Skip to main content

Imaam Ibn Baaz: Haijuzu Kuwakosoa Viongozi Hadharani

Kauli Za Salaf: Manhaj

Haijuzu Kuwakosoa Viongozi Hadharani

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah) amesema:

“Kuwakosoa viongozi na kutaja makosa yao hadharani au katika  minbari si katika manhaj ya Salaf, kwani hiyo inapelekea katika chokochoko (fitnah, mvurugano) na mapinduzi.”

[Uswuwl Ahli-Sunnah Hidaayah wa Amaan (64)]