Kuku Wa Kuchoma Katika Makaa (B.B.Q)

Vipimo
Kuku 10 Ratili (LB)
Thomu na tangawizi 3 vijiko vya supu
Chumvi Kiasi
Bizari mchanganyiko (garam masala) 2 vijiko vya supu
Masala ya Tanduri 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Ukwaju 1/2 kikombe
Siki 3 Vijiko vya supu
Mafuta 1 Vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Safisha kuku kisha mwache achuje maji vizuri.
2. Changaya masala yote kwenye bakuli pamoja na mafuta.
3. Tia masala katika kuku na rowanisha kwa muda wa masaa 6 au zaidi. Na ukipenda rowanisha kuku siku moja kabla uweke katika friji.
4. Mchome katika jiko la makaa huku ukimpaka mafuta kidogo kidogo ka brashi.
Kidokezo : Tolea na saladi ya karoti na ukwaju (Tazama katika saladi)
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


