033-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Ahzaab Aayah 05: ادْعُوهُمْ لآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 05

 

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ ۚ فَإِن لَّمْ تَعْلَمُوا آبَاءَهُمْ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ وَمَوَالِيكُمْ ۚ وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُم بِهِ وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ غَفُورًا رَّحِيمًا ﴿٥﴾

Waiteni kwa (majina ya) baba zao, huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah. Na ikiwa hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na walio katika ulinzi wenu, na wala hakuna dhambi juu yenu katika yale mliyoyakosea, lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu; na Allaah daima ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Ahzaab 33: 5]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 

 

حَدَّثَنَا مُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ الْمُخْتَارِ، حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ عُقْبَةَ، قَالَ حَدَّثَنِي سَالِمٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ زَيْدَ بْنَ حَارِثَةَ، مَوْلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَا كُنَّا نَدْعُوهُ إِلاَّ زَيْدَ ابْنَ مُحَمَّدٍ حَتَّى نَزَلَ الْقُرْآنُ ‏((‏ادْعُوهُمْ لآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ))‏

 

Ametuhadithia Ma’-alaa bin Asad, ametuhadithia ‘Abdul-‘Aziyz bin Al-Mukhtaar, ametuhadithia Muwsaa bin ‘Uqbah, amenihadithia Saalim toka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) kwamba Zayd bin Haaritha mwachwa huru wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) hatukuwa tukimuita isipokuwa Zayd bin Muhammad mpaka Allaah [Ta’aalaa] Alipoteremsha:

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ 

Waiteni kwa (majina ya) baba zao, huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.

 

[Al-Ahzaab (33:5) - Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kumi ukurasa wa 136]

 

[Ameikhariji Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy kwa Isnaad tofauti toka kwa Muwsaa bin ‘Uqbah. Pia Al-Bukhaariy ameikhariji katika Mujallad wa Kumi na Moja, Abu Daawuwd katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 181, An-Nasaaiy katika Mujallad wa Sita ukurasa wa 53, Ahmad katika Mujallad wa Sita ukurasa wa 271, ‘Abdur Razzaaq katika Mujallad wa Saba kurasa za 460 na 461, Ad-Daaramiy katika Mujallad wa Pili ukurasa wa 158, na Ibn Al-Jaaruwd katika ukurasa wa 231]

 

 

Na pia,

 

عَنْ عَائِشَةَ قَالَتْ جَاءَتْ سَهْلَةُ (بِنْتُ سُهَيْلِ بْنِ عَمْرٍو وَكَانَتْ تَحْتَ أَبِي حُذَيْفَةَ بْنِ عُتْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ) رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ: إِنَّ سَالِمًا مَوْلَى أَبِي حُذَيْفَةَ يَدْخُلُ عَلَيْنَا وَأَنَا فُضُلٌ وَإِنَّمَا نَرَاهُ وَلَدًا وَكَانَ أَبُو حُذَيْفَةَ تَبَنَّاهُ كَمَا تَبَنَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَيْدًا فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: ((ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ)) فَأَمَرَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ أَنْ تُرْضِعَ سَالِمًا - قَالَ أَبُو مُحَمَّد هَذَا لِسَالِمٍ خَاصَّةً

 

Toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa), amesema: Sahlah bint Suhayl bin ‘Amri ambaye alikuwa mke wa Abu Hudhayfah alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) akamwambia: Hakika Saalim anaingia chumbani kwetu na sisi hatujajisitiri ipasavyo, na sisi tulikuwa tunamwona kama mtoto wetu [wa kumzaa]. Abu Hudhayfah alikuwa amemfanya mtoto wa kupanga kama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyomfanya Zayd mtoto wa kupanga. Na hapo Allaah Akateremsha:

 

ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ 

Waiteni kwa (majina ya) baba zao, huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah.  

 

Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamuru hapo anyonyeshwe Saalim (na Sahlah).  Amesema Abu Muhammad: “Hiyo ilikuwa makhsusi kwa Saalim pekee.”

 

[Ad-Daarimiy  Hadiyth (2157) Kitaab An-Nikaah Baab Fiy Radhwaa’ai Al-Kabiyr]

 

 

Huenda Aayah ikawa imeteremka kuwazungumzia wote wawili: Zayd na Saalim. [At-Tirmidhiy katika Mujallad wa Nne ukurasa wa 165 amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

 

 

Share