Skip to main content

Tambi Za Kukaanga

Tambi Za Kukaanga

 Vipimo

Tambi pakti moja

Sukari ¾ kikombe cha chai

Mafuta ½ kikombe cha chai

Iliki kiasi

Maji 3 Vikombe vya chai

Vanilla / Arki rose 1-2 Tone

Zabibu Kiasi (Ukipenda)

Namna ya kutayarisha na kupika

Zichambue tambi ziwe moja moja.

Mimina mafuta kwenye sufuria yakisha pata moto mimina tambi,zigeuzegeuze mpaka zibadilike rangi na kuwa brown.

Punguza mafuta kwa kuyachuja na zirudishe jikoni.

Nyunyizia iliki zilizosagwa koroga kidogo na mimina maji na tia arki na acha zichemke mpaka maji yakikaribia kukauka mimina sukari koroga kidogo na punguza moto.

Kisha tia zabibu ukipenda, zifunike ili  zikaukie vizuri.

Zikishakauka pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa

Kidokezi:

Itategemea na aina za Tambi unazopika kwa kukisia maji, kama utaona hazijaiva unaweza kuongeza maji kidogo.