu anafuata yaliyokuja kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake, ama baada ya At-Taabi'iyn (Waliofuata) anayo khiari" [29]
- "Rai ya Awzaaiy, rai ya Maalik, rai ya Abu Haniyfah, zote ni rai, na ni sawa katika macho yangu. Lakini, dalili ni yale masimulizi kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na Maswahaba zake"[30]
- "Yeyote atakayekanusha kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) basi yumo katika ukingo wa kuangamia"[31]
Hizi ndizo kauli za wazi kabisa za Maimaam, Allaah (سبحانه وتعالى) Awe radhi nao, kuhusu kushikamana na Hadiyth na kukataza kufuata rai zao bila ya kuwa na dalili iliyo dhahiri kabisa.
Kwa hiyo, yeyote aliyeshikamana na lolote la Sunnah ambayo imeshuhudiwa kuwa ni Swahiyh hata kama imepinga kauli ya baadhi ya Maimaam, hatokuwa anapingana na madhehebu yao, wala hatopotoka katika njia zao, bali mtu huyo atakuwa anawafuata wote na atakuwa amekamata kile kilichoaminiwa zaidi akishika mkono ambao hautavunjika. Lakini hii haitakuwa hali ya yule anayeziweka kando Sunnah Swahiyh kwa sababu tu zimepingana na rai za Maimaam, bali mtu huyo atakuwa sio mtiifu kwao na amepingia kauli zao hizo za juu. Na tunaona Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:
((فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّىَ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُواْ فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسْلِيمًا))
((La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenyekee kabisa.))[32]
((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))
((Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo))[33]
Haafidhw Ibn Rajab Al-Hanbali (رحمه الله) amesema: "Kwa hivyo ni wajibu kwa mtu yeyote anayesikia amri ya Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) au kuijua, kuielezea kwa Ummah, kuwapa nasaha ya dhati na kuwaamrisha kufuata amri zake japo kama itakuwa ni kinyume na rai ya mtu mkubwa. Hii ni kwa sababu hukmu ya Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ina haki zaidi kuheshimiwa na kufuatwa kupita rai za mtu yeyote mkubwa aliyekwenda kinyume bila ya kujua na amri za Mtume katika jambo lolote. Ndio maana Maswahaba na waliofuatia walimpinga yeyote aliyekwenda kinyume na Sunnah Swahiyh, mara nyingine wakiwa wakali katika kuwapinga kwao[34], sio kutokana na kumchukia huyo mtu, bali alikuwa ni mpenzi wao na mwenye kuheshimiwa, lakini kwa sababu Mjumbe wa Allaah alikuwa mpenzi wao zaidi na amri zake zilikuwa juu ya amri za viumbe wengine. Hivyo inapokuwa amri ya Mtume na ya mtu mwengine zinapingana, amri ya Mtume huwa ndiyo ipasayo kutiliwa nguvu na kutekelezwa. Hakuna katika hili lingeliwazua wasimheshimu mtu waliyempinga kwa sababu wamejua kuwa atasamehewa[35] , bali aliyetajwa mwisho hatojali amri zake kupingwa itakapokuwa amri za Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) zimeonyesha dhahiri kuwa ni kinyume chake [36]
Vipi wachukiwe hayo ikiwa wamewajibisha wafuasi wa kama ilivyo, na kama tulivyoona, kuwa wameamrisha waziache kando rai zao zinazokwenda kinyume na za Sunnah. Bali Imaam ash-Shaafi'iy (رحمه الله) aliwaambia Maswahaba zake kuzihusisha kwake Sunnah zilizo Swahiyh pia, japo kama hakuzitekeleza au katekeleza zilizo kwenda kinyume nazo. Hivyo mhakiki Ibn Daqiyq alipokusanya pamoja katika mjalada mzito, mas-ala ambayo kila mmoja katika kauli za madhehebu ya Maimaam wanne kuwa yamekwenda kinyume na Hadiyth Swahiyh, kama alivyaondika mwanzoni mwake: "Imekatazwa kuhusisha majibu haya kwa Maimaam waliojitahidi na ni fardhi kwa wanasheria wanaofuata rai zao kujua hizi ili wasije kuzinukuu wakawazulia"[37]
Wafuasi Wa Maimaam Kuacha Rai Zao Ikiwa Zinapingana na Sunnah
Kutokana na yote tuliyotaja, wafuasi wa Maimaam, ((Fungu kubwa katika wa mwanzo Na wachache katika wa mwisho))[38] hawakubali rai za Imaam wao, bali wanazipuuza nyingi wanapotambua kuwa zinakenda kinyume na za Sunnah. Hata Maimaam wawili Muhammad Ibn Al-Hasan na Bu Yuusuf (رحمها الله) walikhitilafiana na Shekhe wao Abu Haniyfah 'Fiy Nahw thuluth al-madhhab'[39] kama vitabu vya masaail vinavyothibitisha. Imesemwa hivyo hivyo kuhusu Imaam Al-Muzaniy[40] na wafuasi wengineo wa Ash-Shaafi'iy na Maimaam wengine. Tungelianza kutoa mifano majadiliano yangeliendelea kuwa marefu na tungelitoka nje ya makusudio katika mas-ala utangulizi huu, hivyo tutajiwekea mipaka kwa mifano miwili:
1. Imaam Muhammad amesema katika Muwattwa yake[41] (Uk. 158). "Ama Abu Haniyfah hakuona kuwa kuna Swalah ya kuomba mvua, lakini kauli yetu ni kwamba Imaam anaswali Rakaa mbili na anaomba du'aa na anashika shuka yake…"
2. Tunaye 'Iswaam bin Yuusuf Al-Balkhiy mmoja wa wafuasi wa Imaam Muhammad[42] na mtumishi wa Imaam Abu Yuusuf[43] ambaye akitoa hukmu kinyume na Imaam Abu Haniyfah kwa sababu hakujua ushahidi wake na ushahidi mwingine ulijitokeza kwake wenyewe hivyo alikuwa akiutolea hukmu:[44] . Hivyo alinyanyua mikono katika rukuu (kwenye Swalah) na anaponyanyuka[45] kama ilivyo mutawaatir Sunnah ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) bali Maimaam wake watatu (yaani Abu Haniyfah, Abu Yuusuf na Muhammad) wamesema vinginevyo na hawakumzuia kutekeleza Sunnah. Huu ni mfano ambao kila Muislamu inampasa kuwa nao kwani tumeshaona kutokana na ushahidi wa Maimaam wanne na wengineo huko juu.
[1] Hii ni aina ya taqliyd (kufuata kwa upofu [kiujinga]) ambayo Imaam At-Twahaawiy alihusisha aliposema: "Hafuati rai ila ni mtu mkaidi au mjinga" (kufuata kama kipofu)
[2] Al-A'raaf:3
[3] Ibnul-'Aabidiyn katika al-Haashiyah (1/63) na katika inshaa yake Rasm al-Mufti (1/4 kutoka Mkusanyiko wa Inshaa za Ibnul-'Aabidyin). Shaykh Swaalih Al-Fulaaniy katika al-Iyqaadhw al-Himaam (uk.62) na wengineo. Ibnul-'Aabidiyn amenukuu kutoka Sharh al-Hidaayah ya Ibn Al-Shahnah Al-Kabiyr, mwalimu wa Ibn Al-Himaam, kama ifuatavyo:
"Ikiwa Hadiyth iliyo kinyume na Madhehebu imeonekana kuwa ni Swahiyh basi mtu atende kwa kufuata hiyo Hadiyth na aifanye kuwa ni madhehebu yake. Kuifanyia kazi Hadiyth hakutombatilisha mtu kuwa sio mfuataji wa madhehebu ya Hanafi, kwani imeripotiwa kuwa Abu Haniyfah alisema: "Ikiwa Hadiyth imeonekana kuwa ni Swahiyh, basi hiyo ndiyo madhehebu yangu". Na hii imeelezewa na Imaam Ibn 'Abdil-Barr kutoka kwa Abu Haniyfah na kutoka kwa Maimaam wengine".
Hii ni sehemu ya ukamilifu wa elimu na ucha Mungu wa Maimaam, kwani wameonyesha kwa kusema kwamba wao hawakuwa na maarifa (elimu) kamili ya Sunnah zote. Na Imaam Ash-Shaafi'iy amefafanua wazi wazi (tazama mbele). Hutokea wanapokwenda kinyume na Sunnah huwa ni kwa sababu hawakuitambua. Ndipo walipotuamrisha tushikilie Sunnah na tuizingatie kuwa ni sehemu ya madhehebu yao. Allaah Awashushie Rahma Yake kwao wote.
[4] Sio halaal
[5] Ibn 'Abdil-Barr katika Al-Intiqaa' fiy Fadhwaail Ath-Thalaathah Al-Aimmah Al-Fuqahaa (uk.145), Ibn Al-Qayyim katika 'I'laam Al-Muwaqi'iyn (2/ 309), Ibn 'Aabidiyn katika tanbihi zake kwenye Al-Bahr Ar-Raa'iq (6/ 293) na katika Rasm Al-Mufti (uk. 29, 32) na Sha'raaniy katika Al-Miyzaan (1/ 55) pamoja na usimulizi wa pili. Usimulizi wa mwisho ulikusanywa na 'Abbaas Ad-Dawriy katika At-Taariykh ya Ibn Ma'iyn (6/ 77/1) ikiwa na Isnaad Swahiyh kutoka kwa Zafar, mwanafunzi wa Imaam Abu Haniyfah. Usimulizi uliofanana upo kutoka kwa wafuasi wa Abu Haniyfah; Zafar, Abu Yuusuf na 'Aafiyah bin Yaziyd; taz. Al-Iyqaadhw (uk. 52). Ibn Al-Qayyim alithibitisha kwa nguvu usahihi wake kutoka kwa Abu Yuusuf katika I'laam Al-Muwaqi'yn (2/ 344). Nyongeza ya usimulizi wa pili unarejewa na mwandishi wa Al-Iyqaadhw (uk. 65) kwa Ibn 'Abdil-Barr, Ibn Al-Qayyim na wengineo.
Ikiwa hivi ndivyo wanavyosema kwa mtu asiyejua dalili zao, jibu lao litakuwa nini kwa yule anayetambua kuwa dalili zinapingana na kauli yao, lakini bado anatoa hukumu iliyopinga dalili? Kwa hiyo, fuata usemi huu, kwani pekee unatosheleza kuvunja ufuataji rai kwa ujinga. Ndio maana nilipomlaumu mmoja wa Mashaykh (Muqallid) wa madhehebu katika kutoa fatwa (hukm) kwa kutumia maneno ya Abu Haniyfah bila ya kujua dalili, aligoma kuamini kuwa hiyo ni kauli ya Abu Haniyfah!
[6] Haraam
[7] Fatwa
[8] Mwanafunzi mashuhuri wa Imaam Abu Haniyfah, Abu Yuusuf (رحمه الله)
[9] Hii ni kwa sababu Imaam kawaida hutoa rai yake kutokana na Qiyaas (analojia). Kisha tena hupata analojia iliyo na nguvu zaidi, au Hadiyth ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) humfikia. Kwa hiyo huikubali hiyo na kuipuuza rai yake ya nyuma. Maneno ya Sha'araaniy katika Al-Miyzaan (1/62) yamewekwa kwa mukhtasari kama ifuatavyo:
"Imani yetu na ya kila mtafiti wa Imaam Abu Haniyfah (رحمه الله) ni kwamba, aliishi hadi iliporikodiwa Sharia. Na safari za wahifadhi wa Hadiyth katika miji mbali mbali na mipakani kwa ajili ya kukusanya na kuzipata. Angeliipokea na kupuuza analojia zote ambazo alizozitumia, idadi za Qiyaas katika madhehebu yake zingelikuwa kidogo kama zilivyo katika madhehebu mengine. Lakini kwa vile dalili za Sharia zimetapakaa kwa Waliotangulia na waliowatangulia, na haizikukusanywa wakati wa maisha yake, ilihitajika kuwepo Qiyaas nyingi katika madhehebu yake kulingana na Maimaam wengine. Maulamaa wa baada ya hapo, kisha wakafanya safari kutafuta na kukusanya Hadiyth kutoka nchi mbali mbali na miji na wakaziandika. Hivyo baadhi ya Hadiyth za Sharia zimeelezea nyingine. Hii ni sababu ya kuweko idadi kubwa ya qiyaas katika madhehebu yake wakati kwenye madhehebu mengine ilikuwa ni idadi ndogo"
Abul-Hasanaat Al-Laknawiy amenukuu maneno yake kikamilifu katika An-Naafi' Al-Kabiyr (uk. 135) akiandika na kupanua tanbihi zake. Kwa hiyo yeyote anayependa kutafuta maelekezo yake afanye humo.
Kwa vile hii ni uthibitishaji kuwa kwa nini Abu Haniyfah mara nyingine alikhitilafiana na Hadiyth zilizokuwa Swahiyh bila ya kukusudia na ni sababu barabara ya kukubaliwa, kwani Allaah Haikalfishi nafsi kwa yale isiyoweza kubeba. Hairuhusiwi kumtukana kwa sababu hiyo kama walivyofanya watu wajinga. Bali ni wajibu kumheshimu, kwani yeye ni mmoja wa Maimaam wa Waislamu ambao wameihifadhi hii dini hadi ikafikishwa kwetu kutoka katika kila matawi yake. Na kwa vile yeye analipwa (Na Allaah سبحانه وتعالى) kwa hali yoyote ile; ikiwa kapata au amekosea kwa kutokusudia. Wala hairuhusiwi kwa wafuasi wake wapenzi kuendelea kushikilia kauli zake ambazo zinakhitilafiana na Hadiyth zilizo Swahiyh kwani kauli hizo sio madhehebu yake kama kauli zake hapo juu zilivyosema. Kwa hiyo hii ni mipaka miwili; ukweli na uongo katika yake. ((Na waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala Usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu)) [Al-Hashr 59:10]
[10] Al-Fulaaniy katika Al-Iyqaadhw Al-Himaam (uk.50), ikifuatilia kwa Imaam Muhammad na kisha kusema: "Hii haimhusu Mujtahid, (mwenye kujitahidi kwa elimu yake na kutoa hukmu) kwa vile hakujifunga katika rai zao, bali inamhusu Muqallid (mwenye kufuata).
[11] Ibn 'Abdil-Barr kati
