|
019-Masharti Ya Kushuhudia Kwamba Hapana Mwabudiwa Wa Haki Ila Allaah
Swali:
ما هي شروط شهادة أن لا إله إلا الله التي لا تنفع قائلها إلا باجتماعها فيه؟
Ni yapi masharti ya kushuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, ambayo (shahada hiyo) haimnufaishi anayeitamka isipokuwa yakikusanyika ndani yake?
Jibu:
شروطها سبعة: الأول: العلم بمعناها نفياً وإثباتاً. الثاني: استيقان القلب بها. الثالث: الانقياد لها ظاهراً وباطناً. الرابع: القبول لها فلا يرد شيئاً من لوازمها ومقتضياتها. الخامس: الإخلاص فيها. السادس: الصدق من صميم القلب لا باللسان فقط. السابع: المحبة لها ولأهلها، والموالاة والمعاداة لأجلها.
Masharti yake ni saba:
La kwanza: Ilimu ya maana yake, katika kukanusha na kuthibitisha.
La pili: Moyo kuwa na yakini nayo.
La tatu: Kuifuata kwa utiifu kwa dhahiri na kwa siri.
La nne: Kuikubali, hivyo asikatae chochote katika yanayolazimiana nayo na yanayotakiwa nayo.
La tano: Ikhlaasw (kumtakasia Allaah) ndani yake.
La sita: Ukweli unaotoka kiini cha moyo, si kwa ulimi tu.
La saba: Kuipenda na kuwapenda watu wake, na kufanya urafiki na uadui kwa ajili yake.