Pilau Ya Nyama Kondoo Na Mtindi

Pilau Ya Nyama Kondoo Na Mtindi

 

Vipimo:

 

Nyama iliyokatwa vipande - 1 Ratili (LB)

Mchele Basmati - 2 Magi

Chumvi ya wali - kiasi

Kitungu kilichokatwa katwa - 1 kikubwa

Kitunguu saumu (thomu/garlic) na tangawizi - 1 kijiko cha supu  

Mtindi (yogurt) - ½ kikombe

Mchanganyiko wa bizari ya pilau ya tayari - 2 vijiko vya supu 

Mafuta kidogo yakukaangia

Bizari manjano (haldi) - nusu kijiko

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Osha mchele na roweka nusu saa .
  2. Weka mafuta katika sufuria na kaanga vitungu mpaka viwe rangi ya hudhurungi (brown).
  3. Tia thomu na tangawizi na ukaange kidogo.
  4. Kisha weka bizari ya pilau halafu nyama huku unakaanga lakini nyama isigeuke rangi.
  5. Tia maji gilasi 1½- 2 ichemke mpaka nyama iwive na karibu kukauka.
  6. Mimina mtindi na iachie moto mdogo ikauke kidogo.
  7. Kwenye sufuria nyingine chemsha mchele pamoja na chumvi na mafuta kidogo mpaka uive.
  8. Mimina wali juu ya nyama, kisha nyunyiza bizari ya manjano, kama vile wali wa biriani na ufunike kwa dakika kumi hivi.
  9. Changanya  wali na nyama pamoja ikiwa tayari kuliwa kwa saladi.

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)

 

 

 

Share