Makumi Matatu Ya Ramadhaan Na Yepi Kufanya
SWALI:
Aslaam alayku!
Naomba kupata ufafanuzi wa makumi yoote matatu na taratibu nzuri za kuyataekeleza nayanayotakiwa katika makumi haya matatu ya mwezi wa Ramadhan.
Ishaalah
JIBU
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ramadhaan ni mwezi mtukufu wenye fadhila nyingi, na siku zake zote ni sawa na nyingine, isipokuwa kumi la mwisho ambalo ndani yake kuna siku ya Laylatul-Qadr, siku ambayo ibada yake ni bora kuliko miezi elfu.
Hakuna dalili iliyothibitika kuwa kuna ibada khaswa ya kutekeleza katika makumi matatu ya mwanzo.
Hivyo siku nyingine zote au makumi mengine yote hayana tofauti katika fadhila za mwezi huu, bali ni kutekeleza Swawm ipasavyo, kuswali Qiyaamul-Layl (kusimama kisimamo cha usiku kuswali) na kufanya mengi ya kheri na kuzidishi Taqwa (Ucha Mungu) n.k.
Tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho kusoma yanayopasa kufanya katika kumi la mwisho:
Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhaan
Laylatul-Qadr- Vipi Tunaweza Kuupata Usiku Huu?
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
