Basbusa

Vipimo
Unga wa Semolina 2 Vikombe
Siagi (butter) au samli 3/4 kikombe
Sukari 3/4 kikombe
Mtindi (Yoghurt au buttermilk) 1 1/4 kikombe
Vanila 1-2 kijiko cha chai
Baking powder 1 kijiko cha chai
Baking soda 1 1/2 kijiko cha chai
Lozi zilizomenywa maganda kwa ajili ya kupambia.
Shira
Sukari 1 kikombe
Maji 1 kikombe
Ndimu ya maji 1 kijiko cha chai
Pika shira mapema. Chemsha kwa muda wa dakika 20-25 itakapopoa iwe nzito kidogo sio nyepesi
Namna Ya Kutayarusha Na Kupika
1. Washa oveni moto wa 350ºF
2. Yayusha siagi au samli na iache ipowe.
3. Changanya sukari na mtindi katika bakuli kubwa.
4. Changanya semolina, vanila, baking powder, baking soda katika bakuli jengine.
5. Tia mchanganyiko wa semolina katika bakuli lenye mchanganyiko wa sukari na mtindi na changanya vizuri.
6. Paka siagi katika sinia ya oveni (baking tray) ya saizi 11" x 7 " au 13" x 9" na tandaza mchanganyiko.
7. Weka alama ya kukata vipande vipande vya mraba (square) na katika kila kipande weka lozi moja juu yake kupambia.
7. Iache kwa muda wa dakika 15-20 kabla ya kuipika.
8. Pika (bake) kwa muda wa dakika 30 au zaidi kidogo hadi iwive na igeuke rangi.
9. Epua katika oveni na mwagia shira wakati bado imoto na shira iwe iliyopoa baridi.
Kidokezo:
Ikiwa basbusa ni imoto basi shira iwe baridi, na ikiwa basbusa ni ibaridi basi shira iwe imoto.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


