Chapati

Vipimo
~4 VIKOMBE VYA UNGA WA NGANO MWEUPE
~3 VIJIKO VYA KULIA VYA SAMLI
~2 VIJIKO VYA CHAI VYA CHUMVI
~2 VIKOMBE VYA MAJI VUGU VUGU
~SAMLI YA KUPIKA CHAPATI
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja.
2. Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
3. Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi,
4. Finika na uache mchanganyiko kwenye sinia
5. Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge
6. Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
7. Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
8. Paka samli
9. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha
10. Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.
11. Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
12. Sukuma chapati iwe mviringo

13. Pika chapati kwenye frying pan moto wa kiasi. Ikiiva
upande mmoja na kuanza kufura, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kupress na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha kulia cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifingue vizuri.

14. Endelea namna hii huku unafuta frying pan na kitambaa kisafi au karatasi za jikoni (tissue) baada ya kila chapatti.
Kidokezo
Unapomaliza kuzipika kila moja, zitandaze kwanza chapati katika sahani (au sinia) kubwa zipate kupoa ziwe kavu ili zisinyonyanye mafuta. Kisha tena ziweke katika sahani yako ya kawaida.

Ni nzuri kutolea na jam au asali
.jpg)
Unaweza ku freeze chapati katika Freezer bags. Kunja chapati moja moja ziwe nusu. Zifunike na Wax paper, kisha zitie kwenye freezer bags na uzihifadhi katika freezer. Unapotaka kula, toa kwenye freezer na upashe moto katika Microwave.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


