Skip to main content

Kamba Wa Rojo

Vitoweo

Kamba Wa Rojo

  

Vipimo

Kamba (Prawns) Large   size - 1 Kg

Nyanya zilizosagwa  (crushed) - 3

Kitunguu saumu (thomu/galic) na tangawizi - 1 Kijiko cha soup

  Nyanya ya mkebe (tomatoe paste) - 1 kijiko cha soup

Pilipili kubwa (capsicum) (kata vipande vipande)  - 1

  Pilipili mbichi -  5- 6

Chumvi

Bizari ya pilau (cummin) powder -  ½  kijiko cha chai

Bizari ya giligilani (corriander ) powder  - ½ kijiko cha chai

Bizari ya manjano (Haldi) -  ½ Kijiko cha chai

Ndimu - 1 Kijiko cha soup

Kotmiri (zilizokatwa ndogo ndogo ) -  ½  Kikombe

Mafuta - ¼ Kikombe  

Namna Ya Kupika

1. Katika karai weka mafuta yapate moto, tia thomu na tangawizi.

2. Tia tomato zilizosagwa , kaanga, tia bizari zote endelea kukaanga .

3. Tia Pilipli kubwa, pilipili mbichi, chumvi, endelea kukaanga kidogo tu.

4. Tia Kamba, ndimu,  kaanga, mwisho tia nyanya ya mkebe, endelea kukaanga  kama dakika 5 tu .  

5. Mwisho kabisa mwagia kotmiri na pakua katika sahani.