Skip navigation.
Home kabah

Majuto Ya Nafsi - 2

 

07 Rajab 1426  12-08-2005

 

 

Nafsi ikiendelea kujuta kutamani kuwa ingelipata uongofu.

}}أَوْ تَقُولَ لَوْ أَنَّ اللَّهَ هَدَانِي لَكُنتُ مِنَ الْمُتَّقِينَ{{

{{Au ikasema: Ingelikuwa Mwenyezi Mungu ameniongoa, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa wenye kumcha Mungu}} Az-Zumar:57

 

Nafsi hiyo inapofikishwa na Mola wake kuonyeshwa maandalio yake kama ni jazaa yake kutokumtii alipokuwa duniani, yaani adhabu ya moto wa Jahannam, hutamani kama angelipewa fursa arudi kufanya mema lakini wapi! Tayari keshachelewa!

 }}أ َوْ تَقُولَ حِينَ تَرَى الْعَذَابَ لَوْ أَنَّ لِي كَرَّةً فَأَكُونَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ{{

{{Au ikasema inapo ona adhabu: Lau kuwa ningeli pata fursa nyengine, ningeli kuwa miongoni mwa wafanya mema}} Az-Zumar: 58

Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ametuelezea hali ya majuto hayo  yatakavyokuwa kwa kutupa picha ya watu wa motoni watakavyotamani makazi ya watu wa peponi, na watu wa peponi watakavyoona makazi ya watu wa motoni   katika hadithi ifuatayo:

‏(( ‏عن ‏ ‏أبي هريرة رضي الله عنه  ‏ ‏قال: ‏قال رسول الله ‏ ‏صلى الله عليه وآله وسلم: ‏ ‏كل أهل النار يرى مقعده من الجنة فيقول لو أن الله هداني فتكون عليه حسرة قال : وكل أهل الجنة يرى مقعده من النار فيقول لولا أن الله هداني قال : فيكون له شكرا )) إمام أحمد

((Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه   ambaye alisema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; Kila mtu wa motoni ataona makazi yake (aliyoandaliwa) peponi atasema; "Laiti Kama Mwenyeezi Mungu angelinihidi", kisha huwa majuto kwake. Akasema; Na kila mtu wa peponi ataona makazi yake ya motoni atasema; "Kama ingelikuwa sio Mwenyeezi Mungu kunihidi".  Akasema; kisha itakuwa sababu ya kushukuru kwake))  Imaam Ahmad

 

Na kama tunavyojua kuwa maisha ya Akhera ndio maisha ya milele, na haya ya dunia ni starehe ndogo tu.Kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى  :

}}وَمَا هَذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ{{

{{Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!}} 'Ankabuut:64

Nayo nyumba hiyo ya Akhera ni ya wale wamchao Mungu tu, wenye kufanya vitendo vyema vyenye kumridhisha Mola wao

 }}  وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَلَلدَّارُ الآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ أَفَلاَ تَعْقِلُون{{

{{Na maisha ya dunia si chochote ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini}} Al-An'aam:32

Lakini waovu wote hawatopata neema ya hiyo nyumba bora ya Akhera, bali malipo yao yatakuwa ni makazi mabaya na hali wakiwa na majuto, baada ya kutambua kuwa wako katika khasara kubwa za nafsi zao pamoja na za jamaa zao:

}}قُلْ إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَلَا ذَلِكَ هُوَ الْخُسْرَانُ الْمُبِينُ{{

{{Sema: Hakika walio khasirika ni wale walio jikhasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Tambueni kuwa hiyo ndiyo khasara iliyo dhaahiri.}}

Az-Zumar:15

 

 **********