Swawm Ya Nabii Daawuud
SWALI:
Swawm ya Nabii Daawuud
Asalam alay kum warahmatullahi wabarakatuh
Mimi nataka kuwanafunga swaumu kama ile yana biyyullahi iberaahiym nakula leo nafungakesho lakini mimi napenda kusafiri
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa nia yako njema ya kutaka kujikurubisha kwa Allaah Aliyetukuka.
Hakika
Hakika ndugu yetu hiyo Sunnah uliyoitaja sio swawm ya Nabii Ibraahim (‘Alayhis Salaam) bali ni swawm ya Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam). Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) alikuwa na Sunnah nzuri
Funga hiyo imeelezwa katika Hadiyth kadhaa, baadhi yake ni:
· Amesimulia ‘Abdallaah bin ‘Amru bin al-‘Aasw (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: “Hakika wewe unafunga kila siku na kuswali usiku mzima?” Nikasema: “Ndio”. Akasema: “…Hapana swawm ya mwenye kufunga milele, swawm ya siku tatu kila mwezi ni
· Imepokewa kwa ‘Abdallaah bin ‘Amru bin al-‘Aasw (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Swawm inayopendwa na Allaah ni funga ya Daawuud, na Swalah inayopendwa na Allaah ni Swalah ya Daawuud. Alikuwa akilala nusu ya usiku, akiswali thuluthi yake na kulala sudusi (1/6). Alikuwa akila siku moja na kufunga siku ya moja” (al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaaiy na Ibn Maajah).
Hizi funga na Swalah zilizotajwa ni zile za Sunnah sio za faradhi.
Ni vyema na vizuri kwa Muislamu anapoanza jambo jema (Sunnah yoyote) basi adumu nayo hata kama inaonekana ndogo na
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


