Kuhusu Alhidaaya

 

 

 

Tovuti hii ya Alhidaaya.com imeanzishwa mwaka 1425H (2005M) kwa lengo la kutoa mafunzo ya Kiislamu yaliyo Sahihi kwa kufuata Kitabu cha Allaah na Sunnah Swahiyh za Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mwenendo wa Salafus-Swaalih bila ya kujiegemeza katika dhehebu au kundi lolote lile.  

 

Alhidaaya imeanzishwa na ndugu wenye niyyah ya kuwapatia Waislamu faida mbali mbali za usomaji pamoja na mawaidha kwa lugha yetu ya Kiswahili kwa wepesi kabisa ili waweze kustawisha na kuimarisha ‘ibaadah zao na iymaan zao.

 

Alhidaaya haipati misaada kutoka sehemu yoyote ile bali wanajitolea wenyewe kwa ajili ya Allaah.

 

Alhidaaya haiko chini ya serikali wala chama chochote na hakina mielekeo yoyote ile ya kisiasa.

 

Mnakaribishwa Alhidaaya.com