Keki Ya Nanasi

Keki Ya Nanasi

 

Vipimo: 

Unga  - 2 vikombe vya chai 

Sukari  -  1 ½ kikombe cha chai 

Mafuta -  1 ½ kikombe cha chai 

Baking powder -  2 vijiko vya chai 

Siagi -  ¼ kikombe cha chai 

Mayai -  6 

Sukari ya hudhurungi (brown) - 1 ¾  kikombe cha chai 

Manasi ya kopo yaliyokatwa duara - 1 kopo   

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Unayeyusha sukari ya hudhurungi  pamoja na siagi. Ikishayeyuka vizuri unamimina kwenye sufuria au trei ya kuchomea keki.
  2. Panga vipande  vya nanasi kwenye hiyo sufuria/trei. Weka pembeni. Ukipenda katikati ya duara ndogo ya nanasi weka cheri moja.
  3. Kwenye bakuli la kuchanganyia keki la mashine, piga mayai, sukari, vanilla mpaka iwe kama malai (crème) na nzito.
  4. Mimina unga pamoja na baking powder, piga kidogo, mwisho mimina mafuta.
  5. Mimina huo mchanganyiko kwenye sufuria/trei uliyopanga vipande vya nanasi, tayari kuchoma.
  6. Weka moto 180 C choma kwa muda wa dakika 30 – 35.
  7. Ikishaiva, acha ipowe kwa muda wa dakika 7, mimina chini juu kwenya sahani, tayari kwa kuliwa.

 

 

Share