Nguzo Za Fardhi Za Kiislamu, Zimefaridhiwa Lini?

 

SWALI:

 

Naomba kujua tarehe za kufaradhishwa kwa nguzo tano za Kiislam.

Nawatakia kila la kheri

 

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu  tarehe za kufaradhishwa nguzo za Uislamu.

Nguzo Za Kiislamu zimefaridhiwa kama ifuatavyo:

1.      Shahada – mwaka wa kwanza baada ya kupatiwa Utume, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

2.      Swalaah – miezi 12 hadi 16 kabla ya Hijrah pale Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipopelekwa kwa safari ya Israa na Miyraaj.

3.      Swawm – mwaka wa pili mwezi wa Sha‘abaan baada ya Hijra

4.      Zakaah – mwaka wa pili mwezi wa Sha‘abaan baada ya Hijra.

5.      Hajj – mwaka wa sita baada ya Hijrah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share