Mkate Wa Kifaransa (French Toast)

Mkate Wa Kifaransa (French Toast)

Vipimo
 
 Mayai -  6
 
 Maziwa- 1½ Vikombe vya chai
 
 Vanilla/iliki- Kidogo
 
 Mdalasini ya unga-  ¼-½ Kijiko cha chai
 
 Ganda la ndimu iliyokaruzwa - 1 kijiko cha supu
 (lemon zest)
 
 Maji ya machungwa -  ¼ Kikombe cha chai
 
 sukari -  1 Kijiko cha supu
 
 Mkate wa slesi -    6-8 
 
 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 
 
 1. Changanya pamoja vipimo vyote isipokuwa mkate kwenye bakuli; weka    
      kando.
 2. Panga mikate katika chombo kikubwa(trei) , kisha mimina ule    
     mchanganyiko wa mayai juu yake na iache irowanike dakika 5 hivi. 
 3. Weka chuma kipate moto, kisha tia siagi au/na mafuta na upange mikate
     kadha kama itakavyotosha kwenye chuma cha kuchomea.
 4. Iwche hadi iive na kuwa rangi ya dhahabu, kisha geuza upande wa pili
     na endelea hivyo hivyo mpaka umalize mikate yote. 
 5.Panga katika sahani na itakuwa tayari kuliwa na shira ya matunda kama
    maple syrup.

Share