Wali Wa Karoti Na Nyama

Wali Wa Karoti Na Nyama

Vipimo Vya Wali:

Mchele  -  3 Magi

Mafuta -  1/4 kikombe

Karoti unakata refu refu -  3

Vitunguu maji kata vikubwa vikubwa - 1 kikubwa

Pilipli manga  - 1/2 kijicho chai

Hiliki  - 1/2 kijiko chai

Karafuu ya unga  -  1/4 kijiko cha chai

Mdalasini   wa unga - 1/2 kijiko cha chai

Zaafarani (ukipenda) roweka katika maji -  1 kijiko cha chai

Zabibu kavu (ukipenda) - 1/4 kikombe

Chumvi kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Kwenye sufuria tia mafuta na kaanga karoti kidogo.
 2. Tia vitunguu kisha tia bizari zote.
 3. Tia maji kiasi (kutegemea aina ya mchele) na chumvi
 4. Tia mchele  upike uwive.
 5. Karibu na kuwvia tia zabibu ukipenda.
 6. Funika endelea kuupika hadi uwive.

Vipimo Vya Nyama

Nyama   -  2 Ratili (LB)

Chumvi -   Kiasi

Mafuta  - 1/4 kikombe

Kitunguu (kata virefu virefu) -  1 Kikubwa

Pilipili mboga kubwa -   2 ukipenda moja nyekundu moja kijani unazikata vipande virefu virefu.

Figili mwitu (celery) kata vipande  virefu virefu- Miche miwili.   

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Chemsha nyama hadi iwive
 2. Ikaange kwa mafuta hadi iwe nyekundu
 3. Weka vitunguu, pilipili mboga na figili mwitu
 4. Kaanga kidogo tu kama dakika moja.
 5. Tayari kuliwa na wali.

 

 

 

 

Share