Buns Za Nyama Aina Ya 2

Vipimo
Mayai 4
Mafuta 1 kikombe
Maziwa 1kikombe
Chumvi kiasi
Hamira 1 1/2 kijiko cha supu
Unga kiasi
Habat suda( blackseed) 1 kijiko cha supu
Nyama
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1.
Kwenye chombo kikubwa changanya mayai, mafuta, maziwa, chumvi changanya vizuri
2.
Tia hamira na habat suda kisha mimina unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko ushikane uwe laini .
3.
Iwache ifure,ukisha fura kata madonge ya kiasi ujaze nyama katikati kisha ufunge iwe duwara panga kwenye sinia kisha yapake maziwa kwa juu
4.
Choma kwa moto wa 350 mpaka zibadilike rangi na yawive vizuri .
5. Iwache ipoe kisha itakuwa tayari kuliwa .
Kidokezo: unaweza kujaza feta cheese na zaituni badala ya nyama pia inakuwa nzuri .
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
