238-Asbaabun-Nuzuwul: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Baqarah Aayah 238: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati...

 

حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ﴿٢٣٨﴾

238. Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri), na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu.

 

 

 Sababun-Nuzuwl: Aayah hii: Shikamaneni na Swalaah na khaswa Swalaah ya katikati (Alasiri)... imeteremka kuhusu Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali Swalaah ya Adhuhuri nusu ya mchana wakati jua linaposhtadi na ilikuwa ni Swalaah ngumu zaidi kwa Maswahaba (رضي الله عنهم). Mara nyingine ilikuwa haipatikani nyuma yake ispokuwa swaffu moja au mbili. Baada ya hali hiyo, ikateremka hii Aayah. [Ahmad kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه)].

 

Sababun-Nuzuwl: Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى): “na simameni mbele ya Allaah katika hali ya utiifu” ni kwamba; walikuwa Maswahaba wakizungumza ndani ya Swalaah; mtu anamsemesha ndugu yake katika haja zake akiwa ndani ya Swalaah. Basi hapo ikateremka hii Aayah. [Al-Bukhaariy, Muslim kutoka kwa Zayd bin Arqam (رضي الله عنه)] 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share