Skip navigation.
Home kabah

Kuku Wa Kuchoma Wa Sosi Ya HP


 

 
 

Vipimo

 

 

 

Kuku (miguu)                                      5 pounds (vipande 20-25)

 

Vitu vya sosi (sauce)

 

Thomu na Tangawizi ya kusaga         3 Vijiko vya supu

 

Chumvi                                                Kiasi

 

Sosi ya soy (soy sauce)                     2 vijiko vya supu

 

HP sauce                                             3 vijiko vya supu 

              

Siki au ndimu                                      3 Vijiko vya supu

 

Pilipili manga                                      1 kijiko cha supu

 

Nyanya ya kopo                                 1 kijiko cha chai

 

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
 
 
1.      Msafishe kuku kwa siki au bizari ya manjano kukata harufu.
 
2.      Mtie katika treya ya kuchomea, weka chumvi kisha mchome (bake) kwa muda kiasi hadi karibu na kuwiva.
 
3.      Mwaga maji yatakayotokeza kwa ajili ya kumchoma.
 
4.      Changanya vitu vyote vya sosi (sauce) na tia katika kuku  umchanganye vizuri na sosi  hiyo.
 
5.      Mrudishe katika jiko kwa kumchoma sasa kwa moto wa juu
    (grill) hadi awive vizuri na ageuke rangi na tayari kuliwa.