Vilosa

VIPIMO
Mchele 1/2 Kikombe
Semolin 1 Vikombe
Tui la nazi 3/4 Kikombe
Maziwa 1/2 Kikombe
Mayai 3
Hamira 1 kijiko cha chai kijae
Rose essence kidogo
Zaafarani kidogo
Sukari 1 kijiko cha chai
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUTENGENEZA
1. Roweka mchele tokea usiku
2. Uchuje mchele maji yote
3. Weka kwenye mashine ya kusagia (Blender)
4. Tia mayai, maziwa, sukari, hamira , rose essence, zaafarani. Kasha usagesana mpaka chenga za mchele zote zisagike.
5. Tia semolina na tui la nazi, kasha endelea kusaga katika blender, kidogo mpaka ichanganyike vizuri.
6. Mimina katika bakuli kubwa, funika iwache iuumuke.
7. Ikishaumuka choma
8. Shira ikipowa, tumbukiza Vilosa kwa kiasi kiasi , changanya na uvitoe uviweke upande katika sahani ya kupakulia.
9. Endelea kufanya mpaka vyote vimalizike.
SHIRA : Tengeneza mapema ipowe. Na isiwe nzito
Sukari 2 Vikombe
Maji 1 kikombe
Zaafarani kidogo
Rose Essence
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


