Mirathi – Nyumba
SWALI:
Asalam aleikum nilikua nauliza kuhusu wirathi nilikua nataka kujua tafadhali naomba unijibu nipate kufahamu. Mimi nina mjombangu alinunua nyumba akaandika ile nyumba jina la mamake huyo mjombangu ni ndugu tu na mamangu kwa mama na baba. Huyo mjombangu nae alikufa lakini mamake
yuhayi na huyo mamake mimi hua ni nyanyangu. na ana watoto wengi wanawake na wanaume. Lakini mamangu nae alikufa baada ya mjomba kufa kisha mamangu alikufa kisha nyanyangu nae akafa sasa nauliza mimi narithi. na mamangu amezaa watoto wawili tu wanawake sasa nilikua nataka kuuliza pengine mwaeza kunifahmisha zaidi tafadhali mukiipata munijibu maasalam nawatakia ramadhan kareem.
Ufafanuzi zaidi uliotakiwa na Alhidaaya kuweza kujibu swali:
Shukurani kwa swali lako hili zuri, lakini ili tuweze kukujibu vizuri zaidi tungependa utujulishe yafuatayo:
1. Je, huyu nyanyako, mume wake yuko hai?
2. Je, una ndugu shaqiqi? au ndugu kwa mama tu au kwa baba tu?
3. Je, wazazi wake wapo hai?
JIBU LA MUULIZAJI:
Laa nyanyangu hana mume wake alikufa kitambo
JIBU:
Tunamshukuru Allah kwa kutupatia uhai, afya na neema nyengine nyingi ambazo hazihesabiliki ili tupate Kumuabdu Yeye peke Yake. Swalah na salamu zimfikie Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ahli zake na Maswahaba wake na watangu (waliotangulia) wema mpaka Siku ya Qiyaama.
Ahsanta
Sasa ikiwa mjombako alimnunulia nyanyako na kumpatia tunu (au zawadi) itakuwa ni sawa lau
Hivyo, akiwa ni mjomba wako itategemea kama ameacha mke na watoto wao watakuwa na mafungu
Lakini ikiwa hiyo nyumba ni tunu kutoka kwa mjomba wako kumpatia nyanya yako, mama yako kwa sababu aliaga dunia kabla ya mama yake hatakuwa na fungu lolote hivyo wewe hutapata chochote katika mirathi. Fungu kubwa litakwenda kwa watoto wake (wa nyanya yako) wa kiume na kike na kitakacho baki kitakuwa ni cha kaka zake na dada zake nyanya yako.
Tanbihi kwa wenye kuuliza Maswali ya Mirathi:
1. Kijana mwanamume.
2. Kijana mwanaume wa kijana mwanaume (mjukuu)
3. Baba.
4. Babu wa kwa baba.
5. Ndugu mume wa kwa baba na mama (khalisa).
6. Ndugu wa kwa baba.
7. Ndugu mume wa kwa mama.
8. Kijana mwanaume wa ndugu mume khalisa.
9. Kijana mwanaume wa ndugu mume wa kwa baba.
10. Ami wa kwa baba na mama.
11. Ami wa kwa baba.
12. Kijana mwanaume wa ami wa kwa baba na mama.
13. Kijana mwanaume wa ami wa kwa baba.
14. Mume.
15. Binti.
16. Binti wa kijana mwanaume.
17. Mama.
18. Dada khalisa.
19. Dada wa kwa baba.
20. Dada wa kwa mama.
21. Bibi mzaa baba.
22. Bibi mzaa mama.
23. Mke.
Hii itatusaidia
Na Allaah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



ASALAM ALEIKUM. MIMI NAITWA
ASALAM ALEIKUM.
MIMI NAITWA .....NIMEFIWA NA MUME WANGU MWAKA JUZI, NA NINA WATOTO WANNE WAKIUME WATATU WAKIKE MMOJA NA BADO NI WADOGO WA KWANZA NDIO YUPO KIDATO CHA KWANZA MWAKA HUU.NA KATIKA UHAI WA MUME WANGU MIMI ALINIACHISHA KAZI NA NIFATII AMRI YA MUME WANGU. BABA NA MAMA MKWE WANGU WAMESEMA WAO WATAWALEA HAO WATOTO HAO JE? SASA PAMOJA NA MALI ZA MUME WANGU WANAZO IKIWEMO GARI, JE MIMI HAPO NASTAHILI NINI? NA JE VYOMBO VYA NDANI NANI ANASTAHILI? NAOMBA MSAADA WAKO WA KUJIBIWA SWALI LANGU KWA SABABU MPAKA SASA MIMI NIPO KWETU NA SIJAPEWA KITU CHOCHOTE.
Assalaamu 'alaykum Tafadhal
Assalaamu 'alaykum
Tafadhal tuma swali lako kupitia maswali@alhidaaya.com lipate kujibiwa. Hapa ni mahali pa kuweka maoni tu sio pa kuweka maswali.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA